Hasira za nini Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete?

Hasira za nini Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete?

Mtoa Uzi umedhihilisha ulofa ulokuwa nao!!!! Unafula kisa lowasa??????? Njaa mbaya sana....

Magufuli for president

Wanaompenda lowassa njaa, vp wanao mpenda magufuli. Kujiona nyie ndio bora sikitu kizuri kabisa. Mnakera sn.
Nikweli njaa mbaya ndio maana ccm pia wanatumia kila mbinu kubaki pamoja na kuwa wametawala miaka yakutosha
 
Mzee nae atabaki analinda kura kule Monduli? Au ataacha yake iibiwe? Je watoto wake kina Fred na Pamela watalinda jura au wataacha ziibiwe?

Fred na Pamela wamepangwa vituo, ni mawakala wa cdm kilammoja na kituo chake. Sasa unataka waache waende monduli kulinda kura au unataka kwenda kuwasaidia?
By the way nafsi ikusute, maana kama hukupokea au kutoa rushwa wakati wa kura za maoni basi uliyaona na kuamini kuwa wagombea wengi walihonga ili kupitishwa na hawatacha kuhonga ili kupitisha kura nyingi feki.
 
Ndiyo maana mnainamishwa mitaani kupigishwa deki kisa mmepewa buku tano...mnakatika viunooo weee mnazungushazungush mAunoo weee .....mnakuwa kama magosha vile.......


Magufuli for president
 
Last edited by a moderator:
Naomba ujumbe huu umfikie mh Jakaya Mrisho Kikwete, Amiri jeshi mkuu wa jamhuri ya muungano Tanzania, Rais aliyebakiwa na siku chache, masaa machache kuiacha Ikulu. Swala la kuiacha ikulu ni swala la kikatiba, tena lipo wazi hakuna wa kulipinga.

Nimefuatilia hotuba ya Rais J. K, kwa makini sana, hasa kwenye kipengele kile cha uchaguzi. Ametumia hasira, ameongea kwa ghadhabu na vitisho vingi kwa watu wa upinzani.

Nikajiuliza sana juu ya kauli zake.
Kwanza nilijihoji mwenyewe kwamba haya maazimisho ni ya chama cha mapinduzi CCM au ni maazimisho ya kilele cha Mwenge au ni maazimisho ya kifo cha mwasisi wa Taifa Letu Mwl. J. K. Nyerere? Maswali haya yalinijia baada ya kuona Mh J. KIKWETE ameuvaa U CCM na sio Urais.

Najua sina uwezo wa kumfikia moja kwa moja Mkuu wa nchi, ila ujumbe wangu utamfikia moja kwa moja au kupitia kwa wapambe wake.

Mh Rais naomba utambue mambo mawili matatu toka kwetu sisi tulio malofa na wapumbavu.Na kwa nia njema kabisa naomba ujue kuwa

1.Hatutaogopa kupigwa mabomu, kufungwa, kuuwawa au lolote kwa kutafuta haki yetu ya msingi. Tunaamin kuwa kifo ni siku moja tu wala sio mara mbili.

2.Tutapiga kura zetu na kuzilinda kwa mjibu wa sheria, taratibu na kanuni za uchaguzi wala si vinginevyo.
Hakuna wakututisha hata kidogo ndani ya nchi yetu ambayo tunaamini ni ya kidemokrasia.

3.Tutahakikisha mgombea tunayemhitaji anashinda kwa kumpigia kura nyingi za kutosha na kuhakikisha hakuna atakayeiba kura zetu, najua mwalijua hilo.

5.Kwa umoja wetu tutashirikiana na vyombo vyote kulinda amani ya nchi yetu Tanzania.

5.Tutatoa ushirikiano kwa yeyote anayependa haki itendeke, na tutamdhibiti atakayejaribu kupoka haki yetu.
Ikumbukwe mita 100 sio mbali sana ni sawa na usawa wa gori moja hadi gori jingine katika uwanja wa mpira.

Rais Kikwete kitendo cha kututishia kuwa tutakaolinda kura tutadhibitiwa na umeyaongea maneno haya kwa hasira kuu, unatudhihirishia wazi kuwa Chama chako cha CCM kimejipanga kuiba kura au kufanya kinyume na taratibu za uchaguzi .

Kama mlipanga mbinu chafu mkadhani tutaogopa basi imekula kwenu, tunatambua wazi kuwa, kuna magari mengi ya washawasha, askari wengi, vitendea kazi vya kisasa lakini sisi tunasema hatutaogopa vifaa hivyo kwakuwa sisi sio watu wa fujo ni watu wa haki.

Mwisho napenda Mh J. KIKWETE atambue kuwa yeye kaongoza kwa miaka yake 10 na anakwenda kupumzika, hivyo aende akapumzike kwa amani kabisa, ajiepushe na matamko yatakayokuja kumpeleka ICC wakati hakustahili kwenda huko hata kidogo, na Tr 25/10/2015 akapige kura alipojiandikishia amchague anayempenda yeye, awe diwani, Mbunge au Rais

Japo kwa Heshima na Taadhima namuomba kura yake upande wa Rais ampigie Mh Edward Lowassa, na naamini atampigia kura.

Naomba nimalize kwa kusema WATANZANIA wote tujitokeze Tr 25/10/2015 tukawapigie kura viongozi tunaoona wanafaaa,binafsi nawaomba kura za Mh. EDWARD LOWASSA na naamini tutampigia kura za kutosha na tutazilinda kwa amani bila vurugu yoyote ile. Tudumishe amani na upendo.
Ahsante

mkuu kwanza pole Sana kwa kuwa na mwenyekiti was chama chenu cha chadema hasiye zielewa vizuri sheria za uchaguzi cha muhimu tambua kwamba hakuna sheria ya uchaguzi inayosema watu wakae mita Mia mbili kutoka kwenye kituo cha kupigia kura na kusubiria matokeo ya uchaguzi.ila Kama mbowe aliandika sheria hio anayoisema yeye nenda mkuu afu utaona kitakachokutokeeni
 
Kipindi kama hiki ndo umuhimu wa ICC unaonekana. Hayo maneno yake ya leo ni ushahidi mzuri sana. Likitokea anachoombea basi hawezi kwepa ICC.
Watakufa kina nani ili kina fulani wapelekwe ICC.Je,watakuwemo pia watoto,wake na ndugu wa MBOWE,LOWASSA,MENGI,NDESSAPESSA NA SUMAYE(Maana hapa VITI MAALUMU NDO WATAPEWA.
 
RadioOneStereo
Serikali imeonya kuwa itawachukulia hatua za kisheria watakaobaki katika vituo vya kupigia kura kwa madai ya kulindakura kwa kuwa ni kinyume cha sheria.
1-Tutashinda hata kwa bao la mkono
2-CCM haitong'oka kirahisi kama jino
3-Hatutofanya kosa kukabidhi Ikulu kwa wapinzani
?????????????!!!!!!!!!!!!!
 
POVU Kibao Hoja Za WanaCCM Hazina MASHIKO Kabisaa!! Mnatengeneza Mazingira Ya Wizi Tu!! Sote Tunajua Na Tunaona Jinsi Mawakala Wanavyokuwa Wakinunuliwa!! Mbona WATANZANIA Wanafahamu Hilo!! Kama Viongozi Wakubwa Tu Ktk Siasa Wamenunuliwa Na Kufanya Kazi Za CCM!! Itakuwa Kwa Wanachama WADOGO Tu!!!?? Kuna MSEMO USEMAO " Kila Mtu Ana Bei Yake " Mf. Wakala Wa UKAWA Amepewa Million 1 Tu!! Na Anakuja Mtu Na Million 3 Cash!! Hebu Mtuambie Hapo!! Hapo NDIO WanaCCM POVU Linapowatoka!!
 
sheria ya uchaguzi ya mwaka 1984 kifungu cha 104 na marekebisho yake ya mwaka 2010 ambayo inampa haki mwanachi kukaa kituoni baada ya kupiga kura na ndio maana matokeo yana tangazwa wananchi wasikie na yanabandikwa nje ili wananchi wasome
 
"Mungu akubariki mtoa uzi, umekomaa kifikra (sisi malofa na wapumbavu katika ubora wetu), nikuunge mkono kwamba kwa amani kabisa, kwanza kura zetu kwa Lowassa, halafu tutazilinda kura hata ikibidi kwa masaa 72 hatoki mtu hapo mpaka tumetangaziwa na kujua Nani kashinda kituo husika, hatuogopi wanaotutisha, ila tutaheshimu sheria,taratibu na kanuni, nasi tunashauri, asijidanganye mwanadamu awaye yeyote kujaribu kupokonya haki yetu, hapo ndipo Bensouda wa ICC atakapowashughulikia"
Na muda huo wewe utakuwa wapi mkuu na familia yako??!Lowassa na Sumaye watakuwa wapi pia?Na watoto wao watakufa pia amma vipi?
 
Mkuu kapanic pumzi imekata

Ushauri wangu kwake ni kuwa a-relax akisubiri yeyote atakayepewa kura na watanzania amkabidhi ikulu! Lakini haya mawazo kwamba akiwa magufuli rais ndo apate usingizi yatamtesa bure!!!!
Bado hatujaona mwenye ubavu wa kuzuia mafuriko kwa mkono!!!!! Lipumbi aliwaza tu wala hakuthubutu kujaribu kusogeza mkono wake kuzuia mafuriko maana alijua ni kupoteza muda!
Docta Mihogo yeye alijitahidi kunyosha mkono wake kuzuia mafuriko lakini kilichotokea ni kuwa alisombwa na MAJI na Leo hii ukitaka habari za Dr. Mihogo itabidi ukamtafute kwenye jumba la makumbusho!!! maana huku mitaani keshasahaulika hata magamba wameona haitalipa wakimtumia na wamemwacha kwenye mataa!!!
 
Miaka kumi work done ZERO anafikiri siku kumi alizobakiza atafanya miujiza.

Akalime mihogo Msoga tu, mambo ya kura na jinsi ya kuzilinda atuwachie sisi.
 
sheria ya uchaguzi ya mwaka 1984 kifungu cha 104 na marekebisho yake ya mwaka 2010 ambayo inampa haki mwanachi kukaa kituoni baada ya kupiga kura na ndio maana matokeo yana tangazwa wananchi wasikie na yanabandikwa nje ili wananchi wasome

Hii inashangaza sana! Sheria inapotaka matokeo yabandikwe kituoni maana yake ni kuwa watu watakuwepo ili wasome!
Waachane tu na mazingira yanayotia moyo goli la mkono!!!!
 
anataka anenepeshe ng'ombe ndani ya siku 10 mr paniki
 
Kikwete wa ajabu kweli kweli.
yaani anathubutu kusema wananchi wasilinde kura!!!!!? kwa mtizamo huo haishangazi faru wakimalizwa mbugani, haishangazi tembo wakiendelea kumalizwa hali ya kuwa kuna walinzi wa wanyamapori,
UNAWEZA KUACHA MLANGO WAZI KWA KUTEGEMEA POLISI? UKIACHA UKAIBIWA KISHERIA UTAWASHITAKI POLISI?
NI NINI DHANA YA ULINZI SHIRIKISHI.
KIKWETE USITUTANIE SISI SIO WATANI ZAKO.
 
Kila siku mnasema JK rais dhaifu ili kuthibitisha hilo basi ukishapiga kura baki kituoni uone udhaifu wa JK.
 
Back
Top Bottom