Hasira za nini Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete?

Hasira za nini Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete?

Hata kama JK,Magufuli,Bilal,Mkapa,Mwinyi na wanaCCM Wote wakiamua kumpigia KURA FISADI Lowassa.FISADI LOWASSA Hawezi kuwa RAIS WA NCHI Hii.Beautiful Tanzania Is Not For Sale

Unaelewa ulichoandika? je una uhakika/ushahidi kwamba lowassa ni fisadi? na kama unao kwanini hujaenda mahakamani?? na kama unao na hujaenda huoni wewe ndiye jambazi na usitakiwa kuaminika kwenye hii nchi?
 
M4C na kura tutazilinda tupo tayari kufa watoto wetu waishi vizuri kama ambavyo wao wanakuwa na hasira za kufanikasha wayatakayo kwa manufaa yao na familia zao, sitakuwa wa kwanza kufa ktk kusaka haki na hata kama wao watabaki je watabaki mpaka lini ikiwa kila mwenye maisha ni marehem mtarajiwa...

Daah
maneno .mazitto kwelii kweli:
 
Unaelewa ulichoandika? je una uhakika/ushahidi kwamba lowassa ni fisadi? na kama unao kwanini hujaenda mahakamani?? na kama unao na hujaenda huoni wewe ndiye jambazi na usitakiwa kuaminika kwenye hii nchi?

Lowassa ni Fisadi Papa na Ushahidi anao John Mnyika,Tundu Lissu na Dr. Slaa
 
Kikwete kumwaga damu ya Watanzania wanaodhamiria kulinda haki (kura) zao ni halali. Ila watanzania kuamua kukaa umbali ulioruhusiwa kisheria wa mita 200 kutoka eneo la kupigia kura wakiwa hawana silaha yoyote, huo ni uvunjifu wa amani. Kweli magamba ni hoi bin taaban, yaan mpaka dingi wao anaweka sheria ya kutotoka nje (curfew) siku ya chaguzuuzzz!!!!
 
Sasa mbona mna wasiwasi wa kuibiwa? Tafuteni mawakala mnao waamini ili wa kusimamieni kura zenu, naona mnajijua nyinyi watu dili ndio maana mnawaza kuibiwa, sisi hatuna shida tukimpa wakala wenu sh50,000tuanasaini.mbona viongozi wenu hakukataa pesa kwa Lowasa,mtaisoma namba ccm mbele kwa mbele.
 
Nashangaa mnyika Lissu mbowe na mdee wapo kimya maskini hawana cha kuongea juu ya Lowasa kwani wao ndio walimwita fisadi papa na kujipatia umaarufu juu ya Lowasa leo ndio anataka kuwaongoza kweli mmekwisha, sasa mnatoa hutuba zenu kwa vizia.
 
Nyamagana walionesha mfano 2010. Shinyanga Mjini wanajua msipolinda kura inakuaje na mwaka huu tutakaa kwa utulivu 200m tukunywa maji yetu pale tutangoja msimamizi atangaze matokeo kama mmepanga kutuua mie niueni Maana sitegemewi na mtu sina Chochote ila nahitaji mabadiliko na nitalinda kura yangu kwa mujibu wa sheria
 
Malofa wote, pigeni kura mkitoe, msilete usumbufu lasivyo vilema vitawakuta.
 
Mleta mada umenena,haswa tutapiga kura kwa amani na tutalinda kura zetu.
 
Naomba ujumbe huu umfikie mh Jakaya Mrisho Kikwete, Amiri jeshi mkuu wa jamhuri ya muungano Tanzania, Rais aliyebakiwa na siku chache, masaa machache kuiacha Ikulu. Swala la kuiacha ikulu ni swala la kikatiba, tena lipo wazi hakuna wa kulipinga.

Nimefuatilia hotuba ya Rais J. K, kwa makini sana, hasa kwenye kipengele kile cha uchaguzi. Ametumia hasira, ameongea kwa ghadhabu na vitisho vingi kwa watu wa upinzani.

Nikajiuliza sana juu ya kauli zake.
Kwanza nilijihoji mwenyewe kwamba haya maazimisho ni ya chama cha mapinduzi CCM au ni maazimisho ya kilele cha Mwenge au ni maazimisho ya kifo cha mwasisi wa Taifa Letu Mwl. J. K. Nyerere? Maswali haya yalinijia baada ya kuona Mh J. KIKWETE ameuvaa U CCM na sio Urais.

Najua sina uwezo wa kumfikia moja kwa moja Mkuu wa nchi, ila ujumbe wangu utamfikia moja kwa moja au kupitia kwa wapambe wake.

Mh Rais naomba utambue mambo mawili matatu toka kwetu sisi tulio malofa na wapumbavu.Na kwa nia njema kabisa naomba ujue kuwa

1.Hatutaogopa kupigwa mabomu, kufungwa, kuuwawa au lolote kwa kutafuta haki yetu ya msingi. Tunaamin kuwa kifo ni siku moja tu wala sio mara mbili.

2.Tutapiga kura zetu na kuzilinda kwa mjibu wa sheria, taratibu na kanuni za uchaguzi wala si vinginevyo.
Hakuna wakututisha hata kidogo ndani ya nchi yetu ambayo tunaamini ni ya kidemokrasia.

3.Tutahakikisha mgombea tunayemhitaji anashinda kwa kumpigia kura nyingi za kutosha na kuhakikisha hakuna atakayeiba kura zetu, najua mwalijua hilo.

5.Kwa umoja wetu tutashirikiana na vyombo vyote kulinda amani ya nchi yetu Tanzania.

5.Tutatoa ushirikiano kwa yeyote anayependa haki itendeke, na tutamdhibiti atakayejaribu kupoka haki yetu.
Ikumbukwe mita 100 sio mbali sana ni sawa na usawa wa gori moja hadi gori jingine katika uwanja wa mpira.

Rais Kikwete kitendo cha kututishia kuwa tutakaolinda kura tutadhibitiwa na umeyaongea maneno haya kwa hasira kuu, unatudhihirishia wazi kuwa Chama chako cha CCM kimejipanga kuiba kura au kufanya kinyume na taratibu za uchaguzi .

Kama mlipanga mbinu chafu mkadhani tutaogopa basi imekula kwenu, tunatambua wazi kuwa, kuna magari mengi ya washawasha, askari wengi, vitendea kazi vya kisasa lakini sisi tunasema hatutaogopa vifaa hivyo kwakuwa sisi sio watu wa fujo ni watu wa haki.

Mwisho napenda Mh J. KIKWETE atambue kuwa yeye kaongoza kwa miaka yake 10 na anakwenda kupumzika, hivyo aende akapumzike kwa amani kabisa, ajiepushe na matamko yatakayokuja kumpeleka ICC wakati hakustahili kwenda huko hata kidogo, na Tr 25/10/2015 akapige kura alipojiandikishia amchague anayempenda yeye, awe diwani, Mbunge au Rais

Japo kwa Heshima na Taadhima namuomba kura yake upande wa Rais ampigie Mh Edward Lowassa, na naamini atampigia kura.

Naomba nimalize kwa kusema WATANZANIA wote tujitokeze Tr 25/10/2015 tukawapigie kura viongozi tunaoona wanafaaa,binafsi nawaomba kura za Mh. EDWARD LOWASSA na naamini tutampigia kura za kutosha na tutazilinda kwa amani bila vurugu yoyote ile. Tudumishe amani na upendo.
Ahsante



Huyu jamaa namchukia sana kutoka moyoni natamani siku moja akaishi uhamishoni
 
Nyamagana walionesha mfano 2010. Shinyanga Mjini wanajua msipolinda kura inakuaje na mwaka huu tutakaa kwa utulivu 200m tukunywa maji yetu pale tutangoja msimamizi atangaze matokeo kama mmepanga kutuua mie niueni Maana sitegemewi na mtu sina Chochote ila nahitaji mabadiliko na nitalinda kura yangu kwa mujibu wa sheria
Hata Fred Lowassa hawezi kusema hivyo.Wazazi wako wana HASARA
 
Back
Top Bottom