Hasira za nini Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete?

Hasira za nini Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete?

Kuna sheria gan ya uchaguzi inayomruhusu mpiga kura kulinda kura yake... Acha upotoshaji ww

katiba ndiyo inamruhusu kulinda mali zake na kujilinda mwenyewe, kwa tafsiri ya kulinda mali, kura inatumbukia kwenye kipengele hicho, hakutakuwa na sheria inayokinzana na KATIBA na sheria hiyo ikabaki kuwa sahihi (hii ni kwa mujibu wa katiba)

Hata common sense inaelekeza kuwa HAKUNA KOSA LA KULINDA MALI.
 
Mkuu kayumba yumba,nakupa LIKE.
Umeandika kwa uchungu sana lakini maneno yenye busara,hekima na heshima.
Natamani kama viongozi wetu wa kitaifa wangekuwa wanaongea na kutenda kwa busara,hekima na werevu hata nusu ya wa kwako,tungekuwa mbali mno kama taifa.
Ubarikiwe
 
Kwa hiyo ukivunja sheria uachwe tu,, eti kwa kigezo cha kuogopa amani ivunjike,, nani kakwambia sheria zinatambua mpiga kura kulinda kura yake!!! hao icc sio wehu,, eti upigwe risasi au uumie kwa kulinda kura wakati hilo ni jukumu la serikali halali ambayo ipo madarakani.... Me nafikiri mnataka lowassa ndio apelekwe ICC maana wafuasi wake ndio wataua na kijiua wenyewe kwa kutotii sheria na amri halali ya vyombo vya dola,, CCM nao wakiamua kubaki vituoni kwa kigezo cha kulinda kura zao unafikiri nini kitatokea,, ACT,CHAUMA nao walinde kura zao sasa nini maana ya dola??? Tulipigania suala la katiba mpya tuwe na uchaguzi huru sasa mmewakumbatia wapinga katiba nakuwafanya viongozi wenu wa harakati huku wakifikiria urais na kusahau mengineyo...
ukiwa mzembe utakufa au kupata kilema kwa kumpigania mtu anayetaka kutimiza ndoto yake ya kuwa rais bila kujali damu kiasi gani itapotea,, na huwa mnasahau haraka sana maana lowassa alishawaambia suala la kura mumuachie nyie mpige kura na mkalale mengine alisema mumuachie sasa leo tena sijui imekuwaje hatua 100, siwezi kutoka damu au kufa kwa kupigania aina hii ya mabadiriko yanayoongozwa na watu ambao ni sehemu ya adui tunayepambana naye,,, acha harakati zisubiri hatuna haraka ila tunahitaji uhalisia...

Mnawekaga kura kwenye mahotipoti ya chai! mtu mzima unafanya michezo ya kishetaani kabisa!!
 
M4C na kura tutazilinda tupo tayari kufa watoto wetu waishi vizuri kama ambavyo wao wanakuwa na hasira za kufanikasha wayatakayo kwa manufaa yao na familia zao, sitakuwa wa kwanza kufa ktk kusaka haki na hata kama wao watabaki je watabaki mpaka lini ikiwa kila mwenye maisha ni marehem mtarajiwa...
 
Guyz mi naona ukibishana na mwanaccm muda mfupi ujao unakuwa naww hamnazo mana hawa jamaa walioweng hawatumii vichwa kbs kufikiria
 
Nina uhakika wewe hauishi TanZania na ndiyo maana umeandika utumbo ulioandika, eti uko tayari kufa, unafikiri kuna Mtz ambaye yuko tayari kufa kwa ajili ya fisadi Lowasa? Au hao bodaboda mnaowawekea mafuta na kuwajaza barabarani ndiyo unafikiri watakaposikia risasi bado watabaki kulemazwa na kufa kwa ajili ya fisadi Lowasa na Genge lake ambaye atakuwa amejifungia Masaki aua hata kwenye vila lake Ulaya?
Usichangane mambo, kumbuka TanZania siyo Kenya na wala WatanZania siyo Wakenya, wakenya walipigana na kuuwana kwa sababu kila mtu alikuwa anatetea Kabila lake na alikuwa yuko tayari kufa kwa ajili ya kabila lake sasa Mmachinga wa Masasi awe tayari kufa kwa ajili Mbowe wa kutoka Hai au Mtei wa Tengeru au sijui Tundu Lisi wa Singida kwa lipi?

Kabla kuandika mambo kama hayo jifunze kwanza kidogo Historia ya Dunia labda utaelewa ni mambo gani huwafanya watu wawe tayari kujitoa muhanga na kufa, hakuna Dunia hii aliyetayari kufa kwa ajili tu ya Mwanasiasa ambaye hana uhusiano naye wa karibu kama kikanda, kidini au kidamu!

Kwa kifupi nakuhakikishia hakuna Mtz atakayakaidi agizo la Raisi JMTZ kwa maana hakuna aliyetayari kuumia kwa ajili ya fisadi Lowasa, Mbowe, Tundu Lisu &Co.!

"Amani haipatikani ila kwa......."
 
Guyz mi naona ukibishana na mwanaccm muda mfupi ujao unakuwa naww hamnazo mana hawa jamaa walioweng hawatumii vichwa kbs kufikiria

Nakuonea huruma sana siku Magufuli anapoapishwa naona utajinyonga
 
Zimbabwe kulitokea nini? Unafahamu ugomvi wa Zimbabwe wewe? Kama haufahamu nitakusaidia, Zim kuna makundi mawili Washona na Wandebele, Mugabe ni Mshona na wapinzani akina Tsvangirai ni Ndebele na hawa wana ugomvi wa muda mrefu na ndio maana Zim wameshindwa kumtoa Mugabe kwa kura kwa maana washona ni wengi klk Wandebele na hakuna Mshona anayempigia kura Mndebere Tsangirai na hakuna Mndebele anayempingia kura Mugabe hivyo basi Wandebele wako tayari kufa au kuumizwa kwa kuwa wanatetea Kundi lao, ni rahisi kihivyo tu!

Hivyo hayo mnayoyategemea hapa TanZania hayawezi kutokea, boda boda mtawapa hela wataandamana lkn mmoja akipigwa risasi wote watatawanyika kurudi nyumbani kwani hakuna kinacho waunganisha na fisadi Lowasa isipokuwa fedha na Mafuta ya bure sasa hiyo haitoshi kumfanya binadamu ajitoe mhanga!

Tuna imani hata jeikei atampigia kura Lowassa kwa sababu hata yeye anataka mabadiliko. Na wewe toroka uje.
 
Tuna imani hata jeikei atampigia kura Lowassa kwa sababu hata yeye anataka mabadiliko. Na wewe toroka uje.
Hata kama JK,Magufuli,Bilal,Mkapa,Mwinyi na wanaCCM Wote wakiamua kumpigia KURA FISADI Lowassa.FISADI LOWASSA Hawezi kuwa RAIS WA NCHI Hii.Beautiful Tanzania Is Not For Sale
 
Police wenyewe wako sijui 42000 kulinda tu vituo vya kura hawatoshi ,kama umedhamiria kutumia Jeshi la wananchi Wa Tanzania kupiga raia wao sawa ,vile vile na viongozi Wa taifa hili wajiandae kabisa na consequences zitakazo jitokeza na uharibifu Wa Amani hautakwepeka ,unless other wise they have made a choice they can live with
 
Ujumbe wako una pointi ya msingi kuwa Rais amesema tukimaliza kura ni vema tukarudi majumbani. Kama mkuu wa nchi anawajibika kulinda amani ya nchi na aiyache salama kama alivyokabidhiwa salama. ni busara ya hali ya juu sana.

Tatizo ilivyowekwa au kusomwa kwenye hotuba ya Mkuu ni haikunyooka ndiyo maana inaleta shida. NEC wafafanue sheria ili watu waelewe tufuate kipi? Maana huyo Mbowe ananukuu sheria ya NEC hiyo hiyo kuwaambia wananchi. Hili swala liwekwe sawa tunataka amani ya nchi jamani.

Pia, kasoro niliona ni kufafanua hili swala kwa kuponda majina ya watu sijui Lissu, Mbowe, Mtei, Lowassa... sisi hayo hayatuhusu. tupate kauli tuende nyumbani au tubaki kituoni kutangaziwa matokeo. mimi binafsi ni wagombea wangu vya vyama tofauti nitawapa si wote watapata kura yangu. Diwani, mbunge na rais hao nitagawa kura.

Sasa hiki kituo kilichopo mita 20 kutoka nyumbani kwangu watanizuia kukaa nje? Mimi na familia yangu tuko watu 20 na wakati wa jioni huwa tunakaa nje, je huu utahesabiwa kama mkusanyiko usio rasmi? Wasituzingue hawa mbwai wakubwa!!
 
Hata kama JK,Magufuli,Bilal,Mkapa,Mwinyi na wanaCCM Wote wakiamua kumpigia KURA FISADI Lowassa.FISADI LOWASSA Hawezi kuwa RAIS WA NCHI Hii.Beautiful Tanzania Is Not For Sale

Hujui nguvu ya umma wewe!!
Nilifikiri anaingia kwa mtutu wa bunduki kumbe ni kura .
Akishinda hakuna wa kumzuia. Ni demokrasia.
Marais waote waliboronga labda useme mengine lakini kwa kuuza nchi iloshauzwa kama kule Loliondo na Mtwara.

Nyie CCM mmeiba sana kaeni pembeni watanzania wengine nao wale tu kama mlivyokula nyie .
Watanzania wote tungekua na roho mbaya kama walivyo wanaCCM nchi hii ingekua kama Somalia.
 
Nina uhakika wewe hauishi TanZania na ndiyo maana umeandika utumbo ulioandika, eti uko tayari kufa, unafikiri kuna Mtz ambaye yuko tayari kufa kwa ajili ya fisadi Lowasa? Au hao bodaboda mnaowawekea mafuta na kuwajaza barabarani ndiyo unafikiri watakaposikia risasi bado watabaki kulemazwa na kufa kwa ajili ya fisadi Lowasa na Genge lake ambaye atakuwa amejifungia Masaki aua hata kwenye vila lake Ulaya?
Usichangane mambo, kumbuka TanZania siyo Kenya na wala WatanZania siyo Wakenya, wakenya walipigana na kuuwana kwa sababu kila mtu alikuwa anatetea Kabila lake na alikuwa yuko tayari kufa kwa ajili ya kabila lake sasa Mmachinga wa Masasi awe tayari kufa kwa ajili Mbowe wa kutoka Hai au Mtei wa Tengeru au sijui Tundu Lisi wa Singida kwa lipi?

Kabla kuandika mambo kama hayo jifunze kwanza kidogo Historia ya Dunia labda utaelewa ni mambo gani huwafanya watu wawe tayari kujitoa muhanga na kufa, hakuna Dunia hii aliyetayari kufa kwa ajili tu ya Mwanasiasa ambaye hana uhusiano naye wa karibu kama kikanda, kidini au kidamu!

Kwa kifupi nakuhakikishia hakuna Mtz atakayakaidi agizo la Raisi JMTZ kwa maana hakuna aliyetayari kuumia kwa ajili ya fisadi Lowasa, Mbowe, Tundu Lisu &Co.!

Na lingeni watanzania wajiulize kwanza hasa kwa hao wanaodhamiria kumwaga damu au kufanya fujo kwa ajili ya kiongozi, Je wanauhakika gani wa huyo kiongozi wao kama atafanikiwa kua raisi atawapa maisha mazuri au naye yeye atakularushwa na ufisadi kama viongozi wengine waliopita?
Watanzania tutumieni akili, Tumchague tunayemtaka lakini tukumbuke Mwafrika ni mwafrika tu, katika nchi za afrika kuna nchi gani waliofanikiwa kuondoa ufisadi?? Kila kiongozi anae pata nafasi nae anakua fisadi na kusahau, na wala sikusahau ni kudharau ahadi alizotoa.
Tupigeni kura kwa amani, ndio heshima pekee tuliokua nao hapa Tanzania, AMANI. Kama ni kuondoa ufisadi ni kitu kigumu sana,
 
Naomba ujumbe huu umfikie mh Jakaya Mrisho Kikwete, Amiri jeshi mkuu wa jamhuri ya muungano Tanzania, Rais aliyebakiwa na siku chache, masaa machache kuiacha Ikulu. Swala la kuiacha ikulu ni swala la kikatiba, tena lipo wazi hakuna wa kulipinga.

Nimefuatilia hotuba ya Rais J. K, kwa makini sana, hasa kwenye kipengele kile cha uchaguzi. Ametumia hasira, ameongea kwa ghadhabu na vitisho vingi kwa watu wa upinzani.

Nikajiuliza sana juu ya kauli zake.
Kwanza nilijihoji mwenyewe kwamba haya maazimisho ni ya chama cha mapinduzi CCM au ni maazimisho ya kilele cha Mwenge au ni maazimisho ya kifo cha mwasisi wa Taifa Letu Mwl. J. K. Nyerere? Maswali haya yalinijia baada ya kuona Mh J. KIKWETE ameuvaa U CCM na sio Urais.

Najua sina uwezo wa kumfikia moja kwa moja Mkuu wa nchi, ila ujumbe wangu utamfikia moja kwa moja au kupitia kwa wapambe wake.

Mh Rais naomba utambue mambo mawili matatu toka kwetu sisi tulio malofa na wapumbavu.Na kwa nia njema kabisa naomba ujue kuwa

1.Hatutaogopa kupigwa mabomu, kufungwa, kuuwawa au lolote kwa kutafuta haki yetu ya msingi. Tunaamin kuwa kifo ni siku moja tu wala sio mara mbili.

2.Tutapiga kura zetu na kuzilinda kwa mjibu wa sheria, taratibu na kanuni za uchaguzi wala si vinginevyo.
Hakuna wakututisha hata kidogo ndani ya nchi yetu ambayo tunaamini ni ya kidemokrasia.

3.Tutahakikisha mgombea tunayemhitaji anashinda kwa kumpigia kura nyingi za kutosha na kuhakikisha hakuna atakayeiba kura zetu, najua mwalijua hilo.

5.Kwa umoja wetu tutashirikiana na vyombo vyote kulinda amani ya nchi yetu Tanzania.

5.Tutatoa ushirikiano kwa yeyote anayependa haki itendeke, na tutamdhibiti atakayejaribu kupoka haki yetu.
Ikumbukwe mita 100 sio mbali sana ni sawa na usawa wa gori moja hadi gori jingine katika uwanja wa mpira.

Rais Kikwete kitendo cha kututishia kuwa tutakaolinda kura tutadhibitiwa na umeyaongea maneno haya kwa hasira kuu, unatudhihirishia wazi kuwa Chama chako cha CCM kimejipanga kuiba kura au kufanya kinyume na taratibu za uchaguzi .

Kama mlipanga mbinu chafu mkadhani tutaogopa basi imekula kwenu, tunatambua wazi kuwa, kuna magari mengi ya washawasha, askari wengi, vitendea kazi vya kisasa lakini sisi tunasema hatutaogopa vifaa hivyo kwakuwa sisi sio watu wa fujo ni watu wa haki.

Mwisho napenda Mh J. KIKWETE atambue kuwa yeye kaongoza kwa miaka yake 10 na anakwenda kupumzika, hivyo aende akapumzike kwa amani kabisa, ajiepushe na matamko yatakayokuja kumpeleka ICC wakati hakustahili kwenda huko hata kidogo, na Tr 25/10/2015 akapige kura alipojiandikishia amchague anayempenda yeye, awe diwani, Mbunge au Rais

Japo kwa Heshima na Taadhima namuomba kura yake upande wa Rais ampigie Mh Edward Lowassa, na naamini atampigia kura.

Naomba nimalize kwa kusema WATANZANIA wote tujitokeze Tr 25/10/2015 tukawapigie kura viongozi tunaoona wanafaaa,binafsi nawaomba kura za Mh. EDWARD LOWASSA na naamini tutampigia kura za kutosha na tutazilinda kwa amani bila vurugu yoyote ile. Tudumishe amani na upendo.
Ahsante

Mkuu hii mada yako nzuri sana...imekaa kisomi,kizalendo kiuanaharakati kabisa. Swali la msingi ni moja tu kuwa KWANINI RAIS AONGEE KWA HASIRA NA KUPANIC?
 
Nina uhakika wewe hauishi TanZania na ndiyo maana umeandika utumbo ulioandika, eti uko tayari kufa, unafikiri kuna Mtz ambaye yuko tayari kufa kwa ajili ya fisadi Lowasa? Au hao bodaboda mnaowawekea mafuta na kuwajaza barabarani ndiyo unafikiri watakaposikia risasi bado watabaki kulemazwa na kufa kwa ajili ya fisadi Lowasa na Genge lake ambaye atakuwa amejifungia Masaki aua hata kwenye vila lake Ulaya?
Usichangane mambo, kumbuka TanZania siyo Kenya na wala WatanZania siyo Wakenya, wakenya walipigana na kuuwana kwa sababu kila mtu alikuwa anatetea Kabila lake na alikuwa yuko tayari kufa kwa ajili ya kabila lake sasa Mmachinga wa Masasi awe tayari kufa kwa ajili Mbowe wa kutoka Hai au Mtei wa Tengeru au sijui Tundu Lisi wa Singida kwa lipi?

Kabla kuandika mambo kama hayo jifunze kwanza kidogo Historia ya Dunia labda utaelewa ni mambo gani huwafanya watu wawe tayari kujitoa muhanga na kufa, hakuna Dunia hii aliyetayari kufa kwa ajili tu ya Mwanasiasa ambaye hana uhusiano naye wa karibu kama kikanda, kidini au kidamu!

Kwa kifupi nakuhakikishia hakuna Mtz atakayakaidi agizo la Raisi JMTZ kwa maana hakuna aliyetayari kuumia kwa ajili ya fisadi Lowasa, Mbowe, Tundu Lisu &Co.!

Kanye ulale .
 
Back
Top Bottom