Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,502
- 911,255
Wachumba wengi hili hawataki kusikia
Lakini ukweli lazima tuuanike hadharani
Dunia yenu siyo ila ya enzi zetu kabisa
Utetezi wenu kuwa mbona hatukupimwa
Siyo utetezi kabisa, hiyo siyo busara lol!
Harusi bila kupimwa vvu, ni majuto ya mjukuu!
Harusi nimehudhuria nyingi mno, ama!
Kila harusi siku hizi minong'ono haiishi!
Eti mbona kapigwa, hivi naye vipi haoni?
Eti mbona dalili zote anazo, lakini kicheko!
Jibu hapo ni kupimwa ili ujiondolee shaka,

Miaka michache tu baada ya nderemo
Utasikia eti anatupa mimba kila kukicha
Khofu hutanda kwa wanafamilia, kulikoni!
Lawama huanza kuzagaa kila mahala!
Vikohozi visivyo na tiba kuwagubika!

Wanandugu hudai warithi wao wa kesho
Lakini hapa kitanda hata haramu hakizai!
Kisa ni mgeni kashamiri ndani ya miili yao.
Kila mmoja humtupia lawama mwenzio
Endapo wangelipima kabla ya shari hii..

Kupima siyo kutokuaminiana ila ni kukiri
Kwa kutambua dunia tuliyopo siyo mchezo
Changamoto zake nazo siyo masihara kamwe
Msipopima kila mmoja rukhsa kulaumu mwenzie
Mchafuzi naye kupewa ahueni bila ya shubiri

NB.:- In the memory of a passionate friend who noisily passed away last week......leaving the loser to enjoy it all..............how sad as it lasts!