Harmonize: Nilipewa Mkataba wa kuonewa na WCB na nilisingiziwa kumroga Diamond Platnumz

Mambo yanakwenda kasi sana, joto linazidi kukimbiza huku jua likichoma kishenzi. Wakati tukifikiria ni kwa namna gani tunaweza kusurvive huku maji na umeme vikiwa shida, wasanii nao wanaibuka na mambo yao, yaani ni shida juu ya shida.

Haya! Wengi mmeniambia nije na makala kuhusu jambo hilo, basi niseme ninakuja na hii makala, ila kabla ya kuendelea, weka uteam pembeni kwanza, tuzungumzie mambo halisi.

Mimi sina timu, huwa ninazungumza kitu ambacho ni cha kweli, kile kilichokuwa kwenye mtazamo wangu, kubwa zaidi, huwa si mpenzi wa miziki ya Bongo fleva, hata simu yangu, huwezi kukuta ngoma za hapa Bongo.

Lakini kwenye yote, acha nijaribu kuelezea kile nilichokiona tangu siku ya kwanza Harmonize anapoondoka WCB mpaka leo, nitajaribu kufafanua ninayoyaona, kama una yako, basi na wewe kaandae makala tuje kusoma.

MKATABA WA 40%
Nianze na suala la mkataba. Kwanza kitu cha kwanza tujue unapokuwa huna pesa, una maisha magumu, ukiletewa mkataba wowote ule ambao unaonyesha utakuwa unaingiza pesa ni lazima utausaini kwa sababu usipousaini, inamaanisha unakubaliana na maisha ya dhiki unayoishi.

Leo nikisema ninahitaji waigizaji kwenye filamu yangu, halafu nikisema bwana mimi sina hela ya kumlipa msanii, ila ukifanya kazi na mimi, utapata jina na kuitwa kwenye muvi za watu wengine, utaacha nafasi hiyo kwa sababu hutolipwa? Je, utaendelea kukaa kwenye maisha hayo na kuachana na opportunity ambayo itakufanya kujulikana?

Kwenye hili! Kwanza tusimlaumu Harmonize kwamba kwa nini amesaini mkataba wa kulipwa asilimia 40 kwa sababu naamini hata ungekuwa wewe, kwa maisha ya dhiki, halafu unajua nikifanya kazi na Mondi, nitajulikana na kutengeneza pesa, kwa nini usikubali?

Kampuni nyingi za Tanzania zina mikataba mibovu na tunaiingia kwa sababu tuna shida ya pesa, tupo kwenye maisha ya kimasikini sana, unakubali kusaini mikataba mibovu kwa sababu unataka pesa, ama umaarufu ili baadaye utusue.

Unapoingia kwenye mikataba hiyo, unaona kabisa unanyonywa, ila huna ujanja, kuna kitu unakitafuta lakini moyo wako unasema siku moja nitaondoka tu, nikishapata pesa za kutosha nasepa.

Hilo ndilo wamekuwa wakilisema hata wajasiriamali, unapotaka kuanzisha biashara yako, kwanza anza kuajiriwa, upate pesa kisha ondoka ukaanzishe biashara yako, ndivyo ilivyokuwa kwa Harmonize.

Asingeweza kukaa WCB milele, ilikuwa ni lazima siku moja aondoke. Ukishapata pesa na umaarufu uliokuwa unautaka, sasa unasema huu ndiyo muda wa kuondoka, unaondoka zako, kuna watu wengi wamefanya hivyo, yeye si wa kwanza.

Kosa kubwa wanalofanya WCB ni aina ya mikataba wanayoingia na wasanii, msanii akiondoka, akilipia pesa, imekula kwao ila si kama lebo nyingi za Marekani.

Leo hii Drake, Nicki Minaj hawapo Young Money, ila kwenye kila pesa wanayotengeneza huko walipo, kuna asilimia inaingia kwenye lebo hiyo na maisha yanasonga.

Suala la Harmonize kuingia mkataba wa aina hiyo, simlaumu kwa sababu hata wewe unayesoma hapa, huko kazini kwako umeingia mkataba wa aina hii hii, hujilaumu wewe, unamlaumu Harmonize.

Kijana wa Kitanzania anapotaka kutafuta jina ama pesa, anakuwa tayari kufanya jambo lolote lile. Nilipokea meseji nyingi tu, mtu anakwambia “Bro! Natamani kuigiza, nitaigiza hata bure.”

Unajua anamaanisha nini? Anachohitaji ni kutafuta jina, anaamini hapo baadaye atakuja kuwa na jina na atapiga pesa tu kwani akihitaji pesa sasa hivi, anaweza asizipate na ukawa mwisho wa ndoto zake.

Sasa mtu huyu akikubali kuigiza bure ama kwa malipo madogo, siku akipata jina na kutaka kuondoka, cha kwanza tutatakiwa kupitia mkataba wake, tufanye tulichokubaliana na tuache aondoke.

Maisha popote pale.

HARMONIZE VIJEMBE KWA MONDI
Harmonize aliondoka WCB na kilichofuata ni kutoa vijembe na matatizo yaliyokuwepo hapo. Kuna wengi walisema kwa nini asingesema akiwa hapo? Kama wewe unajiuliza swali hilo, jishike kifuani na sema mimi ni mjinga sana.

Kuna wachezaji wengi wa mpira wakiwa timu fulani, hawazungumzi mbovu, ila wakiondoka ndipo utasikia ile timu mbaya sana, kocha magumashi na mengine mengi.

Ukiwa kwenye nyumba mbaya, husemi kwa watu kwamba ni mbaya, utataka uondoke halafu ndiyo useme ilikuwa nyumba mbaya.

Leo umeoa, huwaambii watu kama mkeo ni malaya, unasubiri umuache ndiyo uanze kusema yule mwanamke alikuwa malaya, halafu hajui kupika, kikojozi na kitandani gogo. Kwa nini usiseme wakati akiwa ndani?

Madhaifu ya sehemu tunayasema tukishaondoka sehemu hiyo.

Suala la Harminize kumpiga vijembe Mondi ni kawaida kila kona. Bado ana hasira, labda kwa yale aliyowahi kutendewa ambayo aliona hayafai, taswira ikimjia, anakuwa na hasira na kujikuta ameropoka hili na lile.

Mtu akiondoka sehemu kwa vita, atahitaji kukaa muda mrefu mpaka akili yake kuja kukaa sawa.

HARMONIZE AMEKOSEA?
Jibu ni ndiyo! Wakati mwingine unapoondoka sehemu, achana na kila kitu, nenda kafanye mambo yako, achana na yaliyopita. Harmonize alishindwa kufanya mambo yake.

Alimkalia Diamond kooni, akaikalia WCB kooni, akawa anatoa vijembe kutwa. Nikahisi labda naye Diamond kwa kuwa amekuwa mkongwe angekaa kimya, ila cha ajabu naye akaanza kumrushia vijembe hasa kwenye nyimbo ambazo alishirikishwa, nikajua wote bado ni watoto ama kila mtu hataki kuonekana mpole kwa mwenzake.

MONDI AMEKOSEA?
Kuna msemo wa Kitanzania unasema ukigombana na mtu mmoja halafu ukasema ana matatizo, basi tunaweza kuamini kwamba kweli ana matatizo, ila ukigombana na watu watano, tutashindwa kukuelewa ukisema wana matatizo, tutakwambia kwamba wewe ndiye una matatizo.

Leo ukiniambia Mondi ana matatizo, nitakataa hilo, yeye hana matatizo bali watu waliomzunguka ndiyo wana matatizo. Namfahamu msela, nimekua naye mtaa mmoja, tangu kishuleshule mpaka alipoanza muziki japo sisi wengine tulikuwa bize na shule.

Jamaa ana uswahili kama sisi ila kuhusu roho mbaya, kwa mchizi hilo nakataa kwa kuwa tabia ni kama ngozi, huwa haijifichi, ningeliona hilo tangu kipindi kile alipokuwa akitoroka shule na kwenda kuimbaimba kila alipoona muziki ama kutafuta hela kwa kuuza nguo kwa kudandia Tandale sokoni.

Unapokuwa unakutana na watu ambao wanaweza kuibadilisha akili yako na kukupa nyingine kabisa. Ukiwapa nafasi, wanachukua maamuzi yao mabovu na kuwa yako, na wanafanya lolote lile ambalo mwisho wa siku litaonyesha taswira mbaya juu yako.

Kama ulifuatilia mwanzoni, vijembe vingi vya Harmonize havikuwa kwa Mondi moja kwa moja, alijua kabisa mchizi alikuwa mtu poa ila kuna mtu ambaye hakuwa poa, na ndiye aliyekuwa akimpiga vita sana.

Na ninadhani baada ya kuonekana hajibu kitu, ni kama akashinikizwa kujibu, naye ndipo alipoanza kujibu.

Kosa la Diamond ni kuanza kujibizana na Harmonize. Angekaa kimya tu, mtu umekwishamtoa, umemfanya kujulikana kupitia wewe, ana kitu gani cha kujimwambafai kwako? Wewe nyamaza tu, dunia itaendelea kujua kwamba bila wewe, yeye asingekuwepo hapo alipokuwa.

Kumjibu Harmonize ni jambo baya sana ambalo Diamond amelifanya, alitakiwa kuwa kimya tu, aendelee kufanya mishe zake kama kawaida kwa sababu siku zote huwezi kumfananisha yeye na Harmonize, bado ni kijana mdogo sana kwenye mafanikio ya muziki.

Kinyago umekichonga mwenyewe, kinakutishaje? Unakiogopea nini? Kama ningekuwa Mondi, nisingemjibu Harmonize ama kumpa kijembe kwenye wimbo wowote ule, ningewakataza Juma Lokole na Baba Levo kumuongelea Harmonize, yaani ningeachana naye mazima. Kumuongelea na kumtupia vijembe inaonyesha kabisa naye Mondi anatamani kusikika mitandaoni akibishana na Harmonize ambaye kiukweli ni mdogo mno kwake.

NI KWELI HARMONIZE AMEBADILIKA?
Bado najiuliza swali hilo. Nakumbuka kipindi cha nyuma wakati akiwa WCB, wakati huo nikiwa mwandishi wa habari. Hakuna kitu ambacho Harmonize anakikataa kama kumuona mtu akipiga picha na Diamond. Yaani alikuwa anakukazia ileile.

Harmonize alikuwa maana halisi ya mringaji, alijua kufanya kitu chochote kile usimfikie Diamond kwa lolote lile, hata ukiwa shabiki wake kwa namna gani, ila leo namuona si Harmonize yule, amekuwa mnyenyekevu, mpole na amekuwa na moyo wa kusaidia wengine, huwa ninajiuliza kutoka WCB kumembadilisha kuwa hivyo ama kule aliambiwa awe na maisha yale hata kuwabania watu kupiga picha na Mondi? Sijapata jibu.

KOVU LA HARMONIZE LITAMTESA MONDI MILELE
Harmonize alikuwa msanii wa Mondi, yaani yeye ndiye ambaye alimchukua yeye kama yeye, si kama hao wengine ambao ameletewa. Harmonize alikuwa kipenzi cha Mondi, aliaminiwa na kuonyeshwa chocho zote.

Kipindi kile Mondi alipokuwa akisafiri, alikuwa akiongozana na Harmonize kila kona, alimtambulisha kwa kila mtu, kwa kifupi alimwamini kwa kuwa alikuwa msanii wake, hakuletewa kama ilivyokuwa kwa hao wengine.

Ukiangalia kipindi hicho, Mondi alikuwa akisafiri sana na Harmonize kuliko hata Rayvanny, alijua kwamba huyu ni msanii wangu mimi, mrithi wangu, halafu ghafla tu, huyo mrithi akasepa zake. Kama ni kupigwa na kitu kizito kichwani, basi Harmonize amejua kumpiga nacho Mondi.

Suala la Harmonize litaendelea kumtesa, kama ni mzimu wake basi utaendelea kumtokea. Rich Mavoko ameondoka WCB lakini humsikii Mondi akimzungumzia, wengine watakuja na kuondoka, hatowazungumzia, ila kwa Harmonize, hatoweza kujishika hata kidogo.

Alitumia pesa na muda kwa ajili yake, alimwamini, akampa kila kitu ili dogo atusuea, kipindi kile akampa mpaka mademu wa kupiga nao skendo, mara katoka na Wolper, mara na huyu, yaani yote ilikuwa ni kumtengenezea jina dogo ili afuatiliwe, mwisho wa siku kilichotokea, kimemuumiza mno mno mno.

HIVI MMEMFIKIRIA RAYVANNY YUPO KWENYE HALI GANI?
Huyu amesahaulika. Jana baada ya kusikia mahojiano ya Harmonize na kuplay ile voice record, nikaanza kumfikiria Rayvanny yupo kwenye hali gani. Kuna jamaa mmoja mpenzi wa WCB aliweka video zikimuonyesha Rayvanny akiwa kwenye mahojiano kipindi cha nyuma akisema alihisi anarekodiwa na Harmonize, nikamuuliza jamaa maswali kadhaa.

Mtu ameondoka WCB kwa ugomvi mzito, leo anaongea na wewe, unajua kabisa unarekodiwa, je, ungeweza kumtemea shit bosi wako? Yaani mimi nimeondoka kwa ugomvi, halafu unaongea na mimi, unajua kabisa nakurekodi, je, ungeongea shit kwa bosi? Jibu ni hapana.

Rayvanny hakuwa akijua hilo ila baadaye akasanuka kwamba inawezekana yale mazungumzo yake na Harmonize yalikuwa yakirekodiwa, akaamua kujitetea mapema kabisa ili siku yatakapokuja kuwekwa hadharani basi tuseme jamaa alijua kama alikuwa akirekodiwa. Wakati mwingine inahitaji akili kubwa kucheza michezo ya kijanja.

CHUKI, HOFU VIMETAWALA BONGO
Kitu ambacho nakataa na nitaendelea kukataa ni pale mtu akiniambia kuna siku muziki wetu utasikika duniani kama ulivyo muziki wa Nigeria, hicho kitu sahau bro!

Sisi tumejaza chuki mioyoni mwetu, Watanzania hatupendani, unaweza kuzungumza na mtu vizuri, kumbe anakuchukia na hujui, anaziba baraka zako na hujui kabisa.

Wanamuziki wanachukiana wao kwa wao, mbaya zaidi kwa sasa wapo kimakundi, yaani kuna Team Mondi, Team Harmonize na Team Kiba, kwa staili hiyo tutafika vipi huko mbele? Hatuwezi.

Leo tutawaona wasanii wakigombea tuzo, bila aibu, nampigia kura msanii wa nje na kumuacha wa ndani, hiki ni kitu ambacho Wanigeria hawakifanyi, wanapoamua kusapotiana, wanasapotiana kwa asilimia mia moja.

Leo Burna Boy anakwenda Marekani kuperform, anawachukua maunderground wake anapaa nao kwenda huko, anawatambulisha jukwaani na ngoma zao zinapigwa, na hata kuperform, wanatangazana tu baadate tunasema huyu Burna Boy na Mondi, Mondi mkongwe, ila leo ukiuliza nani mwanamuziki mkubwa, utasema Burna ni mkubwa mara kumi ya Mondi.

Hatuwezi kufika mbele bila kusapotiana. Kwa kitendo cha Mondi kwenda Marekani bila kuwa na msanii yeyote yule ni kosa, analeta ubinafsi lakini simlaumu sana kwa kuwa yamekwishamtokea puani kwa Harmonize, alimuonyesha njia mwisho wa siku akaachwa kwenye mataa, wakati mwingine bora uonekane mbinafsi kuliko mjinga.

Kwa maelezo ya Harmo kipindi cha nyuma alisema kwamba ukienda Nigeria, ni vigumu sana kusikia klabu wakipiga ngoma za Tanzania, ila cha ajabu, sisi tunaongoza kupiga ngoma zao.

Niwaambie tu, ili muziki wetu ufike mbali, tusubiri hizi zama za Mondi, Kiba na Harmonize zipite, waje wengine wenye kiu ya kuwainua wengine kimataifa, kidogo tutaweza kusogea.

JPM ALIWEKEWA WAKATI MGUMU
Hayati JPM alikuwa kwenye wakati mgumu sana. Mondi na Harmonize walikuwa vijana wake, aliwapenda na kuwapamba wote wawili, mwisho wa siku akapokea simu kutoka kwa Harmonize na kuombwa msaada wa kitu ambacho Mondi hakuwa akikitaka bila shaka.

Kama mzazi, lazima utakuwa na wakati mgumu, hapo ni lazima umfurahishe mmoja na kumliza mmoja, ila alichokiangalia na kukifanya, ni hekima kama mtu mzima, simu yake moja kwa Waziri Mwakyembe ikamuweka Harmonize huru. Pongezi sana kwake kwa hekima zake.

Kuna kila sababu ya Harmonize kulia sana msibani mpaka kuchora tattoo ya Hayati JPM. Alimfanyia mambo mazuri likiwemo hilo, na kwa kile alichomfanyia, tattoo hiyo haitakiwi kufutwa mwilini mwake mpaka kifo chake. Bila yeye, inawezekana asingekuwa huru mpaka leo.

NB: Kweli Konde Jeshi, yaani amekaa na haya yote kwa miaka mitatu na wakati Manara alishindwa kukaa nayo hata kwa wiki moja tu.
Basi sema unakuja saa ngapi ama kwenu umeshakatazwa
Said kichwa nitamueka wapi na mkongo nimeshampakaza
Iyo mitungi ndo usiseme utakunywa utasaza
Kama pesa ndo zipo nyingi kuzigawa nimeshaanza

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Naomba kuweka wazi kabisa kwamba mimi si mpenzi wa Muziki wa Tanzania na wala siwapendi wanamuziki wa Tanzania , hii ni kwa vile wamekuwa mara zote wakitumika na ccm kuwapotosha wananchi , na hasa hawa wanaoitwa Wanamuziki wa kizazi kipya , ambao pia wanatuhumiwa kusafirisha na kusambaza madawa ya kulevya hivyo kuharibu nguvu kazi ya Taifa.

Bali nimesononeshwa sana na yaliyojitokeza kwenye mgogoro wa Harmonize na Diamond , pale huyo Harmonize alipokuwa anaomba kujitoa kwenye lebo ya WASAFI , mengi sana ameongea mwenyewe kila mtu kayasikia wala sina haja ya kuyarudia , bali nitagusia kidogo maeneo mawili tu.

Kwamba Diamond alimwambia Harmonize kwamba anaweza asimkamilishie kile anachotaka na wala hatomfanya chochote na kokote atakakoenda hatofanikiwa , kwa vile HAMUWEZI KISERIKALI , KIFEDHA NA KIUCHAWI , hii ni kauli ya kijinga sana kutolewa na anayeitwa msanii mkubwa , ni kauli ya kishamba sana iliyojaa Utanzania mtupu!

Jambo lingine linalotia aibu ni kitendo cha Harmonize Kuomba msaada kwa Magufuli moja kwa moja baada ya ngazi za chini ikiwemo wizara kumgwaya Diamond , Yaani Rais wa nchi ampigie simu Msela Diamond na kumbembeleza ili akubali kuterminate mkataba wa Harmonize na Wasafi ! hili ni jambo la kutia aibu sana , Yaani inawezekanaje Wizara na BASATA kutiwa mfukoni na msanii mmoja?

Haya mambo yakiachwa iko siku yatakuja kufedhesha mamlaka ya Rais , na sisi kama wananchi hatutakubali.
Leo nakuto... totoo, nakutoa kwenu uje kwangu
Nina hamu yakuto... totoo, kutoa mahali uwe wangu (nyau)

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Tueleweshane.

Harmonize alimpigia simu Rais ili amsaidie katika kuuvunja mkataba?

Huo mkataba haukua na get out clause?

alimpia ili amuamuru diamond akabidhi nyaraka za watu,ambazo si mali yake tena.
 
Nyimbo mbili kwa mwaka na unajigaramia vitu vingine...so na wewe ukaamini aliyosema mmakonde ni ya kweli?

Yaani mtu aliyekuja label hana kitu.....aliwezaje kujigharamia mambo mengine...?

kwamba alisema uongo sababu aliingia akiwa hana hata kitu!!!

kwahiyo hizo 60% zilikuwa zinakatatwa kwenye kaptura ama!!!!
 
1.Pesa ya kuvunja mkataba ilitolewa na sayona CRDB bank na jembe ni jembe sio kama tulivyoaminishwa kuwa sarah alihusika.

2.Diamondi ni mtu mwenye roho mbaya sana rejea kauli za ommy dimpoz, belle 9, shettah rich mavoko.

3.Rayvanny anavumilia kuwa wasafi hajui pa kuanzia kutoka tena kwa yeye wanaweza sema atoe bilion 1.

4.Bila amri ya Magufuli Diamond asingesaini kuvunja mkataba kwa wakati.

5.Harmonize mwaka wa 3 anaendelea kuwepo kwa game nje ya wasafi.

6.Kuna watu huwa wanalazimishwa kumsifia na kumpost Diamond kila kukicha ama akiwa na jambo mfano jana amepostiwa na mama yake uncle shamte baba levo page ya wasafi.

7.Nyimbo zote nzuri za WCM Mondi alikuwa analazimisha aweke mistari yake ili ikitoka ionekane yeye ndio ameibeba nyimbo wakati kiukweli sio sahihi alikuwa hataki kupotea masikioni kwa watu.

8.Uchawi ni sehemu ya maisha ya Diamond.

9.Mameneja na ndugu wa Diamond walichangia ugomvi kuwa mkubwa sana.

10. Mali tunazoaminishwa za Diamond zingine hazina ukweli.
11. Diamond anataka awe mwanamuziki yeye yu TZ

12.Diamond hawezi ushindani
 
Idara Ya auandishi wa Habari Ni Janga lingine kubwa katika Nchi hii....Yaani Mwandishi anauliza Ukiwa Unaandika huwa unafikiria nini....Jamani yaani hilo swali lina mana gani?? Nyie mnaojiita waandishi siku hizi jaribuni Kusoma vitabu..Jaribuni kuwaasikiliza akina Tido Mhando kidogo mpate mwanga..Mko shallow sana sana na mnatia aibu.

Kingine Wewe Harmonize Ongea tu kiswahili unaeleweka....Achana na Kiswanglish cha nini??
 
kwamba alisema uongo sababu aliingia akiwa hana hata kitu!!!

kwahiyo hizo 60% zilikuwa zinakatatwa kwenye kaptura ama!!!!
Mbona suala rahisi hilo mkuu....aliingia akiwa broke. Label ikaweka mzigo...ndipo makato yakaanza pale alipoanza kuingiza income.

Kumbuka kabla hajaanza kukatwa hiyo 60% kuna muda ulipita ambao alirekodi nyimbo na videos kadhaa kwa gharama za label. Kafanyiwa promotions na other costs kwa gharama za label.
Kwa kipindi hiki cha mpito kabla return of investment haijaanza kuonekana...hakuweza kujigharamia. Aliitegemea label kwa kila kitu.

Kwa hiyo hiyo statement kuwa alikuwa akijitegemea kwa nauli na chochote haiwezekani kuwa ya kweli kwa kipindi hicho ambacho label ilikuwa imewekeza milions na bado aikuwa hajaamza kuingiza chochote.
 
Watu Naona Wanachanganya VITU HUMU

Suala la Harmonize Wekeni Utimu Pembeni Halafu Tujadiribkwa Facts.

1. Watu wanalinganisha Diamond Na Clouds. Ieleweke kuwa Diamond Hajawahi Kuwa signed na Clouds Media Group as Company kama Msanii wao. Na wala Clouds Media Group Haihusiani na Kuwasimamia Wasanii. Clouds Media Group ni Compny inayojihusisha na MEDIA + ENTEGNTEIMENT INDUSTRY Basi Haimsimamii msanii. So ukiitwa na Clouds Media Group Twende Kwenye Show, Ni Suala La Makubariano malipo yenu yatakuwaje yaani kwa kifupi unakuwa Day Worker, ukimaliza kazi yako unachukua mpunga Unasepa. Kwa hiyo Diamond Alichokuwa anapishana na Clouds Media Group, ni kumdharau na kutaka kumchukulia poa na kumtumia kwenye Show watakavyo. Diamond Akaweka Standards Kwake na Kwa Wasanii wake Kuwa Mimi Ili nifanye Show Malipo yasiwe chini ya Millioni 11, Ukimtaka Harmonize Malipo Labda yasiwe chini ya Millioni 8 na wengine. So clouds Media Group kwa Wakati huo ndio Media iliyokuwa na Nguvu hivyo wasanii hizi show walikuwa wanakubali kwasababu hakuna mbadala, walivyo ona Diamond Anavimba ndio wakaingia kwenye Ugomvi. So ni Vitu viwili tofauti kabisa.

2. Watu wanaona Kwa Msanii Million 600 ni Nyingi. Lakini Kwa Level Aliyokuwa Amefikia Harmonize Kwa Tanzania Kwa Wakati ule yuko Wasafii Millioni 600 ni hela Ndogo Sana. Kwanini Ni Hela Ndogo. Tuchukue kila Video Aliyoitengeneza Harmonize imegharimu Tsh Ngapi? Kuanzia Aiyola Just Roughly Gharama Za Shooting, kwenda South Africa na Sehemu zingine na Vitu Vyote. Chukua Kila Video Imegharimu Millioni 80 kwa Nyimbo 6 ni Tsh 480M. Production ya Hizo Nyimbo? Utajikuta kwa nyimbo 6 unafikia Millioni 600, Akiwa Chini Ya WCB katoa Video Ngapi na Audio Ngapi? Na kwa Wakati ule Bila Kwenda SA huja Shoot Video. Kumbrand Harmonize Imegharimu Kiasi Gani? Wasanii wangapi Wazuri Tanzania Zaidi Ya Diamond Na Alikiba Wameshindwa Kujibrand? Utaelewa pia Kumbrand Mtu ni Gharama ni pesa Nyingi, na Kwa Wakati huo Kituo Kikubwa Cha Media Kimegoma Kucheza Nyimbo za Harmonize Unatumia Gharama kubwa kiasi Gani Kumbrand Harmonize ili Nyimbo zake Zichezwe Trace, MTV na Nchi Zingine bila Msaada Wa Kituo Cha Radio? Ukijiuliza hayo maswali Utaona Ni Gharama kubwa kiasi gani Ilitumika Kulinganisha Na Millioni 600.

3. By the Time Diamond Anamchukua Harmonize Diamond Alishakua Star, alikuwa akikupost Kuwa Wewe unajua Kuimba Au akapost wimbo Wako basi Utaenda Viral, Na Diamond Alikuwa Na Management, Chukua Diamond Alikuwa Akishirikishwa kwenye Wimbo Analipwa Sh Ngapi? Tuchukue hela ndogo 20M, Harmonize Kafanya Collabo Ngapi na Diamond For FREE ili Dogo Aendee? Na Zote Zilikuwa Moto? Chukua hiyo Gharama the Muone Kama Kulikuwa na Faida na Hiyo 600M ilikuwa kubwa?, Harmonize Alitengeneza Social Media Accounts Ambazo ziliendelea kumlipa sana Kuanzia Youtube Accounts na Instagram amefaidika Vipi na hizo Accounts? Bado WCB walimuachia.

4. Watu Wanasema 600Millioni ni kubwa WCB kuchukua kwasababu walikuwa wanapata 60% kutoka Kwa Harmonize na Harmonize Anapata 40%, Twende Kwenye Jicho La Kampuni… Harmonize Akichukua 40% yeye Hakatwi kitu chochote kile yaani 40% yote Inaingia kwenye Account Yake kwasababu ni Msanii ambaye yupo chini ya Kampuni, Hivyo TRA haikuwa Inamtambua Harmonize ila Ilikuwa inaitambua WCB kupitia ile 60% ambayo Harmonize analalamika alikuwa Ananyonywa. Chukua WCB katika 60% walipe Kodi Halali ya Kitanzania ya ongezeko la Dhamani yaani VAT, katika 60% wanalipa 18% kwa TRA kama Kampuni Inabaki na 42%, Wakati huo Kampuni Ina Waajiriwa Wengie walio kuwa Wanahusika Na Kuhakikisha Show, au kila kitu nyuma Ya Harmonize Kinaenda Sawa na Wapo chini ya Kampuni, hivyo watahitaji mishahara kupitia hiyo 42% iliyobaki, zitahitajika Kumaintaine ofisi katika hiyo 42% na RUNNING COST zingine zote zitatoka kwenye Hiyo 42% unataka kusema katika 60%, PROFIT MARGINE YA WCB Ilikuwa kiasi Gani? Wenye Kampuni wanaelewa nini Nasema au Walio wahi kusimamia Kampuni… Kumbuka Muda Huo Harmonize Yeye Kachukua 40% yake Kaweka Mfukoni. Kama Ilikuwa Ni Show imeandaliwa na WCB As Compny Itagharamika Usafiri, Mavazi na Malazi Ya Msanii kwenye hiyohiyo 42% baada ya VAT Ambayo HARMONIZE ALIKUWA ANALALAMIKA ANANYONYWA. So hii ISSUE inahitaji Kuwa Knowledge ya Biashara Kuelewa COST PER UNIT + RUNNING COST Vs 40% ambayo bila makato inaenda Direct kwa Harmonize. SWALI JE 600M Ni Kubwa?

5. Tunafichwa na Mwamvuli wa Umaskini Kuamini 600M ni Kubwa Lakini Ukiangalia Walicho Spend na Faida Iliyo tengenezwa Utaona Kwa namna Gani Kumsimamia Msanii ni Gharama. Label Ngapi zimevunjika? Label Ngapi Zimeshindwa kuwasimamia Wasanii? Kuwa Na Kampuni ni Stress ndio Maana Kuna Muda Nikisikia Diamond Anatumia Madawa Ya kulevya, Naelewa Ni STRESS kiasi Gani Anapitia Kuhakikisha Kampuni Inaenda. Tunaona Matajiri Wakubwa Wakiingia kwenye matumizi ya pombe kupita kiasi na Bangi kwasababu Ya stress za Kumanage Kampuni.

6. Ukishakuwa Na MKATABA na Kitu Fulani, Tafsiri Yake ni Kuwa Mmetoa Masuala ya Mahusiano na Mmeweka MAANDISHI YAONGEE. Ndio Tafsiri ya Mikataba. Kuna Sheria Tanzania Ambayo Inasimamia MIKATABA YOTE TANZANIA, Hata Mkataba Ulio pewa wakati unaajiriwa unasimamiwa na Sheria ya Mikataba Tanzania. Kitendo cha Ku sign mkataba Kinatafsirika Kama Umesoma na Kuelewa kile kilichopo kwenye Mkataba na SHERIA YA MIKATABA TANZANIA, Inalazimisha Mkataba wowote ule Kusema/ Kutaja Ukomo/Muda wa Mkataba. Sasa Kama Harmonize Either kwa Kuelewa Au Kutokuelewa akawa Alisign Mkataba Labda wa Miaka 15 kuwa Chini ya WCB then Baada Ya Miaka 5 anataka kujiondoa, Sheria Mikataba iko Wazi, Utalipia Miaka 10 iliyobaki. Tuseme Harmonize alikuwa Amepigiwa na Kampuni kila Baada ya Mwaka Anaingiza Faida Ya TSH millioni 60, kavunja mkataba ukiwa bado una miaka 10 inamaana Anapaswa na Sheria Inamtaka alipe Millioni 600 kuweza kuvunja Mkataba Au Na zaidi! Na Mikataba huwa wazi Hutaka kwanza Kufanya Mutual Agreement au pande moja Ilipie Fidia. So Harmonize Angekuwa na Mwanasheria Mzuri, Angepitia Mkataba na Kumshauri kuwa Bwana una Mambo Mawili, 1 vumilia Mpaka mkataba utakapo kuna kuisha Au 2. LIPA PESA YA MIAKA 10 Vunja Mkataba. JE, ILE SIKU ANAHOJIWA KUNA MWANDISHI YEYOTE AU MTU YEYOTE ALISHA WAHI KUMUULIZA HARMONIZE ULISIGN MKATABA WA MIAKA MINGAPI? Kwa Lugha Rahisi Angalieni Uhamisho Wa Wachezaji Mpira Wa Miguu Unavyofanywa mtanielewa kwenye Hili. Hata Nyie kama Kuna Mtu kaajiriwa na Una Mkataba Sheria Inasema Ukiacha kazi Ndani ya masaa 24 unapaswa kumlipa mwajiri wako Mshahara wa Mwezi 1 UKIELEWA HIVYO UTAELEWA KUWA MKATABA JAPO HATUJAUONA ILA HAUKUWA WAKINYONYAJI.

7. MWISHO

JAMANI TUKUBALIANE UKIWA CHINI YA KAMPUNI UNABEBA IMAGE YA KAMPUNI, Hivyo Kitendo Cha HARMONIZE KUFANYA SHOW Sehemu Yoyote ile Bila Ruhusa Ya Kampuni ni KUIKOSEA KAMPUNI YAKE, Na LAZIMA AELEWE DHAMANI YAKE, kwa Wakati ule WCB as Company ndio walikuwa Wanaelewa Dhamani Ya Harmonize Akisimama Kufanya Show, So ili Kujibrand na Kujipa Dhamani Huwezi shuka ovyo ovyo kwa Mashabiki kuwafanyia Show kisa Wamekushangilia so Hizo Millioni ngapi alizo lipishwa ilikuwa SAHIHI 100%, Tujiulize Mlisha Muona Wizkid Anaimba Imba Kwenye Harusi, Birthday, Viwanjani bila Show Maalumu? au Davido au Future au Msanii yeyote mkubwa Marekani? Kuna Muda hata Kwenye Interview hawaendi endi tuuu kisa Umeitwa, Hii yote ni Kujitengenezea Dhamani. Na ndicho walichokuwa wanafanya WCB kwa Wakati huo, Wewe Umeenda Taifa Kuangalia Mechi angalia Mechi maliza nenda, Kushuka Chini Kuimba kama Kampuni Ilikuwa Imepanga Next week Wakupe Show Je? WASANII WENGI WA TZ wanakosea Hapo kujishusha DHAMANI na Ndicho Anacholilia HARMONIZE ana Alicho Taka WCB wafanye.

NISEME TUU, HARMONIZE ALIBAHATIKA KUPATA KAMPUNI AMBAYO NAYO KWA NAMNA MOJA AU NYINGINE WALIKUWA HAWAJUI DHAMANI ZAO. NASHANGAA HATA MANAGEMENT YA DIAMOND kwanini Inamuachia Diamond Anazurulula Ovyo ovyo na Kina Baba Levo na Juma Lokole, anaenda Ovyo ovyo kwenye Vishughuli visivyo na Maana kama Harusi Ni Kujishushia Dhamani JAPO WATU HUMU MUNAWEZA MSINIELEWE.

Ni Hayo tu
Labda mm Sina masikio ,ivi Kuna sehemu harmonize kalalamika kuwa alikuwa ananyonywa au kulalamikia hiyo 40 percent? Huu ushabik naona watz umetuzid Sana aiseee.
Harmonize kwenye maelezo yake yote amesisitiza kuwa alikuwa hatak kutoka wcb kwa lugha nyepes ariridhika na hiyo 40 percentage ,Ila ishu Ni hao machawa wa mond akina Salam na tale ndio walianza kumfitinisha bwana mdogo na Kaka ake ,na maelezo yake ameongea Waz kuwa alipambana Sana ili wawe sawa lakin ilishindikana so ikawa Ni lazima atoke .

Baada ya kugonga mwamba kwa kila jitihada ikabid waanze kumfanyia fitna Mara lete 300 Mara 200 Mara 100 ,na ukumbuke hiyo Bei walijipangia wao lakin kijana akalipa ,ishu ikaja baada ya kulipa hawakuwa tayal Tena kumpa contract termination ,lengo ni nn hapa yaan wanuue dogo jumla kimziki kwa lugha nyepes walitaka kumtapel ,maana ushalipwa chako hutak kusain mkataba wa kuachana maana ake nn had rais kuingilia Kati.

Kilio Cha harmonize Ni fitna na jinsi alivyogombanishwa na Kaka ake pengine huna jicho la kuona mbali ,harmo Wala hakuwa na mpango wa kutoka wcb Zaid kafitinishwa na tokea hapo ni mwendo wa kumsaka kila angle ,Ni bahat tu kijana nae si haba maana alijua michezo yote ya wcb tofaut na hapo angekuwa km mavoko na yule mrundi Ila kijana nae kaiva .

Ushabik mwingine hapana harmo anaonewa hayo mambo ya pesa unaongea wewe na kuyakuza ili yaonekane ndio ajenda kubwa wakat sio ajenda hapa Ni fitna bac, Kama Ni pesa wcb nao washavuna Sana pesa kutoka kwa bwana mdogo Hilo lipo Waz ,hata hiyo 600m Ni nyongeza tu kwa kile walichovuna kwa harmo ,kapiga show ngap hapo wcb why 600m ndio uone Ni pesa kidogo?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom