Harambee ya CHADEMA - Naura Spring, Arusha

Harambee ya CHADEMA - Naura Spring, Arusha

Kuna watu ndani ya CDM ambao ukiwachangia kama vile akina Zitto unaona kabisa umeitea vyema hela yako! But kuwachangia hao ndugu zangu wengine ni kutupa tu hela jalalani!

wewe gamba kweli! Wewe umeona mbunge ndio anachangiwa hapo?
 
Kiukweli kama watanzania ni wazalendo na nchi yao. basi kauli za uongo zinapaswa kupigwa vita. Leo nashangaa kusikia kuwa nchi yetu haikuwahi kuwa na mshikamano, umoja, upendo na amani mpaka hapo ambapo CDM wamekuwa chama cha kwanza kuleta mshikamano hapa Tanzania, ninaweza kuita ni kauli dhaifu kwa kiongozi mkubwa kama yeye (Dr. slaa) unapo utangazia umma kuwa CHADEMA ndo chama cha kwanza kuleta mshikamano Tanzania, naomba tujiulize

1. Tanzania ilipataje uhuru wake bila mshikamano
2. Tanzania iliondoaje ukabila bila mshikamano
3. Tanzania ilishindaje vita vya Idd Amini bila ya mshikamano
... 4. Tanzania imeingiaje kwenye mfumo wa vyama vingi na uhuru wa kuongea(kuropoka, maana wengine wanaropoka tuu kisa yupo huru) bila mshikamano
5. Tanzania imetunzaje amani ya nchi yake bila mshikamano

Je kwa kipindi chote hicho mpaka leo watanzania wanaishije bila ya mshikamano

Je CDM imefanya kipi au imechukua lini madaraka mpaka imeleta huo mshikamano ambao nchi haukuwa nao????????????????

kwa hoja na sio ushabiki naomba kusaidiwa

najua waropokaji watakuja na kuanza kudai oh katumwa. Mimi ni msomi najitambua hivyo sin jinsi ya ya kumfanyia kazi mtu mwingine. but nahitaji kuyajua haya tu.

Mkuu futa kauli ya kuwa wewe ni msomi bali sema umepitia madarasa mengi. Msomi yeyote anajua kuwa Tanzania needs plan B as plan A is not working. Msomi yeyote anajua tunahitaji Mabadiliko. Shame on you
 
Acha hizo hakuna udini katika chadema .umeshiiwa nyimbo kama rafiki zako wakina tyson na chama chao cha kujivua gamba ambalo halivuliki
Achana na gamba la Mtaa wa Lumumba hilo....hapo alipo presure inapanda presure inashuka
 
I have real been moved by the movement of what is going on back home through Chama changu Chadema. Niko nje ya nchi lakini naomba kiongozi wa Chadema anipe PM na kunipa account namba ya chama (siyo ya mtu binafsi) niweze kutumbikiza kamchango changu ka £150

Kwa niaba ya uongozi wa CHADEMA, nakushukuru Ndugu Kagalala. Ukipeleka fedha kwa jina la "M4C" kupitia National Bank of Commerce au CRDB Bank Ltd, zitaingia katika akaunti ya CHADEMA.
 
mimi mbunge wangu wa Moshi(M) Mzee Ndesamburo kanifurahisha sana, pale aliposema ''Nachangia milyioni 20, twenty M!, hii ni kidogo sana, bado ipo mingi tu . . . Ndani ya nchi na nje ya nchi ipo mingiii!'', kwakwel huyu Mzee mungu auongezee uri wa kuishi mara dufu. Amen
 
  • Thanks
Reactions: LAT
Kwa niaba ya uongozi wa CHADEMA, nakushukuru Ndugu Kagalala. Ukipeleka fedha kwa jina la "M4C" kupitia National Bank of Commerce au CRDB Bank Ltd, zitaingia katika akaunti ya CHADEMA.

Asante sana Mzee Mtei. Kesho ntatumbukiza CRDB
 
Hapo Mama Junior anafurahi tu mpunga umeingia, Baba Junior anapiga hesabu ya kumalizia jumba lake la kifahari Kunduchi Beach watu wanachangishwa pesa bila kufahamu zinakwenda wapi CDM bhana.
 
mimi mbunge wangu wa Moshi(M) Mzee Ndesamburo kanifurahisha sana, pale aliposema ''Nachangia milyioni 20, twenty M!, hii ni kidogo sana, bado ipo mingi tu . . . Ndani ya nchi na nje ya nchi ipo mingiii!'', kwakwel huyu Mzee mungu auongezee uri wa kuishi mara dufu. Amen

Ndesamburo bhana, huyo Mzee msanii sana unakuwa kama ule mchezo wa karata kekundu na kaeusi, anajifanya anatoa Ml 20 ili hawavute watu, Wachaga wana mbinu nyingi kwenye pesa.
 
Hapo Mama Junior anafurahi tu mpunga umeingia, Baba Junior anapiga hesabu ya kumalizia jumba lake la kifahari Kunduchi Beach watu wanachangishwa pesa bila kufahamu zinakwenda wapi CDM bhana.
Afadhali watu wanachanga kwa hiari yao kuliko CCM inayochota hazina alafu wafanyakazi wa serikali wanakosa mishahara. Kama huwezi kuona kuwa Chadema ni chama cha watu basi unamatatizo katika uwezo wako wa kufikili.
 
Hawa jamaa wamechoka ile mbaya hadi sasa wana tembeza bakuli, igunga walikuwa na pesa za wafadhili wanagawa ccm 30000, cdm 20000, utaweza wapi kushindana na ccm wanapesa za mafisadi, hao wa meru maisha yenyewe magumu halafu uwakamue shilingi zao, halafu wakupe kura Mawe!!

Fundrising ni hiari ya mtu so sio kila ishu uchangie humu jamvini
 
Kesho tunaongeza chopa ingine kwenye campaign ya ARUMERU, mpunga umeingia banaaa!!!!!!!!!!!!!!
 
Hapo Mama Junior anafurahi tu mpunga umeingia, Baba Junior anapiga hesabu ya kumalizia jumba lake la kifahari Kunduchi Beach watu wanachangishwa pesa bila kufahamu zinakwenda wapi CDM bhana.

tuachie chadema yetu..hata kama slaa atazitumia we inakuuma nini?acha kuwaza kwa kutumia kisigino
 
Hiyo movement yao ingekuwa imefanyikia mikoa ya Lindi, Mtwara,
Ruvuma au Rukwa ningeshiriki! Kwenda kufanyia kitu kama hicho nyumbani kwa CDM kumenidiscourage!
Hata TANU haikuanza kwa kukubalika nchi nzima ya Tanganyika. Kadri siku zinavyosonga CDM itafika huko!
 
Nina amani sana hadi muda huu baada ya kuhakiki suala hili hadi mwisho!
Mungu saidia, acha nikalale tu, Naamini nitapata usingizi murua!
Mungu bariki cdm!...Mungu bariki Watanzania waliojitoa kusaidia ukombozi wa kweli wa nchi hii!
Mkoloni mweusi ni lazima aachie nchi yetu aondoke!
 
There are currently 670 users browsing this thread. (159 members and 511 guests)

Back
Top Bottom