Lunyungu
JF-Expert Member
- Aug 7, 2006
- 8,873
- 1,894
Wakuu wote kabisa bila kujali wapya na wa zamani nawapa salaam zangu za Mwaka mpya 2012 .Ni masaa machache yamebakia lakini naamini Mungu atatuvusha wote .
Mwaka huu unao ishia ulikuwa mgumu sana sana kwangu hasa ki afya .Mtakumbuka mliniombea sana wakati naumwa. Nililala kitandani kwa muda wa miezi 8 .Nikiwa nimvunjika mgongo kwa ajili ya kuumwa cancer aina ya Multiple Myeloma.Hadi nafika ughaibuni kuanza matibabu ilikuwa imesambaa kwa 73%.
Wako wana JF walishiriki moja kwa moja kunisaidia wakati naumwa kama Jimmy Paka .Nikiwa hosp wote kabisa mliniombea mno .Mlinipigia simu na hata kuandik hapa online mkinitakia afya njema .Nikiwa ICU kwa wiki nzima pale St.Antonius hosp siku napata nafuu nilielezwa kwamba wana JFwanakuombea na nilifarijika mno .
Paamoja na tofauti zetu za mtizamo kisiasa hasa lakini kwenye hili hakika mlinipa nguvu mno .Nikiwa hapa Ulaya ndugu zangu walikuwa nyie wana JF .Miezi 7 nimelala nikiwa siwezi lolote nakula kwa mpira puani na kujisaidia haja zote hapo hapo na kupoteza kilo 24 haikuwa rahisi kuamini kwamba nitakuwa nanyi hadi sasa .
Mwaka 2012 uwe mwema kwako wewe na familiaa yako na tafadhali tutotautiane kwa hoja ila upendo na mshikamano wwetu kama Watanzania ubakie pale pale .Tanzania iwe ya kwanza na ubinafsi usiwe na nafasi .
Asanteni sasa na Heri ya Mwaka Mpaya wana JF wote