Happy New Year 2012 wana JF wote

Lunyungu

JF-Expert Member
Aug 7, 2006
8,873
1,894
Wakuu wote kabisa bila kujali wapya na wa zamani nawapa salaam zangu za Mwaka mpya 2012 .Ni masaa machache yamebakia lakini naamini Mungu atatuvusha wote .
Mwaka huu unao ishia ulikuwa mgumu sana sana kwangu hasa ki afya .Mtakumbuka mliniombea sana wakati naumwa. Nililala kitandani kwa muda wa miezi 8 .Nikiwa nimvunjika mgongo kwa ajili ya kuumwa cancer aina ya Multiple Myeloma.Hadi nafika ughaibuni kuanza matibabu ilikuwa imesambaa kwa 73%.

Wako wana JF walishiriki moja kwa moja kunisaidia wakati naumwa kama Jimmy Paka .Nikiwa hosp wote kabisa mliniombea mno .Mlinipigia simu na hata kuandik hapa online mkinitakia afya njema .Nikiwa ICU kwa wiki nzima pale St.Antonius hosp siku napata nafuu nilielezwa kwamba wana JFwanakuombea na nilifarijika mno .

Paamoja na tofauti zetu za mtizamo kisiasa hasa lakini kwenye hili hakika mlinipa nguvu mno .Nikiwa hapa Ulaya ndugu zangu walikuwa nyie wana JF .Miezi 7 nimelala nikiwa siwezi lolote nakula kwa mpira puani na kujisaidia haja zote hapo hapo na kupoteza kilo 24 haikuwa rahisi kuamini kwamba nitakuwa nanyi hadi sasa .

Mwaka 2012 uwe mwema kwako wewe na familiaa yako na tafadhali tutotautiane kwa hoja ila upendo na mshikamano wwetu kama Watanzania ubakie pale pale .Tanzania iwe ya kwanza na ubinafsi usiwe na nafasi .

Asanteni sasa na Heri ya Mwaka Mpaya wana JF wote
 
Mkuu tumeuona mwaka 2012, ni wakati mzuri wa kujipanga upya, yale tuloshindwa kuyatimiza mwaka jana, hatuna budi kuyatimiza mwaka huu.
Stay blessed mkuu.
 
pole sana mkuu. Thanks God tumeshaona 2012. huu ndo ule mwaka wa mazishi ya ccm yatakuwa ni mazishi ya kitaifa tunajiaandaa kwa hamu.
 
Asante mkuu. Mwenyezi Mungu aubariki uwe ni wa mafanikio kwa wana JF wote. Uwe mwaka wa kukemea Mabaya yote hata yale ya mods na invincible kuondoa post zenye ukweli unaokuwa mchungu kwa mafisadi. JF owe kweli ambalo we speak FREE.
 
Wakuu wote kabisa bila kujali wapya na wa zamani nawapa salaam zangu za Mwaka mpya 2012 .Ni masaa machache yamebakia lakini naamini Mungu atatuvusha wote .
Mwaka huu unao ishia ulikuwa mgumu sana sana kwangu hasa ki afya .Mtakumbuka mliniombea sana wakati naumwa. Nililala kitandani kwa muda wa miezi 8 .Nikiwa nimvunjika mgongo kwa ajili ya kuumwa cancer aina ya Multiple Myeloma.Hadi nafika ughaibuni kuanza matibabu ilikuwa imesambaa kwa 73%.

Wako wana JF walishiriki moja kwa moja kunisaidia wakati naumwa kama Jimmy Paka .Nikiwa hosp wote kabisa mliniombea mno .Mlinipigia simu na hata kuandik hapa online mkinitakia afya njema .Nikiwa ICU kwa wiki nzima pale St.Antonius hosp siku napata nafuu nilielezwa kwamba wana JFwanakuombea na nilifarijika mno .

Paamoja na tofauti zetu za mtizamo kisiasa hasa lakini kwenye hili hakika mlinipa nguvu mno .Nikiwa hapa Ulaya ndugu zangu walikuwa nyie wana JF .Miezi 7 nimelala nikiwa siwezi lolote nakula kwa mpira puani na kujisaidia haja zote hapo hapo na kupoteza kilo 24 haikuwa rahisi kuamini kwamba nitakuwa nanyi hadi sasa .

Mwaka 2012 uwe mwema kwako wewe na familiaa yako na tafadhali tutotautiane kwa hoja ila upendo na mshikamano wwetu kama Watanzania ubakie pale pale .Tanzania iwe ya kwanza na ubinafsi usiwe na nafasi .

Asanteni sasa na Heri ya Mwaka Mpaya wana JF wote
Asante sana kwa salamu njema za Mwaka Mpya. Maneno yako ni yenye faraja na kutia nguvu. Sisi sote kama ni Watanzania tuzidi kupendana hata kama tuna tofauti za kisiasa sisi wote bado ni wamoja mbele ya uso wa Mungu.
Mungu azidi kukupa nguvu na kukuponya tupo bado nawe katika sala. Mungu ni mwema na mwaminifu kwetu sote.
Heri ya Mwaka Mpya 2012
 
Mkubwa
SSALAMU tumezipokea, na we ubarikiwe sana katika mwaka huu.
Mwenyezi Mungu akuziodishie afya na uyasahau maumivu yote uliyopitia katika mwaka 2011.
Tuko PAMOJA SANA.

pj
 
Happy_New_year_Cards_2012.jpg
 
Mwaka huu unao ishia ulikuwa mgumu sana sana kwangu hasa ki afya .Mtakumbuka mliniombea sana wakati naumwa. Nililala kitandani kwa muda wa miezi 8 .Nikiwa nimvunjika mgongo kwa ajili ya kuumwa cancer aina ya Multiple Myeloma.Hadi nafika ughaibuni kuanza matibabu ilikuwa imesambaa kwa 73%.

Asanteni sasa na Heri ya Mwaka Mpaya wana JF wote

Lunyungu wewe ni fighter na I like the optimism in you. Fighting cancer is such a big thing, Pole saana na Hongera saana kwa kuweza tambua how Lucky you are. Hopefully you have recovered kabisa na sasa waendelea vizuri kabisa. Tusha ingia mwaka Mpya, Tumuombe Mwenyezi Mungu azidi tubariki na kutuongezea afya njema.

HAPPY NEW YEAR MKUU..... May it be one of your best in your Life.
 
...Mkuu Lunyungu pole sana na Mwenyezi Mungu ashukuriwe kwa kukusaidia katika kipindi kigumu sana ulichopitia Mkuu. Nakutakia kila la heri na baraka ili mwaka 2012 uwe mzuri zaidi kwako na kwa familia yako ukilinganisha na 2011. HAPPY NEW YEAR!!
 
Pole mkuu
sasa unaendeleaje
mnyaaz mungu akupe
nguvu na afya tele,
yeye ndo muamuzi wa
hayo yote uliyopitia
usichoke wala kuacha
kumwomba!happy new year!
 
Pole sana mkuu kwa yaliyokupata na Mungu aliyekuponya uzidi kumwomba akupe afya njema zaid na pia asante kwa salam za mwaka mpya!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom