Leo namzunguzia mwamba Vladimir Putin ni nani na anataka nini katika hii dunia

mchawi wa kusini

JF-Expert Member
Apr 18, 2018
805
809
Habari Ya Jumapili Wana JF Naamini mpo salama ,Wagonjwa Mungu atawasimamia na mtarudi Katika Hali yenu Ya Kawaida Ili Kuja Kulijenga Taifa.

Twende Na Mimi Kuhusu huyu Mwamba Niliyemtaja Hapo.

VLADIMIR PUTIN NI NANI NA ANATAKA NINI?

Kabla sijaandika kuhusu maisha na tabia za Putin Vladimirovich, kwanza tujue anataka nini huko Ukraine,hata ingawa NAAMINI SANA KWAMBA VITA HIVI HAWEZI KUSHINDA:

1) Ameamrisha Ukraine kuacha kabisa vita,bila masharti.
2) Anataka nchi hiyi isifungamane na upande wowote,ibaki yenyewe kama Ukraine,isijiunge na NATO wala EU.Anataka hilo liingizwe kwenye katiba ya nchi hiyo!
3) Anataka Ukraine itambue rasmi kuwa Krimea ni sehemu ya Urusi.
4) Huyu mwamba anataka Ukraine ikubali uhuru na kujitenga kwa Luhansk pamoja na eneo la Donetsk.

Kwanzia mwaka 2014,Ukraine ilipaswa kuingiwa na wasiwasi baada ya Putin kutangaza Krimea kuwa nchi huru.Hawakufanya lolote la maana.

Yaani Putin anagawa nchi ya wenyewe vipande vipande ili kuitawala.Anataka iwe visehem sehemu tu ya Urusi..

Lakini Putin ni nani haswa?

Vladimir Vladimirovich Putin ni rais wa nchi ya Urusi,zamani ikijulikana kama muungano wa Sovieti(USSR,ambayo ilisambaratishwa na Marekani kupitia siasa za vita baridi(cold war)na kubakia Urusi.Nchi zingine zilijitenga na kujitangazia uhuru,ikiwemo nchi ambayo ameamua kuvamia sasa hivi(Ukraine)...

Putin alizaliwa mwezi oktoba,tarehe 7,mwaka 1952,huko Leningrad(kwa sasa St. Petersberg).Ni mwanasiasa na mwanaintelijensia mzuri tu.Alichaguliwa kuwa rais wa nchi hiyo mwaka 2012.Alikuwa pia rais wa mpito mwaka 2000 mpaka mwaka 2008.Alikuwa waziri mkuu mwaka 1999 hadi mwaka 2000,na mwaka 2008 hadi 2012(nitazungumzia hili hapa chini).

Putin ndiye rais wa pili aliyedumu muda mrefu zaidi madarakani hivi sasa huko bara Uropa.Mwingine ni Alexanda Lukashenko wa nchi ya Belarus.

Putin amesomea sheria katika chuo cha Leningrad ambako alifuzu mwaka 1975.Amefanya kazi kama jasusi wa shirika la KGB kwa takriban miaka 16 akianzia nchini Ujerumani.Aliachia ngazi akiwa kwenye cheo cha Luteni Kanali mwaka 1991.

Aliamua kuingia kwenye uwanja wa siasa na akashinda kiti cha umeya huko kwao St Petersberg,kisha akahamia mjini Moscow mwaka 1996 kujiunga na uongozi wa rais Boris Yeltsin.Akiwa Moscow,aliteuliwa kuwa mkurugenzi wa shirika la kijasusi la urusi(Federal Security Services,yaani FSB,zamani iliitwa KGB.Mwezi Agosti mwaka 1999,aliteuliwa kuwa waziri mkuu wa Urusi.Huyu ni mtu aliyeandaliwa kwajili ya kazi maalum ya kirusi!

Baada ya kujiuzulu kwa Yelstin,Bw Putin alichukua nafasi ya rais wa mpito.Baada ya miezi mitatu hivi na siku kadhaa,alichaguliwa kuwa rais wa Urusi.Mwaka 2004,alichaguliwa tena kwenye awamu ya pili.Katiba ya nchi hiyo ilimkataza kugombea tena mfululizo baada ya awamu hizo mbili.

Putin ni mjanja sana.Aliamua "kujiteua" kuwa waziri mkuu tena kwanzia mwaka 2008 hadi mwaka 2012,chini ya rais wa muda Dmitry Medvedev(ambaye hajulikani).Alirudia kugombea urais mwaka 2012 na kushinda kiubishi.Mwaka 2018 akagombea tena na kushinda,huku akiminya upinzani vilivyo.Dunia iliangalia bila kupaza sauti!

Mnamo mwezi Aprili mwaka 2021,alilazimisha upigaji kura nchi nzima kufanyia marekebisho katiba ya nchi hiyo(referendum),ambapo alitia sahihi marekebisho hayo,ambayo ilimruhusu kugombea tena mara mbili zaidi.Hii imemruhusu kuwa rais hadi mwaka 2036.Dunia ilikaa kimya tu!

TABIA NA NDOTO ZA PUTIN

Putin ni mtoto wa tatu kwenye familia ambapo kaka zake wawili hawakuishi,walifariki mapema.

Babu wa Putin(Spiridon Putin)alikuwa mpishi wa Vladimir Lenin na Joseph Stalin.Mmoja kati ya kaka zake hao wawili(Viktor)alifariki kutokana na rapsha za vita vya pili vya dunia baada ya Ujerumani kuvamia Leningrad.

Akiwa mdogo,Vladimir alikuwa na ndoto ya kuwa mjasusi,na alifanya jitihada binafsi kufanikisha ndoto zake.Alijifunza mbinu nyingi za kujilinda(sambo na judo)akiwa mdogo,mwenye umri wa miaka 11 tu. Alikuwa kijana mkimya na msiri sana.Ni mrusi wa kwanza kutunukiwa mkanda mweusi,daraja la dani ya 8 kwenye michezo hiyo mwaka 2012.

Alijifunza lugha ya kijerumani vizuri,alipenda kusoma vitabu vya kifalsafa vya ki-Karl Marx,Fredrich Engels na Lenin.Pia ni mzuri mno kwenye mchezo wa karat.Putin ni mzalendo kupitiliza na ni mtu aliapa kulinda Urusi hadi tone la mwisho la damu yake!

Mama yake alifanya kazi ngumu kwenye viwanda,huku babake akifanya kazi kwenye sabmarini za kisoviet.Baba yake alipata jeraha mbaya sana akiwa mhudumu jeshini,bibi yake aliuawa na jeshi la kijerumani,wajomba zake walipotea kusikojulikana.

Mwaka 1985 hadi 1990,alitumwa huko Dresden,nchini Ujerumani mashariki ambako aliajiriwa kama mkarimani(undercover).Alikuwepo kipindi ambacho Ujerumani mashariki na magharibi ziliungana(mwaka 1989),kipindi ambapo ukuta wa Berlin uliangushwa.

Inasemekana alifanikiwa kuzima maandamano ya wajerumani walioelekeza hasira zao kwenye ofisi za Urusi kwa kuwatishia sana.Kwa kuwa ni mjasiri sana,alienda mwenyewe kwa waandamanaji na kuwambia kwa kipaza sauti kuwa,"Huko mnakoelekea mtakufa,kwa sababu warusi mle ndani wanasilaha nzito mno,nawashauri mgeuke mrudi mlikotoka." Watu hao walitoroka na kutoweka kabisa!

Putin alioa tarehe 28,Julai 1983 na kuishi na mkewe Lyudmila Shkrebneva huko Ujerumani kwanzia mwaka 1985 hadi mwaka 1990.Wamejaliwa watoto wawili wa kike.

Mwaka 2020,jarida la Proekt iliandika habari za mahusiano za siri kati ya Putin na mwanamke aitwaye svetlana Krivonogikh,ambako ilisemekana walikuwa na mtoto mwingine wa kike aliyezaliwa mwaka 2003.Putin alikana kabisa habari hizo.

Aprili 2008,jarida la Moskovsky korrespondent iliripoti kuwa Putin alimpa talaka Lyudmila,na kuwa alikuwa na mahusiano na mwanasiasa chipukizi,mcheza sarakasi na mshindi wa medali ya dhahabu katika mchezo wa olimpik(Alina Kabaeva),Putin alikana vikali na gazeti hilo lilipigwa marufuku.Ilisemekana tayari walikuwa na watoto wengi na huyo dada.

June 6,mwaka 2013,Putin na Lyudmila walitangaza kuachana kirasmi,na Putin aliendeleza mahusiano na Kabaeva.Wamepata watoto watatu na huyo dada.

Vladimir Putin ni bilionea mwenye mali nyingi za siri.Ni mtu mwenye ndoto ya kurudisha sura ya Sovieti ya zamani kwa kumiliki tena nchi zote zilizojiengua na kujitangazia uhuru kutoka USSR.Anandoto ya kutawala dunia nzima na kuandika historia.

Putin ni mtu mjasiri,mpenda siri,asiye na huruma na "mpenda maumivu".Ni mtu aliye na fikra za tofauti na hisia za tofauti na watu wengi.Ni mtu anayefurahishwa na mamlaka makubwa.

Kinyume na watu wanavyodhania kuwa anatafta utajiri wa gesi huko Ukraine,Putin anaamini kuwa ni haki yake kurudisha sehem ya Urusi kwenye ramani ya Urusi.

Ebu tafakari,kwa nini Putin ametuma ndege zake za "White Swan" huko Pretoria?Ndege hizo mbili,ni kati ya ndege 160 aina hizo ambazo zimewekwa tayari kutumika endapo dunia itajaribu kuingilia vita kati ya nchi yake na Ukraine.

Kumbuka hizo ni ndege zenye silaha za kinyuklia,kila mmoja lina uzito wa karibia tani 300,na uwezo wa kuruka siku nzima!

Putin ametuma meseji dunia nzima kupitia hizo ndege mbili tu,"I CAN REACH YOU ANYWHERE IN THE WORLD"(NAWEZA KUWAFIKIA POPOTE PALE DUNIANI).

Kwa Putin,dunia haina namna,sio NATO,sio EU na sio UN.Afrika ndo kabisaa hawafurukuti....

Tukae kimya,muvi inaendelea,na huyo ndiye Putin.

#TheWorldIsAfraidOfWorldWar3
 
Duh! Mwamba anatisha. Kongole mkuu mchawi wa kusini kwa kutujuza hayo kumhusu huyo mwamba. Lakini tusisahau msemo wa Wahenga usemao "Avumaye baharini papa kumbe wengi wapo. Hayo majigambo yake na kulundika masilaha huku na kule inawezekana akayaacha bila hata kuyatumia kwani mahali pa kuyatumia hapatakuwepo. Mfano hai ni pale USSR iliposambaratika bila utumiaji wa silaha. Pia tukumbuke umauti ni lazima kwa kila mtu aliyezaliwa na mwanamke. Muda ukifika(Salio likiisha) lazima utaondoka tuu; taka-usitake. Muda unakwenda mbio sana.
 
Hakuna jipya hapa, hajafikia umwamba wa Hitler hata nusu yake, kilimtokea nini...!?

Hadi Leo hakuna anaye tambua miwili wake ulipo..
 
Nimevutiwa na ndoto zake za kutaka kuirudisha Soviet Union iliyosambaratishwa na Ronald Reagan.
Kongore mkuu kwa andiko lako hili
 
Nimevutiwa na ndoto zake za kutaka kuirudisha Soviet Union iliyosambaratishwa na Ronald Reagan.
Kongore mkuu kwa andiko lako hili
Ndoto za alinacha, yaliyokuwa mataifa ya Kisovieti hayataki kabisa ukaribu na Urusi badala yake yanakimbilia NATO na EU.
 
Umesahau kuweka jinsi ambavyo anawaua wapinzani na wakosoaji wake, anawakimbiza nje ya nchi(exile), anawafilisi na kuwatupa gerezani.
 
Back
Top Bottom