Amicus Curiae
JF-Expert Member
- Sep 12, 2012
- 4,809
- 6,342
Wakuu habarini za wakati huu. Naandika uzi huu nikiwa na simanzi sana!
Nina eneo langu Ukonga KMKM ambapo nimejenga nyumba moja kubwa ya kupangisha na vyumba vingine 4 vyenye sebule na choo ndani. Nimefanya uwekezaji huu kwa kujinyima sana tena nikitumia pesa yangu halali.
Mimi siishi Dsm kwa sasa. Changamoto ipo kwa mpangaji mmoja bwana mdogo ambaye ni Mwanajeshi mwenye cheo cha Coplo, ni rika langu, yuko kati ya 30-37; ananisumbua sana kulipa kodi. Nimemvumilia vya kutosha. Pamoja na kuweka kodi ndogo lakini bado jamaa ananisumbua mno.
So far namdai zaidi ya milioni moja. Kuna wakati nasafiri kwenda Dar kutazama maendeleo ya makazi yangu na nakutanaga nae lakini anaishia kunipiga sound. Jamaa ni mtaratibu sana, anazungumza kwa upole; kila nikijaribu kumtoa hata kwa kumsamehe hiyo kodi huwa napatwa na huruma.
Kwa sasa enough is enough. Mara ya mwisho nimekutana nae Desemba mwaka jana, akakiri kwa maandishi kwamba namdai na atalipa deni lote Jan. 29 mwaka huu. Kilichotokea ni kwamba tarehe 29 imepita na kakaa kimya! Nikimpigia simu zangu hapokei. Kwasababu niko mbali, nimemtuma mpangaji wangu mmoja ninayemwamwini ili anipe nizungumze nae ila inasemekana jamaa hayupo pale kwa takribani wiki 3, kuna tetesi ameenda kwenye kozi Kibaha.
Ningeweza kwenda kumshtaki kambini kwake lakini sijui yuko kambi gani, kuna wanaosema yuko Lugalo ila hawana uhakika.
Naombeni msaada wakuu, naamini kuna watu ni Wanajeshi humu, wengine mna ndugu zenu Jeshini na hamuwezi kukubali dhuluma ya namna hii, naombeni msaada wa namna ya kuitambua kambi yake, majina yake nayajua, niko tayari kumsamehe hiyo kodi ila anipishe ili nitafute mpangaji mwingine.
Naomba kuwasilisha.
N:B: Wapangaji wote wana Mikataba. Kimsingi huyu jamaa ameshavunja terms za Mkataba muda mrefu. Naweza kumdai kodi Kimahakama lakini sitaki kupoteza muda.