Mh Edward Ngoyai Lowassa uko kwenye Safari yako ya matumaini. Nina maswali haya kumi naomba majibu ili iamue kuunga bogi kwenye hiyo safari au nikutose:
1. Je MH. LOWASSA utatumia JIKI ya aina gani kujisafisha na tuhuma ya UFISADI iliyokuganda kama ruba ?
2. Je kwanini BABA WA TAIFA 1995 alisema hufai kabisa kuwa Kiongozi?
3.Je ni kwanini unautaka Urais kwa udi na uvumba, je ukiukosa utajinyonga au utaingia mstuni?
4. Je "FRIENDS OF LOWASSA" ni akina nani? Je unaweza kututajia majina yao? Je huwa wanalipa kodi?Je mabilioni yao hayatokani na MONEY LAUNDERING?
5. Je ukiukosa Urais utaendelea kugawa hayo mamilioni kwa watu na vikundi mbambali au ndo utakula kona?
6. Je wenzako wa CCM waliokwambia wewe ni fisadi na UJIVUE GAMBA ukitwaa Urais utawatia adabu au utakula jiwe na kuwaachia wale nchi ndani ya CCM??
7. Je ni kweli afya yako ni mgogoro na kuwa huwezi kushika kikombe cha chai kwa dakika 3??
8. Je ni kweli huwa unazuka UJERUMANI kutibiwa mara kw mara? Kama ni kweli nchi si itakuwa inaongozwa na Makamu wa Rais muda mwingi?
9. Je washindani wako wa kinyanganyiro cha URAIS utawashikisha adabu au utawaweka kwenye Serikali yako?
10. Je unautaka URAIS ili kujinufaisha wewe binafsi na marafiki zako au una nia njema na madhubuti ya kawaondolea waanchi umasini mkubwa unaoongezeka kila siku?
=======
Feb 2015:
By Kilaza
Wakuu heshima kwenuhaya ni maswali yangu kumi kwa Mheshimiwa Edward Lowassa na Vibaraka wake
1 . Gazeti la Raia Mwema la Novemba 2010 ,liliripoti na kuonyesha picha ya nyumbaambayo familia yako inamiliki Uingereza .Ukasema ni ya mwanao . Je, kwa nchimaskini kama ya kwetu , ni sahihi kwakiongozi mkubwa kumiliki nyumba kubwa naya kifahari nje ya nchi ?
2 . Mkapa alipounda Baraza la Mawazirijipya mwaka 1995 alikuacha . Wengiwanasema kwamba Mwalimu alimwambiaasikupe hata Uwaziri je Kwanini mwalimu Alikukataa???
3 . Tangu mwaka 1994 , yaani miaka 20sasa, Afrika ya Kusini imekuwa inakodishanyumba yako Masaki kama Ubalozi wake .Kuna tetesi kwamba huko nyumba walitakakuhama lakini wakaogopa kuihama nyumbainayomilikiwa na kiongozi mkuu na kunatetesi kwamba sasa wanataka kuhamalakini wanatishiwa kwamba hamuwezikuhama nyumba ya Rais ajaye . Ni kiasigani cha fedha umepata kwa miaka 20 yakukodisha nyumba hiyo ? Je kiasi hichokimeripotiwa kwenye fomu ya maadili?
4 . Kuna maelezo kwamba nyumba hiyo yaMasaki ambayo Mzee Mandela alikujamwaka 1994 kuufungua ubalozi mpya waAfrika ya Kusini ndicho chanzo kikuu chaMwalimu kusema kwamba inakuwaje kijanawa miaka 41 , akiwa mtumishi ya ummamaisha yake yote na mshahara wakeunajulikana , anamiliki hekalu kama lile natena kulikodisha kwa Serikali ya kigeni . Je,unasemaje kuhusu hili ?
5 . Pia unamiliki ranchi kubwa sana kuleMzeri Handeni . Ranchi hiyo ilikuwa ranchiya taifa lakini ukajimegea na sasaumeipanua kwa kumega maeneo zaidi .Ranchi hiyo uliipata ukiwa bado kiongozi waumma. Je, mtu aliyewahi kuwa Waziri waMifugo na Waziri Mkuu kujiuzia ranchiiliyokuwa ya Serikali inaendana na dhanaya uongozi safi na uliotukuka? Tukikupamadaraka makubwa zaidi hautajiuzia kilakitu? Vilevile, katika nchi ambayo wananchiwengi hawamiliki ardhi , kwa kiongozianayetaka kuwa Rais wetu , kuhodhi eneokubwa la ardhi , inatuma picha gani kwawananchi hao ?
6 . Kwenye sakata la Richmond , ujasiri nikusema ukweli au kubwaga manyanga?Kama ungesema ukweli na usingejiuzulukwenye Richmond , Chama kingeathirika vipiwakati unasema hakuna kosa lililofanyika???
7 . Kwanini kwenye kila tukio la kitaifaukisimama tu karibu na Kikweteunahangaika kutuma picha kwenyemagazeti na mitandao yote ???
8 . Katika miaka yako 40 ya utumishi waumma, kuna jipi jipya ambalo umelisahauna sasa utalifanya kwenye Urais???
9 . Umekuwa Waziri wa Ardhi , mbonamatatizo ya ardhi bado tele nchini ?Umekuwa Waziri wa Maji , mbona matatizoya maji bado tele ? Umekuwa Waziri waMazingira, mbona kuna matatizo yauchafuzi wa mazingira ? Umekuwa Waziriwa Mifugo, mbona wafugaji bado maskinina wanahangaika ?? huo urais unautaka wa nini kama uwaziri umekushinda???
10 . Kwenye sikukuu hii , kila MNEC kapatamilioni 1 , hizo ni milioni 370 na kilamjumbe 500 , 000 hizo ni bilioni 2 . Hizi pesazinatoka wapi na zitarudishwa vipi? Je,kuna zoezi la usafishaji wa pesa chafulinalofanywa kupitia kampeni yako???Professor kilaza