Hamas walimkuta Joshua amevaa bulletproof

Hamas walimkuta Joshua amevaa bulletproof

Huyu baba mtu aliyeenda juzi tu kaja na hizi taarifa?

Uchunguzi kaufanyia wapi?

Kama ameweza kuchunguza na kujua kijana alivaa bulletproof kwanini hajui sababu ya kuivaa?
Baba atakuwa anajua kwanini mwanawe alivaa bullet proof. Kama angekuwa hajui basi tungesikia anahoji hapo.
Sirikali iache urafiki na nchi za ajabu ajabu hizi. Dunia ina peaceful countries nyingi sana za kufanya nao urafiki.
 
Hebu acheni akili zenu hizo. Chupi za kijeshi ndiyo huwa zipoje hizo?
Ile chupi ni ya jeshi la nchi gani? Hata mavati ya Jeshi la Israel mnayajua kweli?
Clemence na yeye aliuawa baada ya kukutwa kavaa chupi ya jeshi? Raia wengine wa nchi nyingine waliouawa na walioachiwa na wao walikuwa mamevaa mavazi ya kijeshi? Mnatengeneza story zisizo na kichwa wala miguu ili ku justify mauaji wa kijana Mtanzania mwenzetu ili muwasafishi Magaidi wa HAMAS kisa mna share dini
Subiri kwanza, Joshua alipata wapi bullet proof?
Kama kafa kazini basi hatuna sababu ya kuhoji chochote. Maswali yako ya kipuuzi kaiulize serikali ambayo imeamua kufanya urafiki na nchi yenye vita wakati dunia ina nchi nyingi zenye amani.
 
Accumen Mo, post: 48894118, member: 666454yule ni raia wa nchi yako, unatakiwa uone ufahari kajiunga na jeshi la israel. Je angejiunga upande wa hamas ungejisikiaje?
Kajiunga na jeshi la Israel kwa faida ya nchi yetu?
Upuuzi wake ndio uliompoza kujiunga na wahuni wa Israel wanaopigana na wahuni wenzao wa Hamas.
 
waliwatimua wahamiaji waliovamia ardhi yao tangu enzi za mababu zao, wahamiaji wanadai ardhi ni yao na kuwashambulia wenye ardhi tangu enzi na enzi
Hivi sisi leo tuna haki ya kwenda kuwavamia Wangoni pale Songea na kuwaondoa kwa sababu ni wahamiaji toka South Africa?
 
Kufuatia kifo cha Mtanzania Joshua Mollel aliyeuwawa na kundi la Hamas, Baba yake mzazi amefunguka na kusema kuwa alifika eneo alilokuwa akiishi na mwanae ambapo alipata taarifa kuwa kundi la Hamas liliwavamia na kisha kuua wanajeshi watano, ambao walikuwa wakiishi eneo Moja na Joshua!

Ameeleza pia Joshua alikutwa akiwa amevaa Bulletproof, ambapo walimchukuwa na Kisha baadae kumuua.

Kwa maelezo hayo hakika imeendelea kuleta sintofahamu, iweje Joshua ambaye alikwenda Israel Kama mwanafunzi, kuishine eneo Moja na wanajeshi hao waliouwawa pia.

Vile vile suala la kukutwa akiwa amevaa Bulletproof nalo ni kitendawili, kwamba je alipewa avae kama raia wa kawaida ama ni mazingira gani yalipelekea kuvaa hizo bulletproof.

Lakini pia ikumbukwe Hadi Sasa mwili wake haujapatikana na haieleweki Hamas walikouifadhi ama kuupeleka.

Hivyo ni vyema serikali ikaja na majibu sahihi kufuatia hili jipya lililoibuka.


View: https://www.instagram.com/reel/C1crB_6KGs0/?igsh=OGY3MTU3OGY1Mw==

Nionavyo Mimi inawezekana jushua alidanganywa na majeshi au viongozi kwamba ajitokee kupigana Kwa ujira baada ya Vita atajiunga kwenye jeshi au atapewa malipo mazuri, mambo haya utokea sana duniani hasa nchi zilizoendekea utumia wageni katika Vita ili kulinda watu wao.
 
Tatizo wanafikiria content tu lakini bado sichukulii hiki kitu kama ni cha kawaida.

Naamini katika situation hii, serikali ingekuwa imeshaifikia familia na kuwaomba wasitoe tamko hadi uchunguzi ukamilike

Sasa kama baba mzazi atoe tamko kirahisi lenye kuleta mushkil zaidi. Siddhant kama ni sawa
It's obvious mzee yupo distraughted na ana uchungu. Kuna details lazima awe amezichanganya. Akiwa ametulia vizuri atajieleza vizuri.
 
Joshua katoka SUA, kaenda Israel kufanya internship, hata miezi 6 hajafikisha afu kuna wajinga wanaongozwa na dini bila kufikiri wanasema alikuwa mwanajeshi, hivi kuna mtu anaweza kuingia jeshini bila mafunzo,

Video inaonesha kabisa hana silaha yoyote alafu wapumbavu wanasema alikuwa mwanajeshi na yule mwingine alouliwa wa kutoka SUA alikua mwanajeshi pia??



Acheni kuongozwa na upuuuzi wa dini za kipumbavu, HAMAS ni magaidi
 
Raia wa Tanzania Wanafunzi na ma Diaspora wakifa huwa wanarudishwa na serikali ?

Au wakiwa Israel wanakuwa Wanafunzi Teule na Diaspora Teule ?

..Mazingira ambayo huyo kijana amekufa ndiyo yanalazimisha serikali ibebe jukumu la kurejesha mwili wake.

..Nchi za wenzetu raia wake akitekwa au akiuwawa serikali zao hufanya jitihada wapatikane.
 
Aliuawa na wenzie ila video ndio kwanza inaonyesha yupo barabara na pale ndio wanaanza kumpiga ...Kiufupi ndugu yetu Mtanzania kauliwa ila maelezo ya mzee na video ni vitu tofauti kabisa.

Tukubali amekufa kuchambua hakuna maana kwa vile naona uongo ni mwingi, huyu mzee kapewa story ila haiendani na clip iliyosambaa mwanzoni.

Wanasema kauliwa ila taarifa za awali walisema katekwa yeye na mwenzie.
HAMAS Negative Propaganda!
 
..Mazingira ambayo huyo kijana amekufa ndiyo yanalazimisha serikali ibebe jukumu la kurejesha mwili wake.

..Nchi za wenzetu raia wake akitekwa au akiuwawa serikali zao hufanya jitihada wapatikane.
Mazingira yepi?
 
Inawezekana Alikuwa spy huyo. Hamas Hawaui mtu asienahatia. Inaonekana Isreal inachukua vijana ktk nchi maskini kuwatumika kijeshi
Na wale mabinti waliokuwa kwenye festival waliouliwa na Hamas kwa kumiminiwa risasi Wana hatia si ndio? Vile vitoto vilivyochomwa moto kama ndafu na Hamas vilikuwa na hatia si ndio?
 
Mazingira yepi?

..mazingira kwamba mwili wa Mtanzania mwenzetu uko ktk eneo ambalo ni uwanja wa vita.

..serikali ndiyo yenye uwezo wa kuwasiliana na mamlaka za Palestina au Israel ili mwili wa Mtanzania mwenzetu upatikane na kurejeshwa nyumbani.
 
Kama kafa kijeshi kwanini asizikwe tu huko huko? Na Isreal
..mazingira kwamba mwili wa Mtanzania mwenzetu uko ktk eneo ambalo ni uwanja wa vita.

..serikali ndiyo yenye uwezo wa kuwasiliana na mamlaka za Palestina au Israel ili mwili wa Mtanzania mwenzetu upatikane na kurejeshwa nyumbani.
 
Back
Top Bottom