@Mtazamaji
ardhi haitumiki kuzalisha chakula au mifugo? - mostly chakula
hawakufuata na mamlaka husika haziufuata taratibu taraibu katika kumilikishwa hizo ardhi.? -Process nzima inaghubikwa na utata na kuna dalili za rushwa. Wananchi walikataa kutoa kiasi kikubwa cha ardhi walichotaka (zaidi ya ekari laki moja kwa miaka 99) wakashauri wapewe kiasi kidogo, na pia kwa kuanzia wapewe kwa miaka 20 tu na kama wakifanya vizuri kulingana na terms za mkataba ndio waongezewe muda. Kinyume chake sasa, viongozi wachache (local authority guys) wakapelekwa marekani kwa siku kadhaa na waliporudi mkataba ukasainiwa, wanavijiji wamebaki wanaduwaa! Kituko kwenye huu mkataba uliosukwa huko Marekani kwa kila ekari moja hawa wawekezaji walipa kati ya Tshs 200 -500 tu kwa moja! Narudia, kati ya Tshs 200 - 500 kwa ekari kwa mwaka. Tanzania hii ni wapi unaweza kukodi ekari nzima kwa shilingi 200 au mitano au hata 1,000 kwa mwaka. Pia Miaka 99 ijayo shilllingi 500 itakuwa na thamani gani? Huu mkataba kama haujatoka kwa Chief Mangungo umetoka wapi?
Tatizo kubwa la Zimbabwe ni Landa (Ardhi). Sisi hapa tuna bahati kwamba baada ya uhuru ardhi hakichukuliwa kwa maelfu na maelfu ya ekari na watu wachache. Lakini kama hatukuwa makini hiki wanachokiita UWEKEZAJI na KILIMO KWANZA tutajikuta tumejijengea Zimbabwe. Na huko ndiko tunakoelekea sasa.
Kuna watu amabo hawakulipwa fidia.? - Kuna maeneo wananchi hawana sehemu za kulima au kuchunga mifugo yao kwa sababu mwekezaji kapewa. Kumbuka huyu mwekezaji kawakuta. Yuko mbunge mmoja katoa mfano bungeni kwamba wako wafugaji waliomba ardhi kwa ajili ya mifugo yao eneo fulani, serikali ikasema hakuna ardhi. Lakini baadae ametokeza Mu-Italiano akapewa ekari 3000 sehemu ile ile waliyoomba wafugaji. Na cha ajabu huyu mwekezaji kapewa eneo la mpakani kati ya Tanzania na Kenya. Na hili eneo ni sugu kwa watu wanaoingia nchini kinyume cha sharia kutoka nchi jirani, Kenya, Somalia &Ethiopia .
Nadhani kama Taifa, kuna haja kabisa ya kutoruhusu (kwa sheria)wageni kumiliki ardhi maeneo ya mipaka ya nchi. Ni kama tunakabidhi raia wa kigeni wachunge mipaka yetu!
Wamemilikishwa ardhi na wenyewe wanawakodisha wanakijiji? - Kuna kuzungukana, wanavijiji wanaachwa pembeni kwa kiasi kikubwa. Pia kuna 'vimemo' vinatoka juu kwa maana ya wizarani etc hivyo uongozi wa chini unakuwa na hofu ya kufanya vingenevyo.
Mimi sioni Tatizo kwa mkapa sumaye au ngwilizi umiliki ardhi kama walimilikishwa ihalali nawalifuata taratibu na sheria zote na wanaitumia ardhi kwa malengo yaliyokusudiwa - Nakubaliana na wewe kiasi lakini lazima uhakikishe wanavijiji wa mahala husika wana ardhi ya kutosha na wanahushwa katika mchakato wote. Kenya wana matatizo sana kwa sasa hivi kwa sababu hii hii ya watu wachache kumiliki ardhi ni wangi wamebakia kuwa manamba. Hata ukisoma report ya Kofi Annan aliyotoa wakati wa kusulughulisha mgogoro wa uchaguzi uliopita huko Kenya, anasema kabisa 'Long-term' solution ihusishe ardhi. Watu wapate ardhi!