Halima Mdee: Mimi pamoja na timu yangu (Wabunge 19) tutabaki kuwa WanaCHADEMA kindakindaki. Tutaenda kuyajenga ndani kwetu


Umetafakari ulichokiandika? Yaani unasema Chadema imepoteza kwa kufukuza wanachama wake ambao unakiri 'wamejiuza' kwa 'mahasimu' wao kisiasa?!
 
Inawezekana mkuu, ila kwa hali ilivyo CHADEMA wao walishamaliza mchezo maana walishawaondoa kwenye uanachama sasa mwenye uhitaji ni wao kina Halima siyo CHADEMA
 
Kuna watu hapa Jf waliamini na bado wanaamini Halima Mdee anaweza kwenda kinyume na Mbowe.

Siyo rahisi.

Halima Mdee hawezi kuiacha Chadema hata akikumbatiwa na nani nje ya Chadema.

Mungu wa mbinguni awabariki.

Maendeleo hayana vyama!
Sawa; Atumie utaratibu kukata rufaa!! Atasikilizwa!!
 
Huu ndiyo mfano ulio bayana unaowakumba wadau wa chama chetu kila jambo wanalitolea hukumu kwa namna ya mapenzi yao binafsi kinyume na matakwa ya kidemokrasia.

Nguvu iliyotumika kupinga udhalimu nje ya chama inatumika ndani ya chama kwa ufanisi mkubwa.
Jadi hii ya ubabe pia isingesaidia kuongoza nchi kungetokea mfarakano zaidi ya huu.
 
Ni vyema Chadema mkae mezani na hawa mwanachama 19 ni muhimu mno. Mkiwapoteza itakula kwenu. Hawa wanawindwa kuliko wale waliounga juhudi. Mbunge mmoja kati yao ni sawa na wabunge 200 nWahakikishia muhimu mkutane mjue ukweli then baadaye watajiondoa bungeni kwa kuwa waliteuliwa kibatili na mteuzi asiyejulikana.
 
Chadema hakuna demokrasia,kuna uhuni mwingi kule,lakini this time wamepatwa
Mbona kuna demokrasia kupita vyama vyote Tanzania. Wewe Umeona wapi kamati kuu inafukuza halafu unapewa fursa kukata rufaa Baraza kuu. Membe, Sofia Simba na wengine walitimuliwa na kuambiwa waombe upya.

Kauli ya Jana ya Ndugai na kupaniki kwake niliona ni dalili za kusalimu amri kwa kutemeshwa mzigo. Watakuwa wabunge labda wajiuzuru. Nikionacho mimi ni wao kujiuzuru ili kumuondolea aibu ya kusigina katiba. Hakuna namna wameshikwa pabaya.
Kushindwa kuelewa na kwao ndiko kulikowarudisha kwani wengi hawataki kufa kisiasa baada ya kujengwa na chadema.
 
Wewe utawapa ugali wa kula na watoto??? Msiwadanganye wakabaki kula hewa..hawana kazi nyingine hao jomba...ooohhhh
Hakuna kazi ya ubunge, ila ni huduma. Tunapata watu wa hovyo hovyo kwasababu wamefanya ubunge kama kazi
 
Wewe umeligundua hilo vyema maana kwa hali ilivyo sasa wangesema wamekubali na hawakati rufaa basi ubunge ungekuwa shakani ila kwa kusema watakataa rufaa wanabuy time ndiyo maana wamegoma kuliongelea hilo

Hawa bado waendelee kuchunguzwa move zao na chama chao kuna hidden agenda au script ya awali imebadilishwa
 
Hata ukweli wenyewe hapo hajauzungumzua Sasa ndiyo pengo la hiyo speech... Ila ndiyo turufu kuu iliyobaki nadhani ya kuleta suluhu kati yao na uongozi wa Chadema.

Wakaonelea wasimwage mpunga penye kuku wengi.
Chadema walifanya makosa makubwa Sana kuwafukuza wabunge wao bila ya kubaini ukweli wa Jambo lenyewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…