Halima Bulembo: Bunge si lazima kuonekana live

Halima Bulembo: Bunge si lazima kuonekana live

Jedwali la nini, kivava...Let me ask you one more thing comrade kivava: Je, angekuwa ni baba yako ameandika andiko lile nililoandika mimi, ungeweza kumwandikia kuwa "tupe jedwali tujue unasema ukweli na sio kupumua hewa chafu". Nimekuuliza hivi kwa kuwa wengi humu JF wanatumia ID ambazo hazijulikani na wana heshima yao katika jamii hii. Wanaandika humu ndani ya JF kwa sababu nyingi na moja ya hizo ni kubadilishana mawazo, kuelimishana na kupashana habari. Ila inaelekea watu kama wewe kivava mnachukulia JF kama sehemu ya mzaha, matusi, kejeli na kudhalilisha wengine...ushauri wangu kwako ni kuwa ikiwa hukubaliani na hoja ya mwenzio huna sababu ya kutukana wala kumdhalilisha au kumkejeli. Jenga hoja yako dhidi yake kama sababu na mkakati wa kushinda mjadala kwa hoja na siyo matusi.
Mea culpa
Mea culpa
Mea culpa
Samahani,huwa napandishwa munkari na uongo WA maccm
Hata hivyo viti maalum Chadema safari hii vimetawanywa nchi nzima na wanaouhusiano na viongozi Ni wawili tuu na waKaskazini hawazidi 10%
 
Hivi ni kwanini viti maalumu wasipopitishwa tena wana RIP,mwaka huu naona wale wawili kati ya watatu wa CHADEMA ambao hawakupitishwa hatunao tena
 
Huyu naye katoa mupyaaa!! Hivi ilikuwaje mpaka akapewa ubunge!! Hahahah!!!
 
Siyo yeye tu wabunge wengi humu bungeni ni mizigo hasa hawa wa kuteuliwa, wanakwenda kulinda maslahi yao peke yao na ya waliowachagua. Hii si kwa CCM tu hata upinzani ndiyo maana kwa hili nampenda Zitto kabwe maana yeye hajali kuitwa msaliti pale anapoona kuna ukweli lakini watu walioelimika kama kina Tundu Lisu nao wananaswa katika mtego kama huu hata wale wa CCM walioelimika wanakisemea chama chao CCM bila kujali kama ni kwa manufaa ya umma ama manufaa ya CCM na kundi la majambazi. Demokrasia tanzani ni ya ujanja ujanja tu. Taabu sana ndiyo maana wakati mwingine nashangaa hata sisi wananchi tunaingia katika mkenge wa vyama vyetu ku support kila ujinga ili mradi unatoka katika midomo ya watu wenye itikadi moja na sisi utadhani ni lazima kuunga kila neno analosema Magufuli ama Mbowe tunajisahau kuwa sisi ndiyo mabosi wao hao wanasiasa.
Ni mrembo lazima apate vitu kama hivyo. Kumbuka Chifupa alivyokuwa mrembo
 
Binti wa miaka 24 halafu wa CCM utafikiri ataklua na uwezo gani wa kufikiri? Halafu eti CHADEMA kuna undugu, hivi huu wa CCM sio undugu? Hahahahahaha nimekubali kweli CCM ni Slow learners wa makusudi
Noma sana
 
Urakuruma Masimbaaaaa....................!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Sasa kama yule mwenye shahada ya usanii mlimuamini kwamba angefaaa kua rais wa tz huku kwa huyu mbunge huoni kama unaleta chuki za UKAWA zisizo na msingi wowote?
Kama nchi mlitaka mmuachie msanii?
Degree ya Usanii siyo Elimu? Ronald Reagan alikuwa mcheza sinema akawa Rais wa USA. Schwarzenegger msanii Wa Sinema to Governer. Huyu mzee mnamuonea sana kuhusu hii BBA in Fine Art. Kasoma eti, 3years Udsm si mchezo.
 
viti maalum ni jipu,kichwani kweupe kabisa kilazaaaa
 
Ndyo kazi ya wabunge ccm, anafanya kaz yke
 
Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Halima Bulembo anasema anaunga mkono bunge kutorushwa live na kusema kurushwa live bunge kuna faida kwa wabunge wakongwe pekee.

"Nashangaa kumuona Mbunge kama Mbowe mwenye umaarufu mkubwa anataka aonekane 'live' bungeni, wakati hata mdogo wangu wa miaka sita anamfuhamu vizuri, wabunge vijana ndiyo waliopaswa kulalamikia hili,"

Kama mwananchi wa kawaida unapenda kumwambia nini mbunge huyu
87613147d1f35505f5a4bb3c1e96a63b.jpg

chanzo EAST AFRICA RADIO
Beneficiary wa mfumo hawezi kuongea nje ya hapo. Lakini ni bora kukaa kimya kuliko kuongea mambo ya ovyo. Siyo Wapinzani peke yao wanataka kupata ngoma mbichi kutoka Bungeni. Lakini kwa kuwa Watanzania wamekaa kiushabiki wa vyama, siyo mbaya kusikia leo mtu wa CCM kasema lile, mwingine wa CHADEMA kasema hili, siyo kwa FAVOR ya nchi bali Chama. Ajabu kabisa!
 
Mea culpa
Mea culpa
Mea culpa
Samahani,huwa napandishwa munkari na uongo WA maccm
Hata hivyo viti maalum Chadema safari hii vimetawanywa nchi nzima na wanaouhusiano na viongozi Ni wawili tuu na waKaskazini hawazidi 10%


Sawa, lakini kwa sisi wafuatiliaji na hata wewe ukifuatilia utagundua kuwa pamoja na kutawanywa nchi nzima lakini wako baadhi ya hao wa viti maalum pamoja na kutoka katika mikoa hiyo lakini asili yao ni eneo moja la nchi. Kuna mkoa Fulani kusini mwa nchi yetu baadhi ya wanaChadema walilalamika kuwa inakuwaje mbunge wa viti maalum atoke katika eneo jingine la nchi na kwenda kupandikizwa kwao. Malalamiko ni mengi ndani ya CHADEMA kuhusu tuhuma za upendeleo.

Ni wazi demokrasia ndani ya CHADEMA ni bado sana. Ni kweli CCM ina udhaifu wake lakini katika hili la demokrasia ni afadhali kuliko CHADEMA na vyama vingine vya upinzani.

Ila point muhimu ni kwamba mjadala ndani ya JF uwe kwa hoja na siyo matusi wala udhalilishaji. Ila kinachotokea ni baadhi ya wanachama na hasa waliojiunga katika miaka ya hivi karibuni kuendekeza matusi badala ya hoja. Vitendo hivi vinaishusha hadhi JF mtandao ambao nadhani una nafasi kubwa sana katika nchi yetu katika kubadilishana habari na kuelimishana.
 
Ni ajabu sana unapokuwa na elimu halfu elimu hiyo haikusaidii kuelewa na kupambanua mambo.
Lengo la elimu hasa ya juu ni kumwezesha mtu kuyatawala mazingira kwa kuhoji na kupambanua mambo kwa weledi.
Nina wasiwasi na uwezo wake wa kufikiri. Nadhani hawa ndio wale wanaopitishwa kwa kubebwa.
Kwa nini hamuigi mfano wa aliyekuwa mbunge wa viti maalum ktk bunge lililopita Ester bulaya!

Shame on her!
 
Kuwa CCM lazima ujitoe ufahamu
Kuwa upinzani lazima uwe mnafiki, kabla ya Lowasa kuhamia CHADEMA, tulihaminishwa na CHADEMA /Ukawa, tatizo la Nchi ufisadi, baada ya Lowasa kuhamia CHADEMA, na CCM Kumpata Dr Magufuli, mzalendo wa kweli, upinzani ajenda yao imebadillika, wanasema tatizo la Nchi mfumo, mfumo, mfumo
 
mawazo kama baba yetu hutaki watu wawe na TV huku kwako unayo! Information is power! we need be informed so to become powerful as a nation!

Acheni blabla na kulirudisha nyuma taifa kwa hoja mfu
Sasa ukiliona live kwenye TV furaha yako itakuwa nini? Mimi nafikiri nikimwona mbunge wangu jimboni anahimiza maendeleo ni afya zaidi kwasababu nitajua kuwa anawajibika badala ya kuonyesha sura zenye kutoka mapovu bungeni!
 
Hao wananchi watavidai vp kama hawajaviona yanavyosemwa na mipango kabambe kutoka kwa serikali uko Bungeni?
Au wewe unataka wakae tu washtukie kuna watu wanakuja kuchimba maji?
Kwa mawazo yenu haya hamwezi kuwaletea wananchi maendeleo ata siku moja.
Kaka Mbunge anahimiza maendeleo katika jimbo lake la uchaguzi kwa kuwahimiza wananchi wake kushiriki katika shughuli za maendeleo walizoainisha kwa kipindi tajwa.Mbunge anafahamu kabisa ni miradi gani itatekelezwa katika jimbo lake kwavile yeye anahudhuria vikao vikao vyote kuanzia wilaya hadi mkoa! Hayo maendeleo hayawezi kukwama kwasababu tu bunge halionyeshwi live!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom