Mzee wa Twitter
JF-Expert Member
- Nov 5, 2023
- 1,455
- 2,281
Wadau nawasabahi.
Uchaguzi ndio huo unakaribia. CHADEMA wameshinda pambano lao dhidi ya Halima Mdee na kundi lake kwa kuishawishi Mahakama Kuu kuthibitisha uhalali wao wa kuwafukuza Halima Mdee na kundi lake uanachama.
Pia, CHADEMA wametekeleza wajibu wa kikatiba kulijulisha Bunge na Tume ya Uchaguzi kuwa Halima Mdee na kundi lake sio wanachama wao kikatiba, hivyo hawastahili kuwa bungeni. Lakini bunge, serikali, na tume ya uchaguzi kwa pamoja wameamua kuvunja katiba kwa makusudi kwa kuendelea kuwalipa mishahara na posho kinyume na sheria kwa mujibu wa katiba. Kwani katiba inasema moja ya sababu za mbunge kupoteza ubunge wake ni "kufukuzwa uanachama na chama chake".
Hakika, bunge letu limeweka historia ya kuwa "Bunge lenye wabunge wasio na chama".
Najiuliza, nini hatima ya Halima Mdee na kundi lake baada ya bunge kuvunjwa?
Je, watajiunga na CCM?
Je, watajiunga na vyama vingine ila sio CHADEMA?
Je, CCM itawateua kama wabunge wa viti maalum?
Au watastaafu siasa?
Ngoja tusubiri 2025.