Halima Bulembo: Bunge si lazima kuonekana live

Halima Bulembo: Bunge si lazima kuonekana live

Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Halima Bulembo anasema anaunga mkono bunge kutorushwa live na kusema kurushwa live bunge kuna faida kwa wabunge wakongwe pekee.

"Nashangaa kumuona Mbunge kama Mbowe mwenye umaarufu mkubwa anataka aonekane 'live' bungeni, wakati hata mdogo wangu wa miaka sita anamfuhamu vizuri, wabunge vijana ndiyo waliopaswa kulalamikia hili,"

Kama mwananchi wa kawaida unapenda kumwambia nini mbunge huyu
87613147d1f35505f5a4bb3c1e96a63b.jpg

chanzo EAST AFRICA RADIO
Kwani Ishu ni kuonekana,Dada usijifanye wewe ni kipofu au kiziwi Dada.
 
Ana akili nyingi kama baba yake Dr. Alhaji Abdallah Bulembo (pZd)
 
ndo uwezo wa kufikiri wa think tank wa ccm ulipoishia.

eti huyo nae anawakilisha wananchi,,,,,hii nchi inavituko sana.
 
Huyu ni mojawapo ya wabunge wanaojielewa! Tatizo kubwa la wananchi ni afya, makazi bora,elimu, miundombinu, maji,utatuzi wa migogoro ya ardhi kati ya wakulima na wafugaji na siyo kuangalia tv kama haitaleta suluhisho kwa matatizo yetu!

Hao wananchi watavidai vp kama hawajaviona yanavyosemwa na mipango kabambe kutoka kwa serikali uko Bungeni?
Au wewe unataka wakae tu washtukie kuna watu wanakuja kuchimba maji?
Kwa mawazo yenu haya hamwezi kuwaletea wananchi maendeleo ata siku moja.
 
Ccm kuendelea kubaki madarakani ni janga la kitaifa coz ina rundo la vilaza ambao kufikir ni ziro
 
Sawa, lakini unasemaje kuhusu wabunge wa viti maalum wa CHADEMA na ambao asilimia kubwa wana uhusiano na viongozi wa ngazi za juu wa CHADEMA na ambao asilimia kubwa wanatoka eneo moja la nchi?
Tupe jedwali tujue unasema ukweli na sio kupumua hewa chafu
 
Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Halima Bulembo anasema anaunga mkono bunge kutorushwa live na kusema kurushwa live bunge kuna faida kwa wabunge wakongwe pekee.

"Nashangaa kumuona Mbunge kama Mbowe mwenye umaarufu mkubwa anataka aonekane 'live' bungeni, wakati hata mdogo wangu wa miaka sita anamfuhamu vizuri, wabunge vijana ndiyo waliopaswa kulalamikia hili,"

Kama mwananchi wa kawaida unapenda kumwambia nini mbunge huyu
87613147d1f35505f5a4bb3c1e96a63b.jpg

chanzo EAST AFRICA RADIO
Nkubaliana nae. Lakini mimi sioni umuhimu pia wa kuonesha " LIVE" kipindi cha maswali na majibu kwa vile ni sehemu ya bunge. Inachekesha kuwaona mawaziri kuyasoma tena majibu ambayo tayari ameshajibu na nakala kumpa muuliza swali. Hakuna haja ya waziri ya kuja na kujitekenya mwenyewe. Zuia matangazo yote ya bunge kabisa na pesa zitakazookolewa ziende kwenye mbio za mwenge.
 
Binti wa miaka 24 halafu wa CCM utafikiri ataklua na uwezo gani wa kufikiri? Halafu eti CHADEMA kuna undugu, hivi huu wa CCM sio undugu? Hahahahahaha nimekubali kweli CCM ni Slow learners wa makusudi

Najaribu kumlinganisha na Lucy Owenya.......mzani karibu unitoe ngeu

totetude-tilted-scale.svg
 
Tupe jedwali tujue unasema ukweli na sio kupumua hewa chafu
Jedwali la nini, kivava...Let me ask you one more thing comrade kivava: Je, angekuwa ni baba yako ameandika andiko lile nililoandika mimi, ungeweza kumwandikia kuwa "tupe jedwali tujue unasema ukweli na sio kupumua hewa chafu". Nimekuuliza hivi kwa kuwa wengi humu JF wanatumia ID ambazo hazijulikani na wana heshima yao katika jamii hii. Wanaandika humu ndani ya JF kwa sababu nyingi na moja ya hizo ni kubadilishana mawazo, kuelimishana na kupashana habari. Ila inaelekea watu kama wewe kivava mnachukulia JF kama sehemu ya mzaha, matusi, kejeli na kudhalilisha wengine...ushauri wangu kwako ni kuwa ikiwa hukubaliani na hoja ya mwenzio huna sababu ya kutukana wala kumdhalilisha au kumkejeli. Jenga hoja yako dhidi yake kama sababu na mkakati wa kushinda mjadala kwa hoja na siyo matusi.
 
Huyu ni mojawapo ya wabunge wanaojielewa! Tatizo kubwa la wananchi ni afya, makazi bora,elimu, miundombinu, maji,utatuzi wa migogoro ya ardhi kati ya wakulima na wafugaji na siyo kuangalia tv kama haitaleta suluhisho kwa matatizo yetu!
mawazo kama baba yetu hutaki watu wawe na TV huku kwako unayo! Information is power! we need be informed so to become powerful as a nation!

Acheni blabla na kulirudisha nyuma taifa kwa hoja mfu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom