Sema tuuuuuu baaasi ni kitu ambacho nikikisema natonekana nina nongwa,
Hivi haya maviti maaalumu yanaliingizia hasara shilingi ngapi kwa mwaka,,????
Tubatafuta majipu huku tumekalia MAKANSA sasa sijui
Najua nafasi ya viti maalumu iliwekwa kwa nia njema,, mi naona kubwa zaidi ni kuhakikisha kua awekwe ili afanye vizuri wanainchi walomunyima kura wamuone ili awamu inayofuata achukue kiti rasmi.
Lakini sasa zimekua mzigo kwa taifa,, kwani sijawahi kuona mchango wowote uliotoka kwenye nafasi hii ya kuteuliwa zaidi ya kuongeza neno ndiooooooooo hata kwa upuuuzi wa aliyemteua.
Wanakuja kupunguza kasi ya kujadili vitu vya msingi kwani wao hua huishia tuu kusifia hata kama wanajua sio sawa, na nadhani wao huenda bungeni kupiga kampeni za kupata nafasi hii ya viti vya kuteuliwa na kuingiza serikali hasara kubwa,,
Ikiwezekana, japo najua kua ni ngumu, halitumbuliki kwani sio jipu bali ni kansa,, wacha litutafune mpaka baaaasi
Ukiwa unajua unachokifanya huwezi simama na kisura chako kizuri et unasapoti bunge lisirushwe,, si ni upuuuzi huo??