Hali tete thamani ya Shilingi ya Tanzania ukilinganisha na Dola ya Marekani kwa kipindi linganifu cha mwaka mmoja uliopita (2020)

Chetikungu

Member
May 22, 2018
15
29
Wanajamvi, salaam

Naenda moja kwa moja kwenye point

Hali halisi ya thamani ya pesa yetu inazidi kushuka kwa kasi sanaa ukilinganisha na miaka kadhaa iliopita, ukichukua takwimu za Benki kuu (BOT) kwa haraka tu utaona na kudhibitisha hayo, ukiangalia kwa mwezi July mpaka August 2020 utagundua kulikua na mabadiliko chanya kwenye thamani ya shilingi, tarehe 23 July Dola moja ya Marekani ilikua na thaman ya Tsh 2,309.37, mpaka kufikia tarehe 10 Aug 2020 thamani ya shiling ilipanda na kufikia 2,309.16, hii inamaanisha thamani ya pesa yetu sokoni ilikua kubwa na iliimarika zaidi.

1628681800735.png

Sasa njoo kipindi kama hicho kwa mwaka 2021, tarehe 23 Jul, Dola moja ilikua na thaman ya Tsh 2,310.62, mpaka kufikia tarehe 10 Aug 2021 thamani ya shilingi ilishuka na kufikia 2,310.78, hali hyo ni mbaya sana kiuchumi kwa ujumla, hilo ni anguko la thamani ya pesa yetu, natambua thamani ya pesa haiwezi kua static lakini haiwezi kua inabadilika kila siku, kwa kipindi hiki tulichopo ni wazi sasa thamani ya shiling ya Tanzania kila siku inashuka kwa centi moja, hilo ni anguko, kuna haja ya kupitia sera zetu na kujaribu kucontrol upandishwaji holela wa bei za bidhaa.


July -Aug 2021.PNG

Wadau maoni yenu kwenye hili..

july-aug 2020.PNG
 
Walipomkamata mbowe
Na serikali kuingilia Uhuru Wa mahakama na kuongeza kodi kwenye miamala
Ndio thamani ya shilingi ilipoanzia kuporomoka kwa spidi
Kama hawaamini wamwachie Leo waone
 
Hili ni anguko digo sana lisijutishe.
Ongezeko la senti 10 hadi 50 nikawaida.

Kama unafuatilia Financial movement katik soko la Dunia hiyo movement bado ni ndogo na inaonesha uchumi wetu bado uko STABLE
 
Wee unawazimu. Hakuna wakati ambao shilingi ilikuwa stable ktk historia ya Tanzania kama katika kipindi tajwa. Tuache siasa katika kila kitu.
 
Back
Top Bottom