Ndondocha mkuu

JF-Expert Member
Feb 17, 2014
2,354
2,763
Habari ya jion wana JF,

Ni miezi kadhaa tangu niandike uzi wangu mara ya mwisho ndani ya jf, ni katika harakati za kuendelea kupambana na maisha ya mtaani hasa kwa sisi graduates.

Nikiwa nimekaa mahali napo patia ridhiki juzi nilipitiwa na dogo ambaye nilimuacha akiwa first year pale SUA akiwa na baiskeli mpya aliyonunua kwa thamani ya sh 180,000, alifurah kuonana tena huku shauku yake kubwa ni kuniambia kwanini amerud songea kutokea dsm

Nilifurah baada ya kuniambia lengo kubwa la kurud na kununua baiskeli ni kuweza kuanza kununua mahindi kijijin walau dumla 10 kwa siku na kuuza mjn kwa faida ya sh 500 kwa kila dumla, nilifurah kuona uthubutu wake , na kuona ameficha aibu mfukon na kuamua kufanya kitu ambacho mtu aliyesomanae na akufaulu moja kwa moja atamcheka.

Aliendelea kwa kusema alipomaliza chuo ilimchukua miezi 4 kupata kiasi cha sh 300000 ambacho pia amegawa kununua usafiri.

Na haya ndio maisha yetu graduates.Nilikumbuka baada ya kumliza elimu yangu niliweza kufanya kazi kama kuuza mchanga mgumu lakini yote ni kuepuka kukaa ndani pasipo kazi at least kuweza kuingiza kipato.

Kuna muda huwa nasema maisha hayana huruma na hayapo fair , ukikaa mtaani bila pesa haya unajionea, hasa kukaa bila shughuli, dharau,kejeli, maneno , na hasa wakijua ni mtu uliyekua bora darasani, lakini kwenye kitabu cha benjamin mkapa aliwah sema ' Epuka watu wenye maneno ,kelele na wvu, na usijilinganishe na mtu yeyote katika maisha kwasabbu unaweza ukaumia zaidi'

Tunapitia mengi sana mbaka kufikia mafanikio, ela ni muhimu sana katika maisha, tuzidi kupambana, maisha hayana huruma. Unakuta umetulia kijiwe anakuja mtu anataka ww ndio uanze kumchangamkia kwasabbu tu yeye amepaki gari lake pale na anajua huna kitu tu mfukoni.

Hakuna asiyependa maisha mazuri, panapowezekana tushikane mkono ili maisha yaendelee.

Let love lead.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom