Halahala usimle kuku na mayai yake!

Halahala usimle kuku na mayai yake!

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Posts
219,502
Reaction score
911,255
Acha kujivunia aibu yako
Acha kula kuku na watoto
Acha kuku, kula mayai tu
Acha ubabaishaji wako
Acha, nasema wacha kabisa!
Halahala usimle kuku na mayai yake!

Visingizio vyako nimevikataa kabisa
Katu siafiki huo utetezi wako
Kamwe sitabariki uzandiki huo
Eti yote ni halali yako pia!
Nani kakudanganya hivyo?
Halahala usimle kuku na mayai yake!

Ukitaka maisha marefu, usimle kuku
Ukitaka amani, usimuibe kuku wa watu!
Ukitaka heshima, tafuna yai lake tu!
Ukitaka jina, mwache akutagie mengine
Ukitaka suluhu, mnusuru kuku akutagie
Halahala usimle kuku na mayai yake!

Wanaokula kuku na mayai yake wamelaaniwa
Wasiomwonea huruma kuku ni walafi hao tu
Wasiomjali kuku wamejikosesha mayai yake
Wasiomlinda kuku kututoka kabla ya siku zao!
Wanaoabudu matumbo yao humeza kila kitu!
Halahala usimle kuku na mayai yake!

Waliomtafuna kuku na mayai yake ni wafu!
Kama bado wako hai basi wanasuasua tu!
Kama wako barabarani basi wanachechemea tu!
Kama hawachechemei basi wanameza tunguri tu!
Kama hawamezi ndunga basi ni teja wa mengineyo!
Halahala usimle kuku na mayai yake!
 
wacha kweli,wenzio wala pasi na kifani.
Watu wanajilia,huku nyama,kule mayai na viazi.

Watafanyaje unafikiri?

Tena Imany John umenikumbusha hiki kipindi cha sikukuu........kuku wengi wanachinjwa na mayai yanaliwa haifai kabisa............waaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaache huo upuuuuuuuuuuuuuuuuuzi
 
Last edited by a moderator:
Mpwaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa, sema wewe bhana, kuku mchokozi, yai mchokozi na kifaranga sasa mie nifanyeje? Maadili yakataza, Jamii haikubali lakini hali ya sasa ni tete sana Mpwa, nimependa sana mashairi yako hasa lile la juzi la kusuguana lile...........
 
Mwanasheria wewe ni very clever,
kuna jamaa pale mbeya alimla kuku na mayai yake siyo yai lake ni mayai yake
tena akawa anatamba bila aibu mbele za wenzie,

tena hii inafanya hata watu ..... anyway nitasema baadae.
 
Mpwaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa, sema wewe bhana, kuku mchokozi, yai mchokozi na kifaranga sasa mie nifanyeje? Maadili yakataza, Jamii haikubali lakini hali ya sasa ni tete sana Mpwa, nimependa sana mashairi yako hasa lile la juzi la kusuguana lile...........

Elli.........nasema wachaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
 
Last edited by a moderator:
Mwanasheria wewe ni very clever,
kuna jamaa pale mbeya alimla kuku na mayai yake siyo yai lake ni mayai yake
tena akawa anatamba bila aibu mbele za wenzie,

tena hii inafanya hata watu ..... anyway nitasema baadae.

Mamndenyi huyo mharibifu yuko wapi sasa? Hachechemei kweli?
 
Last edited by a moderator:
Raha ya kuku umle na mayai yake!

MESTOD Raha nyingine zimelaaniwa kabisa..........waaaaaaaacha kabisa. Siyo kila vitamu mdomoni vyafaa kuliwa.............
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom