Lycaon pictus
JF-Expert Member
- Jan 31, 2021
- 7,221
- 12,726
Ukisoma historia ya dunia toka mwanzo utaona kuwa kila kabila la watu lilikuwa na nchi yake. Habari ya makabila mengi kuwa nchi moja ilitokea pale kabila moja kuteka jingine na kulifanya kuwa chini yao. Na hilo lilileta unyonyaji na ubaguzi. Hata wazungu ambao tunaona wamestaarabika wana ubaguzi wa kikabila hadi leo. Waflemish na Wafaransa huko Ubelgiji haviivi. Wabritish na wascottish na wairish nao haviivi. Wacanada wanaoongea Kiingereza na wale wanaaongea Kifaransa hawako bado sawa.
Wazungu walipounda mataifa ya Afrika lengo halikuwa kuunganisha makabila mbalimbali. Lengo lilikuwa kujimegea maeneo makubwamakubwa ya kutawala. Hata wakati wa ukoloni, makabila haya hayakujiona kuwa ni nchi moja. Ndiyo maana walijitambulisha kama Nchi ya Ugogo, Nchi ya Unyamwezi, Uchagga nk nk. tulipopata uhuru ndipo walilazimika kujitambua kama nchi yenye makabila mengi.
Tokea nchi za kiafrika zianze kupata uhuru, miaka 60+ iliyopita, zoezi la kuunda nchi za makabila mengi limekuwa gumu kupita kiasi. Naweza sema ni Tanzania pekee walau imepiga hatua kidogo katika hilo. Nchi zingine imeshindikana kabisa. Rwanda walichinjana kikatili sababu hiyo. Ethiopia bado wapo vitani, Darfur watu walichinjwa kama wanyama. Nigeria haieleweki hata kidogo. Angalia karibu kila taifa la Afrika utaona kuwa zoezi la kuunda nchi ya watu wa makabila tofauti limeshindikana kabisa.
Ukiangalia hali halisi utaona kuwa Nchi ya makabila mengi haiwezi kuwa sawa, na kuwa kila kabila lilipaswa kuwa nchi, kama ilivyokuwa kwa maelfu ya miaka.