Tukiacha ushabiki na kulishwa maneno kama majibu ya maswali yote mawili kwako ni "Ndiyo" basi unatakiwa kuunga mkono dual citizenship kwa wazawa wa Tanzania
1. Je unataka Watanzania wazawa ambao wako nje (Disapora) wapate haki sawa kwenye jumuia ya Africa mashariki kama wenzao wa Kenya na nchi nyingine? Kwa sheria za sasa diaspora wa kenya ana haki nyingi Tanzania kuliko diaspora ambaye ni mzawa wa Tanzania kwasababu diaspora wa Kenya anakuja kama Raia wa Kenya na huyu wa Tanzania anakuja kama mgeni/tourist.
2. Je unataka Watanzania Dispora huko walipo wawe ha haki sawa kama diaspora wa nchi nyingine?.
Hakuna Mtanzania namjua mimi amewahi kukana Uraia. Kukana Uraia ni utaratibu ambao una kuwa na barua ha hati ya kukana au kiapo cha kukana. Sifahamu mtu ambaye amekana Uraia wa Tanzania. Sheria ya Tanzania ndiyo inalazimisha neno Kukana na hii ndiyo kesi iliyopo mahakamani.
Uraia wa huko wanapoishi utawasaidia mambo ya msingi kama
(1) Kupata kazi nzuri
(2) Kupata bima za maisha
(3) Kuweza kusomesha watoto
(4) Kuhakikisha uwekezaji wao unalindwa kisheria.
Ngoja niwape mfano mdogo mimi binafsi mke wangu ambaye hakuwa na Uraia wa USA alikuwa na kuumwa sawa baada ya kumleta kutoka Tanzania. Tulipoenda Hospitali wakasema ni lazima afanyiwe operesheni haraka sana Vipimo tu vilikuwa $30,000 lakini operesheni ilikuwa $235,000. Mimi kwasababu ya bima yangu ambayo nisingeweza kuipata kama nisingekuwa Raia nililipia $3,000 tu na sio $265,000 ambazo ni gharama halisi. Hata Watanzania wenzangu wasingeweza kunisaidia.
Hizi ndiyo sababu kubwa za diaspora kuchukuwa Uraia wa nchi nyingine. Huwezi kukaa sehemu unafanya kazi usaidie familia nyumbani halafu tena kuna haki huna wakati wenzako wa kenya ambao mnashindana kwenye kazi hizo hizo wana haki zote. Hivyo badala ya kulishwa maneno tuwaulize kwanza diaspora ni kwanini wamechukuwa Uraia wa nchi wanazokaa na majibu kwa wanaojua sio ya kibinafsi bali ni ya kifamilia.
Hii ndiyo sababu umeona mabalozi wengi wa Tanzania wanaunga mkono kwasababu wanaelewa maisha halisi ya huku.