Mnaosherehekea Hadhi Maalum kwa Diaspora hamjaangalia upande wa pili wa sarafu

mtanzania in exile

JF-Expert Member
Feb 17, 2012
1,335
1,183
Wana Diaspora

Nimeona ndugu zetu wengi sana hususan wale waliopo USA wanasherehekea sana juu ya ujio wa Hadhi maalum kwa diaspora, kiasi kwamba nahisi mnashindwa kuangalia upande wa pili wa sauli hili. Kwa sababu hiyo basi naomba kuweka point chache tu ambazo tunabidi sote tuzielewe.

Kwanza kabisa kwa miaka mingi sana tu sasa tumekuwa tukipigania turuhusiwe kuwa na uraia pacha. Turuhusiwe kubaki kujulikana kisheria kama ni watanzania asilia. Kuna watu wamekuwa wanasema kuwa haiwezekani kwa sababu tumeukana uraia wa nchi ya asili yetu, jambo ambalo sio kweli. Hakuna mtu ambae alichukua uraia wa nchi nyengine (mfano USA, UK, France na kwengineka) na akatowa kiapo cha kuukataa uzawa wake au uraia wake. Nimeweka pont hii hapa sio kwa lengo la kuijadili leo ila ni kuwakumbusha tu wana diaspora kwa nini tunapigania uraia pacha.

Sasa ukiangalia hadhi maalum, ambayo wengi wetu mnaisherehekea, haibadilishi lolote juu ya kukataliwa kuwa sie tuliochukuwa uraia wa nchi nyengine ni kuwa si watanzania tena! Hadhi maalumu itatutambua kuwa sisi tuna asili ya tanzania lakini si watanzania. Moja ya masharti ya hadhi maalumu ni tutakiwa ku renew hadhi hii kila mara baada ya miaka mitano au kumi (hawajaamua ni miaka mingapi yet bali ni 5 au 10). Sasa kama sisi ni watanzania ni kwa nini tuwe tuna renew utanzania wetu kila baada ya muda fulani? Kwani watanzania wote waliokuwepo nchini nao hufanya renew ya uraia wao kila baada ya muda fulani? Jawabu ni hapa na hiyo inadhihirisha kuwa serikali bado haitutambui diaspora kama watanzania.

Wanaposema kuwa hadhi maalum itatufanya tuwe na haki sawa kama raia wote wa Tanzania, hilo sio kweli kwa sababu ukiwa na hadhi maalumu serikali inaweza wakati wowote kukuvua hadhi maalum kwa sababu zozote zile na inaweza kukufukuza nchini. tafauti kama tukiwa na uraia kamili, serikali haiwezi kumvua uraia mtanzania alikuwepo nyumbani mwenye asili ya Tanzania kwa sababu yeyote ile. Serikali inaweza kumkatalia raia wake kupata passport ya kusafiria lakini haiwezi kumfukuza raia wake nchi mwake.

Kuna wenzwetu mnasherehekea kuwa tutaingia Tanzania bila ya visa, big deal! $50 sio saving kubwa ya kutufanya tusherehekee kama tumepata ushindi gani sijui.

Hii point ya kuwa eti hadhi maalum itawapatia haki za kurithi na kumiliki ardhi n.k sio kweli hata kidogo. Let just be honest here, tupo watanzania chungu nzima huku diaspora ambao tumerithi mali za wazee wetu nyumbani na tunamiliki viwanja na tumejenga, na kila anaetujua anajua kuwa tuna mali zetu Tanzania na sio siri hata kidogo. Hii sheria ya kutuzuia haya hata sijui iko wapi na sijapatapo kusikia hata mara moja kuwa mwana diaspora amepokonywa au amepoteza mali yake kwa sababu ya sheria ya uraia. Kwa Hadhi maalum haibadilishi kitu hapa.

Halafu kuna mheshimiwa fulani alisimama na kusema kuwa kuna nchi kadhaa ambazo haziruhusu uraia pacha ila unaruhusu hadhi maalum, Mheshiwa huyu kwa makusudi mazima na kwa kujua kabisa aliamua kusema ukweli nusu. Aliamua kutosema kuwa kuna nchi ambazo haziruhusu uraia pacha badala yake wanaruhusu hadhi maalum kwa raia wasiokuwa wa nchi yao. Yaani mfano mchina hawezi kuwa na passport ya china na pia ya nchi xyz, lakini wananchi wa nchi ya xyz wanaweza kuwa na passport za china (for example) wakitaka kuwa nazo.

Hivi ndivyo ambavyo ilikuwa na Tanzania ifanye, wageni wanapotaka kuishi indefinitely Tanzania ndio wanapewa hadhi maalum baada ya kukamilisha masharti ya uhamiaji na sio wazawa wa asili ya Tanzania.
 
Aisee!

Ni sawa na mzazi kumbadilishia mtoto wake hadhi ya kimahusiano kisa kaoa au kaololewa. Kwamba mahusiano yao siyo kama ya awali ya mzazi na mtoto, na hivyo kila baada ya miaka kadhaa, hutakiwa kusaini hati inayoonesha aina mpya ya mahusiano yao.

Mzazi unamkataaje mwanao kisa kaingia kwenye ndoa?
 
Mkubaliane tu na huo ukweli. Uzuri mmepewa muda wa kujitathmini. Na isiwe zaidi ya 5 yrs. Quid pro quo
 
Samahani, sijakufahamu hapa. Tukubaliane na ukweli gani? Ukweli wa kitu gani hasa unaoukusudia? Nashindwa kuona point yako ya neno ukweli hapa inahusiana vipi?
 
Back
Top Bottom