Hakuna mwenye akili timamu atakayemuamini Mbowe na Chadema kuchangia hela? Kwanini hazindui ujenzi Arusha au Moshi?

Status
Not open for further replies.

Wakudadavuwa

JF-Expert Member
Feb 17, 2016
17,506
15,997
Ndugu zangu,

Maajabu hayaishi,miaka michache iliyopita Mbowe alinifaika na ongezeko kubwa la ruzuku kila aliposhauriwa ajenge ofisi yeye na wasaidizi wake walitoa maneno makali eti "chama cha siasa sio jengo au nyumba bali ni imani".

Makamanda badala ya kuhoji walishangilia kwa furaha wakijinasibu kuwa "siasa kwao si ofisi bali ni imani.Pia ikumbukwe shilingi milioni 200 zilizotolewa na Mzee Sabodo kujenga ofisi ziliyeyuka bila maelezo.Nani atawaamini tena Chadema?

Siku za karibuni amezindua kadi zenye hadhi tofauti huku ile ya hadhi ya juu ikiwa na thamani ya shilingi 200,000 huku akijinasibu kuwa makamanda hawana mshahara kwa miezi sita nani ataweza kuchangia?ikumbukwe EL ndiye alikuja na wafuasi waliokuwa na uwezo angalau kuchanga chochote lakini sio makamanda hawa tunawajua.

Halafu Mbowe alivyomjanja haya mambo ya kuchangia chama au ujenzi wa ofisi anazungumza akiwa Shinyanga anajua akizunguza haya maneno Moshi au Arusha ataambulia vitasa.

Nimalize kwa kusema "ajizi nyumba ya njaa".
 
Wewe endelea kudadavua wakati wenzako tunasonga, kwani kudadavua na kufikiri ndani ya box ni kitu kimoja,acha wenye uwezo wa kufikiri hata nje ya box wafikiri kwa maono yao.kumbuka wenyewe hawakabidhi akili zao wanopofika getini.
 
Kamanda pole
Wewe endelea kudadavua wakati wenzako tunasonga,kwani kudadavua na kufikiri ndani ya box ni kitu kimoja,acha wenye uwezo wa kufikiri hata nje ya box wafikiri kwa maono yao.kumbuka wenyewe hawakabidhi akili zao wanopofika getini.
 
Nimemsikia Freeman Mbowe Mara kadhaa katika ziara zake amejikita sana katika kukosoa utawala wa Mwendazake Magufuli kuliko kujikita katika current issue za sasa.

Mbowe ameenda mbali zaidi kiasi cha kutetea ukanda flani huku akijua vyema hizo ajenda zinamshushia alama za kiongozi mwenye focus na umoja wa kitaifa na mahikamano.

Vyovyote Magufuli alivyokua kwa hadhi ya Mbowe hakupaswa kuzunguka kuyasema madhaifu yake kwani kwa cheo chake Marehemu si ajenda tena, Magufuli hawezi kurudi na hata kwa aliyoyafanya umma hauwezi kumwadhibu maana hana ijara tena katika ulimwengu huu.

Mbowe kazi ya kusema mambo ya hayati tuachie sisi watu wa mitandaoni kwa nafasi yako hayatakusaidia. Njoo na mikakati mipya na ajenda mpya za sasa kama chama ili wananchi tutembee nazo.
 
Ila Mbowe ipo siku atasababisha watu kujinyonga, chadema ni imani pamoja na KADI za viwango tofauti wapo pia wanachama watapenda changia mpaka mamilion,na tegemea hizo KADI za laki mbili kuchukuliwa Sana kuliko zingine
 
Huyu Mwenyekiti "mfalme" anajishushia sana heshima.

Hivi si huyu ambaye alimuombea msamaha yule ndugu aliyemsema hayati Mzee Mengi?

Leo hii anayarudia yaleyale.

Hivi kwa heshima yake aliyojijengea ndio KUMFANYIA KEDI ,DHIHAKA na KUMSEMA mwendazake JPM?

Hivi hili anadhania ni DOGO?!!

Muda UTAONGEA.....

#KaziIendelee
 
Logic watu tunataka katiba, tume huru, utawala wa sheria , uchumi wa watu na mapandano dhidi ya rushwa na ufisadi.

Bado hakuna rais mwenye nia ya dhati hiyo mbowe anatakiwa kufocus kwenye mambo yanayokuja sio kudeal na past event

Hakuna ambaye aelewi kwamba aliteseka ila yamepita

Mbowe anafanya kosa la kiufundi kumsema mtu ambaye hayupo hai tena kujitetea
 
Ya Maghufuli yashapita bhana , yeye aendelee Tu kumsema jamaa atakuja kustukia na yeye mda wa kupita umefika ....huku Dunia na Tanzania zikiendelea kusonga mbele
 
Logic watu tunataka katiba, tume huru, utawala wa sheria , uchumi wa watu na mapandano dhidi ya rushwa na ufisadi...
Binafsi naona anapoteza muda kwakua kwanza anayemsema au kumfanya ajenda hawezi kurudi, pili nature ya watanzania ni kusahau sasa sijui itamsaidia nini badala ya ku focus kwenye issue za msingi.
 
Hakuna kosa lolote kisheria kumsema marehemu iwe vibaya au vizuri, ndio maana akina Nyerere, mitume kama Yesu Muhammad nk wanasemwa vizuri na vibaya.

Mbowe kaumizwa sana na utawala wa mwendazake mwacheni apumue apate ahueni, kwa upande mwingine anasaidia kueleza ubaya wa mwendazake amabao ulifunikwa na propaganda za uongo na kuonya utawala uliopo kutorudia makosa yaliyopita.

Tunatambua wafuasi wa Magufuli ampendi kuona magufuli akisemwa vibaya na watu makini Kama mbowe, kwa hiyo nyinyi fanyeni mambo yenu na mbowe muacheni na mambo yake, kwani akiaribikiwa yanawahusu nini?.
 
Hakuna mtu mwenye akili anayeweza kusikiliza na kuamini upotolo wako
 
Nimemsikia Freeman Mbowe Mara kadhaa katika ziara zake amejikita sana katika kukosoa utawala wa Mwendazake Magufuli kuliko kujikita katika current issue za sasa.

Mbowe ameenda mbali zaidi kiasi cha kutetea ukanda flani huku akijua vyema hizo ajenda zinamshushia alama za kiongozi mwenye focus na umoja wa kitaifa na mahikamano.

Vyovyote Magufuli alivyokua kwa hadhi ya Mbowe hakupaswa kuzunguka kuyasema madhaifu yake kwani kwa cheo chake Marehemu si ajenda tena, Magufuli hawezi kurudi na hata kwa aliyoyafanya umma hauwezi kumwadhibu maana hana ijara tena katika ulimwengu huu.

Mbowe kazi ya kusema mambo ya hayati tuachie sisi watu wa mitandaoni kwa nafasi yako hayatakusaidia. Njoo na mikakati mipya na ajenda mpya za sasa Kama chama ili wananchi tutembee nazo.
Amesemwa Nyerere atakuwa Magufuli...
Magufuli alikuwa mtu mwovu na genge lake bado lipo, asiposema litatokea jinamizi linguine hatari kuliko Magufuli, acha aseme..

Mfano Suala la Chato kuwa Jiji lilizungumzwa sana na wapiga vigelele wa genge lake sasa ivi hayo mambo yana surface, namshukuru Tibaijuka kasema Ukwel bila hiyana... eti tumnyamazie.. ili iweje na mipango yake 60% ilikuwa imeanza kukamilika... acha akemee bhana

Issue ya Kanda ya kaskazini kuonewa ni valid na haiwez kunyamaziwa ikapita hivi hivi.. siasa za chuki dhidi ya kabila nyingine ni mbaya kuliko hata chama cha siasa kushika Dola.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom