Hakuna Mtanzania atakayempigia kura ya ndio kiongozi aliyemletea tozo za miamala ya simu

Kiboko ya Jiwe

JF-Expert Member
Apr 7, 2020
12,702
36,127
Habari,

Endapo uchaguzi mkuu utafanyika leo au hiyo 2025, hakuna Mtanzania (ukiondoa tabaka tawala) atampigia kura kiongozi ambaye amemletea tozo za hovyo za miamala ya simu kienyeji. Muamala ambao mtu alikatwa shilingi 2700 sasa anakatwa karibu elfu tano nzima.

Mtanzania wa chini alikuwa akitumiwa elfu 10 ya mboga anatoa elfu tisa sasa anatoa elfu nane.

Huyu Mtanzania ambaye ndiye consumer wa huduma za simu ataambiwa nini ili asahaulishwe machungu haya?

Hapa sizungumzii CCM kurudi madarakani bali nazungumzia kupata kura za ndio.

Maana kupata kura ni jambo moja na kuingia madarakani ni jambo jingine pia.

Rafu walizozicheza CCM kwenye chaguzi za serikali za mitaa, uchaguzi mkuu na chaguzi ndogo ndizo zinazowafanya watutawale watakavyo wakijua kuwa wana uwezo wa kubaki madarakani tutake tusitake.
 
# Mh mwigulu nchemba malipo ya property tax kwa njia ya LUKU mbona hatuyaoni kwenye risiti zetu,sisi watanzania tulio wengi tunatamani malipo haya yaanze ili tuweze kuchangia serekali yetu tukufu.
 
Ndugu mtoa mada unawazungumzia waTanzania hawa hawa ambao wapo chini ya utawala wa CCM kwa zaidi ya miaka 50 au wengine?
 
Bila kuwadunda watawala Heshima haitokuja.

Eti wanasema Watanzania watazizoea kodi, eti kodi za kizalendo hizi ni dharau na matusi kabisa. Wamevimbiwa kodi zetu uropokwa maneno.

Watawala na watawaliwa walipigana ulaya heshima ikaja
 
Nani mwenye ushawishi atakayeongoza upinzani kuwatoa CCM?

Ili CCM itoke inahitaji mgombea kutoka upinzani mwenye ushawishi mkubwa sana, akisema tuandamane watu watoke barabarani bila kujali polisi wala jeshi. Sasa ni nani huyo?
 
Kura huwa hawapigiwi miaka yote tatizo walishatuambia hata tusipowachagua wao ndio watatangazwa washindi, Katiba Mpya inahitajika Tanzania hii haraka sana ili maamuzi ya watanzania wengi kwenye sanduku la kura yaheshimiwe.
 
Wanaouliza kwa nini Mbowe amekamatwa sasa na si vinginevyo wanasahau kuwa Mbowe, Lema, Meya wa zamani Ubungo Boniface walikamatwa mara baada ya matokeo ya uchaguzi mkuu kutangazwa na kabla Rais hajaapishwa kwa kuchochea maandamano yasiyo na kikomo kupinga matokeo. Mambosasa alihojiwa na vituo vya ITV na TBC na kutoa madai hayo hayo ya ugaidi.
 
Kwani 2020 hamjajifunza ? Nyie pigeni kura kwingine lakini CCM ndio itaenda kuunda serikali🐒
 
Habari!
Endapo uchaguzi mkuu utafanyika leo au hiyo 2025, hakuna Mtanzania (ukiondoa tabaka tawala) atampigia kura kiongozi ambaye amemletea tozo za hovyo za miamala ya simu kienyeji.
Muamala ambao mtu alikatwa shilingi 2700 sasa anakatwa karibu elfu tano nzima.
Mtanzania wa chini alikuwa akitumiwa elfu 10 ya mboga anatoa elfu tisa sasa anatoa elfu nane.
Huyu Mtanzania ambaye ndiye consumer wa huduma za simu ataambiwa nini ili asahaulishwe machungu haya?.
Hapa sizungumzii CCM kurudi madarakani bali nazungumzia kupata kura za ndio.
Maana kupata kura ni jambo moja na kuingia madarakani ni jambo jingine pia.
Rafu walizozicheza CCM kwenye chaguzi za serikali za mitaa, uchaguzi mkuu na chaguzi ndogo ndizo zinazowafanya watutawale watakavyo wakijua kuwa wana uwezo wa kubaki madarakani tutake tusitake.
Pamoja na wizi wa kura ccm in wachawi sana.
Uchawi unaofanya wananchi wasijitambue hasa wakati nyakati za chaguzi.

Hebu tafakari pamoja na Mimi,mtanzania hali yake ya maisha ni duni kabisa,kila bidhaa imepanda kwaajili ya mafuta kupanda,tozo za miamala juu,mbolea juu.
Elimu bure lakini mbovu,ccm watoto wao wanawalipia shule bora na wengine nje ya nchi.

Mtanzania huyohuyo akidanganywa anakubali kiulauniii kama maiti.
Ili uamini ccm in wachawi.
1. Nenda Dodoma makao makuu ccm utakuta kondoo wanalala pale verandani nje ukiwa unaingia mlango kuu.

Hawana mchungaji, wanatoka asubuhi na kurudi jioni.
2. Mwenge wa Uhuru, ccm hata uwapige shoka la kichwa ukiwataka waachane nao kwakuwa unatutia gharama isiyo ya lazima hawata kuelewa.

Hebu fikiria,mwaka huu sherehe nanenane hazikufanyika nchi nzima.
Naweza sema in sherehe za kiuchumi kwa MTU mmoja mmoja na taifa
kwa ujumla.
Wakulima wanaenda jifunza mbinu za kilimo,ufugaji na uvuvi.
Wanaenda pata mbegu mbora kwa bei nafuu,lakini zimezuiliwa kwasababu ya corona.

Je kwenye mwenve hakuna mkusanyiko wa watu?
Eti unakagua miradi ya maendeleo na kuifungu!!
Viongozi wanafanyakazi gani wakiwemo wabunge?
MWENGE WA CCM UNA KITU NDANI YAKE.

Sent from my TECNO CA7 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom