Hakuna malipo ya NSSF, PPF hadi umri wa kustaafu ufike!

Hakuna malipo ya NSSF, PPF hadi umri wa kustaafu ufike!

Haya ni matokeo ya serikali dhaifu na legelege ...................
 
huyo irene nasali naye kanisa la chuo kikuu! natamani kumpiga na yai visa nikimuona! kwann anapelekwa pelekwa tu na huyu kilaza jk, wate laanakum! ana watoto wawili wakike wadogo, labda atawapeleka nje ili yasiwapate haya, alikuwa stanbic, alivyoenda SSRA akamvuta na shogaye lightness mauki! na ye ni head wa kitu huko! pathetic, nawachukia jopo zima la hawa watu! wanatukandamiza bila sababu!
cacico mie nilivyo na hasira na ujinga wa hawa watu.
Kama wanauchungu na maisha ya Watanzania wakizeeka kwanini wanaangalia wafanyakazi tu hao wazee wa vijijini wenye hali ngumu kiuchumu wao wanawaangaliaje. Na iweje wakuu wa mikoa ,wabunge na wengineo hawahusiki kwenye mifuko hii
Kwani wao hawatazeeka.

Hebu watutolee Ujinga wao huu..haka ka dada Leo katakuwa kwetu watu wana hasira nako kama mpira wa kona ..
Yaani huu ni ujinga na upuuzi kama walijua hivi kwanini wasingetoa notification mapema kuwa ikifika 2012 kutakuwa na mabadiriko haya na haya ..akini wamepewa kufikiri wameshindwa kwanini wanajiamlia wao ???
 
sera hiyo imepitishwa na CCM, itakuwa kitanzi chao hapo 2015

Hata wabunge wetu wa CDM hawakulalamika walikaa kimya wakati muswada huo unapitishwa na kuwa sheria,baada wao kujihakikishia wanapata mafao yao baada miaka mitano ya ubunge kwisha!!!!!!!
 
Ni ni moja ya sheria za kipuzi na kijinga kuwahi kuwepo hapa nchini.
Mimi nadhani waliohusika katika kupitisha sheria hii hakuna hata mmoja inayemgusa.

Kuna mambo kadhaa ambayo tunahitaji majibu ya kina:

1. Nini mantiki ya kuwepo pesheni? Ikiwa ni kumsaidia mstaafu anapokuwa ameacha kazi, sheria hii itakuwa inapingana na hoja hii. Fikiria, viwango vya mishahara yetu. Endapo leo hii itatokea mtu akapoteza kazi kwa sababu yoyote akiwa na umri wa miaka let's say 30. Atatakiwa kuanza kudai hela yake baada ya miaka 25-30. Process inaweza kuchukua zaidi ya miaka 5, je thamani ya hela yake italingana na hali ya maisha ya wakati hou??

2. Ni wazi tangu jambo hili limewekwa hadharani, wafanyakazi ambao nio wadau wakuu wa kadhia hii wamekuwa na manung'uniko ya wazi, lakini waliohusika na kupitisha sheria hii wako kimya. Je, wanadhani malalamiko ya wafanyakazi si ya msingi? Basi watuwambie ni nani mnufaika wa jambo hili.

3.Je, wako tayari kukubali wanachama wote wa mifuko hii kupata hisa au kugawiwa vyumba katika majuma wanayootesha kama uyoga kila kukicha hapa nchini? Wao wanatumia hela zetu kujenga vitega uchumi vyao, vinawazalishia faida mara dufu, halafu wanataka watupatie hela zetu zikiwa zimeisha thamani. Vinginevyo sheria hii ilitakiwa kulitambua hili, kisha ielekeza kuanzishwa mfumo wa riba ili kutunza thamani ya pesa yetu baada ya hio miaka 55-66 wanayosema.

Mimi siku zote huwa nasema, nahitaji hela yangu leo kwa maendeleo yangu ya sasa. Maisha mazuri uzeeni hayatokani na pesheni, ila ni matokeo ya kutumia pesa vizuri wakati wa ujana. Kwamba nahitaji hela wakawa ujana ili nijiandalie maisha bora ya uzeeni. Haiwezekani kuboresha maisha ya uzeeni kwa kupewa pesa yako ikiwa imeishashuka thamani. Hivi tunatambua kama wastaafu wa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki wapo wanaodai shilingi hadi laki 3 tu! Kwa hiyo wanataka kutupatia pesheni ya shilingi milion 10 baada ya miaka 30 ijayo.Itanisaidia nini? Leo hii inaonekana ni kubwa lakini baada ya muda huo itakwa haina tija yoyote, maana itakuwa ni kama kodi ya miezi sita tu.

Ufike wakati jamani tusiendeshe mambo kinadharia namna hii. Tunajua rais akistaafu bado maisha yake yanakuwa salama hadi anapokufa. Na hata wabunge waliopikisha hii kitu, wengi wao ni wazee ambao wanategemea kupata hela yao kesho kutwa tu tena bila usumbufu, kwa hiyo haiwagusi kwa namna yoyote ile na ndio maana hawana uchungu na mambo haya. Na hii ni kwa wabunge wote(CCM na Upinzani). Maana hii sheria imepitishwa kimya kimya na sisi tumekuja kustuka maji yameishamwagika.

TUCTA mtuambie kama nyie hili jambo mna kauli gani. Tunajua ni sheria tayari, lakini tunatakiwa kuonesha kutokuridhishwa na yao. Isiwe tu tunalalamika kwenye magazeti na ndani ya hii mitandao. We need to do something. Right now. Tutaedelea kuliwa hadi lini jamani. Hii kitu ni chungu. Haimezeki kambisa.

Kazini tupo kwa ajili ya kujenga maisha yetu na familia zetu. Sio kujenga maghorofa na PPF na NSSF. Tunalipa kodi kwa ajili ya maendeleo ya nchi. Je hiyo haitoshi mpaka kuingilia pesa zetu kiasi hiki jamani. Hii haikubaliki kabisa.
 
Fikiria kijana kuachishwa kazi leo akiwa 30 yrs apigike mpaka 55. Mchangiaji apewe mafao yake ajipange mwenyewe jinsi atakavyokuwa akiwa 55yrs.
 
Mkuu BAK naomba fanya juu chini utuwekee HANSARD za michango ya wabunge wetu katika kuchangia mswada na hatimaye kupitishwa kwa sheria hii. Najua wakati wa kupitisha Sheria ya Kodi ya Mapato ya mwaka 2004 ilibidi wabunge wawekewe kufungu cha kusamehe kodi kiinua mgongo chao ndio wakaipitisha; nataka kufanya kwenye hii waliwekewa kifungu gani?
 
Last edited by a moderator:
Halafu jana nilimsikiliza yule Mgurungenzi wa SSRA (Irene) na Kibonde, nikapata hasira sana, mojawapo ya hoja zao dhaifu nikuwa, kama 90% umeshindwa kufanya la maana hiyo 90% ndo itakusaidia nini.

Nilimuona mkurugenzi wa SSRA akileta utoto na hoja za kishabiki za ki magamba, na upuuzi tu. Huwezi mumpangia mtu atumie vipi pesa yake na pia asi-generalize kuwa woote wameshindwa kufanya maendeleo na hiyo 90%, ni mpumbavu sana huyu. Unapokuwa unatetea jambo toa hoja, na si kuegemea kwenye sababu DHAIFU. Wameahidi kuja na KANUNI (REGULATIONS) zitakazo eleza ni mazingira gani ambayo mtu ataruhusiwa kuchukua pesa zake.

Lakini suala hapa ni (1) wale ambao wameisha peleka documents zao tangu mwaka jana watasaidiwaje? Manake sheria imekuja tayari wao wako katika mcahakato wa kuchukua bna tayari wameisha fanya mipango yao ya kutumia hiyo pesa.
(2) Mkurugenzi wa SSRA hawaelezi watu kianga ubaga kuwa endapo utafariki, je mafao yako watoto na familia yako watafaidika vipi? Manake hawa jamaa wa Pension Funds wanaurasimu mpaka basi
(3) Kama hiyo michango yetu itatumika kama collaterals kuchukua MORTGAGE bank, mbona sheria aisemi wazi wazi kuwa pesa hiyo itatumika kama collateral, hizi ni siasa, (ngoja tusubiri hizo REGULATIONS)
(4) Atuletee faster hizo formula tuone kama kweli mfanyakazi atanufaika na hiyo pension.
(5) Wana consider vipi TIME VALUE OF MONEY, shillingi yako ya leo niliyochangia haitakuwa na thamani sawa na shilingi utakayonipa baada ya miaka ishirini inayokuja!

Wana JF:
Hapa dawa ni moja tu, hii inaongeza chachu ya sababu lukuki za kuitoa madarakani Serikali DHAIFU mnamo mwaka 2015.
 
Wizi mtupu
1.Huo mswada wa sheria ulienda lini bungeni ?
2.Wadau walihusishwa ni wakina nani ?
3.Hizi hela ni zetu au zao ?
4.Ni kwa manufaa ya nani ?
5.Mafao yatakayotolewa ni kiasi gani?
6.Naruhusiwa kukopa na kuweka dhamana hizo fedha zangu?
Bila kujibiwa maswali haya na hii serikali dhaifu sitwaelewa. Naniii zao.
 
na wabunge wetu nao wasubirie hadi miaka 55 au 60 ndo kitaeleweka,tusiposimamia hilo hawatarekebisha hiyo sheria kandamizi kwa wanyoge tu,ngoja uone kama zito,mnyika na wengineo under 50 watakubali, watafyumuje?
 
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: contentheading, width: 100%"]Sheria mpya mifuko ya jamii yazua mtafaruku nchini[/TD]
[TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] [/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: createdate"]Tuesday, 24 July 2012 21:00[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]
Waandishi Wetu
Mwananchi

Marekebisho ya Sheria za Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ya 2012 yaliyofanywa na Bunge yamezua mtafaruku na sintofahamu, huku wafanyakazi wa sekta mbalimbali wakiyapinga kwa maelezo kwamba ni kandamizi na yanalenga kuwanyima haki ya fedha wanazokatwa kwa mujibu wa sheria kuchangia mifuko hiyo.

Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (Tucta), Nicolaus Mgaya aliliambia gazeti hili jana kuwa, watafungua kesi katika Mahakama ya Kazi nchini, kupinga hatua ya Serikali kubadili Sheria ya muda wa lazima wa kuchukua mafao hayo ambao ni kati ya miaka 55 na 60.

Tangu juzi watu kutoka sehemu mbalimbali hasa jijini Dar es Salaam wamekuwa wakipiga simu katika chumba cha habari cha Mwananchi kwa lengo la kupata ufafanuzi wa mabadiliko hayo ya sheria yaliyopitishwa na mkutano wa saba wa Bunge, Aprili 13 mwaka huu.

Kadhalika sheria hiyo inayozuia mwanachama wa mfuko wowote wa hifadhi ya jamii kuchukua mafao kabla ya umri wa kustaafu kwa mujibu wa sheria ambao ni miaka 55, lilichukua nafasi kubwa katika mijadala ya mitandao ya kijamii ambako wengi wa wanaliochangia, wameiponda sheria hiyo na kuiita kuwa ni ya ‘kinyonyaji’.

Hata hivyo, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Irene Isaka alisema jana kuwa: “Hakuna haja ya watu kuwa na wasiwasi, maana sheria hii itafuatiwa na kanuni na miogozo mingine ambayo ninaamini kwamba itaondoa wasiwasi uliopo”.

Isaka alisema miongoni mwa mambo yatakayozingatiwa katika miongozo hiyo ni iwapo mwanachama atafukuzwa au kuachishwa kazi, wanachama ambao wako kwenye kazi za mikataba na wale wanaopata ulemavu wa kudumu wakiwa kazini.

“Kimsingi ni kwamba suala la mafao ya kuacha kazi kabla ya umri wa kisheria wa kustaafu limefutwa kwa mifuko yote, isipokuwa katika mazingira hayo niliyoyaeleza litawekewa miongozo, na hii ni kwa faida ya wachangiaji,”alisema Isaka.

Alisema baada ya sheria hiyo kuwa imepitishwa na Bunge, kisha kusainiwa na Rais Jakaya Kikwete mwezi Juni mwaka huu, SSRA ilianza mchakato wa kuweka miongozo na baada ya hapo kinachofuatia ni kutoa elimu kwa umma na baadaye kuanza kutumika kwake rasmi.

“Lakini sasa tumelazimika kuanza kutekeleza sheria hiyo mapema kuliko tulivyopanga hasa baada ya kutokea kwa suala hili kwenye public (umma) kabla ya muda tuliokuwa tumekusudia,”alisema mkurugenzi huyo.


Isaka aliongeza kuwa chimbuko la sintofahamu iliyojitokeza ni baadhi ya mifuko kuchezeana rafu kwa lengo la kupata wanachama wapya kwenye migodi na kwamba wao kama wadhibiti tayari wametoa onyo kwa mifuko iliyohusika.

“Kwanza hakuna mfuko wowote ambao una mamlaka ya kutangaza kuanza kutumika kwa sheria, ni SSRA tu wenye mamlaka hayo, kwa hiyo tumewapa onyo, kama wanajitangaza wajitangaze kwa kueleza uzuri wa mfuko wao ni siyo kuchafuana au kuchafua wengine,” alisisitiza.
Wasemavyo wafanyakazi
Mgaya alisema sheria hiyo ni kandamizi kwani inamnyima fursa mfanyakazi aliyestaafu au kufukuzwa kazi kupata malipo yake ambayo ni halali.

“Sheria hii sisi hatuikubali na tunaipinga kwa nguvu zote na tutakwenda Mahakama ya Kazi kufungua kesi ya kupinga kutumika,” alisema Mgaya na kuongeza:

“Tutafanya mawasiliano na Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii kuwaeleza kuhusu sheria hii ili watusaidie na ikishindikana azma yetu ni kwenda mahakamani.”

Katibu Mkuu huyo alifafanua kwamba haiwezekani mtu anafukuzwa kazi akiwa na miaka 45 na baadhi yao hawataki tena kuajiriwa wanataka kufanyabiashara halafu unamnyima mafao yake hadi afikishe miaka 55, kitu ambacho kitamfanya mtu huyo aishi maisha magumu.

“Sheria hiyo ingekuwa na usawa ingetumika kwa wafanyakazi wote wa Serikali na kutowabagua kama inavyojieleza kwamba, Mbunge akimaliza miaka yake mitano anachukua mafao yake. Sasa kwa nini iwe kwao tu na si kwetu pia?,” alihoji Mgaya.

Kwa upande wao Chama cha Wafanyakazi wa Migodini (Tamico) Wilaya ya Geita, kimesema kitapeleka maombi maalumu kwa Rais Kikwete kupinga marekebisho ya Sheria ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii.
Katibu wa Tamico Wilaya ya Geita, Benjamin Dotto alisema wameamua kupiga kura ya maoni juu ya mabadiliko ya sheria hiyo, ili wanachama wao waamue wenyewe kama wanaitaka au la.

”Tunamwomba Rais aagize kupelekwa muswada wa marekebisho bungeni, kwa ajili ya kipengele ambacho kimeleta mtafaruku,” alisema Dotto.

Alisema kipengele cha kuzuia mfanyakazi kuchukua mafao yake hadi afikishe umri wa miaka 55, kinakandamiza masilahi ya mfanyakazi mnyonge ambaye kwa kiasi kikubwa amekuwa akichangia mapato ya nchi kupitia kodi anayokatwa.

Chimbuko la sheria
Mabadiliko ya sheria hizo za mifuko ya hifadhi ya jamii yalifanywa na Bunge Aprili 13 mwaka huu, baada ya muswada husika kuwa umesomwa kwa mara ya kwanza bungeni Februari 1, 2012.

Ibara ya 107 ya muswada huo ndiyo ilipendekezwa kufutwa kwa Ibara za 37 na 44 za Sheria ya Mfuko wa Pensheni wa Mashirika ya Umma (PPF) ambavyo vilikuwa vikiruhusu mafao ya kujitoa.

Meneja uhusiano wa SSRA Sara Mssika alisema jana kuwa kufutwa kwa ibara hizo kulimaanisha kwamba hakuna mfuko wowote unaoruhusiwa kutoa tena mafao ya aina hiyo hadi hapo miongozo mipya itakapotolewa.

“Hakuna sheria ya mfuko mwingine iliyokuwa ikiruhusu mafao ya kujitoa, na kama wapo waliokuwa wakifanya hivyo, basi walikuwa wanafanya hivyo pengine kwa taratibu nyingine ambazo ni nje ya sheria za kuanzishwa kwa mifuko yao,”alisema Mssika.

Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka akiwasilisha maelezo ya muswada huo bungeni alisema lengo la marekebisho katika Sheria za Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ni kuiwezesha SSRA kufanya kazi yake kikamilifu na kusimamia na kudhibiti Sekta ya Hifadhi ya Jamii.

Alisema muswada huo uliandaliwa kwa kuwashirikisha wadau wote wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii, wakiwamo wafanyakazi, waajiri na Serikali, pia
mifuko yenyewe kupitia vikao vya wadau na Baraza la Ushauri wa Masuala ya Kazi Jamii na Uchumi.

“Kimsingi, wadau wote waliunga mkono mapendekezo yaliyomo katika muswada huu,” alisema Kabaka na kuongeza kuwa mabadiliko hayo yatawezesha kupanuliwa kwa wigo wa wanachama kwenye mfuko kwa kuruhusu wafanyakazi wanaoingia kwenye ajira kwa mara ya kwanza ama kujiajiri wenyewe ili waweze kujiunga.


[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

Hapa ndiyo nimeona ulimbukeni wa watanzania
 
wote tulikua tunajiuliza serikali itapata wapi pesa za bajeti yao baada ya kunyimwa misaada na nchi za ulaya nk nadhan sasa wamepata upenyo, wafanyakazi inabidi tusimame imara huu ni wizi wa mchana tutakua tunakufa kama enzi hizo baba zetu wanafuatilia mafao mpaka wanakufa, kwa mfano unapofuatilia mafao unatakiwa ukajaze fomu kwenye hiyo kampuni uliyotoka sasa sie wa sekta binfasi kila siku kampuni zinafungwa tunahama mpaka miaka 55 naweza kua nimefanya kampuni kama 10 sasa ntawapata wapi wakati wengi washafunga na wameishia!
 
Nimesoma barua ya Irene, baadhi ya mambo mazuri yaliyoelezwa kwenye gazeti sijaona kwenye barua yake.
 
Hakika hiki ni kilio cha wafanyakazi kwenye sekta binafsi leo hii ukiachishwa kazi na numri 30's na ukaa bila kupata ajira nyingine then itabidi usubirie mafao hadi utimize umri wa miaka 60.
 
Mbunge gani wa CDM alipinga?

wabunge wote e kwani wewe mgeni hujui wanaosema ndioooooooooooooo na spika kila mara anasema nafikiri walio sema ndio wameshinda halafu wacha hizo sababu kubwa nikupe mfano kagera sugar na kilombero sugar walikopeshwa na nssf billion karibu 80 kwa goverment garantee hii ni kwa mujibu wa taarifa ndani ya bunge je zimelipwa au ni mtindo uleule wa ccm kula sukita?

 
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: buttonheading, align: right"][/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: createdate"] Tuesday, 24 July 2012 21:00 [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD] Irene Isaka alisema jana kuwa: "Hakuna haja ya watu kuwa na wasiwasi, maana sheria hii itafuatiwa na kanuni na miogozo mingine ambayo ninaamini kwamba itaondoa wasiwasi uliopo". Isaka alisema miongoni mwa mambo yatakayozingatiwa katika miongozo hiyo ni iwapo mwanachama atafukuzwa au kuachishwa kazi, wanachama ambao wako kwenye kazi za mikataba na wale wanaopata ulemavu wa kudumu wakiwa kazini. [/TD]
[/TR]
[/TABLE]


Sheria ilitakiwa kutungwa pamoja ni miongozo yake kwa sasa it is too late kueleweka. pia watu wangetangaziwa... Manake hiyo ilitakiwa maoni ya wananchi kuliko hata hiyo KATIBA
 
Back
Top Bottom