Hakuna malipo ya NSSF, PPF hadi umri wa kustaafu ufike!

Hakuna malipo ya NSSF, PPF hadi umri wa kustaafu ufike!

Unataka kusema hii sheria imeletwa na PPF? Vipi ulisoma report ya CAG?

Serikali ndio mkopaji mkubwa kwenye hii mifuko, na kwa jinsi hali ilivyo haiwezekani kuendelea kutumikia vyote, serikali na watu wanaojitoa. Kwa bahati mbaya Tanzania hakuna unemployment benefit ambayo ingetakiwa itoke serikali kuu. Hivyo anayekuwa nje ya ajira kabla ya miaka 55 ana-hang hadi hapo atakapopata kazi nyingine au afikie umri wa kustaafu.

PPF ni mfuko wa pensioni sio provident FUND. Kutokana na ubadhirifu na matumizi mabaya ya madaraka ya uongozi wa PPF chini ya William Erio Mkapa, Mfuko wa PPF umeporomoka na kujikuta hauna wanachama wa kudumu wa kuuendeleza uwe wa pensioni. Katika kutapatapa, ukaanza kuandikisha vibarua, wakata miwa na wachuma chai wenye ajira za miezi mitatu kwa mwaka (misimu ya uvunaji). Hadi June 2012, PPF ilikuwa 42% PENSION na 58% PROVIDENT, yaani wale wa kuingia na kujitoa ndio wengi hivyo kupelekea tishio la kuwa mfuko mfu. Ili kukwepa hilio angalau hadi contract yake iishe, Bw. Erio akatumia, advantage ya kuwa alimlicomend Irene Isaka vizuri kupata kiti SSRA, japo alikuwa wa tatu kwenye usaili, kumdangaya abadili sheria ya WITHDRAWAL BENEFIT?

Kila mfuko uliundwa kwa sheria yake, je! walipounda na kuweka fao hili hawakuona au hawakujua haya wanayoyabadili leo na kuleta usumbufu?
 
Vijana wote jiandae kwa mapambano maana miccm ilichofanya bunguni ni uhuni uhuni uhuni

FUc...k Miccm

vurugu.jpg
 
Mda wa kuanza kujitoa muhanga naona umefika sasa, mimi naona nitakuwa wa kwanza jamani kufa na mtu au watu fulani, kwani watu wanapenda kuwa boko haram?? Hizi ndio sababu zenyewe jamani,,, ni muda sasa wa kuanza kuonyesha hisi zetu kali tulizokuwa nazo Kwa vitendo,,, hakuna matumaini ya kuishi,,,,
 
Jamani huu uamuzi wa leo bungeni ni uonevu mkubwa sana , kwenye sekta binafsi ajira sio za kuzeeka nazo kama serikalini na mtu anaweza kukosa kazi kabisa kwani unemployement hapa kwetu nahisi ni zaidi 50pct. Nisipochangia miaka 15 hiyo michango yangu inaenda wapi?
 
Irene Isaka katumwa na William Erio wa PPF aliyekuwa boss wake kuwa afute hilo fao maana mfuko wa PPF ungekufa hivi karibuni kama hilo fao la kujitoa lingeendelea.

PPF hadi sasa hivi inatakiwa kuwa PROVIDENT FUND sio Pension Fund maana imepoteza sifa hiyo kisheria, ni maiti inayotembea. Wamefilisi pesa yote kwa kugawana kila mwaka wakurugenzi. Wanaochangia walio katika ajira za kudumu PPF ni 30% tu wakati wale ambao wanaweza kujitoa wakati wowote ni 70% na kulipwa withdrawal benefit.

Zitto hana ubavu wa kumwambia chochote DG wa PPF maana amewekwa mfukoni, kila wakati yuko naye eg sabasaba, nanenane etc na kila akija lazima akilimiwe na ktitita. Alionyesha ujasiri kwenye suala la Group Endowment lakini kaishia mfukoni mwa Erio

Huyu Irene Isaka anakaribia kufika safari yake...Mlio na vijisenti vyenu huko jaribuni kutafakari upya.

Serikali yakalia trilioni 8.4/- za PSPF, NSSF, PPF
NA WAANDISHI WETU
21st October 2014
Madeni sugu ya serikali yanatishia uhai wa mifuko ya hifadhi ya jamii nchini huku Mamlaka ya Usimamizi ya Mifuko hiyo ( SSRA) ikitoa angalizo kwa serikali kuhusiana na hali hiyo kufuatia kuidai Sh. trilioni 8.43.

Hali hiyo inaweza kukwamisha mifuko hiyo kuwalipa mafao wanachama wake, kujiendesha yenyewe na kuwekeza katika miradi mbali mbali.

Deni hilo linatokana na serikali na taasisi zake kukopa kwenye mifuko hiyo na kutopeleka michango ya wanachama.

Mkurugenzi wa SSRA, Irene Isaka, alisema deni hilo ni pamoja na lililotokana na ahadi ya serikali kulipa malipo ya pensheni kwa wafanyakazi ambao walikuwa hawachangii kwenye Mfuko kabla ya 1999.

Isaka aliyekuwa akizungumza katika mkutano ulioitishwa na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) na kuwakutanisha wakurugenzi wa kifumo ya hifadhi ya jamii, Wizara ya Fedha, Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Mkuu wa Hesabu za Serikali, SSRA na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), alisema deni jingine ni dhima ya mifuko ambayo ni kifurushi cha ahadi ambacho mwanachama ameahidiwa hadi siku anafariki na kwamba mifuko isipokuwa na hazina ya kutosha inabadilika kuwa kuwa deni.

Isaka alisema iwapo serikali itaendelea kukopa na kutopeleka michango ya wanachama wake, mifuko hiyo itaathirika kiasi cha kushindwa kulipa mafao kwa wanachama wake.

”Athari tuliyonayo, mifuko yetu ni ya pensheni, hasara ni ya mifuko. Mwanachama hatamsamehe mwenye mfuko kwa kushindwa kumlipia, kadri deni linavyoongezeka ndivyo Mfuko unaumia na baadaye kushindwa kulipa mafao yanayotakiwa,” alifafanua Isaka.

Alisema kwa madeni hayo Mfuko ambao unanunua kifurushi cha ahadi kwa mwanachama na unatakiwa kutimiza anapostaafu, utaendelea kuharibika kadri muda unavyozidi iwapo utashindwa kulipa madeni.

Awali, Kaimu CAG, Athumani Selemani, akizungumza alisema zaidi ya Sh. Trilioni 1. 37 ni deni la serikali na taasisi zake walikopa kutoka kwenye mifuko hiyo kwa shughuli mbalimbali.

Alisema zaidi ya Sh. trilioni 7.9 ni deni la PSPF la kuanzia 1999 ikiwa ni fedha za kuwalipa mafao wanachama ambao walikuwa hawachangii kwenye Mfuko lakini kwa mujibu wa sheria walioaswa kulipwa.

Selemani alibainisha deni hilo kwa kila mfuko inavyoonekana kwenye mabano ni PPF ( bilioni 192), NHIF ( bilioni 107), NSSF ( bilioni 467), PSPF ( bilioni 4.29), LAPF ( bilioni 170) na GEPF (bilioni 6.86).

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dk. Servacius Likwelile, alithibitisha serikali kulitambua deni hilo na kwamba ni lazima ilipe ikiwa ni pamoja na deni ya PSPF kabla ya mwaka 1999.

Pamoja ka kukiri na kuahidi kulilipa madeni hayo, Dk. Likwelile hakueleza ni lini serikali italipa wala utaratibu utakaotumika kuyapunguza.

Akizungumza na waandishi wa habari kabla ya kuanza kikao hicho, Mwenyekiti wa PAC, Zitto Kabwe, alisema waliwaita BoT, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, CAG, SSRA, Wenyeviti wa bodi na Wakurugenzi wa mifuko ya hifadhi ya jamii kwa ajili ya kulijadili suala hilo.
Alisema lengo ni kujadili namna ya serikali kulipa deni hilo ili kuiwezesha mifuko hiyo kusonga mbele kwa kulipa mafao wanachama wake na kuwekeza.

Kabwe alisema serikali zote duniani zinakopa kwenye mifuko hiyo, lakini tatizo kubwa kwa serikali ya Tanzania ni kutolipa, jambo ambalo alisema ni hatari kwa uendeshaji endelevu wa mifuko hiyo.

”Tuna tatizo la serikali kukopa kwenye mifuko kwa ajili ya miradi mbalimbali na kutolipa, ni kawaida kwa nchi nyingine duniani kukopa na kurudisha tofauti kwa serikali ya Tanzania hairudishi,” alisema Kabwe.

Aliyataja baadhi ya madeni kuwa ni fedha za ujenzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma Sh. milioni 800 na deni la PSPF la kabla ya 1999.

Alisema hali hiyo ikiachwa kuwa kama ilivyo sasa mifuko itashindwa kuwekeza katika miradi mbalimbali, hivyo ni muhimu madeni yalipwe ili mifuko iendelee kulipa madeni na kwamba itafika wakati itauza samani zake na kushindwa kufanyakazi.

Deni hilo ni takribani nusu ya bajeti ya serikali kwa mwaka wa fedha 2014/15 ambayo ni Sh. trilioni 19.8.

Wakati serikali ikidaiwa na mifuko hiyo, kiasi hicho cha fedha, Deni la taifa hadi Machi mwaka huu, lilifikia Shilingi trilioni 30 ikilinganishwa na Shilingi trilioni 23.6 Machi mwaka uliopita 2013.
 
Wabunge wakija kuomba kura tuwaulize,

Enyi wabunge huko Bungeni, msije kuomba tena kura 2020?

NSSF hawatoi mikopo kwa wanachama wao

NSSF hawatoi dhamana kwa mikopo benki
 
Kulingana na kauli ya M/S Irene Isaka, NSSF hakuna FAO la kujitoa.

Wanachama wa NSSF ni SECTOR binafsi na ajira ni za mashaka. Mishahara ni ya kinyonyaji, Mishahara midogo sana.

Pili, Hakuna uhakika wa ajira mpaka mtu astaafu miaka hiyo 55. Kwa hiyo mtu akiacha kazi au kufukuzwa afanyeje? Si bora mtu apewe chake akajiajiri....

Jamani enyi wabunge, hamjui hili? Mh. Jafo...Uliongelea hili ila sasa ni waziri......Mbunge yupi awe mkombozi wa Mtanzania?

Kinachotia hasira zaidi ni NSSF kukataa kutoa mikopo kwa wanachama wake.... Au kukataa kutoa dhamana kwa mwanachama ili akope benki...

NSSF wana share kubwa AZANIA BANK, kwa nini msitoe scheme ya mikopo?

Wabunge ombeni hoja ijadiliwe
 
Kulingana na kauli ya M/S Irene Isaka, NSSF hakuna FAO la kujitoa.

Wanachama wa NSSF ni SECTOR binafsi na ajira ni za mashaka. Mishahara ni ya kinyonyaji, Mishahara midogo sana.

Pili, Hakuna uhakika wa ajira mpaka mtu astaafu miaka hiyo 55. Kwa hiyo mtu akiacha kazi au kufukuzwa afanyeje? Si bora mtu apewe chake akajiajiri....

Jamani enyi wabunge, hamjui hili? Mh. Jafo...Uliongelea hili ila sasa ni waziri......Mbunge yupi awe mkombozi wa Mtanzania?

Kinachotia hasira zaidi ni NSSF kukataa kutoa mikopo kwa wanachama wake.... Au kukataa kutoa dhamana kwa mwanachama ili akope benki...

NSSF wana share kubwa AZANIA BANK, kwa nini msitoe scheme ya mikopo?

Wabunge ombeni hoja ijadiliwe

Jafo kama waziri ana nafasi kubwa kuliko mbunge yeyote. Yeye anaweza kuliongea kwenye kabineti lakini bungeni pale ni porojo.
 
Ipo siku watu watajifunga baruti hii nchi.
No jambo ambalo haliingii akilini niache/ishwe kazi halafu eti hela yangu niisubiri miaka ishirini ijayo wakati hakuna uhakika wa kupata kazi hapa katikati. Kuna gharama za kila siku kuishi, kusomesha,kujitibu na hata kufanya.biashara huku ukilipa kodi lakini wamekomaa na pesa.
Miundombinu.gani ipo tanzania kuhakikisha watu datasets kuishi kucreate retaliation?
Nchi za watu wao wanapewa posho kama hawana kazi, nyumba zipo.za kuishi na hapo.ndipo unapokutana na uzazi wa mpango.

Nchi Imejaa mijizi, watu wanajilipa $20,000 wakati wanasimamia mali.umma tu na wala sio kiwanda kinachozalisha faida.

Kwa kweli yale ni machaka ya watu.kujipigia.

Hii nchi ipo siku, nyie ngojeni njaa iwaume watu wakati pesa wanajua iko wapi.
 
Jafo kama waziri ana nafasi kubwa kuliko mbunge yeyote. Yeye anaweza kuliongea kwenye kabineti lakini bungeni pale ni porojo.
Tatizo nchi hiii watu wengi ni wanafiki.
Sasa wewe Mswaada wa sheria ulijadiliwa na wadau, alafu sheria ikapiotishwa, kisha ikaanza kutumika. Baadae wadau haohao ndio wa kwanza kujifanya wanawatetea wananchi kua wanaonewa.
 
GPF na PSPF Wana FAO la kujitoa ila NSSF hapana....

Sasa nashangaa, kwani wanachama wa NSSF ni ajira yao ni Serikali au Mashirika ya Umma?

Mimi naona watu wasijiunge tena na NSSF na watu waruhusiwe kuhama kutoka NSSF kwenda PSPF...

Jamani nani ana Contact wa Wabunge au Waziri wa Utumishi?
 
GPF na PSPF Wana FAO la kujitoa ila NSSF hapana....

Sasa nashangaa, kwani wanachama wa NSSF ni ajira yao ni Serikali au Mashirika ya Umma?

Mimi naona watu wasijiunge tena na NSSF na watu waruhusiwe kuhama kutoka NSSF kwenda PSPF...

Jamani nani ana Contact wa Wabunge au Waziri wa Utumishi?
Mkuu kwani NSSF nao tayari wamesitisha?maana PPF ndo tangu mwezi wa tano.
 
Wiki iliyopita tulimsikia Irene Wa SSSR akisema NSSF na PPF hakuna FAO la kujitoa....

Matatizo makubwa yako hapa.....Kuna mkono wa Serikali au kuna ufisadi wa kutisha.....There is a secret....

NSSF ni mfuko wa wafanyakazi sekta binafsi...Sekta binafsi ni sekta ngumu na Kampuni inaweza kufilisika au kufungwa pia, example General Tyre, Kibo Match Moshi, Mahoteli, Makampuni ya ulinzi, na makampuni mengine kupunguza wafanyakazi.

Kwa hali hii mtu akipoteza kazi akiwa na miaka 35 let say, je ataishije mpaka afikishe miaka 55 ili aanze kupata hiyo pensheni? Kwa nini mwanachama wa NSSF asipewe fao lake akalime kuongeza tija au kujiajiri?

NSSF hawatoi mikopo kwa wanachama wake au haitoi dhamana kwa mwanachama ili akope benki...

Je kuanzia miaka 55, utaishi miaka mingapi? (Kwa huduma nzuri zipi za afya)

Kwa gharama zipi nafuu za maisha?

CCM waliahidi cementi 8000 kwa mfuko, ziko wapi?
 
Mtu amefanya kazi miaka 3 tu kafukuzwa kazi akiwa na umri wa miaka 23. Jumla ya michango yake ni 36 sawa na 1,800,000TZS hakuna uwezekano tena wa kupata kazi nyingine ili aendelee kuchangia. Mtu huyu asubiri miaka 37 ipite ili afikishe miaka 60 ndipo achukue pesa yake mbaya zaidi kiasi ni kilekile 1,800,000TZs cha miaka 37 iliyopita? Maana michango yake haijafika kiwango kinachohitajika iliapate pension! Inaingia akilini? Huu utakuwa zaidi ya wendawazimu!!!
 
Back
Top Bottom