Kwenye gazeti la leo la jambo leo Kuna habari inahusu mfuko mmoja wa kijamii wa PSPF, kwamba uko hoi kifedha, wakaenda mbali zaidi wakasema umeathiliwa na uchaguzi wa mwaka jana, unahangaika kuwalipa wastaafu, sasa kwa Hali hii wanaodai fao la kujitoa lazima wazinguliwe, nafikiri SSRA inatumia njia hii kurescue situation ya mifuko hii ina hari mbaya kifedha, kwa hiyo inalazimisha watu wasijitoe ili watengeneze pesa kwanza, yaani inauma ile mbaya kwa sisi walala hoi, ukifukuzwa kazi basi uende unahangaika, hata kuazisha kamradi ushindwe huku unafedha yako wamekalia watu fulani, na vitu wanavyojitete havina maana kwani wanasema mtu akijitoa anaenda kuishi maisha magumu lakini hawajatupa utafiti waliofanya na kufuatilia watu walio jitoa kwenye hiyo mifuko, wanafanya kazi kwa hisia , ili tukubaliane na matakwa yao, yaani mimi binafsi nimeshitushwa na hii mambo.