Hakuna malipo ya NSSF, PPF hadi umri wa kustaafu ufike! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hakuna malipo ya NSSF, PPF hadi umri wa kustaafu ufike!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by allydou, Dec 5, 2011.

 1. a

  allydou JF-Expert Member

  #1
  Dec 5, 2011
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 1,485
  Likes Received: 572
  Trophy Points: 280
  Habari wana JF

  Ni muda sasa, tangu mwezi wa sita hivi nimekuwa nikisikia kwamba Serikali ipo katika hatua za mwisho za kuzuia wafanyakazi wa sector binafsi kuchukua NSSF zao mpaka wafikishe umri wa kustaafu uliowekwa na seerikali, like 60yrs.

  nilisikia kwamba mpango huu ulikuwa uanze mwaka huu mwishoni, lakini ikashindikana kutokana na maandalizi kutokuwa yamekamilika vizuri.

  Nimesikia tena leo mjadala huu ukiendelea kwenye forum moja ya watu wanaofanya kazi kampuni mmoja through outlook mails kwamba mpango huu utakuwa implemented kuanzia 1st march 2012 bila kukosa.

  Nilisikia pia kupitia wana forum hao kwamba bunge lilipisha muswada huu na Rais kuusaini kinyemela tangu mwaka jana, kitu ambacho kinaniumiza kichwa, inakuwaje muswada nyeti kama huu upitishwe kwenye bunge hili la sasa la ushindani wa kisiasa na hoja zenye mantiki kutoka upinzani bila wanachi kufahamu.

  mwenye uhakika na suala hili please naomba unifahamishe vizuri.

  Itakuwa ni vizuri zaidi kama utaleta na official data kuleta uhakika zaidi.

  Aksanteni.
  Ufafanuzi Kutoka Mamlaka ya Usimamizi na Udhitibi wa Hifadhi ya Jamii

   
 2. Masika

  Masika JF-Expert Member

  #2
  Dec 6, 2011
  Joined: Sep 18, 2009
  Messages: 731
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Labda hizi ni tetesi mimi sijawahi kusikia
   
 3. b

  bagain JF-Expert Member

  #3
  Jun 23, 2012
  Joined: Jul 21, 2011
  Messages: 274
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 60
  Hi wana JF,

  Nimesikia kuwa kuna sheria imepitishwa kuwa HAKUNA TENA kuchukua hela za NSSF ukiacha kazi HADI UMRI wa kustaafu
  ufike.

  Mwenye kujua UKWELI atuhabarishe zaidi (NSSF au watunga sheria wetu).

  Wafanyakazi wa sekta binafsi mnalijua hili?
   
 4. Mnwele

  Mnwele Senior Member

  #4
  Jun 23, 2012
  Joined: Feb 4, 2010
  Messages: 163
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Bargain,

  Hii sio tetesi maana haijawa kama hivyo. Lakini umefanya vizuri kuleta hii habari katika kipindi hiki na kuwafanya waajiriwa wote Tanzania wakae mkao wa kula.

  Ukweli ni kwamba serikali ina mpango wa kupeleka bungeni marekebisho ya muswada wa sheria wa mafao ya wafanyakazi kama ulivyopitisha ba bunge ili sasa kufanya wafanyakazi wote wanaokatwa akiba ya mafao (PPF,NNSF, PSPF,LAPF,GEPF n.k) kulazimika kutopata mafao yao kama hawajatimiza umri wa kustaafu(55-60).Mpango huu unaletwa kwa sababu serikali yenu haina namna ya kufanya na ingependa kupata boost ya mapato toka mifuko hii ili kuleta pesa kwa ajili ya miradi ya maendeleo.

  Mpango huu wa aibu na kandamizi utawaathiri wafanyakazi zaidi ya 700000 serikalini lakini kwa kipekee utaathiri na kuua ndoto za wafanyakazi zaidi ya 3000000 walio katika sekta binafsi kama vile makampuni, NGOs na wale waliojiajiri wenyewe na ambao wanatumia mifuko hii.

  (Una imani kubwa kwamba wabunge wetu hasa wa upinzani wataupigia ngumu mpango huu nyonyaji ambao ni wa aina yake katika nchi zote za Afrika. Hii pia inatoa fursa kwa wafanyakazi wote nchini (hasa vijana) kutafakari na kuona jinsi serikali yenu inavyopanga kufifisha mipango yenu ya muda mfupi na ile ya kati. Kazi kwenu simameni na Chukueni Hatua Sasa.

  HABARI NDO HIYO
   
 5. B

  BARRY JF-Expert Member

  #5
  Jun 23, 2012
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 366
  Likes Received: 118
  Trophy Points: 60
  Hili ni pigo kwa wafanyakazi wa sekta binafsi. Lengo ni nini?
   
 6. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #6
  Jun 23, 2012
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 897
  Trophy Points: 280
  naona sasa wanataka tuwashkishe ukuta.

  anywayz nimechukuwa cheki yangu jusi baada ya kusungushwa karibu miezi miwili.
   
 7. Bavaria

  Bavaria JF-Expert Member

  #7
  Jun 23, 2012
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 44,100
  Likes Received: 11,251
  Trophy Points: 280
  na ukifa kabla ya muda wa kupokea mafao?
   
 8. Bavaria

  Bavaria JF-Expert Member

  #8
  Jun 23, 2012
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 44,100
  Likes Received: 11,251
  Trophy Points: 280
  hapo kuna haja ya kucheza na mwajiri asipeleke hela NSSF
   
 9. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #9
  Jun 23, 2012
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,316
  Likes Received: 618
  Trophy Points: 280
  Nikiacha kazi leo wanangu wafe njaa kisa sijafikisha miaka 60? Wabunge wakipitisha hii tuwapige mawe.
   
 10. D

  Dr Know know Member

  #10
  Jun 23, 2012
  Joined: Aug 20, 2011
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamii forums inawachangiaji mbalimbali wakiwemo wataalamu kutoka kwenye mashirika yanayohusika na mifuko ya jamii.Naamini katika mashirika haya kuna maafisa mahusiano ambao wanapaswa kutolea ufafanuzi mabo mbalimbali likiwepo hili.,kwa fursa hii mnaombwa kutufahamisha wafanyakazi na wananchi kwa ujumla .
   
 11. O

  Omonto Member

  #11
  Jun 23, 2012
  Joined: Feb 13, 2012
  Messages: 38
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Usawa haki na maisha bora kwa wafanyakazi wa tanzania unakaribia kufutika maana haina maana yoyote ya kufanya kazi kwa mkataba ktk mashirika binafsi. Tutaishi maisha ya kufikirika tabu na mateso ndiyo furaha ya serikali yetu
   
 12. M

  Makupa JF-Expert Member

  #12
  Jun 23, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,742
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Tatizo la hii mifuko ya hifadhi za jamii ni kwamba, waliwekeza sana kwenye vitaga uchumi ambavyo rejesho la uwekezaji ni la muda mrefu sana hivyo hawana jinsi.
   
 13. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #13
  Jun 23, 2012
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  kwa nini wafanye hivyo lakini?
   
 14. b

  bagain JF-Expert Member

  #14
  Jun 23, 2012
  Joined: Jul 21, 2011
  Messages: 274
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 60
  Mnwele

  Asante kwa ufafanuzi.

  Shida ni kuwa likishafika BUNGENI watasema NDIOOOOOOOOO wale wabunge wa CCM na kwa kweli hali haitakuwa nzuri hasa kwa sekta binafsi.

  Wafanyakazi tulio PRIVATE toeni michango yenu ya mawazo nini kifanyike kuzuia udhalimu huu unaotaka kufanyika.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 15. M

  MZALAMO JF-Expert Member

  #15
  Jun 23, 2012
  Joined: Jul 6, 2009
  Messages: 471
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 60
  Hii sheria ikipitishwa itawaadhiri wafanyakazi wengi wa sekta binafsi na itakuwa imeharibu ndoto za vijana wengi wenye nia ya kujiajiri labda serikali nayo ipunguze umri wa kustaafu kutoka miaka 55 kwa hiari hadi miaka 45 na hii inatokana na wastani wa umri wa mtanzania kuishi ni miaka 45 tu.
   
 16. D

  DUBE Senior Member

  #16
  Jun 23, 2012
  Joined: Apr 29, 2012
  Messages: 197
  Likes Received: 111
  Trophy Points: 60
  Hi hatari sana tena sana kama wabunge wakipitisha hilo basi nitajua wabunge ni washezi na hawafai itakuwa ni haki kuwapinga maye,mi nilitegemea waweke sheria ya mtu kuacha kazi au kufukuzwa kazi alipwe mara moja mafaao ya NSSF sio kuzungushwa kama ilivyo sasa, ni tabu sana kuipata hela ya NSSF ni usumbufu wa hali ya juu.

  Kwanza ukiacha kazi eti usubili mpk miezi 6 ndio uanze kudai,lakin walivyo wajinga kwa wafanyakazi wa BARRICK MINING eti ukiacha kazi unalipwa ndani ya wiki 2,sasa hio ni akili au matope,hilo la BARRICK MINING nina ushahidi kwani nilishakuwa mfanyakazi wa barrick,tutapinga kwa nguvu zote wao wapitishe waone.
   
 17. Ozzie

  Ozzie JF-Expert Member

  #17
  Jun 23, 2012
  Joined: Oct 9, 2007
  Messages: 3,234
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 135
  Kwa life expectancy ipi? Waache wenye pesa wajichukulie pale wanapotaka.
   
 18. b

  bagain JF-Expert Member

  #18
  Jun 23, 2012
  Joined: Jul 21, 2011
  Messages: 274
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 60
  Wana JF kumbukeni,

  Bunge lilipitisha WAFANYAKAZI WA SERIKALI hawalipi kodi kwenye ALLOWANCES lakini PRIVATE lazima ulipe kodi ya allowances zote (eg house allowances e.tc).

  Je TUKINYAMAZA katika hili la HELA ZETU si nalo litapitishwa?

  Tuamke tutake kuelezwa ukweli na Serikali.
   
 19. M

  Mama Ngina Member

  #19
  Jun 23, 2012
  Joined: Feb 6, 2012
  Messages: 27
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama itapita hakika itakuwa kilio kwa wafanyakazi wengi;
  Kwa maisha ya sasa yalivyo na ugumu wa kila hali; magonjwa ya kila aina , BP, kisukari, HIV/AIDS , TB , malaria etc. Bado wanategemea watu tufike 55- 60yrs old. ..............Eeh Mungu tusaidie waja wako.
   
 20. b

  bagain JF-Expert Member

  #20
  Jun 23, 2012
  Joined: Jul 21, 2011
  Messages: 274
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 60
  Hapo kwenye nyekundu, hii ni KASHFA ya wazi. WHY BARRICK??????
   
Loading...