Kutokana na Jazba kubwa juu ya kufutwa kwa mafao ya kujitoa, nimeona nitupie hii hapa ili tujadili, nikiamini we are all gret thinkers, na kama mtu unaona huna cha kusema angalia wengine wanasema nini. Najua watu wamesoma fani mbali mbali na kila mtu akiwa anafanya kazi hata kama una kampuni yako, so long as infanya vizuri na kujulikana huenda umejikuta unachangia Mfuko wa Pensheni, sasa je nataka niulize msitukane, kuna haja ya kuwa na pensheni ya uzeeni? na kama kuna haja muundo wake uwe vipi, mifuko ifanye nini ili watanzania waone inafaa kwa wao kuchangia, na je mafao yale y kujitoa ni kweli tunakuwa tumeacha kazi au tumehama? na hapo ulipo utakuwa umeona ndugu yako au anybody aliyestaafu, je pebsheni inamsaidia? na je umewahi kuona mtu amestaafu bila pensheni? na je anaishije? ni vyema kuendelea na informa safety nates zetu? yaani hakuna haja yamifuko mtu asaidiwe na watoto wake? Mimi maoni yangu ni kama ifuatavyo!
1. Kila mtu mwenye kazi au kipato achangie mfuko,
2. hakuna kujitoawala mafao ya kujitoa hadi 55 au zaidi
3. kiwango cha michango yetu na ya mwajiri kipungue kwa asilimia 2 na kiasi hicho kiingizwe kwenye mfuko maalumu kwa ajili ya pensheni ya kila mtu tanzania angalu 20,000 kwa mwezi,
4. Mafao yapungue kwa asilimiahiyo mbili, na huu mfuko uchangiwe na kodi nyingine pia ili ujiendeshe hapa hakuna haja ya pesa nyingi zipatikane za kila mwaka tu,
5. sisi amabao naamini tunajua maana ya hii mifuko tushauri positively bila kuleta siasa, na makundi maalumu yafikiriwe tofauti kama wale watu wa migodini ambao life expectancy yao ni ndogo.
Mi nawasilisha tu maoni yangu.