Michael Scofield
JF-Expert Member
- Jul 30, 2011
- 1,225
- 473
Hawa ccm bahada ya kufanya uchunguzi wamegundua karibu wanachama wote wa NSSF ni wafanyakazi wa viwandani! na sekta binafsi, madini, ulinzi (security guard), mahotel n.k
Ambazo wafanyakazi wa hizi sekta ni aghalabu kabisa kuvuka miaka 10, tena kwa wenzetu masecurity guard wao wakidumu miezi 6, basi ulienda kwa professa maji marefu,
Karibu sekta zote hizi waajiri wake ni kama sio raia kutoka nje Asia, basi ni watanzania wachache wanaoshea na waasia.
Na kabla mifuko mingine ya kijamii haijajiingiza katika katika hifadhi kwa sekta binafsi, NSSF ndio aliekuwa anakomba mahela ya wafanyakazi hawa.
Sasa ukiangalia kwa jinsi mazingira yalivyo ya ufanyaji kazi katika sekta zetu hizi binafsi, mtu anakuajiri leo kesho anakutimua na ukiangalia karibu ya nguvu kazi ndio mimi na wewe wenye umri wa miaka 25-30.
Tena kwa wenzetu wengine unakuta kampuni yenyewe unayofanya kazi hata haijasajiriwa!
Hawa wameona kuna wimbi kubwa la wanaoacha uanachama na kulamba chao, sasa wakaona kama wakiweka hii sheria na kuwazuia basi wataitumia pesa za wanachama watakavyo bila kuulizwa, Wanataka waturudishe miaka ya themanini mtu mpaka anakufa ajapata chake! mara "kumbukumbu zako zimepotea!" mara "ooh mwajiri wako alikuwa hawasilishi michango yako!"
Sasa kama ulichangia kipindi una miaka 20-25 ukaacha kazi ukaamua kujiajiri mwenyewe, umefika miaka 55 unaenda kudai chako unaambiwa wanakutambua kama ni mwanachama lakini hawaoni chochote ulichokichanga je utafanyaje?
Huu ni wizi wa mchana kweupeeeee