Hakuna malipo ya NSSF, PPF hadi umri wa kustaafu ufike!

Hakuna malipo ya NSSF, PPF hadi umri wa kustaafu ufike!

[h=2]Mkutano kwa wafanyakazi wote wanaochangia Pension Funds[/h]Wafanyakazi wote wanaalikwa kuchangia mjadala jinsi ya kujikomboa dhidi ya Uonevu.

Inahusu zaidi Michango yetu (jasho letu) katika Mifuko ya Pension and ufujaji unaofanywa kwa masilahi ya siasa.

Inatakiwa kuchangia kwa kupiga kura ya kusema HAPANA kuonewa (Poll)

Pia kuchangia mada siku ya hii tarehe 24 july, Jumanne.

Matokeo yake - Hitimisho tuwapelekee wabunge wetu akina Tundu Lissu, Zitto, Halima Mdee, Deo Filikunjombe, JJ Mnyika, Wenje na wengine ili wapeleke Hoja Bungeni liwe jambo dharura kujadiliwa.

Joke: " Hatuhitaji kura za wafanyakazi 2015"
 
Nimekuja kugundua kua Chadema katu hawawezi kulisemea hili suala mda huu.....wanasubiri wakati muafaka. Hii ni point ya kuwaingiza chadema madarakani,litasemwa sana wakati wa kampeni na ndo litakua jambia la kukatisha maisha ya Mahututi CCM
 
Inakera mno. Hivi walikuwa wapi hawa tunaowaita wapinzani? Na kwa nini wafanyakazi hatukushirikishwa hata kidogo?
 
Sijashangazwa na michango yenu humu kwa sababu nafikiri Watanzania bado hatujaelewa maana ya pensheni ni nini, lakini huu ni utaratibu wa watu angalau kuweka akiba, ili unapofikisha umri mkubwa huna uwezo wa kufanyakazi upate maisha yenye hadhi kwa kutumia ile akiba yako ambayo sasa inaweza kufidia kiasi cha fedha kwa kukosa mshahara, maana wakati huo hujiwezi....

Ndugu 'Kibai', unaandika hapa kama vile wewe ni mgeni nchi hii ya Tanzania, au unaandika kutetea jambo usilolijua.
Nchi hii iko kama ifuatavyo:-
  • Mtu wa hali ya chini hatetewi wala hakuna wa kumjali, sijua wewe unatoa wapi dhana kuwa sheria hii inawatakia mema watanzania. Angalia matumizi mabaya ya fedha za umma wakati wananchi wanateseka (mfano, chai na maandazi ya wafanyakazi serikalini ni sh. 15 billion !!! kwa mwaka, halafu dawa hospitalini hamna !!)
  • Mifuko ya pensheni inakopesha serikali pesa ambazo hazirudi (mfano ujenzi wa machinga complex !!)
  • Kumbuka swala la wastaafu wa iliyokuwa jumuiya ya afrika mashariki. Unakumbuka ?? Hawajalipwa hayo mafao yao kwa miaka 30 sasa !! Wamedai sana, walichoambulia ni virungu vya FFU !!

Hii ndio maana watu wengi wanaona bora kuchukua mafao yao mapema wakiwa na nguvu zao, kuliko kusubiri wakishazeeka (miaka 55 hadi 60). Maana wakienda kudai katika uzee huo, wataambulia virungu vya FFU kama wenzao wa afrika mashariki !!

Hapo vipi ??? Bado unaendelea kutetea udhalimu huu ???
 
Mimi nafanya kazi na mojawapo ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii. Jambo hili ni kweli, lilikuwa linasubiri muda mwafaka. Hakuna nchi duniani zenye mfumo wa pensheni kama wa kwetu zinzoruhusu wafanyakazi kuchukua hela zao wakiwa bado vijana. Ni Tanzania tuu ilikuwa na Mfumo huu. Mwisho wa siku mfanyakazi anastaafu anakuwa hana pensheni. Hivyo Mamlaka imefanya vyema kuzuia.

Usijisifu kwa kukopy na kupest mifumo ya watu wengine bila kuifanyia kazi. Hizo nchi zina mifumo ya hifadhi ya jamii inayojali mfanyakazi wakati wote,hata akiacha kazi kabla ya umri wa kustaafu.

Siyo hii yenu mnayotaka kumjali mtu wakati wa uzeeni bila kujali atafikaje uzeeni. Kama hakuna matibabu, hakuna ajira, hakuna mafao ya aina yoyote ya kukuwezesha kufika uzeeni unategemea kufika uzeeni?

Hizo nchi wana unemployment alowance schim au ajira mbadala mpaka unapofikia umri huo. Wafanyakazi tusimame imara tusidhulumiwe kwa namna hii.
 
tukisema tutumie vyama vya wafanyakazi naona kama vilelitakuwa hatujalipa uzito unalostaili, kwanini nasema hivi ni kwasababu hiki kitu kimepitishwa wakati vyama vyote vipo bungeni na hakuna mbunge hata mmoja aliyetuambia kitu chochote kuhusu ili jambo

Hii ilichomekwa kama ile ya gharama za uchaguzi .
 
Upuuzi gani tena huu unaletwa na kikwete?.........kwa hili sitakubali hela zangu wazichezee mafisadi nataka nikiacha kazi nichukue changu kwa sababu nnapoacha kazi ndo kustaafu kwangu kwa hiyo sina haja ya kusubiri miaka 55...............huu ni uhuni mwingine na kwa hili ccm inaweza kukosa kila kitu inaweza kukosa hata wenyeviti wa vijiji pale 2015.............alaaaaa
 
Kuna tetesi kuwa NSSF imepungukiwa sana na hela baada ya kuikopesha serikali na serikali kushindwa kulipa rejesho la mkopo hivyo wameona ni bora kuzuia watu kuchukua hela hivi sasa mpaka baadae watakapokuja na marekebisho ya sheria na kurudisha mfumo wa watu kuchukua hela zao pindi wnapoacha kazi, ngoja tuone...
Noti
 
Last edited by a moderator:
Ccm na serikali yao wasituletee upuuzo huo kwani nitahamasisha hata peke yangu ccm ikose hata wenyeviti wa vijiji ktk uchaguzi wa 2015.............hakuna mtu yeyote anayeweza kunishawishi kuwa nikifikisha umri huo ndo pesa zitakuwa na faida badala ya miaka yangu 30 nikiwa na akili na nguvu za kuwekeza kile nilichokuwa naweka huko.......ccm wasifanye mchezo na maisha ya watu na kwa taarifa yao hapo watakuwa wamegusa sehemu mbaya sanaaaaaaaa
 
Sasa wanalazimisha mpaka nifikishe miaka 55 ndo nichukue mafao yangu.. Wamechungulia huko kwa Mungu kujua ntadedi nikishapita hiyo miaka..? Huu ni uonevu..
 
Naona mwanzo ilikuwa kama tetesi naona wameamua kufanya kweli!
 
mazingira ya kuanzisha mfuko mwingine nauona!
sione manufaa yake kwanza hela tunaweka wenyewe huu nikama ujinga sasa
 
Mimi nafanya kazi na mojawapo ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii. Jambo hili ni kweli, lilikuwa linasubiri muda mwafaka. Hakuna nchi duniani zenye mfumo wa pensheni kama wa kwetu zinzoruhusu wafanyakazi kuchukua hela zao wakiwa bado vijana. Ni Tanzania tuu ilikuwa na Mfumo huu. Mwisho wa siku mfanyakazi anastaafu anakuwa hana pensheni. Hivyo Mamlaka imefanya vyema kuzuia.
Nimekutukana sana kindanindani ili nisipate ban!!!!
ninyi ndo mnagawana pesa zetu,mnawekeza kijingajinga kwa matakwa ya wanasiasa halafu unaleta uharo wenu hapa.
halafu wee jamaa mi nina hasira sana, kwanza siamini bado kuwa nitaikosa 30M yangu ambayo iko due mwezi ujao ila personally sintokubali kuikosa....

Kila mfumo unafanya kazi mazingira tofautitofauti...wajasiriamali unaowaona hapa tz waliotoka kwenye ajira wametokea hizo pension na ndo wanaajiri vijana wengi halafu unatuletea habari za nchi zingine wakati hujatuambia wazee wa nchi hizo wanaishije????

Wazee wetu hapa tz wanalala barabarani na wanaishia kumwagiwa *****..na ndo sababu serikali yenu imelaaniwa, unammwagia ***** bibi??!!! unategemea nini???
 
Huu ni uonevu wa wazi. Kwanza, sheria inasema kuwa ni lazima upeleke fedha kwenye mifuko ya jamii. Hiyo mifuko wanatumia michango yetu kufanya big investments (hasa kwenye majengo) ambazo sina uhakika kuna wanachama wanafaidika na faida inayopatikana. Sasa jamani, kama naanza kazi na miaka 25; halafu unihifadhie pesa zangu ambazo nitazipata nikifika 60 (35 years later); is it fair?

Nadhani kuna sababu nyingine behind this. Inawezekana ni masuala ya kupata ela ya ku-support existence ya CCM n.k. Another poor thinking by whoever proposed this change of law!

Waajiri watusaidie katika hili. Ni afadhali sehemu kubwa ya mishahara wahamishie kwenye other allowances kama housing etc. Hatuihitaji fedha wakati tukiwa na 60;tunahitaji fedha NOW ili tuweze kujijengea mazingira ya kuishi vizuri at 60.
 
huu ni wizi wa mchana hadharani kweupe kabisa, .........majambazi makubwa haya! .......manyonya damu! Lengo lao watu wooooote tuwe masikini hadi uzeeni na yenyewe yawe yanatumbua tu jasho letu mpaka yatakapo kufa! .............nitaichukia ccm mpaka tone la mwisho la damu yangu!
 
Wafanyakazi wa mgodi wa ggm kwa upande wa mining operation waligoma kufanya kazi kwa muda wa masaa 6 wakishinikiza uongozi kuwapa ukweli kuhusu taarifa ya NSSF, kwani wao hawakujulishwa mapema, mazungumuzo yalidumu kwa muda mrefu bila mafanikio kwani viongozi waliokuepo hapo pamoja na mwanasheria wa ggm walidai kua od & hr (philemon tano) pamoja na md (gary daniel) wote walisafiri kwenda dar kufuatilia suala ilo.

Kwa kweli hali si swari sana ndani ya mgodi kwani kila mtu anadai ana mkataba mfupi na ggm sasa hawezi kusubiri mpaka 55yrs,na isitoshe pesa yenyewe haina riba.

Nawaomba sana watu wote tushirikiane tukatae upuuzi huu na utapeli wa ccm na nssf ya ccm
nilishidwa kupiga picha kwani tunapoenda kazini haturusiwi kua na simu,hasa sisi wanafunzi tunaofanya field
 
jamani Hkuna umasho wa wafanyakazi kwa hili!? agrrrrrr!!!!!!!!!

Kwa hili Serikali imejivua nguo... walahi nitaongoza mgomo kama mtaniunga mkono... haiwezekani, niache kazi leo waniambie nasubiri mafao yangu niliysevu kwa miaka 2 tu mpaka nitakapofikia umri wa kustaafu.... yaani akitokea mtu akakufukuza kazi ukawa jobless, ukaamua kurudi bushi kulima, ca u imagine inasubiri mafao yako ya sh 960,000 mfano mtu wa mshahara wa sh 200,000, na ana umri wa miaka 27- akifanya kazi kwa miaka 2, akaundiwa zwengwe akifukuzwa kazi et asubiri for another 28 years ndo apate sh 960,000 yake... with iflation rate sijui.....

jamani akina Mgaya, Mkoba na sisi wote... si tukatae hili...
 
Watanzania hasa wafanyakazi, huu ndio Wakati wa kung'oa serikali ya magamba na kuweka serikali ya Watu inayosikiliza. Kuna mantiki gani ya Kuzuia withdrawal benefits Wakati serikali hailipi unemployment benefits?

Kwa nini uzuie withdrawal benefits? Fedha za wafanyakazi zinaenda kuwekezwa Kwenye miradi mfu Kama kigamboni bridge, kiwira coal mine, machinga complex halafu unasema mfanyakazi asilipwe withdrawal benefits kweli serikali hii inamjali mwananchi wake?

Tuzinduke watanzania Muda wa CCM umekwisha!
 
jamani, tunakutana wapi kujadili au kufanya tukio?

Hakuna movements zozote zilizoanza, nataka kujiunga.
 
Back
Top Bottom