Hakuna malipo ya NSSF, PPF hadi umri wa kustaafu ufike!

Hakuna malipo ya NSSF, PPF hadi umri wa kustaafu ufike!

Mliwaleta NetGroup solution. Tukapiga kelele, mkawaweka kwa nguvu -tukaa kimya
Mkawaleta wahindi kuendesha TRL -tukakaa kimya
Mmegawana hela za EPA -tukakaa kimya
Mkatuletea mitambo feki ya kufua umeme -tukakaa kimya
Mkaona hatuongei, mmeamua kutufuata hadi chumbani. Nawaambieni siku tukiamua kuongea, hakuna atakayeweza kutunyamazisha
 
Hii habari imenichanga mpaka njaa inaniuma sana, wacha nikale halafu nioshe uso labda nitapata picha, very sad.
 
Ebanaa Dah!..kweli jamaa wamepania kutumaliza watz,eti..."Tunaondoa withdraw benefit ili wanachama waweze kukopa nyumba"....shit!....nyumba zenyewe mmejenga ngapi za kuwatosha wachangiaji wenu wote, kwa nini basi msitukopesha pesa zetu nyumba tujenge katika viwanja vyetu.....hakika hili linahitaji mass strike shime wakuu tutafakari.
 
Hii kitu imeniconfuse sana...nimeshapandisha kuta za nyumba yangu naisubiri pension yangu nipaue na nilishaanza kumjibu landlord kwa kujiamini...naona sasa inabidi nirudishe unyenyekevu....duh hii serikali tukiendelea kunyamaza watakuja kutunga sheria kuwa tusilipwe mshahara wote zingine serikali ikutunzie.....kama jeshini wanakatwa 5000 kila mwezi za kusafirishia maiti yako ukifa na usipokufa mpaka ukastaafu ndo basi tena imeenda hiyo ..lakini! Mtu anakulipa fedha ukiwa umekufa who knows kuwa umetendewa haki????kwenye hili la mafao mpaka miaka 55 wakati wanasema life expectance ni miaka 45????kuna dhuluma hapa si bure!!!!
 
Hii serikali ni ya *******, chama kinachoiongoza ni cha *******, na viongozi wake ni dhaifu mno.

Hivi hii ppf wafanyakazi wamepigania kutoka huko lakini sasa ndio serikali inapitisha sheria ya ******* hivi ili kuwabana wafanyakazi! Yaani unamlazimisha mtu kufanya kazi kwa muda asiojisikia? Who the hell is Irene? Kama mafao ni mpaka miaka 55 na mtu akijitoa hapewi mafao, kwa nini pia isiwe hiari kujiunga? Nadhani hata magamba wafanyakazi kama wana akili hata za kubangaiza wataona usenge wa serikali na wakuu wao. Huu usenge ukomee 2015. Hata mnipige burn potelea mbali

Hebu kuwa na staha. Kumbuka huu ni mwezi gani!
 
Hii itasababisha wafanyakzi waingie mtaani

Kama kujoin wanatwambia tuingie kwa hiari kwanini watupangie kutoka?
 
I'm Ok if they take a good consideration of TIME VALUE OF MONEY..Wakikaa na mil100 yangu leo thamani yake si mil100 tena in 30 years. Considering inflation na other economic factors, wawe tayari kunipa zaidi ya mil100 na walipe riba kwa kukaa na pesa yangu miaka yote hiyo kama wanavonidai nkikaa na pesa yao ya serikali
 
Nani alikwambia kwamba unemployment benefit ni sawa na withdrwal, pamoja na mapovu yote lakini unashindwa kutofautisha hiyo kitu rahisi namna hii, okay sasa ukiacha kazi kampuni A ukaajiriwa kampuni B unalipwaje unemployment benefit? Kilichopo ilikuwa na lies, mtu unahama kazi unasema umeacha kazi halafu ulipwe withdraw! No way, hiyo ni sawa kabisa ifutiliwe mbali, kinacho wasumbua ni kwamba hamuoni mbali, na kwa taarifa yako sheria hizi huwa ni za lazima, hivi hivi nani ataweka akiba, kuna mtu eti anasema anaweka volunatary akitaka anachkua, hii mifuko siyo benki, kama CRDB, kikiingia hakitoki hadi labda ufe au uzeeke, na kwa taarifa yenu hata hao wenye mafao amabyo ni makubwa huwa hizi hela hazitoshi wakifikia huko, wewe unazitaka leo uzifanyie nini? niliwahi kusema hapa, zaidi itakuwa ni mipombe na kiti moto tu! halafu nenda usome vizuri tofauti ya unemployment benefit na withdrawal, withdrawal siyo benefit!
Below ni ILO standard unemployment benefit ndo imeondolewa kama withdraw benefit

ILO Minimum Standards.​
International Labour Organisation set an instrument which was adopted at its35​
th session in June 1952, popularly known as ‘Social Security (minimumStandards) Convention No. 102. Itemised number of contingencies andbenefits required in the minimum standards convention include’ Old Age,Invalidity, Survivorship, Employment Injury, maternity, medical Care, sickness,​
Unemployment and Death.
 
Jamani kwa msio elewa kama Rejao miner tunalalamika kuhusu nssf kwa sababu kwanza security ya kazi migodini haipo supervisor akigombana hata na wife wake akija kazini anamalizia hasira kwako na kazi inaiisha on the same day unapewa mshahara uliofanyia kazi na nauli ya mizigo ambayo ni sh.400 kwa km pamoja na watoto kama ukifukuzwa tarehe tano ya mwezi wanadeduct siku ambazo hujafanyia na nssf yako sasa haitoki tuje kwenye makosa yanayoweza kukufukuzisha1.pombe kila siku esp pay day getini hauingii mpaka upmwe sasa hapo ujue ukiwa day shift ukikaa bar mpaka saa tatu kesho kipimo lazima kikukamate maeneo kama Dar mtu anatoka job anakaa bar mpaka saa ngapi sijui na kesho job kama kawa mgodini kinaota,kuvuta sigara kusiko ruhusiwa no job,kuendesha gari bila kufunga mkanda dereva au abiria wote kazi hamna kutofata sheria ya usalama mf kutovaa p.p.e kama miwani au gloves kaZi hamna hebu niambie kwa haya machache wewe unaweza kudumu hata miaka mitano wewe yaani mining watu kila siku wanafukuzwa kesho wanaajili ndiyo maana hamna wasomi wanaokaa mgodini kwanza kama Hr akienda against na wazungu nae wanafukuzwa mifano ipo juzi wamemfukuza manager hour halafu wakamrudisha mwingine waliye mfukuza nyuma yake kwamba ni mzee anatakiwa astaafu kisa anakataa kuendana nao ndiyo maana siye watu wa migodini kimbilio letu lilikuwa nssf bado mf underground kuna fumes mmbaya shimo liko km.2kwenda chini unakwepana na mwamba masaa kumi na mbili kila mwaka watu wanakufa na silicosis sancoma haitibiki mpaka india wanachofanya ni kukufukuza kazi kwamba wewe ni mzembe guys na mengine mengi tu sisi tunaomba msaada na sapoti zenu kwani tusha kufa tayari tunasubiri siku tu usinilinganishe kazi yangu na mwalimu au mtu wa IT au mtu wa serikalini ilitakiwa serikali ingeanzia na sheria za kulinda ajira zetu kwnza kabla ya kuleta sheria hii
Angalizo kwa wabunge wote ambao majimbo yao yapo maeneo yenye migodi kama hamta tupa ushirikiano kwenye hili jambo 2015 nanyie.mna kazi kubwa kurudi bungeni kwani migodi hii ina maelfu ya watanzania. Kwa uchache ni pamoja na mh.Maige wa Msalala,Lembeli Kahama,Kigwangala Nzega,na mbunge wa Geita jina limenitoka mie naona kuwapa kazi wakina Zitto au Mnyika nikuwaongezea majukumu ambayo siyo yao
 
malalamiko yaishe. haya semeni sasa Wafanyakazi tuchukue hatua gani?
 
Nani alikwambia kwamba unemployment benefit ni sawa na withdrwal, pamoja na mapovu yote lakini unashindwa kutofautisha hiyo kitu rahisi namna hii, okay sasa ukiacha kazi kampuni A ukaajiriwa kampuni B unalipwaje unemployment benefit? Kilichopo ilikuwa na lies, mtu unahama kazi unasema umeacha kazi halafu ulipwe withdraw! No way, hiyo ni sawa kabisa ifutiliwe mbali, kinacho wasumbua ni kwamba hamuoni mbali, na kwa taarifa yako sheria hizi huwa ni za lazima, hivi hivi nani ataweka akiba, kuna mtu eti anasema anaweka volunatary akitaka anachkua, hii mifuko siyo benki, kama CRDB, kikiingia hakitoki hadi labda ufe au uzeeke, na kwa taarifa yenu hata hao wenye mafao amabyo ni makubwa huwa hizi hela hazitoshi wakifikia huko, wewe unazitaka leo uzifanyie nini? niliwahi kusema hapa, zaidi itakuwa ni mipombe na kiti moto tu! halafu nenda usome vizuri tofauti ya unemployment benefit na withdrawal, withdrawal siyo benefit!
kibai wewe ni kilaza wa kutupa KALALE WEW BADO MTOTO try kutumia hata akili yako ugoogle kidogo see below how WIthdraw benefits are defined by pension scheme

PPF
[TABLE="align: left"]
[TR]
[TD="colspan: 2"]WITHDRAWAL BENEFIT
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: news, colspan: 2"]Qualifying condition
Where a member ceases employment through summary dismissal or termination.
Mode of granting withdrawal benefit
i) Granted as Lump sum immediately on ceasing employment


SOurce: :: PPF Pensions Fund ::-


LAPF

WITHDRAWAL BENEFIT


This is a lumpsum payment equal to members’and employers’ contributions plus accrued interest payable to a member who has resigned from employment, has been retrenched, dismissed or terminated on medical grounds, abolition of office, or any other cause.


soURCE:LAPF Tanzania: Withdrawal Benefits





PSPF

WITHDRAWAL BENEFIT



[TD="width: 513"] Marriage: Payable to a female member who due to marriage proves to the satisfaction of the Director General that she has permanently given up employment and will not seek any gainful employment in the
Public service;
Maternity : Payable to a female member who proves to the satisfaction of the Director General that in consequence of her giving birth to a child she has permanently given up employment and will not seek any gainful employment in the public service;
Emigration: Payable to a member who proves to the satisfaction of the Director General that he is emigrating or has emigrated and has no intention of returning to the United Republic of Tanzania and has not been employed by employer who is liable to make contributions in respect of himself for at least six months
Qualifying conditions
  • Should be a member registered with the Fund;
  • Should have contributed to the Fund.
[/TD]


[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

 
Last edited by a moderator:
Kweli hii Nchi itajengwa na Wananchi na italiwa na wenye chama. Bilioni zipo Uswiz zinawasubiri wakuu wastaafu wazitumbue fresh! Wakuu naomba mnieleweshe kitu kinachowasumbua Wazee wetu wa Afrika mashariki ni nini kinachosumbua kulipwa pesa zao za mafao?
 
Mbona mimi sielewi,kila kukicha zinapatikana habari mpya.
Tarehe 18 jully 2012 baada ya taharuki kuzidi kwa wafanyakazi baada ya mifuko ya hifadhi ya jamii NSSF NA PPF kufanya semina hapa geita gold mine (GGM) na kukiri kuwa hili jambo lipo na litaanza kufanya kazi hivi karibuni
jambo lililopelekea watu wengi kuacha kazi.
Tarehe 18Jully 2012 katibu wa TAMICO wilaya ya geita akiandamana na viongozi wengine alienda Dar es salaam kuonana na mkurugenzi wa SSRA na kufanya nae kikao.
Mkurugenzi wa SSRA alieleza kuwa ni kweli mswada huo wa marekebisho ya mifuko ya hifadhi ulipitishwa na bunge kuwa sheria na bunge mwezi April 2012.
Lakini wanasubili Rais atie saini ili sheria hiyo ianze kufanya kazi rasmi na aka ahidi kuja kufanya kikao na wadau mwanzoni mwa mwezi wa nane hapa Geita.
 
Kwa hali ilivyo sijui hicho kikao cha kukusanya maoni ya utungwaji wa kanuni itakuwaje?
Wameshindwa kuwashilikisha wadau kwenye utungwaji wa sheria wanataka kutuvika kengele kwenye kanuni.
Kimsingi mimi binafsi sikubali hasa ukizitia ajila za wafanyakazi wa migodi hazilindwi kisheria.

Ikiwa takilibani miaka kumi(10) toka migodi mingi ianzishwe tayari tumeshuhudia watu wengi wakipata madhala ya kuugua migongo na kupata ulemavu wa viungo kama mapafu na wengi huishia kufukuzwa kazi wakiwa katika matibabu sasa unapomzuia huyu mtu kuchukua fedha zake unataka afe kwa kukosa matibabu
sababu kile alichokuwa anakitegemea kimsaidie ndio unakizuia.

Pili makampuni ya migodi yakitu kinachoitwa BLACK LIST ambacho kina mzuia mfanyakazi anapofukuzwa na kampuni moja kutoajiliwa na kampuni nyingine
hata pale mtu anapopata ajali ya mashine au gari habari zake huwekwa kwenye blacklist.unategemea mtu huyu atafanya nini zaidi ya kuchukua hizo fedha za hifadhi ili japo apate mtaji aweze kujikimu yeye na familia yake?
Kwa hili nipo tayari kufa ili niipate haki yangu,Jamani hivi kweli hawa walioipitisha huu mswada kuwa sheria wanajua suluba tunazozipata huku migodini?
Pamoja na kodi( PAYE) kubwa tunazo katwa sasa wameamua kuchukua hata kidogo tulichonacho?
Kwa hili mimi nasema hapana hakuna mtu anayeweza ku operate Dump truck,Dozzer na Excavetor kwa miaka 15 ili awe na sifa ya kupata mafao kabla hajaugua mgongo.
Kwa hili nasema hapana.
Waziri wa kazi alipokuja hapa geita aliogopa kupanda kwenye Trex truck kutakana na ukubwa wake,Lakini hakusikitishwa na kitendo cha watanzania kilipwa fedha za madafu wakakati wana operate mashine inayobeba tonne 250.namashine hiyohiyo watu wanalipwa us dollar 3500-4500. Wangebolesha kwanza maslahi yetu halafu ndio walete hili.
 
UFAFANUZI KUHUSU FAO LA KUJITOA KATIKA MAREKEBISHO YA SHERIA ZA MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII.

Ufuatao ni ufafanuzi mfupi kuhusu marekebisho ya Sheria za Mifuko hasa kuhusu fao la kujitoa.

20 JULAI, 2012

1. Kama mtakumbuka Sheria za Mifuko ya Hifadhi ya Jamii pamoja na Sheria ya Mamlaka zimefanyiwa marekebisho na kupitishwa na Bunge tarehe 13 Aprili, 2012. Sheria hiyo tayari imeshasaininiwa na Mheshimiwa Rais na imeanza kutumika rasmi. Marekebisho haya yanawahusu wafanyakazi wote nchini mwetu bila kubagua sekta yoyote ile.

2. Kwa mujibu wa marekebisho hayo fao la kujitoa (withdrawal benefits) yamefutwa na kuanzia sasa hayatakuwepo. Mafao hayo yalikuwa yanatolewa pale mwanachama alipokuwa anaacha kazi. Sasa mwanachama wa Mfuko atapata mafao yake pale atakopfikisha umri wa kustaafu kwa hiari (miaka 55) au kwa lazima (miaka 60) au pale anapopata ulemavu wa kudumu.

3. Kwa kuzuia fao la kujitoa mwanachama anapata fursa ya kupata mikopo ya nyumba kwa kutumia dhamana ya michango yake kama ilivyoelezwa kwenye Sheria ya SSRA kipengele cha 38.

4. Marekebisho hayo kuhusu kuzuia mafao ya kujitoa yamefanyika ili kutimiza lengo na madhumuni ya hifadhi ya jamii ambayo ni kuhakikisha kuwa mwanachama anapostaafu anapata mafao bora yatakayomwezesha kumudu maisha ya uzeeni wakati ambapo nguvu ya kufanya kazi tayari imeshamwishia.

Mafao ya kujitoa yanapunguza na hata kuondoa kabisa kinga ya mfanyakazi pale anapoumia kazini au anapofika uzeeni.

5. Tunawaomba muwaelimishe wafanyakazi umuhimu na madhumuni ya mafao ya hifadhi ya jamii. Hifadhi ya jamii ni nyenzo mahususi iliyowekwa kuwasaidia wafanyakazi kuendesha maisha yao wakati wanapokuwa wameishastaafu tayari. Umasikini wa kipato wakati wa uzee ni mojawapo ya changamoto ngumu kukabiliana nazo kwa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla. Tunawasihi tena muelimishe wafanyakazi kuhusu jambo hili. Tafadhali msisite kuwasiliana na Mamlaka pale ufafanuzi zaidi utakapohitajika

6. Kwa kuwa marekebisho hayo yamesainiwa na kuanza kutumika rasmi kama sheria, mafao ya kujitoa hayawezi kutolewa tena na wafanyakazi watakaoacha kazi kwa sababu ya marekebisho ya kipengele hicho watakuwa hawajaijitendea haki wao wenyewe na pia itakuwa ni kunyume cha Sheria.

Mamlaka inaandaa kanuni za mafao ambayo lengo lake ni kuboresha maslahi ya wanachama, kanuni hizo zitajadiliwa na wadau wakiwemo vyama vya wafanyakazi na waajiri ili kupata maoni yao.

7. Tafadhali muwaelimishe wafanyakazi kwamba pamoja na kuzuia fao la kujitoa, mafao mengine ambayo ni muhimu kwa sekta ya Madini yataendelea kutolewa kama kawaida. Mafao hayo ni Kama vile kuumia kazini pamoja na fao la ulemavu

8. Tumesikia kwamba tayari kuna hofu imejijenga kwa wanachama kuhusiana na fao la kujitoa. Ikumbukwe kwamba baadhi ya Mifuko ilikuwa inatoa fao hilo kinyume cha Sheria kwani katika Sheria zao hakuna fao la kujitoa. Tunapenda kusisitiza kwamba wanachama wawe watulivu wakisubiri miongozo.

9. Tunapenda kuwahakikishia kwamba katika hili maslahi ya wanachama yatalindwa na hakuna mwanachama atakayepunjika kutokana na utaratibu huo.

Mamlaka imepanga kutembelea wafanyakazi wa sekta ya madini katika juma la kwanza la mwezi Agosti 2012 ili kutoa ufafanuzi zaidi kwa wanachama wote.

Tunatanguliza shukrani za dhati kwa ushirikiano.

Wenu.
Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Hifadhi ya Jamii

Irene Isaka
MKURUGENZI MKUU

 
hii nayo ni namna ingine ya kufanyia ufisadi pesa zetu...ni wangapi wanaofikisha hayo ma-miaka ya kustaafu kwa siku hizi? lifespan yenyewe imeshuka mpaka 45 years, sasa hizo hela watampa nani? ina maana kwa sasa ukimwagwa kibaruani unasota weeee..mpaka uonekane umzeeka ndio ukadai hela zako...total rubbish kuanzia aliyetunga mpaka na aliyesaini hilo lisheria libovu!!!!!
 
Kwa mujibu wa marekebisho hayo fao la kujitoa (withdrawal benefits) yamefutwa na kuanzia sasa hayatakuwepo. Mafao hayo yalikuwa yanatolewa pale mwanachama alipokuwa anaacha kazi. Sasa mwanachama wa Mfuko atapata mafao yake pale atakopfikisha umri wa kustaafu kwa hiari (miaka 55) au kwa lazima (miaka 60) au pale anapopata ulemavu wa kudumu.

Sasa jamani nauliza ina maana nikiachishwa kazi au nikaamua kuacha kazi kabla sijatimiza miaka 55.sitoweza kupata mafao yangu??. da hii balaa sasa.......nawaonea huruma wafanyakazi wa migodini na sekta nyingine ngumu ambao wanafanyakazi ktk mazingira magumu halafu maisha yao kufikisha miaka 55 ni ndoto. si uonevu huu.

hizo fedha wanabaki nazo ili iweje kama sio wizi.

Nawakilisha!
 
napata wasi wasi na hawa watu wa JF so called great thinker. yaani hivi ni kweli hamjui kuwa lengo la hiyo hifadhi ni kukusaidia while huna uwezo wa kufanya kazi tena' fainal uzeeni ' . sasa wewe unataka upewe ufanye biashara ukifika fainali utapata wapi pesa za kujinunulia pad wakati unaharisha kama ngisi kitandani hata kujiosha huwezi.

think hard great thinkers
 
Back
Top Bottom