Hakuna malipo ya NSSF, PPF hadi umri wa kustaafu ufike!

Hakuna malipo ya NSSF, PPF hadi umri wa kustaafu ufike!

Watanzania wana matatizo sana, nani aliwadanganya eti Pension ni kama Bank?, kwamba unaweka leo na muda wowote ukijisikia unaenda kuchukua?. Kuchangia mifuko imewekwa kisheria na kuwa lazima kwa sababu kuu hizi ambazo zote ni katika kucover social distress/ problems:

1. Unaweza ukaumia kazini na ukashindwa kabisa kuendelea na kazi maisha yako yote, fungu lako liliko katika hifadhi litakuhifadhi.
2. Unaweza ukafariki (wote tutakufa), na bahati mbaya hujajipanga au hata kama umejipanga..wale warithi wako wanapata walau pa kuanzia kupitia michango yako uliyokuwa ukichangia.
3. Ukazeeka na ukiwa hauna nguvu ya kuendelea kufanya kazi, lakini kupitia mifuko hii ukawa unapata pensheni ya kila mwezi ambayo ni kama ulivyokuwa ukipata msharhara japo itakuwa by 60-80% ya mshahara na marupurupu yako ya awali ila inasaidia kuliko kukaaa miaka hadi mia huna kipato chochote.
4. Kufaidika kwako binafsi Mfano NSSF jana wamezindua kukopesha SACCOS, PPF wanayo hiyo..so kama ni member na mko kwa SACCOS hizo mnakpoeshwa kisha unaendelea na maisha.
5. Kuwa sehemu ya msaada kwa jamii i.e Mifuko inajenga hospitals ambazo kama hazitakusaidia wewe basi mjomba, shangazi, kaka, dada au hata watoto wao etc etc.
6.nakadhalika.

Hawa wanaojifanya wanaacha kazi ili wachukue hela zao 'masikini ya Mungu' hawajui maana ya pension sheme. Inabidi mifuko ifanye kazi ya ziada kuwaelimisha kwa kina.

Hivi hizo hela unazokimbilia kuzichukua sasa hivi (i.e 10% ya kwako na 10% ya mwajiri) kama ungepewa kila mwezi sasa hivi ungekuwa nazo kweli?. Angalia salary slip yako kisha ujipe majibu..huenda ndo ingekuwa ya BAR, Mafuta ya gari, kuhonga, kununua nguo etc! But MIFUKO inatunza kwa niaba yetu, inafanya investments ili kuja ku-cover social distress that may happen now or in future na kukupatia mafao Bora.

Guys, be great thinkers ki kweli kweli na mjisumbue kufuatilia mambo. JF isiwe mahali pa kupoteza watu, kila jambo linawekwa kisiasa siasa tuu.

I salute you Mr. Donyongijape,

I must admit to be impressed with your extensive and staunch comments in favor of the enacted law in question.

I have, however, little trouble with your premises. It's fine from academic view-stand, also in some quantity from a pParliamentarian mindset. But since you are as learned as your herein work goes, just bother to behold from those standing on the other side of the hill. I deduce from their opinions several things, probably more:-

1) Practically real-life experience view

This group is variant in composition but shares same and similar philosophy. As such They need to be won. They expect to be convinced. They don't want their future being held in perpetual ransom with this/any failed government...similarly to previous govts in all areas of fundamental basic human needs.


2) Moral authority from political platform - the lack of

a) Simply put, if it was that good intentioned law then why not one of government faces bothered to propagate the trumpet for such a law?

b) If it was that important an act why the secrecy of its establishment? Will you freely attach transparency to its creation?

c) The records of both, the major beneficiary (i.e the govt) and the scandalous-run social funds, begs more than a mere selective approach of adding an act to an evidently unjust and unfair social plane.

d) Any good success expected should be travelled in the vehicle of trust which thru justice will buy legitimacy. What do you think is relationship of wananchi and the govt in the view of the above?
 
Kukitokea maandamano ya kupinga hii kitu nitajitokeza kwa nguvu zangu zote,chuo kwenyewe nimesoma kwa shida nikiungaunga,nashinda njaa mpaka nikaambulia ulcers,sikupata mkopo wa wa kusoma elimu ya juu,halafu leo wanataka kuninyonya na kunikosesha uhuru na fedha nilizochuma kwa tabu,kodi kubwa nayo wanakata sasa mi nibaki na nini,ajira zenyewe hazina security ukifukuzwa kazi unaweza kukaa maisha yote bila kazi,hiyo miaka 55 utafikisha vipi kwa hali hii mbaya ya huduma za afya, ni uonevu mkubwa
 
nssf wanafanya biashara kwa kutumia fedha za hifadhi ya wanachama wake, tatizo uwekezaji wa nssf umekuwa wa maamuzi ya kisiasa zaidi kuliko ya kiuchumi. hili ndilo tatizo lilosababisha viwanda vya serikali kufilisika na kuishia kubinafsishwa. sitashangaa kama nikisikia nssf imeshafulia. hebufikiria uwekezaji kama machinga complex kweli ni economical justifiable?
 
Hivi sijajua will it take in consirderation the time value for money? Mimi nina mil. 5 nssf nimeacha kazi recently na nina miaka 30 so nitapata baada ya miaka 25. My major concerns are, 1. Since i was working with a very small enterprise will the firm exist by that time? 2.Will the signatory be still living by that time? 3. How much is 5 mil gonna worth in the next 25 yrs? 4. What did mr. dhaifu see to be very important for this?
 
Wakuu naomba kurekebisha hapo hii sheria sio ya NSSF pekee bali ni ya mifuko ya jamii so PPF,PSPF,LAPF na mingineyo huu kweli ni uthibitisho wa viongozi wetu kufilisika fikra....
 
Jaribu kuelewa jinsi hii mifumo inavyofanya kazi.Lengo lake ni kuwafaa wafanyakazi uzeeni au wanapopata ulemavu wa kudumu kazini. Hii siyo 401k type.

well sasa inaonekana hujaelewa wenzio wanagombea nini... siwezi kukusaidia kwa kweli.
 
Hii ndiyo standard procedure ya PENSION FUNDS duniani karibia kote, hakuna cha ajabu hapa.

Ukiruhusu mtu achukue pesa wakati wowote basi mfuko unashindwa kujiendesha na kuleta matatizo makubwa kwenye jamii.

Angalia hapa kwa pension UK:
Can I withdraw money from my pension scheme? | Money | guardian.co.uk

Kuna pension ambazo zinaruhusu kutoa mapema ila na penalty kubwa kama 10%, lakini wangeweka hiyo nadhani watu wangekuwa wanalalamika kwa nini wanakata 10%.

Pia kusema life-expectancy Tanzania ni 45 inapotosha ukweli, life-expectancy ni 45 kwa sababu ya infant mortality rate kubwa kwa Tanzania, infants hawajawahi kuchangia pension fund yoyote.

Edit:Life expectancy ya Tanzania ni 53 so hata hiyo namba ya 45 naona imepitwa na wakati. Ukitoa watoto itavuka 55 im sure.
 
Nimekuwa najiuliza nini kilitokea siku ilipopitishwa sheria hii. Ina maana wale mabeki VISIKI na MAKINI pale bungeni(DEO,JJMNYIKA,LISU,ZITO,HAMAD RASHID,KAFULILA,MACHALI,MKOSAMALI,MDEE,MSIGWA,NYERERE J,ZAMBI,MAKAMBA. hakuwepo hata mmoja? Mbona hawakufurukuta kuzuia jamani au ilipitishiwa magogoni mbele ya madiwani wa chama chao?najua mpo humu baadhi yenu waheshmiwa tafadhali tupeni mwanga nn kilitokea.
 
Nimekuwa najiuliza nini kilitokea siku ilipopitishwa sheria hii. Ina maana wale mabeki VISIKI na MAKINI pale bungeni(DEO,JJMNYIKA,LISU,ZITO,HAMAD RASHID,KAFULILA,MACHALI,MKOSAMALI,MDEE,MSIGWA,NYERERE J,ZAMBI,MAKAMBA. hakuwepo hata mmoja? Mbona hawakufurukuta kuzuia jamani au ilipitishiwa magogoni mbele ya madiwani wa chama chao?najua mpo humu baadhi yenu waheshmiwa tafadhali tupeni mwanga nn kilitokea.
 
unajua ndugu, wakati ule kulikuwa na zuala la Kukusanya saini 70 za kumng'oa PM, hiyvo haikuwa rahisi sana kulipatia umakini suala hili hata kidogo. kama inavyojua suala la ripoti ya CAG lilizua mtafaruku na sana wakati ule!!
 
hivi wewe mpaka leo hujui kelele za hao wabunge uliowataja ukimtoa mnyika tuu ni za kuomba rushwa. kalaga baho!
 
Nimesiktishwa sana na sheria ya mafao ya wafanyakazi ambayo kimsingi inamlazimisha mfanyakazi kuchukua mafao yake ambayo ni sehemu ya mapato yanayokatwa kwenye mshahara wake kuwa eti atalazimika kuyachukua baada ya kufikisha miaka 60.Huu ni wizi wa wazi kwa wafanyakazi maana wanaofikisha miaka tajwa ni wachache sana ukilinganisha na hali ya mazingira ya kazi yalivyo si rafiki. Nafikiri walioandaa sheria hii ni wazee ambao wamebakiza miaka mitano au miwili kufikisha miaka 60 au 55. Wangekuwepo vijana ambao wanaanza kazi na miaka 25 hakika wasingekubali sheria hii kupitishwa maana ni kandamizi sana na wale ambao wanakufa kabla, wategemezi wao wanapata tabu sana kupata mafao ya wazazi.Ni vema viongozi na watetezi wa haki za binadamu kupinga sheria hii na kumtengenezea mfanyakazi sheria inayoruhusu kila baada ya miaka 5 anaweza kuchukua mafao yake ya miaka mitano au 10.Zaidi ya hapo wafanyakzazi wanaibiwa sana na wanaofaidi ni wale watumishi wa taasisi zenyewe ambao pengine si wachangiaji .
 
siku yangu imeharibika.. eti PPF wananiambia wanasubiria muongozo namie nilikuwa nimeshajafaza fomu ya kuwithdrawal na wawo wamepewa na SSRA muongozo kuzuia malipo yote ya watu wanaotaka kujitoa huu ni udhalimu aiseeeeeeeee
 
Nikiacha kazi leo wanangu wafe njaa kisa sijafikisha miaka 60? Wabunge wakipitisha hii tuwapige mawe.


Mh

Hivi tuna serikali kweliiii? au ni wakolini wamerudi tena?

Mwanangu hana ada, nisubirie mpaka nisataafu au nikope benki kwa riba wakati nina hela zangu kwa maIlluminati!

Huu ni ukoloninuliopitiliza, tufanye massive campaign
 
Wafanyakazi wote wa secta binafsi tugome!

Tufanye mgomo usio na kikomo kubadili hii sheria.
 
Sasa kama nchi yetu inafanya maamuzi kama haya, tutawezaje kuukimbia ushoga? Mi nafikiri ni muda tu haujafika, watapitisha sheria ya ushoga huku wakituonyesha na mfano kabisa. Evil spirit runs this world.

Eti wanakuja na gear ya kukukopesha hela zako kwa riba ya 22% . Whaaaaaat! Adonaaaaaay, Its time you rescue us
 
Back
Top Bottom