Hakuna malipo ya NSSF, PPF hadi umri wa kustaafu ufike!

Hakuna malipo ya NSSF, PPF hadi umri wa kustaafu ufike!

life expectancy ni 47, mafao yenyewe milioni saba, thamani ya shilingi ndio usiseme

tatizo
 
Tumekwisha. Twaliwa twajiona. Yaani tokea 2003 napiga mzigo kule NSSF kuna kama Hiace nne leo wanasemaje? Du tumekwisha. Mgaya upo wape wewe??????
 
Jamani hii ni hali ya hatari kwa wafanya kazi kwani yanayosemwa kuwa haya mabadiliko ni kwa manufaa ya mfanyakazi ni uongo mtupu.
Cha kujiuliza ni kuwa kwa nini SSRA ijali maisha ya mfanyakazi baada ya miaka 60 bila kwanza kujali maisha yake ya kabla ya miaka hiyo ya 55 -60?
Irene anasema kuwa mafao mengine ya manufaa kwa wafanyakazi yataendelea kutolewa kama mafao ya kuumia kazini na ulemavu lakini ni kwa mfanyakazi ambaye yuko kazi. Hakuna mafao ya ulemavu kama umeshaacha kazi, Hakuna mafao ya matibabu, wala ya kuumia ukiwa nje ya ajira.
Kwa lugha raisi ni kusema kuwa hakuna uhusiano kati ya mwanachama aliye nje ya ajira na mifuko ya jamii, sasa kwa nini waendelee kushikilia fedha zako wakati hawajui utafikaje mika hiyo ya sitini?

Kwa taarifa mimi niko mgodini Geita, watu wameshaweka tools down mpaka walipwe au waakikishiwe kuwa fedha zao watazipata wakati watakapokuwa na mahitaji nayo na si kwa wakati watakapotaka SSRA. Wafanyakazi tuungane katika hili.
 
Tumekwisha. Twaliwa twajiona. Yaani tokea 2003 napiga mzigo kule NSSF kuna kama Hiace nne leo wanasemaje? Du tumekwisha. Mgaya upo wape wewe??????

Huyu wala usimtegemee.......kanunuliwa kama fungu la nyanya gengeni
 
payee wanazotulamba kila mwezi haziwatoshi bado wanataka na mafao!! na hawa wabunge walipitisha vipi!!!!! hivi haikuwa sahihi kujadiliana na wafanyakazi kwanza???????????????? miaka 55!!!!!!!!!!!
 
huyu dada alikuwa stanbic bank, sasa ndio yupo hapo SSRA! basi tena hawezi kuwa kama alivyokuwa stanbic, roho ya kizalendo imemuhama, inabidi afuatishe jk anavyosema! shame on them na mafao yetu! wanaamua, kwani walitushirikisha??? i hate this government! hiyo 2015 ifike haraka!
 
I am supporting this move. Wengi wetu tutaishia kuwa masikini huko uzeeni iwapo huu utaratibu wa kuchukua mafao hautasitishwa. Plus hizi senti zetu ndogo ndogo zikikusanywa pale zinasaidia kuiletea nchi maendeleo.Naona ni win-win situation.
 
  • Thanks
Reactions: UKI
Mishahara mikubwa lakini take home kidogo. PAYEEE inaumiza leo tena NSSF kimeo?? du WatZ hapa tuamke.
 
Huu ni ujambazi mbaya sana uliofanywa na serikali yetu dhaifu kwa kutumia sheria za kinyonyaji na kuhalalisha na bunge la ndiooooo...hakika kwa hili nitaandamana hadi kieleweke
 
I am supporting this move. Wengi wetu tutaishia kuwa masikini huko uzeeni iwapo huu utaratibu wa kuchukua mafao hautasitishwa. Plus hizi senti zetu ndogo ndogo zikikusanywa pale zinasaidia kuiletea nchi maendeleo.Naona ni win-win situation.

Ni nani aliwahesabu? Maendeleo ya nchi yaletwe na michango ya wafanyakazi? Kodi inafanya nini? Unless you are a practical joker!
 
This is too much now, hivi wanataka watanzania sasa wasiishi tena, watamtawala nani sasa, huu ni uchizi wa serikali dhaifu. Hii sheria ilivyopitishwa chadema walikuwepo bungeni au walitoka nje, siamini kama nao walishiriki kupitisha upuuzi huu.
 
Huu ni udikteta, na napenda wafanyakazi kote ambao ni wanachama wa mifuko hii wapinge kwa nguvu zote!
Kikwete anasaini tu kichwa kichwa bila kuangalia impact ya sheria hii.
Hii mifuko miwili NSSF na PPF zipo kibiashara. ni wao wanaoongoza kwa majengo ya kibiashara kama hoteli na nyumba za kupangisha!
 
Wakuu si kuna wastaafu wengi tu, mbona sioni manufaa yoyote ya mifuko hii kwao?.
Au hii mifuko itaanzia kwa vijana wa sasa?
Naomba huyu mama aweke wazi hiyo sheria ya mikopo kwa wanachama asilete siasa kwenye hela zetu!.
 
Duu,mi npo barrick mgodin uku kahama,w2 wamekua wajanja mapema wamejitoa kazin na kuomb mafao yao mapema..manake mtu uku anadai hadi million 150 afu eti iliwe kizembe hvyo.hii nchi cjui vpi.
 
Wadau, hii sheria ilipitishwa lini? Mbona kama huu mjadala kama ulifanyika bungeni ulinipita! hivi, wabunge wa CDM, TLP, udp, NCCR walikuwemo? mbona ni kama umepitishwa kinyemela nyemela. Hili ni jambo linalogusa wafanya kazi wengi mno.

Je, kweli watz tumefurahi? Mimi mwenzenu nataka kuelimishwa zaidi kuhusiana na hili jambo, isije ikawa tunaliwa kweupe! Au ndo NSSF, na PPF inafilisika kwa kuikopesha serikali dhaifu nasa wame device means za ku-withhold pesa za wanachama wazishikilie kwa muda; mpaka mwanachama apitishe miaka ya wastani wa mtanzania kuishi (47). Mi kama sielewi elewi hivi! mbona kama naogopa ogopa hii sheria mpya!
 
Hivi hizi sheria zinapitishwa na kusainiwa kimya kimya..............how come watu sasa ndio wanashtuka na kupiga kelele?
 
Kama Mnyika, Zito au Mbunge yeyote wa upinzani embu aje atueleze hii ilipita pita vipi hii? Mbona sijawahi kusikia au kuna taratibu za kupitisha sheria by pass Bunge???

Wenye uwelewa zaidi waje watupe kidogo.
 
Ndugu zangu nafikili mtanishangaa sana kwa maelezo hayo ila kwa ukweli kama hili la mafao litaachwa lipite hivihivi basi itakuwa haina maana ya kuwa na chama cha upinzani kwa kuwa itaonyesha wazi kuwa na wao kumbe wanaangalia maslai yao kwanza, kwahiyo itakuwa ni bora ccm waendelee kutubuluza tu, na ndio utakuwa mwisho wangu wa kuangaika na siasa za ushabiki ambazo zitakuwa zimeproof kushindwa hapa tanzania.

Pata picha mm nilipanga kuanza kujiajiri kuanzia mwakani lakini bajeti yangu ilikuwa imeinclude na nssf sasa naona ndoto zangu zinapotea na kunifanya niendelee kuwa manamba.

hivyo ndivyo nitakavyokuwa
 
natamani siasa ziingie hapa ndo itakuwa suluhu ya hii kitu. wasipoangalia sasa kila mtu atachukua mkopo then tutaingia kwenye criss kubwa sana. ni bora wangeliachia watu wazichukue kuliko kuzibana.

by the way nimegundua kwa investment iliyofanya na serikali kwa kutumia fedha za mifuko hii kule udom wameona watu wakizitaka fedha zao itakuwa ngumu kupatikana kirahisi ivyo wakaona option raisi ni kuzibania hadi uzeeni.hii haikubaliki.Please Nakuomba Mwenyezi Mungu uliyewezesha watu wako wakavuka mto Yordani utuwezeshe angalau siasa ziingie katika jambo hili na tuweze kupata Muafaka sisi wanao tuna miaka michache ya kuishi tunakuomba utuwezeshe watengue haya maamuzi.
 
Back
Top Bottom