Hakuna malipo ya NSSF, PPF hadi umri wa kustaafu ufike!

Hakuna malipo ya NSSF, PPF hadi umri wa kustaafu ufike!

napata wasi wasi na hawa watu wa JF so called great thinker. yaani hivi ni kweli hamjui kuwa lengo la hiyo hifadhi ni kukusaidia while huna uwezo wa kufanya kazi tena' fainal uzeeni ' . sasa wewe unataka upewe ufanye biashara ukifika fainali utapata wapi pesa za kujinunulia pad wakati unaharisha kama ngisi kitandani hata kujiosha huwezi.

think hard great thinkers

I swear to god If you were near I would have punched you on the face.
 
UFAFANUZI KUHUSU FAO LA KUJITOA KATIKA MAREKEBISHO YA SHERIA ZA MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII.

Ufuatao ni ufafanuzi mfupi kuhusu marekebisho ya Sheria za Mifuko hasa kuhusu fao la kujitoa.

20 JULAI, 2012

1. Kama mtakumbuka Sheria za Mifuko ya Hifadhi ya Jamii pamoja na Sheria ya Mamlaka zimefanyiwa marekebisho na kupitishwa na Bunge tarehe 13 Aprili, 2012. Sheria hiyo tayari imeshasaininiwa na Mheshimiwa Rais na imeanza kutumika rasmi. Marekebisho haya yanawahusu wafanyakazi wote nchini mwetu bila kubagua sekta yoyote ile.

2. Kwa mujibu wa marekebisho hayo fao la kujitoa (withdrawal benefits) yamefutwa na kuanzia sasa hayatakuwepo. Mafao hayo yalikuwa yanatolewa pale mwanachama alipokuwa anaacha kazi. Sasa mwanachama wa Mfuko atapata mafao yake pale atakopfikisha umri wa kustaafu kwa hiari (miaka 55) au kwa lazima (miaka 60) au pale anapopata ulemavu wa kudumu.

3. Kwa kuzuia fao la kujitoa mwanachama anapata fursa ya kupata mikopo ya nyumba kwa kutumia dhamana ya michango yake kama ilivyoelezwa kwenye Sheria ya SSRA kipengele cha 38.

4. Marekebisho hayo kuhusu kuzuia mafao ya kujitoa yamefanyika ili kutimiza lengo na madhumuni ya hifadhi ya jamii ambayo ni kuhakikisha kuwa mwanachama anapostaafu anapata mafao bora yatakayomwezesha kumudu maisha ya uzeeni wakati ambapo nguvu ya kufanya kazi tayari imeshamwishia.

Mafao ya kujitoa yanapunguza na hata kuondoa kabisa kinga ya mfanyakazi pale anapoumia kazini au anapofika uzeeni.

5. Tunawaomba muwaelimishe wafanyakazi umuhimu na madhumuni ya mafao ya hifadhi ya jamii. Hifadhi ya jamii ni nyenzo mahususi iliyowekwa kuwasaidia wafanyakazi kuendesha maisha yao wakati wanapokuwa wameishastaafu tayari. Umasikini wa kipato wakati wa uzee ni mojawapo ya changamoto ngumu kukabiliana nazo kwa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla. Tunawasihi tena muelimishe wafanyakazi kuhusu jambo hili. Tafadhali msisite kuwasiliana na Mamlaka pale ufafanuzi zaidi utakapohitajika

6. Kwa kuwa marekebisho hayo yamesainiwa na kuanza kutumika rasmi kama sheria, mafao ya kujitoa hayawezi kutolewa tena na wafanyakazi watakaoacha kazi kwa sababu ya marekebisho ya kipengele hicho watakuwa hawajaijitendea haki wao wenyewe na pia itakuwa ni kunyume cha Sheria.

Mamlaka inaandaa kanuni za mafao ambayo lengo lake ni kuboresha maslahi ya wanachama, kanuni hizo zitajadiliwa na wadau wakiwemo vyama vya wafanyakazi na waajiri ili kupata maoni yao.

7. Tafadhali muwaelimishe wafanyakazi kwamba pamoja na kuzuia fao la kujitoa, mafao mengine ambayo ni muhimu kwa sekta ya Madini yataendelea kutolewa kama kawaida. Mafao hayo ni Kama vile kuumia kazini pamoja na fao la ulemavu

8. Tumesikia kwamba tayari kuna hofu imejijenga kwa wanachama kuhusiana na fao la kujitoa. Ikumbukwe kwamba baadhi ya Mifuko ilikuwa inatoa fao hilo kinyume cha Sheria kwani katika Sheria zao hakuna fao la kujitoa. Tunapenda kusisitiza kwamba wanachama wawe watulivu wakisubiri miongozo.

9. Tunapenda kuwahakikishia kwamba katika hili maslahi ya wanachama yatalindwa na hakuna mwanachama atakayepunjika kutokana na utaratibu huo.

Mamlaka imepanga kutembelea wafanyakazi wa sekta ya madini katika juma la kwanza la mwezi Agosti 2012 ili kutoa ufafanuzi zaidi kwa wanachama wote.

Tunatanguliza shukrani za dhati kwa ushirikiano.

Wenu.
Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Hifadhi ya Jamii

Irene Isaka
MKURUGENZI MKUU

Kwisha habari yetu kudagadeki walai
 
It is interesting to learn that average life expectancy is 52.85 years but pension benefits to be released after 55-60 years. Is there any logic?
 
Hata kama wazo ni kuwa mafao hayo ni kukusaidia uzeeni,labda kungekuwa na justification as how many Tanzanians wanafika huo umri wa kustaafu wakati tunajua life expectancy yetu ni chini ya hapo.kinachosumbua viongozi wetu wengi huwa ni wavivu wa ku-rationalize na kuona relevancy ya policies,thats why we've many policies kabatini wakati utekelezaji wake ni mdogo,tunamtungia nani sera ambazo relevancy yake ni issue,hili ni tatizo! I swear time will tell!Hilo la kusema ni ili upate security ya kukopea nyumba,labda watuambie hadi sasa mwamko wa ukopaji kwa ajili ya nyumba ukoje.Haya mambo ya kufanya mambo kwa ajili ya 'hand to mouth' yanachosha sasa!
 
Ningesema sheria hii ianzie kwa wabunge wanapomaliza muda wao ila kwa bahati mbaya sana wengi wa wapitishaji wa hii sheria dhalimu na kandamizi (magamba) wako juu ya 55-60.
 
Hapa hakuna jipya. Ni pesa ya kuendea uchaguzi mkuu ujao na ccm tayari wameona wameshikwa pabaya.
Hii ni pesa ya rushwa, kofia, fulana na tshirt ikiwemo vyakula na wasanii!!!!

Wakimaliza uchaguzi basi watatukamua na kurudisha na ndo hapo utaambiwa 5trillion zimetumika kwenye magari ya serikali!!

Lakini wanajamvi kuna mambo mengi ya kujiuliza kwenye hili:
  1. wamehusisha wadau kwa maana ya wenye pesa yao?
  2. je, hela ya mashirika haya inatumikaje kipindi chotempaka kustaafu?
  3. mfumko wa bei nao unakadiriwa kwenye kipindi chote cha pesa ikiwa mikononi mwa mashirika?
  4. na issue ya wafanyakazi Iren Isaka kujilipa mamilioni kwa mwezi linasemwaje hilo?
 
Mo' worries!

SSRA: Hakuna kujitoa NSSF, PPF





Na Hellen Mwango

23rd July 2012

Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), imesema kuanzia sasa mwanachama wa mfuko wowote hataruhusiwa kuchukua mafao yake kutokana na sababu yoyote mpaka hapo atakapofikisha miaka 55.

Hata hivyo, licha ya kuzuia fao la kujitoa na kutoruhusiwa kuchukua mafao yao, mwanachama wakiwamo wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) na Mfuko wa Pensheni ya Mashirika ya Umma NSSF) atapata fursa ya kupata mikopo ya nyumba kwa kutumia dhamana ya michango yake kama ilivyoelezwa kwenye sheria ya SSRA.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi Mkuu wa SSRA, Irene Isaka, mabadiliko hayo yametokana na sheria za mamlaka hiyo kufanyiwa marekebisho na kupitishwa na Bunge Aprili 13, mwaka huu na kwamba imeshasainiwa na Rais Jakaya Kikwete na imeanza kutumika rasmi.

Kwa mujibu wa marekebisho hayo fao la kujitoa yamefutwa na kuanzia sasa hayatakuwepo.

"Mafao hayo yalikuwa yanatolewa pale mwanachama alipokuwa anaacha kazi lakini kuanzia sasa mwanachama wa mfuko atapata mafao yake pale atakapofikisha umri wa kustaafu kwa hiari (55) au kwa lazima (60) au pale anapopata ulemavu wa kudumu" ilisema taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana na kufafanua kuwa:

"Marekebisho hayo kuhusu kuzuia mafao ya kujitoa yamefanyika ili kutimiza lengo na madhumuni ya hifadhi ya jamii ambayo ni kuhakikisha kuwa mwanachama anapostaafu anapata mafao bora yatakayomwezesha kumudu maisha ya uzeeni.

Taarifa ya Mkurugenzi huyo iliendelea kusema kuwa mafao ya kujitoa yanapunguza na kuondoa kinga ya mfanyakazi pale anapoumia kazini au anapofika uzeeni.

Hata hivyo, ilisema pamoja na kuzuia fao la kujitoa, mafao mengine ambayo ni muhimu kwa sekta ya madini yataendelea kutolewa kama kawaida ikiwemo kuumia kazini pamoja na fao la ulemavu.

Ilisema wanachama wanatakiwa kuwa watulivu kuhusiana na mabadiliko hayo na kwamba maslahi yao yatalindwa na hakuna atakayepunjwa kutokana na utaratibu huo.

SOURCE: Nipashe

 
Wakuu hii habari si kweli. Mimi niliacha kazi toka Oktoba 2010. Niliamua kufungua madai mwezi Machi 2012 na mpaka kufikia Mei 2012 nikalipwa kitita changu chote. Labda kama hili suala limeanza Julai hii.
 
Kwa hili nitawaunga mkono UAMSHO, tufanye kazi kwani huu ni upuuzi wa Wajinga wachache wanaofaidi posho, na huyo mkurugenzi wa SSRA, Nina wasiwasi nae, anaitwa nani na alitokea wapi kabla ya kuajiliwa hapo??? alishindanishwa na wengine???
 
Watoto wa masikini watasoma kweli ??? kwani huu ni mkakati wa kuwaua watanzania masikini wao kila siku india
 
wakuu mashaka niliyonayo ya kuwa mpango huo unaweza kuwa haramu kwa kuwa umekuwa ukitangazwa uchochoroni na kimya kimya kama halali kwa nini wasitangaze publicity?utasikia mara huyu kasema hili mtandaoni mara kurugenzi huyu katuma ka email haka yaani upumbavu mtupu hili jambo ni kubwa nyinyi wapuuzi wa mifuko ya jamii katangazeni kwenye vyombo vya habari kitaifa kuliko mnavyofanya sasa kwa staili hii naona mpango mzima ni mchafu ungekuwa msafi kwa nini mnasema kimitegomitego?
 

Attachments

Kama hela nakatwa mimi kwanini nisiwe mtu wa mwisho kuamua njia sahihi ya kuchukua akiba zangu pindi ninapo acha kazi au kuachishwa? wale vinara watakaosimamia kupitishwa sheria hii tutawalimboka.. hatuna njia nyingine
 
Wana JF,

Hii ni 20% ya watu kabisaaaaaaaa wala halina mjadala,

Serikali imechukuwa pesa zote za walipa kodi imezimaliza na sasa haina pesa na dawa ni kutupa proposal zisizo na kichwa kabisa maana utekelezani wake utakuwa ni zero kabisaaaaaaaa.

Serikali imeshindwa kuja na plan impya imekimbilia NSSF me nasema hivyo kwanini hapa tulipo tuuuu matibabu kwa ujumla nchi nzima ni duni kabisaaaaaaa kwani 97% ya matibabu ya mtanzania anajitibu mwenyewe tena kwa Salary yake ambayo ilisha katwa PAYE ukitumia zile kararasi za Pension ndio kabisaaaaa unaambiwa kiwango hiki ndicho mwisho sasa pesa yetu unaifanyia biashara sisi ndio wadhamini wakuuu kwako kwa kufanya miradi yako na unabenefit kwa hilo. kwa nyakati hizi tuuuuuu hujatuonyesha faida au matunda ya Pension zetu leo unakuja na proposal mpya tena duuuuh.

Hapa unawapa wafanyakazi matumaini gani kwa sasa maisha ni magumu shilingi imeshuka thamani mshahara ndio huo kodi imeongezeka, Resource za taifa hili GOLD,DIAMOND,TANZANITE,GAS,URANIUM,NATIONAL PARK hizi zote hatujaona matunda yake kwa muda wa 50 yrs from Independence leo hiii mwaja na mipango yenu ya 20% kweli sasa nadhani mwatulazimisha kukubali maoni yenu kwanini msituulize kwanza tutililike ukweli wa wakwepa kodi na walipa kodi na nani watatunyima keki yetu ya nchi hii na inaliwa na watu wachache?

My Take:

Serikali imeshindwa kuja na mbinu mbadala kukusanya kodi imekuja na mbinu mbadala kunyonya rai wake, serikali imekuwa ni ya kutoa ahadi tuu Juzi JK kaenda fungua mradi wa maji Mbeya anajisifi wakati huo mradi ni haki ya kimsingi ya wananchi wa mbeya na watanzania wote hilo mmoja alitambue pili katika ILANI ya CCM mradi huo ulikuwa ni wa mwaka 2005 sasa kwa kipindi chote hicho ametimiza hilo la maji hiyo gap hapo ya kutimiza ahadi kweli ni haki kuja leo kujitapa kwa wananchi huoni wananchi wanaiona serikali ilivyo DHAIFU sasa lini nchi nzima itakuwa na maji safi na salama ya kunywaa?

Uwajibikaji wa viongozi wetu ndio unatupa mashaka sana kwa hizi Bill zilizopo bungeni then zinakuwa sheria maana mapicha picha ni mengi kweli kwa mfano huo wa maji safi mbeya umechukuwa almost miaka 7, iweje hii ya NSSF?

Wajua hawa wazeee wanakaribia kustaaafu kumbukeni hilo wao wanajiandalia maisha bora na sio kwetu maaana vijana wengi wa lika hili tuna almost 30 yrs to come ili tufike 55yrs kwa maisha haya kuna maisha kweli huko mbeleni au twawaandalia wazeeee wa sasa na baadae tunaibadilisha iyo sheria inakuwa ya vizazi vijavyo.

Twaomba Pension Fund Zote zije kutupa elimu ya hiyo sheria waone watu kama hawajaamka na nyie,
 
Kweni hao SSRA wanalazimisha waajiriwa wote wawe Pensionable? Contract zote za ajira ktk private sector walizipitia na kukubaliana na wadau? Hivi kweli binti wa miaka 19 anayeacha kazi pale Billicannas baada ya kufanya kazi mwaka mmoja na kuolewa then atangojea takribani miaka 36 then apewe akiba yake aliyovuna kwa mwaka mmoja?

SSRA imeanzishwa 2008? wakati watu waliajiriwa 2005 huko, sheria hii inawezaje kuvunja mikataba ya nyuma ambayo watu tayari walishawekeana na waajiri wao? leo ukiingia kwenye website ya NSSF bado inasema hivi...

"Shirika pia hulipa mafao ya kujitoa uanachama kwa mfumo wa akiba kwa mwanachama aliyeondoka katika ajira kwa sababu mbali mbali na ikiwa hajapata kazi nyingine kwa zaidi ya miezi sita".

Yaelekea hata NSSF hawajashirikishwa kwa undani ktk jambo hili, Mwisho huyo Mama namshauri aende akawatembelee jamaa hao akiwa kasindikizwa na Batallion moja hivi
 
Na Hellen Mwango | 23rd July 2012

Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), imesema kuanzia sasa mwanachama wa mfuko wowote hataruhusiwa kuchukua mafao yake kutokana na sababu yoyote mpaka hapo atakapofikisha miaka 55.

Hata hivyo, licha ya kuzuia fao la kujitoa na kutoruhusiwa kuchukua mafao yao, mwanachama wakiwamo wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) na Mfuko wa Pensheni ya Mashirika ya Umma NSSF) atapata fursa ya kupata mikopo ya nyumba kwa kutumia dhamana ya michango yake kama ilivyoelezwa kwenye sheria ya SSRA.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi Mkuu wa SSRA, Irene Isaka, mabadiliko hayo yametokana na sheria za mamlaka hiyo kufanyiwa marekebisho na kupitishwa na Bunge Aprili 13, mwaka huu na kwamba imeshasainiwa na Rais Jakaya Kikwete na imeanza kutumika rasmi.

Kwa mujibu wa marekebisho hayo fao la kujitoa yamefutwa na kuanzia sasa hayatakuwepo.

"Mafao hayo yalikuwa yanatolewa pale mwanachama alipokuwa anaacha kazi lakini kuanzia sasa mwanachama wa mfuko atapata mafao yake pale atakapofikisha umri wa kustaafu kwa hiari (55) au kwa lazima (60) au pale anapopata ulemavu wa kudumu" ilisema taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana na kufafanua kuwa:

"Marekebisho hayo kuhusu kuzuia mafao ya kujitoa yamefanyika ili kutimiza lengo na madhumuni ya hifadhi ya jamii ambayo ni kuhakikisha kuwa mwanachama anapostaafu anapata mafao bora yatakayomwezesha kumudu maisha ya uzeeni.

Taarifa ya Mkurugenzi huyo iliendelea kusema kuwa mafao ya kujitoa yanapunguza na kuondoa kinga ya mfanyakazi pale anapoumia kazini au anapofika uzeeni.

Hata hivyo, ilisema pamoja na kuzuia fao la kujitoa, mafao mengine ambayo ni muhimu kwa sekta ya madini yataendelea kutolewa kama kawaida ikiwemo kuumia kazini pamoja na fao la ulemavu.

Ilisema wanachama wanatakiwa kuwa watulivu kuhusiana na mabadiliko hayo na kwamba maslahi yao yatalindwa na hakuna atakayepunjwa kutokana na utaratibu huo.


CHANZO: NIPASHE
 
Wewe ndiyo kilaza namba moja, hizo ni marketing language za mifuko, withdrawal siyo benefit, ni unajitoa kwa kiswahili, kujitoa maana yake hauna benefit tena, na halafu bado hujatofautisha withdrawal na unemploment benefit, kilaza mkubwa wewe, na wewe hata kwenye utoto hu qualify, hakuna ku google mimi najua bila kugoogle, kujitoa maana yake unapoteza, angalia unachokipata kwa kujitoa na linganisha na pensheni ambayo ungepata, we vipi! Achana na hayo makaratasi ya markrting eti withdrawal ni benefit ili wakienda migodini waandikishe watu, sasa kama una akili angalia hiyo interest ya PPF unapata ngapi kama siyo 1% simple, tumia akili zako kwanza siyo haya madesa ya NET. Unaweza kuni PM nikupe ushauri ili usiendelee kuwa mjing.a.
kibai wewe ni kilaza wa kutupa KALALE WEW BADO MTOTO try kutumia hata akili yako ugoogle kidogo see below how WIthdraw benefits are defined by pension scheme

PPF
[TABLE="align: left"]
[TR]
[TD="colspan: 2"]WITHDRAWAL BENEFIT

[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: news, colspan: 2"]
Qualifying condition
Where a member ceases employment through summary dismissal or termination.
Mode of granting withdrawal benefit
i) Granted as Lump sum immediately on ceasing employment


SOurce: :: PPF Pensions Fund ::-


LAPF

WITHDRAWAL BENEFIT


This is a lumpsum payment equal to members’and employers’ contributions plus accrued interest payable to a member who has resigned from employment, has been retrenched, dismissed or terminated on medical grounds, abolition of office, or any other cause.


soURCE:LAPF Tanzania: Withdrawal Benefits





PSPF

WITHDRAWAL BENEFIT

Marriage: Payable to a female member who due to marriage proves to the satisfaction of the Director General that she has permanently given up employment and will not seek any gainful employment in the
Public service;
Maternity: Payable to a female member who proves to the satisfaction of the Director General that in consequence of her giving birth to a child she has permanently given up employment and will not seek any gainful employment in the public service;
Emigration: Payable to a member who proves to the satisfaction of the Director General that he is emigrating or has emigrated and has no intention of returning to the United Republic of Tanzania and has not been employed by employer who is liable to make contributions in respect of himself for at least six months
Qualifying conditions

  • Should be a member registered with the Fund;
  • Should have contributed to the Fund.


[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

 
Hata hivyo, licha ya kuzuia fao la kujitoa na kutoruhusiwa kuchukua mafao yao, mwanachama wakiwamo wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) na Mfuko wa Pensheni ya Mashirika ya Umma NSSF) atapata fursa ya kupata mikopo ya nyumba kwa kutumia dhamana ya michango yake kama ilivyoelezwa kwenye sheria ya SSRA.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi Mkuu wa SSRA, Irene Isaka, mabadiliko hayo yametokana na sheria za mamlaka hiyo kufanyiwa marekebisho na kupitishwa na Bunge Aprili 13, mwaka huu na kwamba imeshasainiwa na Rais Jakaya Kikwete na imeanza kutumika rasmi.

Kwa mujibu wa marekebisho hayo fao la kujitoa yamefutwa na kuanzia sasa hayatakuwepo.

"Mafao hayo yalikuwa yanatolewa pale mwanachama alipokuwa anaacha kazi lakini kuanzia sasa mwanachama wa mfuko atapata mafao yake pale atakapofikisha umri wa kustaafu kwa hiari (55) au kwa lazima (60) au pale anapopata ulemavu wa kudumu" ilisema taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana na kufafanua kuwa:

"Marekebisho hayo kuhusu kuzuia mafao ya kujitoa yamefanyika ili kutimiza lengo na madhumuni ya hifadhi ya jamii ambayo ni kuhakikisha kuwa mwanachama anapostaafu anapata mafao bora yatakayomwezesha kumudu maisha ya uzeeni.

Taarifa ya Mkurugenzi huyo iliendelea kusema kuwa mafao ya kujitoa yanapunguza na kuondoa kinga ya mfanyakazi pale anapoumia kazini au anapofika uzeeni.

Hata hivyo, ilisema pamoja na kuzuia fao la kujitoa, mafao mengine ambayo ni muhimu kwa sekta ya madini yataendelea kutolewa kama kawaida ikiwemo kuumia kazini pamoja na fao la ulemavu.

Ilisema wanachama wanatakiwa kuwa watulivu kuhusiana na mabadiliko hayo na kwamba maslahi yao yatalindwa na hakuna atakayepunjwa kutokana na utaratibu huo.
Wasomi wetu bwana........anaongelea uzee upi wakati ujana wenyewe mgumu hivi?
 
Back
Top Bottom