hakuna kitu kinaitwa laana,Ona hizi fix.

hakuna kitu kinaitwa laana,Ona hizi fix.

Mpaka sasa upande wenye kupinga uwepo wa laana wameweza kujibu kwanini wakati mwengine watu hutokewa na madhara baada ya kutolewa laana, wamesema huwa ni hofu yake tu(nocebol effect) ndio yenye kusababisha kujiletea hayo madhara lakini si laana ndio maana wengine hawapatwi na madhara yeyote hata baada ya kupewa laana.

Wenye kuamini katika laana bado hawajajibu ni nguvu ipi yenye kusababisha hayo madhara kwa muhusika baada ya kupewa laana na kwanini wengine laana hatuoni kuwaletea madhara hata baada ya kulaaniwa?
 
Tatizo ni Unataka wavune kwa namna unayoamini wewe, Ila Uhalisia ni Kila mtu anavuna kwa namna yake. Na ni hapahapa Duniani, sio huko pa kusadikika Mbinguni.

Mtu awe mvivu alafu awe na mafanikio? Mtu aendekeze zinaa alafu Asipate maradhi? Uliona wapi Boss?

Usipojituma Utatumwa ambapo ni matokeo ya Uvivu.
Kuna mavuno ya duniani ambayo Mungu humjaalia kila amtakae na humnyima amtakae...Halafu kuna mavuno baada ya kifo hayo yameandaliwa kwa wale walioamini na kutenda mema. Cheo na mafanikio yako ya mali na watoto hapa duniani havitakufaa chochote baada ya kufa kwako.

Imepokewa kauli kutoka kwa Mtume Muhammad (pbuh)


Kutoka kwa Anas -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- akisema

"Yanamfuata maiti mambo matatu: familia yake na mali yake na matendo yake, vinarudi vitu viwili na kinabakia kimoja: wanarudi familia yake na mali yake, na yanabakia matendo yake"

~(bukhar na Muslim)



Wote tunapokufa tunakuwa katika hali moja kama vile ambavyo tulikuja duniani tukiwa hatuna kitu na tunaondoka tukiwa hatuna kitu.

Kila unachomiliki wewe ni cha muda mfupi tu, Ukifa MUNGU anavirithi vyote na kuwapa watu wengine..Kitakachokusaidia baada ya kufa ni imani yako juu ya Mungu na matendo yako mema uliyoyatenda hapa ulimwenguni.

Asset ya kweli ambayo haishuki thamani kwa mwanadamu sio dhahabu wala fedha bali ni matendo mema anayojiwekezea hapa duniani ili yaende kumfaa siku ya malipo aka siku ya hukumu (judgement Day)
 
Basi utakuwa hata haujui nature inafanya kazi vipi.

Labda nikudokeze tu, nature is neutral, haina upendeleo na haiwezi kusikiliza maneno ya wazazi wako tu.
kwahiyo wewe kiumbe huru huna urithi wa vinasaba (I.e genetic make up (DNA)) kutoka kwa Baba na mama yako?
 
Mpaka sasa upande wenye kupinga uwepo wa laana wameweza kujibu kwanini wakati mwengine watu hutokewa na madhara baada ya kutolewa laana, wamesema huwa ni hofu yake tu(nocebol effect) ndio yenye kusababisha kujiletea hayo madhara lakini si laana ndio maana wengine hawapatwi na madhara yeyote hata baada ya kupewa laana.

Wenye kuamini katika laana bado hawajajibu ni nguvu ipi yenye kusababisha hayo madhara kwa muhusika baada ya kupewa laana na kwanini wengine laana hatuoni kuwaletea madhara hata baada ya kulaaniwa?
Jibu lako ni hili

"
Kutoka kwa Jabir (Radhi za Allah ziwe juu yake) amesema:
Mtume Muhammad (Swalla Allahu 'alayhi wa sallam) amesema:
"Msijilaani ninyi wenyewe, wala msiwalaani watoto wenu, wala msilaani mali zenu; msije mkasadifu (mkakutana na) wakati kutoka kwa Allah ambao dua (maombi ) hupokelewa, na akawakubalika (dua yenu ya laana)."

[Imepokelewa na Muslim].
 
Mara ooh mama yako akikwambia maneno mabaya utateseka sana kwenye hii Dunia , uongo

Baba yako akivua ngua akanyoosha uume juu huku akisema kama kweli wewe ni mwanangu nimekuzaa ufe ahivi unakufa hapohapo , uongo

Dada yako akikasirika akavua chupi akakupiga nayo utateseka maisha yako yote, uongo

Usipowasaidia wazazi wako,ndugu wakikasirika na kukunenea maneno mabaya basi lazima utese tu, uongo

#Be open minded
Ingekuwa kuna hizo laana vijana wa kizungu leo wangekuwa wehu hohehahe! Wazazi wengine ni pasua kichwa watakutesa ufe fukara, kiujumla watakulostisha!
 
Pia ifahamike kuwa sio kila laana au dua mbaya kutoka kwa wazazi kwenda kwa watoto wao hufanya kazi au kukubaliwa na Mwenyezi Mungu (Allah).
Ingawa dua ya mzazi (iwe ya heri au ya shari) ina nafasi kubwa na inaweza kujibiwa,

Wanazuoni Kiislamu wanaweka wazi mipaka muhimu kuhusu jinsi na lini maombi haya hasi yanavyoweza kufanya kazi:

Masharti na Ufafanuzi Kuhusu Laana za Wazazi
  • Wakati wa Hasira Kali: Kwa rehema na ustahimilivu wake mkubwa, Mwenyezi Mungu huwa hakubali haraka dua zinazofanywa na watu dhidi ya watoto wao, nafsi zao, au mali zao wakati wa hasira kali ya mpito. Allah anajua kuwa mzazi hakusudii madhara ya kudumu katika hali hiyo ya kihisia, hivyo kwa wema wake ALLAH hayatimizi maneno hayo ya hasira.
  • Mtoto Lazima Awe Anastahili: Laana au dua mbaya haitampata mtoto ikiwa mtoto huyo hajastahili au hajafanya kosa lolote linaloasababisha laana hiyo. Allah ni Muadilifu (Al-A'dl) kabisa; laana isiyo na msingi au ya kidhuluma haimdhuru mtu asiye na hatia, badala yake haikubaliwi au inarudi kule iliyotoka.
  • Katazo kwa Wazazi: Uislamu unakataza vikali wazazi kuwalaani watoto wao au kuwaombea mabaya. Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) aliwaonya waumini wasiwaombee mabaya watoto wao, kwa sababu dua hiyo inaweza kusadifiana na muda ambao maombi yanajibiwa. Wazazi wanaamrishwa kuwaombea watoto wao uongofu na heri, hata wanapokuwa wamewakasirisha.
Nadhani hapo tumeelewana.
 
Uadilifu wa Mungu ndio hupelekea kuzuia dhulma ya laana isimfike mtoto..mfano mdogo tu Mzazi labda kampigia simu mwanawe amsaidie pesa na Mtoto akamjibu kuwa sina...so kutokana na hasira, mzazi akatoa maneno mabaya ya laana kwenda kwa mtoto....Hapo hiyo dua inaweza kujibiwa ama kutojibiwa.

Anayejibu dua ni Mungu...na YEYE ndiye mwenye uchaguzi wa kujibu ama kutokijibu...akiamua akupe mitihani wewe mtoto basi atajibu hiyo dua na mitihani itakufika kweli na akiamua hajibu na hakuna litakaloweza kukufika.

So tuwe waangalifu kwenye kutoa maneno maana kuna chances pia za hayo maneno ya laana kukubaliwa. Hakuna ajuae GOD's wills.
 
kwahiyo wewe kiumbe huru huna urithi wa vinasaba (I.e genetic make up (DNA)) kutoka kwa Baba na mama yako?
Yes, nina DNA yao, lakini hiyo DNA ilishatengeneza mwili wangu nikiwa tumboni, nimezaliwa na kuwa mtu mzima, mzazi hawezi ku-edit au kubadilisha DNA yangu kwa maneno ya mdomo wake. DNA yangu haisikilizi voice commands kutoka kwa baba au mama, that's all.
 
Kuna mtu alinifanyia fitna nililia sana kwa Mwenyezi Mungu karibia mwezi nilimlaani yule mtu haikuchukua muda alitolewa kwenye ile nafasi
 
laaana ipo angalia wale wanaoua wenzao wote huishia papaya…..madikteta wote hufa vifo vya ajabu
 
Ingekuwa kuna hizo laana vijana wa kizungu leo wangekuwa wehu hohehahe! Wazazi wengine ni pasua kichwa watakutesa ufe fukara, watakuliga, kiujumla watakulostisha!
Na hapo ndio kuna haja kubwa kwamba tunapozungumzia mambo kama haya tuweze kutofautisha kati ya jamii moja na nyengine.
 
Back
Top Bottom