Hakuna binadamu anayekupenda kwa dhati

Hakuna binadamu anayekupenda kwa dhati

maisha nikuishi na kujifunza ,tunaishi ili kujifunza ,na Tunajifunza ili tuishi,

maisha haya kumejaa watu wengi masnitch ,kunzia ndgu jamaa hata marafiki ,wote sio wakuwaamini ,

wapo ambao wanapenda wakusikie una shida ili wakusaidie ,hawatapenda kukuona ukipata wanachotaka wao siku zote uwe chini yao ,

.wapo ambao kila siku wao ndo wenye shida na kupenda kusaidiwa wao ,hata kama watapata ,basi hawatoweza kukusaidia ,kama ntapata elfu 50 wote basi itatumika ya kwako yake itabaki ,

kuna mengi nimepitia ,toka kwa ndugu jamaa na marafiki ,yamenifunza nikusimama na Nafsi yangu familia yangu na watoto wangu ,yaan wamenifanya niwe m'binafsi kuangalia maslahi yangu kwanza kabla ya mtu yeyote ,maana hata wao hawajali ya kwako
 
Inawezekana labda.Lkn sija experience hilo.Mara nyingi hutokea ikiwa sio Ndugu wa tumbo moja, yaani baba mmoja na mama mmoja.
Hao ndugu wa tumbo moja wasikie tu hivyo hivyo...wewe hujawai ona mifano ya baba anatangulia mbele ya haki...nduguze wa damu kabisa ndiyo wanageuka watesi wa familia yake?

Wanadhulumu mali na vitu kama hivyo..n.k ndugu wa damu kabisa anaweza kukudhulumu au kukuibia fedha ktk biashara. Tena ndugu ndiyo wabaya sana...though hii si kwa wote.

Wanadamu tuna uchoyo wa kujijali kwanza sisi kabla ya maslahi ya wengine. Labda ukutane na mtu aliyebadilishwa na Mungu na kuwa mwema.
 
Nimekupata Mkuu.Ndugu wa damu akikusaliti inaweza kuwa hatari Zaidi kuliko mtu mwingine.
 
Mimi naamini hivyo pia kwamba upendo wa kweli upo lakini umepungua sana. Hata kwenye mapenzi naamini upendo wa BF kwa GF au Husband kwa wife na vice versa upo pia lakini uwe na bahati ya Mtende.

Tunapendana sana shida yangu shida Yao furaha yangu furaha Yao, I'm so blessed kwa kweli upendo huo sijawahi upata popote
 
Mimi naamini hivyo pia kwamba upendo wa kweli upo lakini umepungua sana. Hata kwenye mapenzi naamini upendo wa BF kwa GF au Husband kwa wife na vice versa upo pia lakini uwe na bahati ya Mtende.
Shida kwenye mahusiano wengi huwa wameunizwa so huamua kuendelea kuumiza wengine, ila kupendana huwa raha Sana hasa watu wakisahau past pain
 
Hilo ndiyo tatizo kubwa sana. Mtu bado ana donge la kuumizwa kwa hiyo anaingia kwenye penzi jipya huku akiwa hana mapenzi ya kweli. Nia yake ni kuumiza au kukomoa matokeo yake mapenzi yanakuwa na migogoro chungu nzima hatimaye kuvunjika.

Ni sahihi watu kuliko kuingia kwa mahusiano mapya ni heri wajipe mda wa heal kwanza kuliko kutafta mahusiano mapya na kwenye hayo mahusiano wanafanya wengine waingie dip then wanawabadilikia na kuwaumiza wasio na hatia huo ni ujinga mwengine ndio maana watu wanakuwa hawana hisia ni kama wanyama tu
 
Back
Top Bottom