Hakuna binadamu anayekupenda kwa dhati

Hakuna binadamu anayekupenda kwa dhati

Umekata tamaa sana, kuna wanaokupenda ila hawajapata access na wewe. Mwanadamu yoyote anapendwa na wastani wa watu wasiopungua 5 kati ya billion 7 waliopo.

Kule kwetu kuna usemi wa "mbwa hakosi wifi" ukilenga kumaanisha hakuna "aso mtu"..
Umenena vyema mkuu,
Umekomaa vyema kifikra.

Mifano miwili aliyoitoa mleta uzi ni dhaifu na haikidhi kuhalalisha hoja yake.
Kwani mdogo wake alipofungwa jela ndugu wote walikuja kumwona?
Marafiki wa kweli wapo na marafiki wabaya wapo
Ndugu wema wapo na wafitini wapo
Wapenzi wa kweli wapo na wapita njia wapo
Wazazi wenye upendo wapo na wasiojielewa wapo

Ishu sio kwamba hawapo tatizo ni umekutana na nani, wapi,
bond yenu ikoje
Mmeunganishwa na nini
Unawezaje kukutana na mtu kazini au company ya kunywa bia na stories alafu utegemee mtu huyo awe msaada mkubwa kwenye matatizo ilhali hamna bond yoyote zaidi ya bia.
Hiyo sio sawa.
 
Angawa tunapaswa kuwapenda wengine kama vile maandiko matatifu yasemavyo lakini jambo la kuzingatia na kwamba "AKIBA YAKO NDIO NDUGU YAKO/RAFIKI YAKO WA KWELI HAO WENGINE WATA ANGALIA UNA NINI KAMA UKO UKO VIZURI KIUCHUMI NDIO WATA JIDAI WAKO KARIBU NA WEWE "kwa hiyo tuishi kwa akili ndi o mfumo wa ulimwengu ulivyo .
 
maisha nikuishi na kujifunza ,tunaishi ili kujifunza ,na Tunajifunza ili tuishi,

maisha haya kumejaa watu wengi masnitch ,kunzia ndgu jamaa hata marafiki ,wote sio wakuwaamini ,

wapo ambao wanapenda wakusikie una shida ili wakusaidie ,hawatapenda kukuona ukipata wanachotaka wao siku zote uwe chini yao ,

.wapo ambao kila siku wao ndo wenye shida na kupenda kusaidiwa wao ,hata kama watapata ,basi hawatoweza kukusaidia ,kama ntapata elfu 50 wote basi itatumika ya kwako yake itabaki ,

kuna mengi nimepitia ,toka kwa ndugu jamaa na marafiki ,yamenifunza nikusimama na Nafsi yangu familia yangu na watoto wangu ,yaan wamenifanya niwe m'binafsi kuangalia maslahi yangu kwanza kabla ya mtu yeyote ,maana hata wao hawajali ya kwako
Hakika ndivyo ilivyo, watu huzaliwa wema lkn binadamu ndio wanawafanya watu wema kubadilika na kuwa wabaya.
 
99% ya marafiki ni wanafiki, wazandiki, wanye kupenda kutatuliwa shida zao pasi na kikisaidia ww. Yaan its better to be alone lather than being in bad company
Sahihi kabisa, nadhani ndio maana Wanafalsafa waliwa kusema "The strongest man stends alone".
 
Kwa hiyo mkuu hela ya mipango yake ulitaka akupe wewe? Labda jamaa limefanya saving kwa jasho na damu mwaka mzima anunue bodaboda apige kazi,kafikisha 2m anapelea laki tu achukue kitu. Halafu na wewe unakuja na shida zako wakati hata yeye ana shida zake
Kwa hiyo Mimi nilipokuwa namkopesha pesa yangu,pesa yangu haikuwa na kazi?,Je,sikuipata kwa Jasho??.
 
Umenena vyema mkuu,
Umekomaa vyema kifikra.

Mifano miwili aliyoitoa mleta uzi ni dhaifu na haikidhi kuhalalisha hoja yake.
Kwani mdogo wake alipofungwa jela ndugu wote walikuja kumwona?
Marafiki wa kweli wapo na marafiki wabaya wapo
Ndugu wema wapo na wafitini wapo
Wapenzi wa kweli wapo na wapita njia wapo
Wazazi wenye upendo wapo na wasiojielewa wapo

Ishu sio kwamba hawapo tatizo ni umekutana na nani, wapi,
bond yenu ikoje
Mmeunganishwa na nini
Unawezaje kukutana na mtu kazini au company ya kunywa bia na stories alafu utegemee mtu huyo awe msaada mkubwa kwenye matatizo ilhali hamna bond yoyote zaidi ya bia.
Hiyo sio sawa.
Visa hivyo ni dhaifu kwa mtizamo wako kwasababu hujawahi kutana na hali hiyo.Utamu wa ngoma ikia ucheze mwenyewe.
 
angawa tunapaswa kuwapenda wengine kama vile maandiko matatifu yasemavyo lakini jambo la kuzingatia na kwamba "AKIBA YAKO NDIO NDUGU YAKO/RAFIKI YAKO WA KWELI HAO WENGINE WATA ANGALIA UNA NINI KAMA UKO UKO VIZURI KIUCHUMI NDIO WATA JIDAI WAKO KARIBU NA WEWE "kwa hiyo tuishi kwa akili ndi o mfumo wa ulimwengu ulivyo .
Asante Chifu, nimekupata.
 
Kwa hiyo Mimi nilipokuwa namkopesha pesa yangu,pesa yangu haikuwa na kazi?,Je,sikuipata kwa Jasho??.
Si uliitoa kwa roho moja?!mimi hapa nimekopeshwa na wanangu tofauti tofauti kama 6m hivi,nataka kufanya deal ya 50m wiki ijayo. Hivi ikitokea mtu anataka kunikopa itakuwaje? Lakini haimaanishi wale walionikopesha wajinga,Hapana kuna timing ya matumizi ya hela
 
Rafiki wa kweli ni ndugu zako wa damu, familia na watoto the rest do not care about you aisee.
Mifano ipo mingi sana...

Ila huu nimeshuhudia kwa macho.. ..ndugu

Wa kuzaliwa baba na mama mmoja ..wanazungukana na kuharibiana

Maisha si kazini..kwenye ndoa..biadhara mpaka kupelekana jela ...yaani mtu anamtengenezea kesi ndugu yake na kusimamia show ili akaozee jela. ..

Shukuru Mungu kupata ndugu na mkawa ndugu kweli..sio kwa vile ni damu moja tu

.... Naa huyo mtu alitolewa jela kwa msaada wa rafiki zake tu ..walijichanga changa..

Sasa hivi imani inatoweka... .. tunakoelekea ndugu /rafiki atakuwa ni pesa yako na akili yako tu...

Maana hata wazazi na watoto wanasalitiana..
 
Inategemea mkuu huwa Kuna ndugu vichomi kuliko kichomi chenyewe na hawapendani hata kidogo, na hyo chuki huwa ni asili tu ya baadhi ya Koo familia kwa familia so inakuwa kama ni utamaduni wa kuendekeza kuchukiana.
All in all nyakati hizi upendo na utu umepungua sana kupata mtu mwenye utu wako wachache sana aisee. Mungu atusaidie tulee familia zenye utu na upendo
 
Back
Top Bottom