Hizo ni Biashara huitwa Social Enterprises, Biashara za mazoea na sio za kukupeleka kwenye Utajiri. Unless utengeneze Class unrealistic, zile za kuuza Bia moja 6,000+, VIP kiingilio 50k na other Creativity.
BUT Mostly ni biashara ambayo wanufaika wake (Wanaotajirika), ni wale wanaouza huduma kuzunguka hio Biashara ya Bar, Mfano Ma - Dj's, Wanaokuuzia Pombe, Muziki, wanaokuuzia Bidhaa za Chakula, Viungo, Events managers n.k.
Zile Biashara za pembeni zinazolisha Biashara ya BAR ndio huwa wana chance ya kutajirika, na sio mwenye Bar. Matumizi ya hela zako nyingi huishia kuwanufaisha wao ili Biashara yako ya Bar iweze kuendelea. Na uzuri wa hizi biashara ni kwamba, wakati wengine wanazifunga huwa kuna wapya wengi wanafungua(so haziwezi kuisha). ILA wanaodumu 5years+ ni wachache sana.
Nje ya Mada: ukitaka ufanikiwe, Chagua biashara ambazo zitalisha Social Enterprises( zile Biashara watu hufanya kwa mazoea), Mfano, Uza Kuku wa kienyeji kwenye Restaurants, Uza Spare za Bodaboda, Bajaji, Daladala nk, Uza vyakula na dawa za mifugo, Uza vifaa vya ujenzi, Uza viwatilifu kwa wakulima, MC wa kwenye Sherehe na nyingine kibao.
Inshort, angalia zile biashara watu wanafanya kwa mazoea, kisha wewe wapelekee vitu vitakavyofanya waendelee kuzifanya miaka na miaka