Hakuna biashara pasua kichwa kama biashara ya Bar

Hakuna biashara pasua kichwa kama biashara ya Bar

ngara23

JF-Expert Member
Joined
Aug 31, 2019
Posts
16,810
Reaction score
39,554
Biashara ya Bar ina changamoto sio poa
Hii biashara unaweza kukufirisi unalia
Faida sio kivile ila changamoto ni nyingi mno

1. Unahitaji uwekezekajo sio kinyonge, mzigo, Mziki, viti, jiko n.k

2. Ushindani ni mkubwa, unaweza ukawa umewekeza ukadhani umemaliza, ***** akatokea mhuni akaweka bar nzuri wateja wakahama

3. Ugomvi
Walevi wanapenda ugomvi kupigana kuuana ni jambo kufikia

4. Usumbufu wa police wa doria

5 wateja kutoroka na hela

6.kuibiwa na wafanyakazi

7 Rundo la tozo, kuanzia TRA, watu wa taka, TFDA, n.k
 
Kwenye namba sita kuna ile mfanyakazi hakuibii directly ushtuke, ila anachofanya ana anzisha biashara yake ndani ya biashara yako. Mfano akishajua weekend bar inauza kreti kumi, atanza kuagiza zake mbili tatu. Weekend ijayo atauza zako nane na zake mbili. Ukipiga hesabu zimenyooka ila mauzo yameshuka. Kwenye biashara ujasusi wa ndani na nje ni muhimu.
 
Kwenye namba sita kuna ile mfanyakazi hakuibii directly ushtuke, ila anachofanya ana anzisha biashara yake ndani ya biashara yako. Mfano akishajua weekend bar inauza kreti kumi, atanza kuagiza zake mbili tatu. Weekend ijayo atauza zako nane na zake mbili. Ukipiga hesabu zimenyooka ila mauzo yameshuka. Kwenye biashara ujasusi wa ndani na nje ni muhimu.
Hii mbinu ni hatari
 
Hizo ni Biashara huitwa Social Enterprises, Biashara za mazoea na sio za kukupeleka kwenye Utajiri. Unless utengeneze Class unrealistic, zile za kuuza Bia moja 6,000+, VIP kiingilio 50k na other Creativity.

BUT Mostly ni biashara ambayo wanufaika wake (Wanaotajirika), ni wale wanaouza huduma kuzunguka hio Biashara ya Bar, Mfano Ma - Dj's, Wanaokuuzia Pombe, Muziki, wanaokuuzia Bidhaa za Chakula, Viungo, Events managers n.k.

Zile Biashara za pembeni zinazolisha Biashara ya BAR ndio huwa wana chance ya kutajirika, na sio mwenye Bar. Matumizi ya hela zako nyingi huishia kuwanufaisha wao ili Biashara yako ya Bar iweze kuendelea. Na uzuri wa hizi biashara ni kwamba, wakati wengine wanazifunga huwa kuna wapya wengi wanafungua(so haziwezi kuisha). ILA wanaodumu 5years+ ni wachache sana.

Nje ya Mada: ukitaka ufanikiwe, Chagua biashara ambazo zitalisha Social Enterprises( zile Biashara watu hufanya kwa mazoea), Mfano, Uza Kuku wa kienyeji kwenye Restaurants, Uza Spare za Bodaboda, Bajaji, Daladala nk, Uza vyakula na dawa za mifugo, Uza vifaa vya ujenzi, Uza viwatilifu kwa wakulima, MC wa kwenye Sherehe na nyingine kibao.

Inshort, angalia zile biashara watu wanafanya kwa mazoea, kisha wewe wapelekee vitu vitakavyofanya waendelee kuzifanya miaka na miaka
 
Back
Top Bottom