Haji Manara (Msemaji wa Yanga SC) katamba kuwa Wameuza mno Jezi Msimu huu sasa mbona wamezipunguza Bei?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,694
109,126
Kwenu Wabobezi wa Marketing hivi Kupunguza Bei ya Bidhaa ili Uuze nyingi na Utambe kwa Watu ndiyo Mafanikio Kibiashara au Mafanikio zaidi ni Kuuza kwa Bei ya Juu hata kama utauza Chache ile utaingiza Pesa nyingi na pia Utakubalika kwa Ubora ( Quality ) ya bidhaa?

Leo Klabu ya Yanga imeamua Kushusha Bei ya Jezi zake kutoka Tsh 35,000/ mpaka Tsh 30,000/ hali ambayo imetushtua zaidi Great Thinkers wachache tuliobakia sasa Ulimwenguni.

Je, Uongozi wa Yanga SC umeamua haraka sana Kuishusha hiyo Bei ili zinunulike nyingi na waweze Kumlinda Msemaji wao Haji Manara hasa baada ya Wiki Mbili nyuma kusikka akisema kuwa Yanga SC ndiyo Klabu pekee iliyouza Jezi nyingi Afrika Mashariki na Kati?

Shukran nyingi na za dhati kabisa ziende kwa Uongozi wa Simba SC na Mbunifu wa Jezi za Simba SC Fred Nganjiro ( Fred Vunjabei ) kwa Kusimama na Bei ile ile ya Jezi za Simba SC zinazouzwa Tsh 40,000/ na ambazo zimeuzika nyingi na zinaendelea tu Kuuzika huku kila Siku tu zikitolewa za Muundo mpya na anbazo zinapendeza vile vile Mwilini ukivaa ( ukizivaa )

Hivi Mashabiki wa Mpira wenye Akili zao Timamu kabisa waache Kununua Jezi za Klabu ambayo sasa ndiyo Balozi wa Watanzania, wa Rais Samia na wana Afrika Mashariki kisha wanunue Jezi za Timu ambayo haishiriki Mashindano yoyote ya Kimataifa na Kutwa tu inapishana na Malori ya Mkaa, Mafuta na Takataka katika barabara za Vumbi tupu na Milima mingi huko Mikese, Mdaula, Ubena Zomoni, Turiani na Msamvu.
 
Mkuu ,matamang'eo au mabangusilo yamekosa soko lazima yashushwe bei. Mtu mwenye akili timamu hawezi kutembea na mafuvu ya watu kwenye nguo
 
Mfanyabiashara Yeyote Akisha-Meet Target Hana Hasara Tena Hata Akianza Kuuza Kitu Kile Kile Kwa Nusu Bei.
Kwani mkisema kuwa zimedonda ni dhambi, mbona mnapenda kujifanya kuwa juu kila kitu ilhali uwezo wenu ni mdogo tu..!

Nyie mpo tu Nyumbani muuze zaidi kuliko Simba SC wa Kimataifa? Nani kasema..!

Na hivi karibuni mtazitupa kwa mashabiki uwanjani kama mnavyofanya zile zingine..!
 
Yanga imekua timu ya siasa nyingi na propaganda. Waache wapige domo mwisho wasiku hata ubingwa hawapati. Ndio bwana manara atajua watu wa yanga sio watu wazuri watamcharaza bakora.
 
Yanga imekua timu ya siasa nyingi na propaganda. Waache wapige domo mwisho wasiku hata ubingwa hawapati. Ndio bwana manara atajua watu wa yanga sio watu wazuri watamcharaza bakora.
aisee siasa gani Sasa hapo? Hataa man u wanauza jezi kwa discount. Kwani lengo la Yanga si watu wave jezi za timu yao? Halafu eti bei ya jezi ya Simba 40 elfu. Genta acha masikhara.
 
Mfanyabiashara Yeyote Akisha-Meet Target Hana Hasara Tena Hata Akianza Kuuza Kitu Kile Kile Kwa Nusu Bei.
ulaya the last Friday of November inaitwa "financial panic" au wengi wanaita "Black Friday". Hii ni siku ya kujijazia vitu vya thamani kwa nusu bei! huwa ni raha sana! huku home bado sana!!

Yanga wengi ni wazungu wanajua bizness ni kuuza sana ukusanye faida hata kwa watu wa hali ya chini ambao ni wengi!
 
Back
Top Bottom