Wakili wa Moyo-31
ILIPOISHIA:
Tutawarudishia fedha zao.
Wee mwana tutazipata wapi?
Mi najua pa kuzipata.
SASA ENDELEA...
Hebu mwanangu nieleza tatizo nini, kama Colin amekukosea bado tuna nafasi ya kuzungumza tukalimaliza.
Mama Colin hajawahi kunikosea toka tujuane, ila mimi ndiye nimekuwa nikimkosea muda wote. Najua ananipenda sana na uamuzi wangu utamchanganya, lakini ukweli utabakia palepale si chaguo la moyo wangu. Nimejilazimisha kumpenda lakini moyo umekataa hivyo sina budi kuusikiliza moyo wangu unachotaka.
Siku zote moyo wa mtu huwa ndiyo muamuzi kwa jambo lolote kwa vile wenyewe ndiyo unaopokea furaha kwa jambo zuri au la huzuni kwa jambo baya.
Kwa hiyo unasema hujakosana na Colin?
Walaa, najua Colin ananipenda sana na ataumizwa na uamuzi wangu lakini sina jinsi kila ndege hutua mti aupendao.
Mage upo sawa mwanangu?
Nipo sawa mama.
Kauli ile ilimfanya mama yake akae kwenye kitanda baada ya miguu kukosa nguvu.
Mage mwanangu mbona sikuelewi, kipi kimekusibu mama?
Mama najua itakuwa vigumu kunielewa lakini utanielewa tu.
Mara simu ya Mage iliita, aliichukua na kuitazama na kuirudisha bila kuipokea kitu kilichomfanya mama yake kuuliza.
Mbona hupokei kwani inatoka wapi?
Kwa Colin.
Sasa kwa nini hupokei?
Sasa nitazungumza naye nini?
Pokea mwambie leo huwezi kwenda, hujisikii vizuri.
Siwezi kuzungumza naye kwa leo, nitajisikia vibaya.
Simu iliita tena lakini haikupokelewa mpaka ikakatika, baada ya muda msichana wa kazi alimwita mama Mage kuwa kuna simu yake inaita.
Alitoka na kuichukua, ilikuwa inatoka kwa mama Colin, akaipokea mara moja.
Haloo dada.
Eeh! Kuna usalama huko?
Kiasi.
Kulikoni?
Mage kichwa kilimshika ghafla.
Jamani mkwe wangu! Vipi hali yake?
Kidogo hajambo amelala kwa sasa.
Basi tunakuja kumuona.
Usisumbuke, hayupo serious sana.
Basi augue pole maana mwenzake alikuwa na wasiwasi baada ya kupiga simu bila kupokelewa.
Mwambie asiwe na wasiwasi ni kichwa tu lakini anaendelea vizuri kesho atakuwa hajambo.
Basi niwatakie usiku mwema.
Na ninyi pia.
Mama Colin baada ya kumaliza kuzungumza, alimgekia mwanaye aliyekuwa pembeni yake akifuatilia mazungumzo yale.
Vipi mama?
Kumbe kichwa kilimshika ghafla amekunywa dawa kimetulia, alitaka kuja lakini mama yake kamwambia alale kwa leo atakuja kesho.
Duh! Afadhali, nilikuwa na wasiwasi sana.
Kapumzike, kesho mchumba wako atakuja.
Sawa mama.
Colin alikwenda chumbani kwake, kabla ya kulala alichukua simu yake na kuangalia picha zote alizopiga na Mage na nyingine iliyopigwa siku ile mchana aliyotumiwa na Mage alipokuwa na shoga yake Brenda Mlimani City- Samakisamaki.
Aliibusu picha kubwa ya mpenzi wake iliyokuwa katika tabasamu la kufa mtu na kusema kwa sauti ya chini.
Mage wewe ndiye mke wa maisha yangu, aliikumbatia na kujilaza.
***
Mama Mage usingizi uligoma kabisa na kukiona kichwa kikitaka kupasuka kutokana na kuchanganywa na kauli ya mwanaye, alijiuliza kama mwanaye atasimamia uamuzi ule angeuweka wapi uso wake, wasiwasi wake huenda amemfumania Colin na mwanamke mwingine na kuamua kuvunja uchumba.
Bado aliona kama ni hivyo linazungumzika kwa vile wote wamejuana wakiwa tayari wanayajua mapenzi. Alinyanyuka kitandani na kutoka kwenda kwa mwanaye kupata ukweli kwani alikuwa amechanganyikiwa sana.
Alitoka taratibu, taa ya sebuleni ilikuwa imezimwa. Kulikuwa na hali ya ukimya kutokana na watu wote kuwa wamelala.
Hakutaka kuwasha taa ya sebuleni, alitembea taratibu hadi chumba cha Mage. Alipotaka kuushika mlango, alimsikia mwanaye akizungumza na simu, alitulia ili asikilize anazungumza nini na nani. Alimsikia mwanaye akisema:
Kama hivyo nimeisha tibua yote kwa ajili ya mapenzi yangu mazito kwako, kama umejitoa muhanga kwa ajili yangu nami sina budi kujitoa kwa ajili yako. Najua uamuzi wangu utamchanganya mama na yule mchovu lakini wewe ni zaidi yao wote, nakupenda sana zaidi ya kukupenda. Nipo radhi vyote duniani viondoke ubakie peke yako.
Please mpenzi usinitende, kosa lako ni mauti yangu, nashukuru kwa kujali mapenzi yangu kwako. Asante mpenzi wangu naomba ulale usingizi
Mkuu mbona umeruka sehemu ya 30? ITAENDELEA..................