mizambwa
JF-Expert Member
- Oct 8, 2008
- 4,421
- 1,792
- Thread starter
- #101
Wakili wa Moyo-26
ILIPOISHIA:
Mkuu wa Polisi, Mr. Clarence alimchukua Mage na kumrudisha nyumbani.
Mama yake alifurahi kumuona mwanaye akiwa na Mr. Clarence Mulisa.
"Asante shemeji."
"Kawaida, nina imani Hans akipata nafuu kila kitu kitakuwa wazi."
SASA ENDELEA...
"Tena Mungu ampe afya ili kuwaumbua wenye roho mbaya wanaotaka kuiharibu harusi ya mwanangu."
"Usiwe na wasiwasi, kila kitu kitakwenda kama kilivyopangwa na aliyetenda unyama ule atajulikana kwani mkono wa dola ni mrefu."
Mkuu wa polisi aliaga na kumuacha Mage na mama yake, baada ya kuondoka Mage aliangua kilio.
"Mama kosa langu nini? Mbona familia ya akina Hans wameniandama namna hii?, Mimi nimuue mke wa Hans pamoja na mwanaye ili iweje?"
"Ndiyo dunia ilivyo mwanangu, kwa vile baba yako yupo atakusimamia."
"Unajua mama mimi nilikuwa na wasiwasi labda aliyefanya vile ni Colin."
"Wee! Temea chini tena usirudie kusema kitu kama hicho, Hans na Colin wapi na wapi?" Mama yake alijibu kwa ukali.
"Basi mama nisamehe ni mawazo tu."
"Tena umeniudhi sana, wee kidogo ufe na presha kwa kusingiziwa unataka kumpaka shombo mtoto wa watu."
"Basi mama nisamehe, ulikuwa wasiwasi wangu."
"Nataka uoge ubadili nguo uende kwa mwenzio ukamtoe hofu usimueleze ya kupelekwa polisi."
"Sawa mama."
Mage alikwenda kuoga na kubadili nguo ambapo alichukua gari na kwenda kwa Colin, akiwa njiani alijawa na mawazo juu ya familia ya Hans.
Alijiuliza kipi hasa kilichofanya wamfikirie yeye kwanza. Aliona jinsi gani familia ile ilivyokuwa ikimchukia na kuamini kauli ya mama yake kuwa hata kama angeolewa asingedumu kwenye ndoa yake kwa vile hakuwa chaguo la familia.
Alijikuta taratibu mapenzi yake yote akiyahamishia kwa Colin na kuuapia moyo wake kumpenda kwa nguvu na akili zake zote. Alipofika nyumbani kwao Colin baada ya kuteremka kwenye gari aliingia ndani huku akikimbia kama mtu aliyepagawa. Sebuleni alimkuta mama Colin, alishtuka kumuona katika hali ile.
"Vipi Mage?"
"Mama, mume wangu yupo wapi?" aliuliza akionesha kuchanganyikiwa.
Wakati huo Colin alikuwa akitokea chumbani kwake kuja sebuleni, alipomuona alimkimbilia na kumkumbatia.
"Jamani mume wanguu!"
"Vipi mbona hivyo?" Colin alishtuka uchangamfu wa Mage uliopitiliza.
"Najua nimekuudhi nisamehe sana, mama nimemuudhi sana mume wangu," Mage alisema huku akilia.
"Hujamuudhi chochote," mama Colin alisema.
"Najua nimemuudhi, Colin naomba twende chumbani."
Walishikana mikono na kuelekea chumbani na kumuacha mama Colin akiwatazama na kuchekelea moyoni na kusema kwa sauti ya chini. "Kweli wanapendana." Aliwatazama mpaka walipopotea machoni kwake.
Colin na Mage walikwenda hadi chumbani, alipofika ndani Mage alijitupa kifuani kwa mpenzi wake na kuanza kulia kitu kilichomshtua Colin na kuhoji.
"Vipi mpenzi?"
"Colin nisamehe sana mpenzi wangu."
"Kwa lipi?"
"Najua leo nimekukosea kwa kuondoka bila kukuaga kitu kilichokufanya usumbuke kunitafuta, kibaya zaidi sijapokea simu zako na kukataa kuzungumza na wewe uliponifuata nyumbani."
"Kumbe ni hayo? Achana nayo."
"Hapana najua umenikubalia ili yaishe lakini umejenga picha mbaya juu yangu."
"Walaa."
"Colin nihukumu hukumu yoyote lakini elewa nakupenda sana mpenzi wangu, nilitaka kufanya surprise lakini ikaenda ndivyo sivyo. Nilishindwa nikueleze nini kwa vile sikuwa na la kukueleza kwa wakati ule hasa baada ya Brenda kunichanganya."
"Yote mama alinieleza ndiyo maana nilikuelewa toka asubuhi."
"Colin lakini si unajua nakupenda?" Mage alimuuliza kwa sauti ya kudeka.
"Najua, ndiyo maana upo hapa."
"Nashukuru kulifahamu hilo."
Siku ile Mage alishinda pale na kufanya kazi zote za nyumbani ikiwa ni pamoja na kupika chakula cha jioni. Colin alijikuta akisahau yote na kujiona kama tayari ameshamuoa Mage.
Siku ile muda wote walikuwa pamoja kama kumbikumbi kwa kufanya kazi kwa kusaidiana.
Mama Colin muda wote alikuwa mtu wa tabasamu na kuona ndoa ya mwanaye jinsi itakavyojaa furaha na upendo.
Aliwaangalia walivyopendeza kwa kusaidiana kazi zote za jikoni mtu na mchumba wake. Alifumbata mikono yake na kuomba kwa sauti ya chini.
"Eeh! Mwenyezi Mungu baba ijalie ndoa ya wanangu iwe yenye matunda," baada ya dua alipiga njia ya msalaba kumshukuru Mungu.
Siku ile ilikuwa ya furaha kwa wapenzi wawili kwa Mage ambaye alihamishia mapenzi yake yote kwa Colin baada ya kujua hata kama angempenda vipi Hans asingekuwa na nafasi ndani ya familia yake. Aliona jinsi gani isivyompenda mpaka kumzushia shutuma nzito za mauaji ya shambulio la kuua.
Kingine kilichomuweka njia panda kama Mungu atamsaidia Hans kupona atamchukuliaje, lazima naye angeamini muhusika ni yeye. Lakini kwa upande wa Hans alijua ni vigumu kumshuku yeye kutokana na ukaribu wao ulivyokuwa.
Angekuwa na wasiwasi kama angekuwa akilipigania penzi la Hans. Kama tatizo lile lingemtokea baada ya kuoa lazima Hans angejua ni yeye, lakini baada ya mkewe kupata ujauzito na kujifungua penzi lake alilizika rasmi.
Aliamini ule ndiyo muda wa kulionesha penzi lake halisi kwa Colin, siku ile alilala tena na kuondoka siku ya pili huku kila mmoja akifurahia penzi la mwenzake.
Ukaribu wa Mage na Colin kwa kufuatana muda wote kama kumbikumbi, ulifanya Colin ashindwe kutekeleza ahadi yake kwa kina Cecy. Baada ya kusubiri kwa wiki bila kuonekana dalili zozote za kutekelezwa ahadi. Cecy aliyekuwa amejilaza kitandani na kukosa usingizi.
Itaendelea............