Hadithi: Wakili wa moyo

Hadithi: Wakili wa moyo

Wakili wa Moyo-29


Waliongozana wote hadi kwenye gari.

"Ingia mlango wa nyuma," Brenda alimwambia Mage, naye hakubisha, aliingia.
Ndani ya gari kulikuwa na giza, Brenda baada ya kuingia mbele aliwasha taa na kumfanya Mage ashtuke kumuona Hans.

"Ha! Hans?"

"Ndiyo mimi Mage samahani kwa kukushtukiza."

"Bila samahani, kwanza unaendeleaje?"

"Namshukuru Mungu sijambo kabisa."

"Pole na kufiwa mke na mtoto."

"Asante, pole na wewe kutokana na ulichotendewa na familia yangu."

"Hans achana na hayo yameshapita, nina imani kuna kitu kimekuleta naomba tuzungumze kwa haraka nataka kwenda kwa mume wangu muda si mrefu."

Hans alijikuta akitulia huku maneno yakigoma kutoka mdomoni, Mage alishangaa kuona mpenzi wa zamani akitokwa na machozi. Brenda alitoka nje ya gari na kuwaacha wapenzi ndani ya gari wazungumze yao.

"Jamani nipo nje."

"Hakuna tatizo, usikae mbali natoka sasa hivi," Mage alisema.

Baada ya kutoka, Mage alimuuliza Hans aliyekuwa akitokwa machozi.

"Hans umeniita kuona machozi yako au kuna kitu kingine? Kama ni machozi nimeisha yaona, naomba niende zangu," Mage alizungumza kwa sauti ya upole huku akimtazama usoni Hans.

"Ma..ma..ge," Hans alisema kwa kigugumizi.

"Jina langu."

"Kilichonileta si kuja kukuonesha machozi bali moyo wangu umejaa maumivu makali."

"Najua inauma kupoteza mke na mtoto si kitu cha kawaida yataka moyo wa chuma kuyashinda maumivu yake lakini Mungu siku zote ni mfariji na atakufanya utayasahau yote kisha atakuletea mke mwingine."

"Mage mimi na wewe tuliahidiana nini?"

"Kuoana kuwa mke na mume."

"Baada ya matatizo ya familia yangu nilikueleza nini?"

"Ulisema huwezi kuzaa na yule mwanamke, baadaye utamuacha na kunioa mimi."

"Kwa nini umekubali kuolewa na mwanaume mwingine?"

"Kwa sababu umevunja ahadi yetu."

"Mage nina imani unajua jinsi gani ninavyokupenda?"

"Siyo unavyonipenda bali ulivyokuwa ukinipenda."

"Mage moyo wangu hautachoka kukupenda, nilikueleza nini baada ya kulazimishwa kuoa mwanamke mwingine?"

"Ulisema wakikulazimisha kuoa utajiua."

"Ulinishauri nini?"

"Nilikuwa radhi uoe lakini si kukupoteza maishani, ulichoniahidi ndicho kilinipa moyo na kuwa radhi kukusubiri hata miaka mia. Lakini wewe ndiye ulivunja mkataba na kuamini sina changu na kuamua nami kutafuta wangu japokuwa ilikuwa sawa na kunimezesha mfupa."

"Ndiyo sababu ya mimi kuja kuzungumza na wewe, baada ya kunisikiliza uamuzi utakaoutoa hapa sitapingana nao hata kama utaniumiza."

"Haya niambie hicho kilichokuleta."

Hans alianza kuzungumza kwa sauti ya chini yenye kisikika huku machozi yakiweka michirizi kwenye mashavu. Mazungumzo yalikuwa ‘off air' ambayo hayakutakiwa mtu yeyote kusikia zaidi ya watu wawili tu. Hans alimaliza kuzungumza huku machozi na kamasi zikimtoka chapachapa.
[/FONT]

Itaendelea...........

Wakili wa Moyo-30



Muda wote Mage alijitahidi kumbembeleza Hans japokuwa naye alikuwa akilia.

"Hans nimekuelewa lakini hukutakiwa kufanya hivyo."

"Sikuwa na jinsi, hukutaka kunisikiliza nilikuwa na wakati mgumu wa kuweza kunisikiliza. Kama ningekufa bila wewe kuujua ukweli wa moyo wangu ningekuwa nimekufa kibudu.

"Kama ningeshindwa kabisa ningekuja kujiua kwenye harusi yako ili ujue nilichokuahidi hakitabadilika moyoni mwangu kuwa kifo pekee ndicho kitanitenganisha na wewe."

"Mmh! Mbona Hans unanipa mtihani mkubwa, japokuwa uamuzi ni wangu lakini dunia itanitenga."

"Lakini Mage nilikueleza kila kitu juu yetu, wewe ndiye uliyeshikilia uhai wangu kwa mara nyingine, wa kuniua au kuniacha hai."

"Hans hata siku moja kifo chako hakitatoka mikononi mwangu, naomba uniache kwa leo, mengine tutazungumza kesho, kichwa changu kimevurugika hata sielewi nifanye nini."

"Ila kumbuka uhai wangu umeubeba wewe."

"Naelewa Hans."

"Kwa hiyo niondoke na jibu gani?'

"Niache kwa leo, nimekuelewa Hans."

"Sawa lakini bado nipo njia panda."

"Hans kuwa muelewa, nimekueleza nimekuelewa unataka nini tena?"

"Basi nashukuru."

"Nikutakie usiku mwema."

"Na kwako pia."

Mage aliteremka kwenye gari na kumuaga shoga yake huku akifuta machozi yaliyokosa kizuizi kisha alielekea ndani mwao. Brenda aliingia ndani ya gari na kushangaa kumkuta Hans akifuta machozi wakati Mage naye alitoka akifuta machozi.

"Vipi kuna usalama?"

"Kiasi."

"Mmeelewana?"

"Ndiyo."

"Kwa hiyo tunaweza kwenda."

"Ndiyo."

Brenda aliwasha gari na kuliondoka kuelekea walipokuwa wameliacha gari la Hans, njiani alijaribu kudodosa kwani kila mmoja alionekana kulia.

"Hans Mage anasemaje?"

"Hana la kusema bali nilitaka tu kumfikishia ujumbe, nashukuru amenisikiliza."

"Kwa hiyo roho yako imetulia?"

"Nashukuru, tukifika kwenye gari nitakupa zawadi yako niliyokuahidi."

"Nitashukuru."


***

Muda ulizidi kukatika bila Mage kuonesha dalili zozote za kutoka kwenda kwa Colin, kitu kilichomshtua mama yake ambaye aliwahi kurudi kwa ajili ya mwanaye kwenda kwa mchumba wake, aliangalia saa ya ukutani ilimuonesha inakaribia saa nne usiku. Alijiuliza labda mwanaye ametoka bila yeye kujua.
Ilibidi amuulize msichana wa kazi kama Mage ametoka yeye akiwa chumbani.

"Sofi Mage ametoka saa ngapi bila kuniaga?"

"Mmh! Mama sijamuona kutoka."

"Unamaanisha yupo chumbani kwake?"

"Sijajua ila sijamuona."

Mama Mage alinyanyuka na kwenda chumbani kwa mwanaye, alikuta mlango umerudishwa, alisukuma na kuingia bila hodi na kumkuta Mage amejilaza akiwa amekumbatia mto huku machozi yakimwagika kama maji. Mama yake alishtuka na kutaka kujua kulikoni mwanaye kuwa katika hali ile.

"Mage! Nini mwanangu?"

"Mamaa..maamaa," Mage alishindwa kuzungumza, aliangua kilio.

"Mage una nini?" mama yake alizidi kumshangaa.

"M..m..maa..ma," Mage kila alipotaka kusema maneno yaligoma kutoka mdomoni.

"Mage mwanangu umepatwa na nini, hebu nieleze mimi ndiye mama yako nipo tayari kukusikiliza na kukusaidia."

"Mama nipo kwenye wakati mgumu sana maishani mwangu."

"Kwa nini unasema hivyo?"

"Najua nitakuudhi wewe mama yangu lakini nina imani ndiyo tiba sahihi ya moyo wangu ambao umekuwa matesoni kwa muda mrefu."

"Unamaanisha nini?" mama yake alishtuka mpaka mapigo ya moyo yalianza kumwenda kasi.

"Mama nitakachokisema najua kitakuwa sawa na kumng'oa mtu jino bila ganzi."

"Unamaanisha nini?"

"Mama sitaki kuolewa tena."

"Niniii?" mama alishtuka.

"Mama sitaki kuolewa na Colin."

"Kwa nini?"

"Si chaguo la moyo wangu."

"Mwanangu unasema ukweli au unatania?"

"Nasema kweli kabisa."

"Mmh! Na mipango ya ndoa?"

"Tunasitisha kwa vile muda bado."

"Na watu tuliowachangisha fedha za send off."

"Tutawarudishia fedha zao."

"Wee mwana tutazipata wapi?"

"Mi najua pa kuzipata."


Itaendelea ...............

Hapana bwana hayajaoneshwa pale

Sumu iliyomvuruga Mage hii.
 
Wakili wa Moyo-33



ILIPOISHIA:
SIKU ya pili, Mage aliamka asubuhi, akaoga na kujipamba kisha alitoka, alimkuta mama yake amekaa sebuleni ameshika tama.
"Mama vipi mbona hivyo?" alimuuliza huku akijilazimisha kujenga tabasamu.
SASA ENDELEA

"He! Safari ya wapi?"

"Naenda kwa Colin mama."

"Kweli?" mama yake alishtuka.

"Ndiyo mama."

"Haya wasalimie."

"Sawa mama, ila sitakuwa hewani kwa siku mbili."

"Kwa nini?"

"Utajua nikirudi."

"Kwani mnakwenda wapi?"

"Utajua tu mama."

"Haya mwanangu safari njema."

"Asante mama."

Mage kabla ya kutoka, alimbusu mama yake na kuelekea nje na kumfanya mama yake kumsindikiza kwa macho kisha alinyanyua mikono juu kumshukuru Mungu kwa kuweza kumbadili msimamo wake. Alijiuliza kama angesimamia msimamo wake, kwake ingekuwa aibu na fedheha ya kuvunjika kwa harusi aliyoiandaa kwa nguvu kubwa.

Toka aamke alikuwa hajaoga zaidi ya kukaa sebuleni kutafuta njia ya kuinusuru ndoa ya mwanaye ambayo aliamini ni muujiza pekee ndiyo wenye kuiponya kwa kuamini nguvu za kibinadamu zisingeweza.
Alinyanyuka na kwenda kuoga ili apate kifungua kinywa.

Mage alikwenda kuchukua gari aina ya Nissan Patrol nyeupe na kutoka kuelekea nyumbani kwa kina Colin.

Aliendesha gari taratibu tofauti na siku zote alizoendesha kwa kasi. Alirudisha kumbukumbu ya muda mfupi ya picha ya mama yake aliyokuwa amekaa ameshika tama kuonesha kabisa uamuzi aliochukua umemchanganya sana na kumnyima raha.

Alipeleka macho yake kwenye simu yake iliyokuwa pembeni yake na kuichukua alitafuta namba ya Hans na kumpigia. Iliita kidogo na kupokelewa.

"Haloo my sweet."

"Vipi umeamka salama?" alimuuliza kwa sauti iliyopooza.

"Mmh! Naweza kusema nimezaliwa upya nimelala usingizi mtamu nilioukosa muda mrefu."

"Nashukuru kama ni hivyo."

"Mmh! Niambie moyo wangu?"

"Hans nilitaka kukujulisha kuwa sitakuwa hewani kwa siku mbili ila ya tatu nitarudi kama kawaida."

"Kuna nini?"

"Utajua baadaye."

"Upo wapi?"

"Nimetoka mara moja."

"Sawa nimekuelewa mpenzi."

"Basi nikutakie siku njema yenye furaha."

"Na kwako pia."

Mage alikata simu na kumpigia shoga yake Brenda, haikuchukua muda ilipokelewa upande wa pili.

"Vipi shoga?"

"Poa, za asubuhi?"

"Nzuri tu."

"Nilitaka kukujulisha sitakuwa hewani kwa siku mbili."

"Kwa nini shoga halafu mbona leo kama hujachangamka?"

"Aah! Nipo katika kipindi kigumu lakini nitakivuka tu japokuwa najua jasho la damu lazima litoke."

"Bado una msimamo uleule?"

"Utajua baada ya siku mbili."

"Sasa upo wapi?"

"Nakwenda kwa Colin."

"Loh! Afadhali shoga maana mimi mwenyewe nilikuwa sina amani moyoni mwangu."

"Basi ndiyo hivyo tutawasiliana kesho kutwa."

"Na kesho?"

"Sitakuwa hewani kwa siku mbili."

"Mmh! Umeamua, safari njema msalimie sana shemu Colin, mwambie nimemmisi."

"Salamu zimefika."

Baada ya Mage kukata simu, shoga yake Brenda alitupa simu kwenye kochi na kushika kifua na kusema:

"Ooh! Afadhali Mage kabadili uamuzi sijui kama mama yake angenielewa."

Mage baada ya kumaliza kuzungumza na Brenda, aliweka simu pembeni na kuiweka mikono yote juu ya usukani na kukanyaka mafuta kuelekea nyumbani kwao Colin. Macho yake yalitulia kutazama mbele huku machozi yakijaa taratibu katika macho yake.

Alijikuta akisema kwa sauti kama anazungumza na mtu:

"Mapenzi haya! Kwa nini Mungu uliumba mapenzi, kwa nini yamekuwa kila siku yanachukua furaha yangu badala ya kunifariji?"

Alichukua kitambaa pembeni yake, alifuta machozi na kuendelea na safari. Alisimamisha gari mbele ya geti la nyumba ya kina Colin, geti lilifunguliwa na kuingia ndani.

Aliliweka kwenye maegesho kabla ya kuteremka, alivaa miwani ya jua ili kuficha macho yake na kuteremka. Wa kwanza kuonana naye alikuwa mama Colin ambaye alimkimbilia na kumpokea Mage.

"Wawaooo mkwe wangu."

"Waawoo mama, shikamoo."

"Marahaba."

" Colin yupo wapi?"

"Yupo chumbani kwake, aliniambia utakuja."

"Ndiyo mama."

"Vipi unaendeleaje?"



Itaendelea.................
 
Wakili wa Moyo-34



ILIPOISHIA WIKI ILIYOPITA:
"Wawaooo mkwe wangu."
"Waawoo mama, shikamoo."
"Marahaba."
"Colin yupo wapi?"
"Yupo chumbani kwake, aliniambia utakuja."
"Ndiyo mama."
"Vipi unaendeleaje?"

SHUKA NAYO...


"Namshukuru Mungu nipo sawa."

"Haya mwanangu kamuone mwenzio maana alikuwa na kimuhemuhe hasa baada ya kusikia unaumwa."

"Sawa mama."

Mage alielekea chumbani kwa Colin, mlango ulikuwa umerudishwa, aliusukuma bila hodi na kuingia ndani. Alimkuta Colin akibandika picha kubwa ya rangi ukutani wakiwa ufukweni wamelaliana chini ya picha ile kulikuwa na maneno ya rangi nyekundu yaliyokuwa yanasomeka: ASANTE MUNGU KWA KUNIPA MKE MWEMA na chini kuliandikwa: MAGRETH NAKUPENDA ZAIDI YA KUPENDA .

Mage aliposoma yale maneno na kuiona ile picha, moyo ulimuuma na kuangua kilio cha sauti, Colin alishtuka kusikia sauti ya mchumba wake, alipogeuka alimuona Mage amesimama akiwa ameshika kifua chake. Aliteremka haraka kitandani alipokuwa amepanda kubandika picha ile kubwa na kumfuata alipokuwa amesimama na kumkumbatia kifuani.

"Vipi mpenzi kipi kinakuliza?"

"Najua nina mtihani mzito moyoni mwangu lakini Mungu atanipa nguvu na nitashinda."

"Kuna nini mbona unanitisha?"

"Kawaida tu, Colin naomba ujiandae tuna safari."

"Ya wapi?"

"Surprise."

"Waawoo!" Colin alisema huku akimkumbatia Mage.

Kwa vile alikuwa ametoka kuoga, alibadili nguo na kumweleza Mage.

"Nipo kamili mpenzi."

"Chukua na nguo nyepesi za kupumzikia."

"Tunaenda wapi?"

"Utajua tu."

Walichukua begi dogo na kuongozana hadi sebuleni, walimkuta mama Colin akimuelekeza jambo msichana wa kazi, alipowaona aliacha na kuwageukia.

"Jamani wapendanao safari ya wapi?"

"Tunatoka kidogo," alijibu Mage.

"Haya mwende salama."

"Asante mama, ila hatutakuwa hewani kwa siku mbili."

"Kwa nini?"

"Utajua tu," Mage alijibu

"Kwa hiyo leo hamrudi?"

"Ndiyo mama, tutarudi kesho kutwa."

"Mmh! Haya wanangu nawatakieni safari njema," mama Colin aliwakumbatia wote na kuwabusu kisha aliwasindikiza nje hakuondoka mpaka walipotoka nje ya geti ndipo aliporudi ndani.


***

Baada ya gari kuingia barabarani, Mage alimgeukia Colin aliyekuwa ametulia na kumwambia.

"Colin zima simu yako."

"Kwa nini?"

"Sitaki uwasiliane na mtu yeyote zaidi yangu."

"Sawa mpenzi," Colin alizima simu yake.

"Zima na yangu."

Colin alichukua simu ya Mage na kuizima, safari iliendelea. Gari lilielekea barabara ya Kawawa mpaka Mwenge na kukata mtaa wa viwanda mpaka njia panda ya Kawe. Mage hakukunja, alinyoosha na kutokea Afrikana, alikata kulia kuelekea Tegeta. Colin hakuhoji gari lilivuka Tegeta likaingia Boko likavuka Bunju na kuitafuta Bagamoyo.

Ndani ya gari muziki laini uliendelea kuunguruma, kila mtu alikuwa kimya kutokana na mwendo wa kasi.

Alisimamisha gari mbele ya Hoteli ya Oceanic Bay, baada ya kusimamisha gari alimgeukia Colin aliyekuwa ametulia akiuangalia umahiri wake wa kuendesha gari.

"Nina imani tuna siku mbili za kila mmoja kumaliza hamu zake kwa mwenziye."

"Mage mpenzi siku zote kitamu hakiishi hamu, penzi lako kwangu siwezi kulikinai."

Mage hakuongeza neno, alimshika mkono na kuongozana naye mpaka mapokezi na kukodi chumba kizuri kwa siku tatu.

"Mage si umesema tunarudi kesho kutwa?"

"Tatizo nini hata tukikaa mwaka kuna mtu anatudai."

"Hakuna."

Baada ya kupata chumba walikwenda chumbani kwao, chumba kilikuwa kizuri sana.

"Colin unakionaje chumba hiki?"

"Kizuri sana, unaonaje fungate yetu tuje tuifanye huku."

"Tutaangalia muda ukifika."

Baada ya kuoga, kwa vile muda ulikuwa umekwenda, walivaa nguo nyepesi na kwenda hotelini kupata chakula cha mchana kisha walihamia ufukweni kupata upepo wa bahari, muda mwingi Colin alikuwa mtu mwenye furaha kuwa karibu na mpenzi wake, mchumba wake, mkewe mtarajiwa.

Lakini Mage alionekana kulazimisha furaha kutokana na siri nzito iliyokuwemo moyoni mwake.
Baada ya kutosheka na upepo wa bahari, walirudi ndani na kujilaza kitandani mkao wa mahaba huku wakiangalia video. Colin muda mwingi alijiuliza kwa nini wamezima simu ilibidi amuulize Mage
.
"Mpenzi kwa nini tusiwashe simu hata kwa muda?"

"Colin hizi ni siku zetu ambazo ni muhimu kwetu, sitaki kusikia chochote masikioni kwangu zaidi ya sauti yako."

"Nimekuelewa mpenzi wangu."

"Colin," Mage alimwita.

"Naam mpenzi."

"Hivi mfano uwe nyumbani kwenu, mara mama anakupigia simu kukueleza nimefariki, utafanyaje?"

"Mage hayo ni maneno gani, umesema tupo kwenye furaha sasa maneno ya kifo yanafuata nini?"

"Najua hapa siyo sehemu yake lakini naomba unijibu."

"Kwa kweli nitachanganyikiwa, naweza hata kufa."

"Hivi umpendaye akifa kuna sababu ya kuchanganyikiwa? Kwani baada ya mazishi yake, si kuna wengine wapo pengine zaidi ya yule aliyeondoka."

"Ni kweli, lakini kinachomtesa mtu ni mazoea si uzuri wa sura wala umbile la mtu."

"Kwa mfano mimi nikisema sikupendi utafanyaje?"

"Nitafanyaje nawe umeamua."

"Hutaumia?"

"Nitaumia lakini nitafanya nini, lakini naamini mimi na wewe tunapendana, hakiwezi kutokea kitu kama hicho."

Mage alibadili mazungumzo kwa kumshika mkono Colin na kuelekea naye bafuni kuoga, waliingia kwenye jakuzi na kuoshana kisha walirudi kitandani kuburudisha mioyo yao.

Mage alimpa penzi Colin, penzi shatashata ambalo lilimrusha akili, naye alijibu mashambulizi kitu kilichomfanya Mage aangue kilio na kumshtua mpenzi wake.

"Vipi mpenzi mbona unalia?"

"Colin sina jinsi lazima iwe."

"Iwe nini?"

"Utajua tu."

Mage alimvamia Colin na kuendelea kustarehe bila kuliweka wazi jambo lililokuwa likimliza, alijitahidi kurudi katika hali yake ya kawaida ya uchangamfu na kumfanya Colin asahau kitendawili chake.


Itaendelea.................
 
Mapenzi kizunguzungu, Mapenzi hayana dawa............Saida Karori.
 
Back
Top Bottom