Hadithi: Wakili wa moyo

Hadithi: Wakili wa moyo

nahisi mage ndo anamuaga colin kijajnja kwa kumpa kamchezo ili hata wakiachana colin roho isijutie sana.., mawazo yangu tu hayo ni mizambwa atategua kitendawili
 
Last edited by a moderator:
Mkuu siku hizi unatutesa sana ... hii kitu hauirushi kama ilivyokuwa mwanzo
 
jamn mizambwa mbn ivo ujue hadith zako ni nzur na pia zinasomwa na watu wengi sasa cjaelewa tatzo ni wapi jmn mpk unakuwa unatuma hadith moja af unakaa siku nne badae ndo unatoa au tupe utarbu bas coz kwenye hisia zangu toka majuz hamna kitu tusikilize bas maombi yetu mizambwa
 
Wakili wa Moyo-35


ILIPOISHIA:
Mage alimvamia Colin na kuendelea kustarehe bila kuliweka wazi lililokuwa likimliza, alijitahidi kurudi katika hali yake ya kawaida ya uchangamfu na kumfanya Colin asahau kitendawili chake.
SASA ENDELEA...


Walikaa kwenye hoteli ile kwa siku mbili huku wakiongozana kama kumbikumbi, kila mmoja alijua wawili hao wanapenda mapenzi ya dhati.

Siku moja mchana baada ya kupata chakula, walipumzika kwa muda kabla ya kujiandaa kurudi mjini.
Mage akiwa amejilaza pembeni ya Colin, alimnyanyua na kumgeukia mpenzi wake na kumwita.

"Colin."

"Naam mpenzi."

"Hivi unajua kwa nini toka juzi sijakuita mpenzi?"

"Sijajua."

Mage alitulia kwa muda akimtazama Colin usoni mara machozi yalianza kumtoka, Colin alizidi kumshangaa mpenzi wake kwani toka wamefika Bagamoyo ameshindwa kumuelewa.

"Colin," alimwita tena.

"Naam."

"Najua unanipenda."

"Sana."

"Najua kabisa nitakachokueleza kitakushtua na kukumiza moyo wako, sawa na kuupasua bila ganzi kwa kisu butu. Lakini ukweli utabakia palepale sina jinsi, nina imani penzi la kweli huwa halitengenezwi na mtu bali mhusika mwenyewe."

"Ni kweli."

"Unajua penzi letu halikuwa la sisi kupendana bali kutengenezwa na wazazi wetu?"

"Najua lakini tulipoonana kila mtu alimpenda mwenzake."

"Unajua hiyari yashinda utumwa?"

"Najua."

"Nina imani nilikueleza jinsi mapenzi yalivyoniumiza."

"Ndiyo."

"Na aliyesababisha nilikueleza."

"Ndiyo."

"Basi napenda kukueleza hili ambalo moyo wangu unavuja damu kwa maumivu kwa vile sikupenda liwe kwani hiyari yashindwa utumwa, lazima niseme ukweli wa moyo wangu kuwa Colin nilikupenda lakini Hans nilimpenda zaidi. Hans baada ya kufiwa na mkewe amerudi kwangu na yupo tayari kutimiza ndoto yetu tuliyoiweka muda mrefu,"

Mage alimeza mate huku akiendelea kutokwa na machozi kisha aliendelea kuzungumza kwa sauti ya chini yenye mchanganyiko na kilio.

"Najua kauli yangu itakuumiza lakini ndiyo ukweli wenyewe, Colin nimeamua kwa hiyari na mapenzi yangu kuuvunja uchumba wetu kwa hiyo harusi yetu haitakuwepo tena, penzi tamu tulilopeana ndilo la mwisho. Tukitoka hapa kila mtu ashike hamsini zake."

"Mage," Colin alimwita kwa sauti ya chini.

"Abee."

"Unasema kweli au unatania?"

"Nasema kweli," Mage alijibu huku akikaza macho.

"Hapana, acha utani Mage unaweza kuniua kwa presha."

"Huwezi Colin, wewe ni mwanaume umeumbwa kukabiliana na matatizo, kumbuka amenikuta tayari nimeshaanza uhusiano na mtu ambaye ndiye aliyenionjesha dunia ya mapenzi na aliniahidi kunioa. Toka niachane naye sikuwahi kuwa na mwanaume mwingine zaidi yako, kilichotokea ni kutoelewana lakini sasa hivi tumeelewana na mipango yetu lazima itimie."

"Mage japo Hans ndiye aliyekuonjesha dunia ya mahaba lakini alikutenda, Mage nimekukosea nini mpaka uchukue uamuzi mzito na wa kikatili kama huo?" Colin aliuliza huku machozi yakimtoka.

"Hujanikosea kitu, hata mimi nilikupenda sana, lakini siwezi kuishi na wewe kwa kujilazimisha au kukufanya kama bodi lakini injini awe Hans. Colin, Hans nampenda sana aliniudhi na kuumiza moyo wangu lakini siku aliponiomba msamaha moyo wangu uliyeyuka kama bonge la mafuta kwenye kikaango cha moto. Siwezi kuwa nawe kimwili wakati mawazo yangu yote yapo kwa mwanaume mwingine.

"Narudia, naomba ukubaliane na uamuzi wangu wa kuvunja uchumba tukiwa na mioyo safi, kuachana kwetu kusijenge uadui. Tuendelee kuwa marafiki kwenye harusi yangu uje, ya kwako nije."

"Mage uamuzi uliochukua ni kuupasua moyo wangu bila ganzi, naomba urudishe moyo nyuma, mpenzi wangu bora ungeninyang'anya kila kitu katika mwili wangu na kuniachia moyo wako kwani ni muhimu kuliko chochote duniani japo nipo nawe kwa muda mfupi lakini nimekuzoea sana."

"Siwezi kuishi mapenzi ya kuigiza niache nimpende aliyechaguliwa na moyo wangu."

"Mage siwezi kukubali kirahisi namna hiyo, nasema sikubali, lolote na liwe nasema huondoki kama sivyo, nitamwaga damu ya mtu," Colin alisema huku akisimama.

"Colin mapenzi si kulazimishana, usisababishe nikakasirika na kutoa maamuzi yatakayokuumiza mara mbili."

"Nasema sikubali...toa uamuzi wowote kumbuka nimekutoa kwenye mateso ya kutendwa, leo nikuache uondoke hivihivi? Sikubali," Colin alikuwa mkali.

"Colin nasema hivi, kila usemalo ni kweli tupu na una haki yoyote ya kufanya lakini kumbuka penzi halilazimishwi, nina imani umenielewa, kuwa mstaarabu tuachane kwa usalama."



Itaendelea baadaye leo
 
Mkuu no. 34 mbona haipo? kwa mwenye nayo p'se?


Sent from my iPhone using JamiiForums mobile app
 
Wakili wa Moyo-36



ILIPOISHIA:
"Colin nasema hivi, kila usemalo ni kweli tupu na una haki yoyote ya kufanya lakini kumbuka penzi halilazimishwi, nina imani umenielewa, kuwa mstaarabu tuachane kwa usalama."
SASA ENDELEA…


Mage alinyanyuka na kumsogelea Colin aliyekuwa ameinama akilia na kumpigapiga mgongoni.

"Sweet naomba usilie mwanaume kaumbwa kukabiliana na matatizo, hili ni moja wapo."

Colin alinyanyuka kama mbogo na kumsukuma Mage aliyeanguka chini huku akibwata.

"Muongo mkubwa, mnafiki unanipaka mafuta kwa mgongo wa chupa, eti sweet."

"Huwezi amini Colin nakupenda sana japo Hans nampenda zaidi, nipo tayari kulipa gharama zote za maandalizi ya harusi yetu pia hata kulipa gharama zozote ili kuhakikisha nawe unakuwa na mke atakayeziba pengo langu."

Mage pamoja na kusukumwa, hakukasirika akaamka pale chini, Colin hakumjibu neno lolote zaidi ya kuinama huku akilia.

Mage alimshika mkono na kumnyanyua, alimtazama kwa macho yaliyojaa machozi na kusema kwa sauti ya chini.

"Colin nisamehe sana siwezi kuwa mnafiki mapenzi nayajua, nipe ruksa mpenzi wangu. Nilikuja huku ili tupate muda wa kulizumgumza hili, sikutaka tulizungumze juujuu. Nakupenda lakini sitaki nikutese kwa kukunyanyasa kimapenzi kwa vile mapenzi nayajua yanavyoumiza."

Colin alitulia huku akimtazama Mage aliyekuwa akitia huruma, alijiona mjinga kulazimisha mapenzi. Alikohoa kidogo na kusema:

"Sawa nimekuelewa."

"Nashukuru."

"Kuna la zaidi?" Colin alimuuliza Mage.

"Hakuna."

"Tunaweza kuondoka."

Walichukua vitu vyao na kuelekea nje kwenye gari ili warudi mjini.
***
Cecy baada ya kutoka twisheni, alisimama chini ya mti kuagana na shoga yake huku wakijikumbusha baadhi ya mada walizopewa wakasome nyumbani. Alikuwa amepiga hatua kubwa katika kusoma na kuandika hata kuzungumza lugha ya Kingereza baada ya kusoma kwa uchungu mkubwa.

Siku zote aliamini kumkosa Colin kulitokana na kukosa elimu, kwake umaskini hakuuona sababu kama angekuwa na elimu yake ambayo hata mama Colin angeiheshimu.

Toka aanze kusoma alionekana ndiye mwanafunzi aliyetaka kujua lugha, kuisoma, kuiandika na kuizungumza.

Japokuwa hakukijua sana Kiingereza lakini aliweza kumsikia mtu na kumuelewa hata kumjibu mawili matatu, ile ilimpa kiburi cha kuzungumza muda wote hata alipokosea hakujisikia vibaya kwa vile alielekezwa. Baada ya kujadiliana na shoga yake, alisogea mbele kuelekea njia ya kwao japo palikuwa mbali kidogo lakini hakujali umbali ule kutembea kwa miguu kwa vile alikuwa akitafuta kitu.

Siku zote aliingia darasa la mchana kwa vile asubuhi alikuwa akienda kwenye biashara zake.

Ada ya mwanzo alitumia fedha aliyoachiwa na Colin siku aliyompeleka kwao na kuwaacha kwenye mataa kwa ahadi tamu ya kuyabadili maisha yao. Alikumbatia daftari lake na kutembea taratibu kukifuata kichochoro cha kuingilia njia ya mkato. Aliangalia saa yake, ilimuonesha ni saa kumi na moja na nusu jioni.

Alishtushwa na sauti ya gari aina ya Nisan Patrol New Model jeupe lililosimama nyuma yake, alipogeuka aliona msichana akiteremka kwenye gari huku akibwata kwa sauti kuonesha anazozana na mtu ndani aliye ndani ya gari.

Alipomuangalia aligundua ni Mage, mwanamke aliyezima ndoto zake za kuwa mke wa Colin. Alisimama nyuma ya mti kumuangalia, alimsikia akisema kwa sauti:

"Wewe mtu gani unayelazimisha mapenzi, nimekueleza ninaye ninayempenda hutaki kunielewa. Naomba uteremke kwenye gari langu, siwezi kutembea na mtu asiyeelewa. Sasa hiyo elimu uliyosoma inakusaidia nini ikiwa hutambui nini maana ya upendo?

"Nasema teremka la sivyo nitakuachia gari niondoke zangu."

Baada ya muda, Cecy alishtuka kumuona mwanaume aliyekuwa akiambiwa vile ni Colin, baada ya kuteremka kwenye gari kinyonge, alisogea pembeni na kusimama bila kujua nyuma yake yupo Cecy.

Cecy roho ilimuuma kuona mtu ampendaye anadhalilishwa vile. Colin alitokwa na machozi kitu kilichozidi kumuumiza moyo Cecy na kushangaa watu ambao muda si mrefu walitegemea kufunga ndoa lakini ajabu mwanamke anatoa maneno makali kama yale ya kumdhalilisha mumewe mtarajiwa.

Alitulia aione sinema ile inaishaje kwa kujificha nyuma ya mti ili wasimjue, baada ya muda alisikia sauti ya Colin.

"Mage pamoja na hayo lakini kumbuka ...



Itaendelea............
 
mizambwa dah haya mkuu asante sana ila unatutesa aise inakuwa fupi mno bana
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom