Hadithi: Wakili wa moyo

Hadithi: Wakili wa moyo

Wakili wa Moyo-24

ILIPOISHIA:
“Hapo ndipo ninapochanganyikiwa, mama kitendo walichonifanyia familia ya kina Hans, sitawasahau.”
“Umeona eeh, nilikueleza toka zamani familia ile ilikuwa haikupendi kama ungeolewa na Hans ndoa yako isingedumu. Mungu amekuletea mwanaume wa maisha yako unamchanganya.”
“Mama nimesha fanya kosa, naomba msaada wako, nitamweleza nini Colin anielewe.”
“Wala usiwe na wasi kamwambie kuwa ulimtuma Brenda cheni ambayo ulipanga kumpatia kama ‘surprise’ umekuta hajaitengeneza na kujikuta umekasirika na kuanza kulia.”
“Mmh! Atanieleza? Naona kama utetezi mwepesi.”
“Walaa, ye anajua ulikuwa kwa Brenda, nilimwambia kuna kitu mmeshindwa kuelewana ndiyo maana ulirudi katika hali ile.”
“Mmh! Basi ngoja nidanganye hivyo.”
Wakiwa katikati ya mazungumzo simu yake iliita, ilikuwa ikitoka kwa mama Colin.

SASA ENDELEA...

“Mkweo,” mama Mage alisema.

“Mmh! Lazima ataulizia kilichotokea.”

“Ngoja nimsikilize,” alisema huku akibofya cha kupolelea na kuweka simu sauti ya nje.

“Haloo mama Colin.”

“Eeh! Dada kuna nini huko?”

“Kwani vipi?”

“Naona Colin ananichanyanyia maneno wala simuelewi.”

“Wala hakuna kitu cha kutisha bali mkweo aliudhiwa na shoga yake, lakini kwa sasa yupo sawa na wakati wowote atakuja huko.”

“Mmh! Afadhali maana nilikuwa na wasiwasi.”

“Wa nini?”

“Nilijua Colin kisha mtibua mkwe wangu.”

“Walaa, sema mkweo ana hasira za kitoto kitu kidogo analia kama kafiwa.”

“Basi nikuacheni muendelee na mambo mengine.”

Baada ya simu kukatwa mama Mage alimgeukia mwanaye na kumwambia.
“Unaona ulivyotaka kumsababishia matatizo mwenzako?”

“Mama lazima niende sasa hivi najua mpenzi wangu hayupo kwenye hali nzuri.”

“Fanya hivyo na...” mama Mage alinyamaza baada ya mlango kugongwa.

“Unasemaje?” aliuliza kwa sauti.

“Kuna wageni.”

“Nakuja,” mama Mage alitoka nje kwenda kumsikiliza mgeni.

Alitoka hadi getini na kukutana wa wanaume wawili na mwanamke mmoja, aliwatazama walikuwa wageni kwake.

“Karibuni.”

“Asante.”

Aliwakaribisha hadi sebuleni, baada ya kuketi mama Mage alitaka kujua wana sida gani.
“Ndiyo jamani mna shida gani?”

“Sisi ni maafisa wa polisi,” walitoa vitambulisho vyao.

“Ndiyo, mna shida gani?”

“Tuna imani hapa ndipo anaishi Magreth Chogo.”

“Ndiyo.”

“Yupo?”

“Mna shida gani?”

Kabla hajajibu Mage alitoka chumbani ili awaone wageni ni kina nani, askari mmoja baada ya kumuona alijua ni Mage alibahatisha kwa kumwita jina.

“Mage.”

“Abee.”

“Upo chini ya ulinzi,” alisema askari wa kike.

“He! Kwa kosa gani?” Mage alishtuka.

“Kutokana na tukio lililomtokea mpenzi wako wa zamani.”

“Sasa mimi nahusika kivipi?”

“Utajua yote kituoni.”

“Mi siendi,” Mage alitaka kugoma kwenda.

“We nenda wala usihofu, ila jamani chondechonde mwanangu asiguswe wala kulazimisha kusema uongo tutaelewana vibaya.”

“Hakuna tatizo, atakuwa salama baada ya mahojiano atarudi.”

Itaendelea...................
 
Mkuu kwema? ??? Unatupia kidogo dogo sana. Tuendelee banaa na huu utamu

Wakili wa Moyo-25

UKUOISHIA:
"We nenda wala usihofu, ila jamani chondechonde mwanangu asiguswe wala kulazimisha kusema uongo tutaelewana vibaya."
"Hakuna tatizo, atakuwa salama baada ya mahojiano atarudi."
SASA ENDELEA...

Ilibidi Mage achukuliwe kupelekwa kituo cha kati cha polisi, mama yake alichukua simu na kumpigia mkuu wa polisi ambaye alikuwa rafiki mkubwa wa mzee Chogo baba yake Mage.

"Vipi shemeji?" ulipokewa upande wa pili.

"Mwanao Mage amekamatwa na vijana wako sasa hivi."

"Kwa kosa gani?"

Alimuelezea kila kitu, baada ya kumsikiliza alimjibu.

"Basi hakuna tatizo shemeji nitalishughulikia mwenyewe, yupo kituo gani?"

"Cha kati."

"Usiwe na wasi waache wamuhoji watamwachia tu."

"Sawa shemeji kwa hiyo niende."

"Hapana nitamfuta mwenyewe."

"Asante shemeji."

Mama Mage baada ya kukata simu alijikuta njia panda, alijifikiria kumpigia simu Colin lakini alijiuliza akimpigia atamwambia nini. Aliamua kukaa kimya ili kusubiri hatima yake ndipo ajue afanye nini.

***

Mage alipelekwa hadi kituoni na kuingizwa chumba cha mahojiano, Inspekta Koleta alikaa mbele ya meza aliyokuwa amekaa Mage na karatasi ili kuandika mahojiano yale.

"Unaitwa nani?"

"Mage."

"Nataka jina kamili."

"Magreth Chogo," Mage alijibu kwa sauti ya chini kidogo.

"Una umri gani?"

"Miaka 24."

"Unamfahamu vipi Hans?"

"Namfahamu kama mpenzi wangu wa zamani."

"Ulijuaje amepata matatizo?"

Mage alielezea jinsi alivyopigiwa simu na shoga yake Brenda ambaye alipigiwa simu rafiki yake Hans, Ndubukile.

"Wewe ulikuwa wapi?"

"Kwa mchumba wangu."

"Anaitwa nani?"

"Colin."

"Inasemekana mlikuwa ikipendana sana na Hans kwa nini hakukuoa akamuoa msichana mwingine?"

"Alichaguliwa na wazazi wake."

"Unafikiri kwa sababu gani alichaguliwa msichana mwingine wakati wewe ndiye uliyekuwa mpenzi wake kila mtu alijua."

"Kwa kweli kwa hiyo siwezi kujua."

"Hans alipoona mwanamke mwingine wewe ulichukuliaje?"

"Sikuwa na jinsi ila roho iliniuma sana."

"Ulifikiria kufanya nini baada ya kuachwa na Hans?"

"Nilipanga kutojishughulisha na mapenzi tena."

"Hukupanga kulipa kisasi?"

"Kisasi cha nini?"

"Kwa vile ndoto zako zilikuwa kuolewa na Hans."

"Ni kweli ndoto zangu zilikuwa kuolewa na Hans lakini sikuwa chaguo la wazazi wake."

"Unafikiria kwa nini unahusishwa na matukio ya mauaji na shambulizi la Hans?"

"Hata mimi nashangaa."

"Kuna ukweli gani umelipa kisasi cha kuachwa kuolewa?"

"Hakuna ukweli wowote kwa vile sasa hivi nami nipo katika maandalizi ya ndoa yangu, kwanza nifanye vile kwa ajili gani kwa vile Hans sijagombana naye ameoa tukiwa tunapendana. Pia sikuwa na kinyongo na familia yake."

"Unaweza kufikiria nani aliyefanya vile?"

"Mmh! Kwa kweli sijui kwa vile niliisha kata mawasiliano na Hans toka alipooa."

"Kuna taarifa mlikuwa na penzi la siri na Hans?"

"Si kweli, mara nyingi Hans alinitafuta kuniomba msamaha nilimkatalia kwa vile yeye ni mume wa mtu, sikutaka kuonekana naingilia ndoa yake hasa baada ya familia yake kutonihitaji."

Wakiwa katikati ya mazungumzo, mkuu wa polisi aliingilia Mr Clarence, Inspekta Koleta alinyanyuka na kupiga saluti. Mage alipomuona alifurahi kwani siku zote alikuwa mtu wa karibu katika familia yao.
"Shikamoo baba."

"Marahaba, kuna nini?"

"Mkuu kuna tukio la mauaji na mashambulizi ambayo inaonekana mshukiwa wa kwanza ni huyu binti," alijibu Inspekta Koleta.

"Hebu nipe hiyo kalatasi ya maelezo."

Mkuu wa Polisi Mr Clarence aliichukua na kuisoma kisha aliomba kuzungumza na Mage kidogo. Baada ya kupishwa alimuuliza maswali kuhusiana na tukio lile.

"Mage."

"Abee baba."

"Naomba uniambie ukweli ili nikusaidie hata kama umehusika niambie ili nijue jinsi ya kukusaidia," Mr Clarence alimwambia kwa upole.

"Baba, haki ya Mungu sijui chochote zaidi ya kupigiwa simu asubuhi nikiwa kwa mkweo, kwa vile Hans ndiye aliyekuwa chaguo la moyo wangu pia sikukosana naye, bali penzi letu lilivunjwa kwa nguvu ya wazazi wake nilishtuka sana kupata habari ile. Huwezi kuamini taarifa ile ilisababisha nitoke hata bila kumuaga mkweo hivi ndiyo nilikuwa najiandaa kwenda kuzungumza na mkweo japo sikutaka ajue nimekuja kumuona mpenzi wangu wa zamani."

"Una muda gani hujaonana na Hans?"

"Mmh! Sasa ni mwaka na nusu."

"Kwa nini?"

"Baba, yeye kaoa na mimi Mungu kanipa wangu kuna umuhimu gani kuendeleza ukaribu?"

"Nimekuelewa, sasa nitawaambia utoke kazi yote niachie mimi."

"Asante baba."

Mkuu wa polisi alimwita Inspekta Koleta na kumueleza amwachie Mage na kumueleza waendelee na upelelezi kwa vile Mage hahusiki na matukio yake. Walikubaliana na Mage aliruhusiwa kutoka. Mkuu wa Polisi Mr Clarence alimchukua Mage na kumrudisha nyumbani.
Mama yake alifurahi kumuona mwanaye na Mr Mulisa.

"Asante shemeji."

"Kawaida, nina imani Hans akipata nafuu kila kitu kitakuwa wazi."

Itaendelea...........
 
Unatukata handas bhana

Sent from my iPhone using JamiiForums mobile app
 
Fanya fanya basi Mizambwa unajua hadithi zako zina nipunguzia stress
 
Fanya fanya basi Mizambwa unajua hadithi zako zina nipunguzia stress

Hii hadithi mbona imefika mbali sana, inatoka kila jumamosi gazeti la risasi, tembelea global publishers
 
Back
Top Bottom