Hadithi: Wakili wa moyo

Hadithi: Wakili wa moyo

Nahisi huyo bint Cecy atagongwa na gari then jamaa amkimbize hospt afu huko atakuja kutana na Mage afu kitanuka...just prediction!
 
Wakili wa Moyo-22

ILIPOISHIA:
“Cecy leta ndizi mbili.”
Kwa vile taa ziliruhusu, aliliondoa gari na kwenda kulipaki kituo cha mafuta cha Magomeni, alilizima na kutoka nje. Kwa vile Cecy alikuwa amevuka barabara kwenda kuuza ndizi maeneo ya hospitali, alimtuma kijana mmoja aliyekuwa akiuza miwa.
“Samahani mkubwa, naomba kamwambie yule msichana alete ndizi kumi.”
Yule kijana alimfuata Cecy aliyekuwa ametua beseni lake chini akiuza ndizi, alipofika alimwambia.
“Dada peleka ndizi kumi kwenye lile gari.”
“Kumi hazitafika zitabaki sita.”
“Mpelekee zote.”
SASA ENDELEA...

“Sawa, ngoja nichukue hela.”

Baada ya kuuza alibeba beseni lake na kuvuka barabara mpaka kwenye gari, kioo cha gari kilikuwa kimepandishwa kidogo hivyo hakumuona aliyekuwa kwenye gari. Aligonga kioo kidogo ili auze ndizi.

“Kaka.”

Colin aliteremsha kioo na kufanya Cecy amuone vizuri kitu kilichomfanya ashtuke.
“Ha! Colin?” mshtuko alioupata ulifanya adondoshe beseni la ndizi.

Hakuliokota, alibaki amesimama mpaka Colin alipoteremka kwenye gari na kuokota ndizi zote kisha alimshika mkono Cecy.

“Cecy.”

“Abee,” Cecy aliitikia huku machozi yakimtoka na mwili kumtetemeka.

“Unalia nini mchumba?”

“Colin mimi si mchumba wako, mchumba wako Mage,” Cecy alijibu kwa ukali kidogo.

“Kwa nini unasema hivyo?”

“Mama yako alichonifanya kwa ajili yako, Colin lini nilikutamkia nakupenda?”
“Hujawahi hata siku moja.”

“Kwa nini mama yako amefunga safari ya kuja kunitukana kuwa naingilia ndoa yako na kutudhalilisha kwa ajili ya umaskini wetu. Colin maskini hapendi?”

“Anapenda.”

“Ni kweli Colin nakupenda zaidi ya kukupenda, nailaumu nafsi yangu kuchelewa kukueleza ukweli kuwa nakupenda. Najua haikuwa bahati yangu, unayetaka kumuoa ndiye chaguo la moyo wako. Kipi kilichomtuma mama yako kuja kunitukana na kutudhalilisha bahati yake sikumkuta najua ningemfanya nini!” Cecy alisema kwa sauti ya hasira.

“Lini?”

Cecy alimtajia siku na kukumbuka siku ambayo Colin alikumbuka ndiyo siku aliyokamata picha kumbe alikwenda kumtukana Cecy bila kutaka kuujua ukweli.

“Cecy samahani sana, pia pole kwa kushindwa kuujua upendo wako.”

Alimueleza ukweli juu ya uchumba wake na Mage alivyotengenezwa na mama yake.

“Kwa hiyo Mage si chaguo lako ni la mama yako?”

“Hapana, mwanzo lilikuwa chaguo la mama baada ya kumuona nilikubaliana naye na ndiyo tulipanga kuoana.”

“Kwa hiyo siku ile uliniita kuja kunidhalilisha na kuumiza moyo wangu?”

“Hapana nilikualika kama wageni wengine, pia nina mpango mkubwa sana kwako ambao utakusaidia kimaisha.”

“Colin mpango ambao naukubali kwako labda niwe mkeo lakini zaidi ya hapo usijisumbue,” Cecy alisema kwa sauti ya kike kwa kujiamini.

Colin alijitahidi kumuelewesha sababu ya picha zake na kipi alichokipanga juu yake.
“Hivi leo hii nifanye kazi kwenye kampuni yetu mama yako atakubali anajua sisi ni wapenzi, kuna kazi hapo?”

“Kwanza hebu nieleze sababu ya wewe kuwa kwenye hali hii?” Colin alimuuliza huku akiangalia mavazi na hali aliyokuwa nayo Cecy.

“Sina thamani, haya ndiyo maisha niliyoyachagua ili mama yako akiniona asiwe na wasiwasi na ndoa yako.”

“Cecy nitakutafuta tuzungumze akili yako ikitulia.”

“Usijisumbue.”

“Lazima nijisumbue kwako kwa vile kuna kitu ndani yako nilichokiona.”

“Colin niache nirudi nyumbani.”

“Unakaa wapi nikupeleke.”

“Colin unataka mama yako aje kuchoma pagala letu, aliona picha ikawa vile vipi anione kwenye gari lako?”

“Hawezi na ungeniambia alichokifanya ningempa ukweli, tabu ya kina mama wa kiswahili, wazungu hawajali vitu vya kijingakijinga.”

“We nenda tu.”

Colin alimbembeleza sana Cecy, kwa vile naye alikuwa akimpenda, akaingia kwenye gari na kurudishwa nyumbani kwao. Alipomfikisha Colin, naye aliteremka na kuongozana hadi kwa kina Cecy ambako kulikuwa na nyumba ya vyumba viwili na sebule. Lakini nyumba ilikuwa ya hali ya chini, bati zake zilikuwa na kutu na juu waliweka mawe ili kuzuia bati lisiezuliwe na upepo.

Cecy baada ya kufika eneo la kwao, alishukuru na kuanza kuelekea nyumbani, lakini Colin alimsemesha.

“Cecy mbona unaniacha mgeni?”

“Colin nashukuru umenileta, lakini naomba usifike nyumbani.”

“Kwa nini unasema hivyo?”

“Nimekueleza mara ngapi kuhusu mama yangu, unataka mama yako aje akitie moto kibanda chetu.”

“Cecy suala la kuhusu mama yangu niachie mimi, naomba nimsalimie mama mara moja.”

“Mmh! Sawa.”

Waliongozana Cecy na Colin hadi nyumbani kwao ambako alitambulishwa kwa mama yake na kumfanya mama Cecy ashtuke.

“Ha! Wewe ndiye unayemnyanyasa mwanangu?”

“Kumnyanyasa kivipi mama?”

Mama Cecy alimueleza mateso yote ya mwanaye juu yake na jinsi mama yake alivyokwenda kuwatukana huku akitishia maisha ya Cecy kama ataharibu ndoa yake na Mage. Colin baada ya kusikia maneno yale, aliyarudia maneno ya Cecy juu ya mapenzi yake kwake.

Akashangaa kuona penzi la Cecy kwake lilikuwa wazi kwa mama yake lakini mhusika mkuu alikuwa hajui kitu zaidi ya kumuona Cecy kama msichana mzuri lakini hakuwa na uwezo wa kumtamkia chochote kutokana na mama yake kumtafutia mwanamke aoe, kwa upande wake aliungana na uchaguzi wa mama yake.

“Mzazi wangu, kwanza niwaombeni radhi kwa yote yaliyotokea kwa mama yangu kuja kuwatukana bila sababu. Naweza kusema labda makosa nimefanya mimi kwa kutomjulisha nini nilichotaka kukifanya na Cecy.

“Najua mama yangu alimpenda Cecy lakini si kuwa mke wa mwanaye bali msichana mzuri anayejiheshimu. Inawezekana kigezo cha elimu ndicho kilichomfanya mama yangu amtafute Mage, nina imani kama Cecy angekuwa na elimu kama ya Mage basi angekuwa chaguo la kwanza la mama.

Itaendelea..............
 
Wakili wa Moyo-22

ILIPOISHIA:
“Cecy leta ndizi mbili.”
Kwa vile taa ziliruhusu, aliliondoa gari na kwenda kulipaki kituo cha mafuta cha Magomeni, alilizima na kutoka nje. Kwa vile Cecy alikuwa amevuka barabara kwenda kuuza ndizi maeneo ya hospitali, alimtuma kijana mmoja aliyekuwa akiuza miwa.
“Samahani mkubwa, naomba kamwambie yule msichana alete ndizi kumi.”
Yule kijana alimfuata Cecy aliyekuwa ametua beseni lake chini akiuza ndizi, alipofika alimwambia

This is very interesting story indeed!!!Nice Work.
 
Daaaahh!!!
 
mkuu mbona unauonjesha tu hafu kimya kirefu....?? weka mzigo hapo tububurudike, hakika story ni nzuri na tamu.., hongera mizambwa
 
Last edited by a moderator:
Wakili wa Moyo-23

ILIPOISHIA:
"Najua mama yangu alimpenda Cecy lakini si kuwa mke wa mwanaye bali msichana mzuri anayejiheshimu. Inawezekana kigezo cha elimu ndicho kilichomfanya mama yangu amtafute Mage, nina imani kama Cecy angekuwa na elimu kama ya Mage basi angekuwa chaguo la kwanza la mama.
SASA ENDELEA...

"Wasiwasi mkubwa wa mama ulianzia siku alipomuona Cecy kapendeza, naweza kusema aliwashinda wote waliokuwa kwenye sherehe yangu. Kilichomshtua zaidi ni baada ya kunikuta na picha ya Cecy aliyokuwa amependeza sana. Aliamini kabisa ni mpenzi wangu hivyo akaamua kujihami kabla mambo hayajaharibika kutokana na harusi yetu kuandaliwa kwa fedha nyingi.

"Lakini hakutakiwa kuchukua uamuzi aliochukua bila kuniuliza mimi japokuwa nilimweleza sababu ya kuwa na picha ile. Ila napenda kuwaeleza kitu kimoja kuwa, sitauacha upendo wa Cecy upite hivihivi, najitolea kumsomesha ili aongeze elimu na ujuzi.

Baada ya elimu hiyo, nitafanya naye kazi ndani na nje ya nchi ambayo naamini itamweka katika maisha mazuri na ramani ya dunia. Pia nitahakikisha naijenga nyumba yenu katika hadhi ya kisasa pia mama nitakufungulia mradi ili muendeshe maisha yenu," Colin alieleza nia yake nzuri kwa Cecy na mama yake.
"Asante baba.."

"Mama nani kamwambia sisi tuna shida ya vitu hivyo? Kama kilichonitesa nimekikosa, sihitaji kitu kingine toka kwako," Cecy alimkatisha mama yake na kumjia juu Colin kwa kauli yake.

"Cecy mimi na wewe nani mwenye kosa, ulilolisema leo ungelisema mapema tusingefika huku," Colin alijitetea.

"Muongo! Colin hata ningesema ingekuwa sawa na kazi bure kwa vile tayari mama yako aliishakuchagulia mwanamke," Cecy alisema kwa hisia kali.

"Kabla ya kutoa uamuzi ningechagua."

"Mimi na Mage unampenda nani?"

"Nawapenda wote, ila kwa sasa Mage kwa vile ndiye tupo katika mipango ya ndoa."

"Kwa kauli hiyo naomba tukomane, kila mtu ashike hamsini zake ukinikuta njiani nipite kama nguzo ya umeme," Cecy alisema kwa hasira.

"Cecy kuwa na adabu, heshimu anachokisema mwenzako...Baba kama una nia hiyo ifanye faida hataiona leo, lakini baadaye atakushukuru."

"Sawa mama nimekuelewa, Cecy punguza hasira nina nia nzuri na wewe, uzuri wako nitaulinda na baadaye utakuingizia fedha nyingi na kumsaidia mama. Utauza ndizi mpaka lini?"
Cecy hakujibu kitu aliinama chini, Colin alimsogelea na kumbembeleza kitu kilichomfanya Cecy aangue kilio na kusema:

"Colin nisamehe kwa yote, hujui kiasi gani penzi lako lilivyouathiri moyo wangu, najua nilikupenda bila kushauriana na moyo wangu. Mnaweza kuniona mdogo lakini nami nina hisia za mapenzi kama wengine," Cecy alisema huku akimtazama Colin kwa macho yaliyojaa machozi.

"Najua Cecy, isingekuwa mipango ya harusi ningeweza kufanya chochote ili ujue nauthamini upendo wako."

"Sawa Colin nimekuelewa."

Kwa vile muda ulikuwa umekwenda, Colin aliaga kuwahi nyumbani. Alikwenda kwenye gari na kuwaletea laki moja, walimshukuru naye aliondoka kuelekea nyumbani. Njiani alijikuta akimuwaza Cecy msichana mdogo lakini alikuwa jasiri kuzielezea hisia zake japo aliamini mama yake asingemkubali kutokana na uduni wa maisha na kukosa elimu.

Kwa upande mwingine aliamini kabisa kutokana na kasi ya mabadiliko duniani, Mage ndiye mwanamke sahihi kwake. Kwani aliamini maisha ni zaidi ya mapenzi kwa vile maisha yakiwa vizuri kila kitu kinakwenda. Aliamini kwa umbile adimu la Cecy angeweza kuifanya kazi yake vizuri ya maonesho ya mavazi.

Kitu kikubwa aliamini Cecy kama atapata twisheni ya kingereza, ataweza kuongeza uwezo wake hata kusafiri nchi za nje kufanya kazi ya maonesho ya mavazi pia kupata tenda ya kupamba majarida. Aliamini akimtumia vizuri Cecy, kampuni yake itafika mbali na yeye kujitengezea kipato kikubwa.

Alipanga kuwekeza fedha nyingi kwa Cecy baadaye angevuna fedha nyingi kwa kuamini alikuwa na kitu cha ziada ambacho wasichana wengi hawakuwa nacho. Japokuwa alikuwa na wasiwasi na kikwazo cha mama yake, lakini kwa vile yupo kikazi alijua mama yake angemuelewa tu.
Alipanga ndani ya wiki mbili nyumba ya kisasa ya kina Cecy iwe imesimama huku akimtafutia twisheni nzuri ili kuijua lugha haraka.

Alipanga kufungua duka mbele ya nyumba yao ambalo litawafanya waingize kipato kila siku. Kutokana na kuzama kwenye mawazo ya kumuwaza Cecy, alijikuta akimsahau Mage mpaka alipofika kwao.

***

Alipoingia ndani alikutana na mama yake ambaye alishangaa kumuona mwanaye akiteremka kwenye gari.

"Colin unatoka?
"
Colin ilibidi amweleze mama yake kilichotokea, baada ya kumsikiliza alimuuliza:

"Colin mwanangu umemfanya nini mtoto wa watu?"

"Mama sijamfanya kitu chochote kama nilivyokueleza."

"Mage si mjinga kulia tu na kukataa kuzungumza na wewe wakati mlikuwa pamoja?"

"Yaani sijui kitu labda uulize wewe utapata jibu."

"Nitauliza, lakini Colin kuna kitu unanificha haiwezekani Mage aondoke bila kukuaga kisha akatae kuzungumza na wewe wakati usiku mmelala pamoja?"

"Mama piga simu uulize labda utagundua kitu."

"Mmh! Sasa nimepata jibu," mama Colin alisema huku akitikisa kichwa kama kakumbuka kitu.

"Jibu gani?"

"Maana lazima kuna kitu Mage amegundua kuhusu wewe na Cecy, nasema hivi ndoa ikivunjika Cecy atanitambua."

"Mama unamuonea bure mtoto wa watu, toka siku ile ya sherehe sijaonana na Cecy," Malki alidanganya.

"Muongo umemkataza asilete ndizi ili mkutane sehemu nyingine. Colin Mage akinieleza kuwa amegundua una uhusiano na msichana mwingine pagala lao nakwenda kulitia moto sasa hivi."

"Mama kwa nini unanihukumu kwa kosa nisilofanya, nimekueleza piga simu uulize unaanza kutengeneza mawazo yako. Cecy amekukosea nini mpaka kumchukuia hivyo, ni wewe ndiye uliyekuwa naye karibu?"
Mama Colin hakusema kitu, aliingia ndani kuchukua simu ili ampigie Mage kujua amepatwa na nini.

***

Baada ya Colin kuondoka, mama Mage alimfuata mwanaye chumbani aliyekuwa amezama kwenye dimbwi la mawazo juu ya hali ya Hans na familia yake ilipomtenga na kumuona kama kinyesi. Moyo ulimuuma na kujua hakukuwa na haja ya yeye kwenda hospitali pia kumuacha mchumba wake, mumewe mtarajiwa akiwa amelala na kuondoka bila kumuaga.

Alijilaumu kwa kitendo chake cha kumpita Colin bila kumsemesha, alijiuliza atamfikiriaje. Alijiuliza ndoa yake ikivunjia na ijulikane sababu ya Hans mwanaume asiye na mapenzi naye ataiweka wapi sura yake. Lakini alijiuliza angesimama na kuzungumza na Colin angemwambia anatoka wapi na kwa nini hakumuaga?

Akiwa katika mawazo hayo, mama yake aliingia na kumkuta amejilaza chali huku ameukumbatia mto wake na macho yake yalikuwa yakiangalia darini.

"Mage..Mage."

"A..a..bee."

"Mbona sikuelewi mwanangu?"

"Mama nahitaji msaada wako najua nimechanganya madawa."

"Nikusaidie nini?"

"Sijui Colin atanielewaje maana nilichomfanyia si kitu kizuri."

"Kwa kweli hatua tuliyofikia huku vikao vikienda vizuri halafu mwenzako abadili uamuzi sijui sura zetu tutaziweka wapi?"

"Hapo ndipo ninapochanganyikiwa, mama kitendo walichonifanyia familia ya kina Hans, sitakisahau."

"Umeona eeh, nilikueleza toka zamani familia ile ilikuwa haikupendi kama ungeolewa na Hans ndoa yako isingedumu. Mungu amekuletea mwanaume wa maisha yako unamchanganya."

"Mama nimeisha fanya kosa naomba msaada wako, nitamweleza nini Colin anielewe."

"Wala usiwe na wasiwasi, kamwambie kuwa ulimtuma Brenda cheni ambayo ulipanga kumpatia kama surprise umekuta hajaitengeneza na kujikuta umekasirika na kuanza kulia."

"Mmh! Atanielewa? Naona kama utetezi mwepesi."

"Walaa, ye anajua ulikuwa kwa Brenda, nilimwambia kuna kitu mmeshindwa kuelewana ndiyo maana ulirudi katika hali ile."

"Mmh! Basi ngoja nifanye hivyo."

Wakiwa katikati ya mazungumzo, simu iliita. Ilikuwa ikitoka kwa mama Colin.

ITAENDELEA....................
 
Mkubwa mambo vp? Naona tunasonga ila kwa spidi ndogo sana. Jamaa lazma aje amng'oe cecy.

Wakili wa Moyo-23

ILIPOISHIA:
“Najua mama yangu alimpenda Cecy lakini si kuwa mke wa mwanaye bali msichana mzuri anayejiheshimu. Inawezekana kigezo cha elimu ndicho kilichomfanya mama yangu amtafute Mage, nina imani kama Cecy angekuwa na elimu kama ya Mage basi angekuwa chaguo la kwanza la mama.
SASA ENDELEA...

“Wasiwasi mkubwa wa mama ulianzia siku alipomuona Cecy kapendeza, naweza kusema aliwashinda wote waliokuwa kwenye sherehe yangu. Kilichomshtua zaidi ni baada ya kunikuta na picha ya Cecy aliyokuwa amependeza sana. Aliamini kabisa ni mpenzi wangu hivyo akaamua kujihami kabla mambo hayajaharibika kutokana na harusi yetu kuandaliwa kwa fedha nyingi.

“Lakini hakutakiwa kuchukua uamuzi aliochukua bila kuniuliza mimi japokuwa nilimweleza sababu ya kuwa na picha ile. Ila napenda kuwaeleza kitu kimoja kuwa, sitauacha upendo wa Cecy upite hivihivi, najitolea kumsomesha ili aongeze elimu na ujuzi.

Baada ya elimu hiyo, nitafanya naye kazi ndani na nje ya nchi ambayo naamini itamweka katika maisha mazuri na ramani ya dunia. Pia nitahakikisha naijenga nyumba yenu katika hadhi ya kisasa pia mama nitakufungulia mradi ili muendeshe maisha yenu,” Colin alieleza nia yake nzuri kwa Cecy na mama yake.
“Asante baba..”

“Mama nani kamwambia sisi tuna shida ya vitu hivyo? Kama kilichonitesa nimekikosa, sihitaji kitu kingine toka kwako,” Cecy alimkatisha mama yake na kumjia juu Colin kwa kauli yake.

“Cecy mimi na wewe nani mwenye kosa, ulilolisema leo ungelisema mapema tusingefika huku,” Colin alijitetea.

“Muongo! Colin hata ningesema ingekuwa sawa na kazi bure kwa vile tayari mama yako aliishakuchagulia mwanamke,” Cecy alisema kwa hisia kali.

“Kabla ya kutoa uamuzi ningechagua.”

“Mimi na Mage unampenda nani?”

“Nawapenda wote, ila kwa sasa Mage kwa vile ndiye tupo katika mipango ya ndoa.”

“Kwa kauli hiyo naomba tukomane, kila mtu ashike hamsini zake ukinikuta njiani nipite kama nguzo ya umeme,” Cecy alisema kwa hasira.

“Cecy kuwa na adabu, heshimu anachokisema mwenzako...Baba kama una nia hiyo ifanye faida hataiona leo, lakini baadaye atakushukuru.”

“Sawa mama nimekuelewa, Cecy punguza hasira nina nia nzuri na wewe, uzuri wako nitaulinda na baadaye utakuingizia fedha nyingi na kumsaidia mama. Utauza ndizi mpaka lini?”
Cecy hakujibu kitu aliinama chini, Colin alimsogelea na kumbembeleza kitu kilichomfanya Cecy aangue kilio na kusema:

“Colin nisamehe kwa yote, hujui kiasi gani penzi lako lilivyouathiri moyo wangu, najua nilikupenda bila kushauriana na moyo wangu. Mnaweza kuniona mdogo lakini nami nina hisia za mapenzi kama wengine,” Cecy alisema huku akimtazama Colin kwa macho yaliyojaa machozi.

“Najua Cecy, isingekuwa mipango ya harusi ningeweza kufanya chochote ili ujue nauthamini upendo wako.”

“Sawa Colin nimekuelewa.”

Kwa vile muda ulikuwa umekwenda, Colin aliaga kuwahi nyumbani. Alikwenda kwenye gari na kuwaletea laki moja, walimshukuru naye aliondoka kuelekea nyumbani. Njiani alijikuta akimuwaza Cecy msichana mdogo lakini alikuwa jasiri kuzielezea hisia zake japo aliamini mama yake asingemkubali kutokana na uduni wa maisha na kukosa elimu.

Kwa upande mwingine aliamini kabisa kutokana na kasi ya mabadiliko duniani, Mage ndiye mwanamke sahihi kwake. Kwani aliamini maisha ni zaidi ya mapenzi kwa vile maisha yakiwa vizuri kila kitu kinakwenda. Aliamini kwa umbile adimu la Cecy angeweza kuifanya kazi yake vizuri ya maonesho ya mavazi.

Kitu kikubwa aliamini Cecy kama atapata twisheni ya kingereza, ataweza kuongeza uwezo wake hata kusafiri nchi za nje kufanya kazi ya maonesho ya mavazi pia kupata tenda ya kupamba majarida. Aliamini akimtumia vizuri Cecy, kampuni yake itafika mbali na yeye kujitengezea kipato kikubwa.

Alipanga kuwekeza fedha nyingi kwa Cecy baadaye angevuna fedha nyingi kwa kuamini alikuwa na kitu cha ziada ambacho wasichana wengi hawakuwa nacho. Japokuwa alikuwa na wasiwasi na kikwazo cha mama yake, lakini kwa vile yupo kikazi alijua mama yake angemuelewa tu.
Alipanga ndani ya wiki mbili nyumba ya kisasa ya kina Cecy iwe imesimama huku akimtafutia twisheni nzuri ili kuijua lugha haraka.

Alipanga kufungua duka mbele ya nyumba yao ambalo litawafanya waingize kipato kila siku. Kutokana na kuzama kwenye mawazo ya kumuwaza Cecy, alijikuta akimsahau Mage mpaka alipofika kwao.

***

Alipoingia ndani alikutana na mama yake ambaye alishangaa kumuona mwanaye akiteremka kwenye gari.

“Colin unatoka?
”
Colin ilibidi amweleze mama yake kilichotokea, baada ya kumsikiliza alimuuliza:

“Colin mwanangu umemfanya nini mtoto wa watu?”

“Mama sijamfanya kitu chochote kama nilivyokueleza.”

“Mage si mjinga kulia tu na kukataa kuzungumza na wewe wakati mlikuwa pamoja?”

“Yaani sijui kitu labda uulize wewe utapata jibu.”

“Nitauliza, lakini Colin kuna kitu unanificha haiwezekani Mage aondoke bila kukuaga kisha akatae kuzungumza na wewe wakati usiku mmelala pamoja?”

“Mama piga simu uulize labda utagundua kitu.”

“Mmh! Sasa nimepata jibu,” mama Colin alisema huku akitikisa kichwa kama kakumbuka kitu.

“Jibu gani?”

“Maana lazima kuna kitu Mage amegundua kuhusu wewe na Cecy, nasema hivi ndoa ikivunjika Cecy atanitambua.”

“Mama unamuonea bure mtoto wa watu, toka siku ile ya sherehe sijaonana na Cecy,” Malki alidanganya.

“Muongo umemkataza asilete ndizi ili mkutane sehemu nyingine. Colin Mage akinieleza kuwa amegundua una uhusiano na msichana mwingine pagala lao nakwenda kulitia moto sasa hivi.”

“Mama kwa nini unanihukumu kwa kosa nisilofanya, nimekueleza piga simu uulize unaanza kutengeneza mawazo yako. Cecy amekukosea nini mpaka kumchukuia hivyo, ni wewe ndiye uliyekuwa naye karibu?”
Mama Colin hakusema kitu, aliingia ndani kuchukua simu ili ampigie Mage kujua amepatwa na nini.

***

Baada ya Colin kuondoka, mama Mage alimfuata mwanaye chumbani aliyekuwa amezama kwenye dimbwi la mawazo juu ya hali ya Hans na familia yake ilipomtenga na kumuona kama kinyesi. Moyo ulimuuma na kujua hakukuwa na haja ya yeye kwenda hospitali pia kumuacha mchumba wake, mumewe mtarajiwa akiwa amelala na kuondoka bila kumuaga.

Alijilaumu kwa kitendo chake cha kumpita Colin bila kumsemesha, alijiuliza atamfikiriaje. Alijiuliza ndoa yake ikivunjia na ijulikane sababu ya Hans mwanaume asiye na mapenzi naye ataiweka wapi sura yake. Lakini alijiuliza angesimama na kuzungumza na Colin angemwambia anatoka wapi na kwa nini hakumuaga?

Akiwa katika mawazo hayo, mama yake aliingia na kumkuta amejilaza chali huku ameukumbatia mto wake na macho yake yalikuwa yakiangalia darini.

“Mage..Mage.”

“A..a..bee.”

“Mbona sikuelewi mwanangu?”

“Mama nahitaji msaada wako najua nimechanganya madawa.”

“Nikusaidie nini?”

“Sijui Colin atanielewaje maana nilichomfanyia si kitu kizuri.”

“Kwa kweli hatua tuliyofikia huku vikao vikienda vizuri halafu mwenzako abadili uamuzi sijui sura zetu tutaziweka wapi?”

“Hapo ndipo ninapochanganyikiwa, mama kitendo walichonifanyia familia ya kina Hans, sitakisahau.”

“Umeona eeh, nilikueleza toka zamani familia ile ilikuwa haikupendi kama ungeolewa na Hans ndoa yako isingedumu. Mungu amekuletea mwanaume wa maisha yako unamchanganya.”

“Mama nimeisha fanya kosa naomba msaada wako, nitamweleza nini Colin anielewe.”

“Wala usiwe na wasiwasi, kamwambie kuwa ulimtuma Brenda cheni ambayo ulipanga kumpatia kama surprise umekuta hajaitengeneza na kujikuta umekasirika na kuanza kulia.”

“Mmh! Atanielewa? Naona kama utetezi mwepesi.”

“Walaa, ye anajua ulikuwa kwa Brenda, nilimwambia kuna kitu mmeshindwa kuelewana ndiyo maana ulirudi katika hali ile.”

“Mmh! Basi ngoja nifanye hivyo.”

Wakiwa katikati ya mazungumzo, simu iliita. Ilikuwa ikitoka kwa mama Colin.

ITAENDELEA....................
 
Mkuu hivi hii hadithi unaweka kila baada ya siku ngapi?
 
Back
Top Bottom