Hadithi: Wakili wa moyo

Hadithi: Wakili wa moyo

Wakili wa Moyo-12



ILIPOISHIA:

Wakati Cecy anatoka alipishana getini na Mage aliyekuwa kwenye gari aina ya Toyota Land Cruiser V8. Colin aliyekuwa ghorofani alishtuka kuona gari la kifahari likiingia nyumbani kwao.

SASA ENDELEA...

Hakuteremka chini haraka, alisubiri kumuona nani anaingia. Baada ya gari kusimama kwenye maegesho alishtuka kumuona Mage akiteremka.

Alijikuta akimsahau Cecy ghafla kutokana na jinsi Mage alivyokuwa amependeza kwa vazi la gauni fupi la rangi nyeusi na weupe lililoishia chini kidogo ya makalio.

Alijikuta akijisemea mwenyewe moyoni.

“Mage ni msichana mrembo sana.”

Aliteremka chini kwenda kumpokea, Mage alipomuona alimkimbilia na kumrukia kwa furaha.

“Waaaooh! My husband to be.”

“Waaaooo my wife.”

Walishikana mikono na kuelekea ndani kila mmoja akiwa na furaha tele moyoni. Wakiwa wanaelekea ndani, Mage alimwambia Colin:

“Baby, naomba ujitayalishe tuna mtoko mdogo.”

“Wapi baby?”

“Surprise.”

“Mmh! Haya.”

Walikwenda wote chumbani kwa Colin, ili kuokoa muda aliingia bafuni kuoga ili watoke. Akiwa bafuni Mage alimfuata.

“Vipi Mage,” Colin alishtuka huku akigeuka nyuma.

“Nimekuja kukuosha mpenzi wangu, au kuna ubaya?”

Colin hakuwa na jinsi alikubali kuoga na Mage, baada ya kuoga waliondoka kuelekea mjini. Mage alimpeleka kwenye duka la nguo na kumtaka mpenzi wake achague nguo itakayompendeza kwenye sherehe yake ya kuzaliwa.

“Colin mpenzi nataka uchague suti nzuuuri, itakayokupendeza jioni ya leo. Nami unichagulie nguo nzuri ambayo tukisimama wakati wa kulishana keki kila mtu moyo umchome.”

“Suti nichagulie wewe, nguo yako nitakuchagulia mimi,” Colin alijibu huku akitabasamu na kufanya Mage auone vizuri uzuri wake.

“Sawa.”

Walikubaliana kila mmoja kumchagulia mpenzi wake nguo nzuri.

***

Cecy baada ya kutoka kwa kina Colin hakuwa na biashara yoyote, alirudi moja kwa moja nyumbani kwao akiwa na shauku ya kuiona zawadi aliyopewa.

Alijikuta akianza kuiamini ndoto yake kuwa Colin naye anampenda kama yeye bila kujali elimu yake ya kata.

Kutokana na kuchanganywa na zawadi, alipofika kwao alisahau kumsalimia hata mama yake aliingia moja kwa moja chumbani kwake na kutoa vilivyokuwemo kwenye mfuko na kuviweka kitandani.

Alikuta gauni zuri la rangi ya zambarau lenye mchanganyiko mweusi kwa mbali. Alishtuka kukuta nguo za ndani mbili moja nyekundu na nyingine nyeupe.

Viatu vilikuwa vya kisigino kirefu kidogo chenye mikanda. Alivaa na kuzunguka chumbani kama miss aliyekuwa akitafuta pointi. Aliufungua mkebe kidogo na kukuta mkufu mdogo na fedha.

Aliuvaa na kuchukua kioo na kujikuta akitabasamu huku akiwa na hamu ya kutoka nje ili walimwengu wamuone alivyopendeza.

“Kumbe na mimi mzuri namna hii, kwa nini Mungu umeninyima elimu?” Cecy alijikuta akianza kulia.

Mama yake alikuwa amesimama mlangoni baada ya kupitwa na mwanaye bila kumsemesha na kuacha kazi zake kumfuata ili kujua mwanaye amepatwa na kitu gani.

Alipofika alimuona akitoa vitu kwenye mfuko, alitulia mpaka aone mwisho wake. Alishtuka kumuona akitoa nguo za gharama na kuvaa. Alijiuliza amezitoa wapi, lakini hakutaka kumuuliza haraka, alisubiri aone mwisho wake.

Kauli ya mwanaye ya kujisifia ilimfanya atabasamu, lakini alipoanza kulia huku akimlaumu Mungu kukosa elimu alimshtua.

“Cecy.”

Cecy alishtuka na kugeuka bila kuitikia huku akifuta machozi, alipomuona mama yake aliitikia.

“Abee mama.”

“Unalia nini?”

“Roho inaniuma kukosa elimu pia nipo njia panda kwa Colin.”

“Kwanza nguo hizi umetoa wapi?” mama yake alikaza sauti.

“Kanipa Colin.”

“Ili?”

“Mama alisema atanipa zawadi, nilipofika kwao leo alinipa na ameniomba leo nihudhurie kwenye sherehe yake ya kuzaliwa.”

“Saa ngapi?”

“Saa moja usiku.”

“Utakwendaje usiku na utarudije?”

“Amenipa fedha ya kukodi gari.”

“Mmh! Haya, mwisho wako na Colin tutauona.”

“Mama unavyonifikiria sivyo,” Cecy alijitetea.

Mama yake aliachana na mwanaye na kurudi nje kuendelea na kazi zake na kumuacha Cecy akibadili nguo. Aliziweka vizuri nguo zake ambazo alitakiwa kuzivaa jioni ya siku ile.

***

Cecy alitumia zaidi ya nusu saa bafuni kuoga na saa nzima kujipamba kuhakikisha ile inakuwa kete ya kumfanya Colin aamini yeye ni msichana mrembo.

Kabla ya kutoka alimwita mama yake aongeze vikorombwezo vya kumremba.

“Mmh! Mwanangu inatosha.”

“Mamaa! Sitaki nionekane tofauti na nitakaowakuta si unajua lazima kutakuwa na wageni wengi.”

Mama yake alimtengeneza mwanaye kwa kumpaka vizuri poda lipstiki na wanja mwembamba na kumfanya Cecy kuwa kama malkia. Baada ya kujiamini amependeza alitembea taratibu kuelekea barabarani na kukodi gari kuelekea kwa kina Colin.

***

Sherehe ilifanyika kwenye ua wa jengo la nyumba ya kina Colin na kupambwa vizuri kuwafanya wageni wafurahie maandhari ile. Wageni walifika kwa wakati, kila mmoja alionekana ana maisha mazuri kutokana na magari ya kifahari kupaki kwenye maegesho.

Asilimia kubwa ya wageni walikuwa wamefika na kukaa kwenye nafasi zao huku wakiendelea kutumbuizwa na muziki laini. Kutokana na foleni, Cecy alikuwa wa mwisho kuingia, ilikuwa dakika chache kabla ya sherehe haijaanza.

Baada ya kuteremka kwenye teksi, alishika gauni lake kwa kulipandisha juu na kusogea mlangoni. Mlinzi alimfungulia bila kumfahamu kama ni Cecy muuza ndizi kwa jinsi alivyokuwa amependeza kupita kiasi.

Aliingia kwa mwendo wa taratibu kuelekea kwenye kiti kilichokuwa wazi. Kila mmoja aligeuka kumuangalia Cecy msichana maskini mwenye elimu duni lakini mwenye urembo wa asili.

Mama Colin aliyekuwa amekaa na mama Mage alishtuka kumuona msichana mrembo lakini mgeni machoni mwake. Alimsindikiza kwa macho mpaka alipokwenda kuketi.

Baada ya Mage kukaa na kupatiwa kinywaji, zilipita dakika tano sherehe ya kuzaliwa Colin ilianza kwa Colin kutokeza akiwa ameongozana na Mage. Moyo ulimshtuka Cecy lakini hakujua yule msichana aliyetoka naye ndani ni nani yake.

Lakini hakutaka kuumiza moyo wake kwa kuamini kabisa huenda yule ni mpambe aliyechaguliwa kwa ajili ya kumsindikiza.

Alijikuta akiingia wivu kwa kujiuliza kwa nini hakuchaguliwa yeye ndiye awe mpambe wake.

Lakini kwa upande mwingine aliamini huenda kutojua kiingereza kulichangia, kwa vile mambo mengine yanayohitaji kuzungumza kingereza yangemshinda.

Wazo lile aliliafiki na kujiona ana deni la kwenda twisheni kujifunza maneno mawili matatu ya kingereza ili aendane na Colin.

Kila alivyomuangalia Colin alivyokuwa amependeza katika vazi la suti, moyo wake ilizidi kuteketea na kutamani siku ile ndiyo ingekuwa siku ya kuvishwa pete ya uchumba na kila mtu kujua yeye ni mchumba wa Colin, angekuwa juu zaidi ya mawingu.

Wakati sherehe ikiendelea Colin alishtuka kutomuona Cecy kwenye sherehe ile. Pamoja hakuwa mpenzi wake lakini alitokea kupenda kumuona kutokana na jinsi alivyojiweka na kuwa tofauti na wasichana wengi wanaotoka familia duni.



JE NINI KITAFUATIA? TUKUTANE...............
 
Wakili wa Moyo 13



Wazo lile aliliafiki na kujiona ana deni la kwenda twisheni kujifunza maneno mawili matatu ya Kiingereza ili aendane na Colin.

Kila alivyomuangalia Colin alivyokuwa amependeza katika vazi la suti, moyo wake ulizidi kuteketea na kutamani siku ile ndiyo ingekuwa ya kuvishwa pete ya uchumba na kila mtu kujua yeye ni mchumba wa Colin, angekuwa juu zaidi ya mawingu.

Wakati sherehe ikiendelea, Colin alishtuka kutomuona Cecy. Pamoja hakuwa mpenzi wake lakini alitokea kumpenda kumuona kutokana na jinsi alivyojiweka na kuwa tofauti na wasichana wengi wanaotoka familia duni.

JIACHIE NAYO MWENYEWE...


lijikuta akiwa na wasiwasi wa kutomuona kwenye sherehe yake wakati alimualika. Aliondoka kwenye kiti chake na kumfuata mama yake kumuuliza kama amemuona Cecy.

"Vipi Colin?" mama yake aliinama kumsikiliza.

"Eti, hujamuona Cecy?"

"Cecy! Yupi?"

"Mkweo."

"Mmh! Sikumualika si unajua watu waliokuja hapa ni wenye hadhi zao, hivyo angekuwa tofauti na wengine."

"Mimi nilimualika."

"Sasa Colin... yule msichana atavaa nini ili alingane na hadhi ya sherehe hii. Inawezekana kabisa John kamzuia getini kutokana na hadhi ya sherehe yako."

"Kama atakuwa amefanya hivyo atakuwa hakutenda haki kwa vile mimi ndiye niliyemualika."

"Achana naye, si muhimu kama sherehe yako," mama Colin alijibu kwa mkato huku akichukua glasi ya kinywaji na kupeleka mdomoni.

"Hapana," Colin alisema huku akielekea getini.

Mama yake hakushughulika naye, alimuacha aende. Alipofika alimuuliza John kama amemuona Cecy.

"Sijamuona, sidhani kama anaweza kuja kwenye sherehe ya watu wazito kama hii. Kila mmoja kaja na gari la kifahari, msichana mmoja ndiyo kaja na gari la kukodi, muuza ndizi kama Cecy atakaa wapi?" John alisema kwa dharau.

"John au umemkatalia?" Colin alimuuliza huku akimkazia sauti na macho.

"Hapana bosi," John aliingiwa hofu.

"Sasa kesho aje aseme umemzuia jihesabu huna kazi."

"Sijamuona kwa kweli, kama akifika nitamruhusu aingie."

Wakati Colin akirudi ndani, Cecy alikuwa akitoka msalani na kukutana uso kwa uso. Kwa vile Colin alikuwa na hasira, alimuona msichana mrembo lakini akili yake haikumtambua.
Baada ya kusalimiana alimchangamkia kama wageni wengine na kutaka kuelekea ukumbini.

"Colin jamani ndiyo nini?" Cecy alimsemesha.

Sauti ya Cecy ilimshtua Colin na kugeuka na kujikuta akitazamana na msichana mrembo.

"Mungu wangu, nini wewe Cecy?" Colin alishtuka.

"Naam, ni mimi," Cecy alisema kwa sauti ya kike huku akishika mkono mmoja kiunoni na kunesa kwa madaha na macho kuyarembua.

"Yaani huwezi kuamini, natoka nje kukuuliza."

"John kasemaje?"

"Cecy ulivyopendeza umetuchanganya wengi, kuanzia mama mpaka John getini amekusahau. Anasema hajakuona."

"Jamani! Ndizi ni kazi lakini umbile kazi ya Muumba, ninyimwe kila kitu? Nimemkosea nini Mungu?" Cecy alisema kwa sauti ya kinanda na kumfanya Colin aamini kama si kutangaza uchumba basi yeye angekuwa chaguo lake.

"Basi nimefurahi kukuona pia hongera umependeza sana na karibu sana."

"Asante."

"Wacha niwahi sherehe inanisubiri mimi."

"Hakuna tatizo tupo pamoja."

"Usisahau kumsalimia mama ajue upo."

"Sawa."

Cecy baada ya kuagana na Colin alikwenda mpaka alipokuwa amekaa mama Colin na kumsemesha.

"Shikamoo ma' mkwe," alimsalimia huku akipiga magoti kwa heshima.

"Ha! Cecy mkwe wangu jamani, nisamehe sana nilikusahau nawe umependeza sana."

"Ni kawaida yangu."

"Karibu mkwe."

"Asante, nipo mbele."

"Hakuna tatizo."

Mama Colin alimsindikiza mpaka anakaa na kutikisa kichwa na kujisemea moyoni: Cecy msichana mzuri sana.
Sherehe iliendelea huku kila mmoja akiifurahia na MC akieleza kila hatua iliyokuwa ikiendelea.
Ilifika wakati wa kukata keti, kama kawaida Mage ndiye aliyekata keki na kumlisha Colin kisha Colin akamlisha Mage.
Keki ilikatwa vipande vipande kisha Colin alipita kila meza ya wageni na kumlisha mmoja mmoja huku akipiga naye picha.

Baada ya zoezi lile alimwambia mpigapicha ahakikishe anampiga Cecy picha zaidi ya ishirini za mikao tofauti na kumpelekea.
Mpiga picha alifanya kama alivyoelekezwa kwa kumfuata Cecy na kwenda naye kumpiga picha tofauti.
Baada ya zoezi la kulishana keki, Colin aliomba kipaza sauti na kuzungumza machache kuhusiana na sherehe yake kwa kuwashukuru wageni waalikwa.

"Kwanza nawashukuru wazazi wangu kwa kunizaa, mama yangu kwa kunilea na hata baba yangu ambaye ametangulia mbele za haki. Pia nawashukuru wageni waalikwa kwa kufika katika sherehe ya kuzaliwa kwangu.


Itaendelea kesho.....................
 
Aisee ukiwa unaiendeleza hii hadithi uwe unanitag ... sawa? ?? Lasivyo manundu yatakuhusu.


Ni mambo haya tena !!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!


cheka-img_3703.jpg

Itanibidi na mimi nianze mazoezi
 
Wakili wa Moyo- 14



Ilipoishia:
Baada ya zoezi la kulishana keki, Colin aliomba kipaza sauti na kuzungumza machache kuhusiana na sherehe yake kwa kuwashukuru wageni waalikwa.
"Kwanza nawashukuru wazazi wangu kwa kunizaa, mama yangu mzazi kwa kunilea na hata baba yangu ambaye ametangulia mbele za haki. Pia nawashukuru wageni waalikwa kwa kufika katika sherehe ya kuzaliwa kwangu.
JIACHIE NAYO...

"Leo ni siku muhimu na maalumu katika historia ya maisha yangu. Kitakachofuata ni hatua moja kuelekea katika maisha yangu ya kujitegemea. Wazazi wangu na wageni waalikwa, natumia siku ya kumtambulisha mchumba wangu kwa kumvisha pete."

Kauli ile ilisababisha moyo wa Cecy ulipuke paa! Ulimfanya mapigo ya moyo yaende kwa kasi.
Alijiuliza kauli ile anayoisikia ni ya kweli au anaota ndotoni.

Akili yake ilipata jibu la kupewa nguo nzuri na kualikwa kwenye sherehe ile. Aliiona ndoto yake ya mchana kuwa mke wa Colin ilikuwa ikitimia muda si mrefu.

Alitulia akijipa ujasiri ili kunyanyuka kwenda kuvishwa pete mbele ya umati ule akiitwa. Colin aliendelea kuzungumza huku akiingiza mkono mfukoni na kutoa mkebe wenye pete ya uchumba.

"Jamani naomba mpenzi wangu wa moyo ambaye anatarajiwa kuwa mama wa watoto wangu asogee mbele."

Kauli ilimfanya Cecy atake kunyanyuka akiamini kabisa yeye ndiye mchumba wa Colin. Kabla hajanyanyuka kwenda mbele alishangaa kumuona Mage msichana aliyetoka naye ndani akisogea mbele akiwa ameshika kifuani asiamini kilichosemwa.

Baada ya kufika hapo, MC alichukua kipaza sauti na kuongoza zoezi lile. Wakati huo Cecy alikuwa ameingiwa ganzi mwilini na kuona kama Colin kumuita kwenye sherehe ile ilikuwa amemtendea unyama.
Alijiuliza kitu gani alichomtendea Colin mpaka kumfanyia ukatili kama ule. Alijitahidi kuzuia hali ile kwa kushika mkono kifuani kuzuia mapigo yaliyokuwa yakienda kasi huku kijasho chembamba kikimtoka.
Wakati wa kuvishwa Mage pete, kilikuwa ni kipindi kigumu kwa Cecy. Ilikuwa sawa na kupasuliwa moyo wake kwa kisu butu bila ganzi.

Bila kujielewa presha ilimpanda, alishindwa kuizuia na kujikuta akianguka chini kama mzigo na kuwashtua waliokuwa wamekaa naye karibu.

Kitendo kile kilizua taharuki na kusababisha sherehe kusimama wakati huo zoezi la pete lilikuwa limeisha. Colin na mama yake walishtuka kusikia aliyeanguka ni Cecy.

Walikimbia eneo la tukio na kumkuta amezungukwa na watu.

"Vipi?" waliuliza kwa sauti ya mshtuko.

"Hata sijui, nilimuona akishika kifuani na kuhema kwa kasi kisha kufumba macho. Nilipotaka kumuuliza nilimsikia akisema Mungu wangu na kushangaa kumuona akianguka chini. Nilijitahidi kumuwahi, nilichelewa tayari alikuwa ameanguka chini," alisema dada mmoja aliyekuwa amekaa meza moja na Cecy.

"Labda ana kifafa?" mmoja alichangia.

"Hapana kile si kifafa, kwa jinsi nilivyomuona si kifafa," alijibu aliyekaa naye meza moja.

"Kifafa gani kisicho na povu," mwingine aliongezea.

"Jamani tumuwahishe hospitali," mama Colin alisema.

"Mama we' baki na wageni acha mimi nimpeleke," Colin alisema huku akipiga magoti na kushika kichwa cha Cecy aliyekuwa ametulia kama amelala.

"Hapana Colin wewe baki na wageni kumbuka sherehe ni ya kwako pia umemaliza kumvisha mchumba wako pete muda mfupi, hivyo unatakiwa kuwa naye karibu. Endeleeni na sherehe mimi ninatosha."
Colin alikubaliana na mama yake, yeye alibaki na kuendelea na sherehe na mama yake alimchukua Cecy na kumuwahisha hospitali.

***

Cecy baada ya kufikishwa hospitali, alichukuliwa vipimo na kuoneka hana tatizo kubwa ila presha ilikuwa juu. Lilifanyika zoezi kuishusha mara moja na kurudi katika hali ya kawaida.

"Nafikiri tatizo siyo kubwa sana, baada ya kumaliza dripu nitamruhusu," daktari alisema.

"Itachukua muda gani?"

"Si muda mrefu mtaondoka naye."

Mama Colin alitoka na kukaa kwenye makochi huku amekasirika na kulaumu kitendo cha mwanaye kumualika msichana yule ambaye hakuwa na hadhi ya sherehe ile na kufikia hatua ya kuharibu starehe yake kwa kuacha shughuli ya mwanaye kwa ajili ya msichana kapuku kama yule.

Alipanga kupiga marufuku ukaribu wa Cecy na Colin kwa vile aliuona unataka kwenda ndivyo sivyo. Yeye alitengeneza utani ambao ulimtia wasiwasi kwa mwanaye kuamini ni kweli.

Akiwa katikati ya mawazo, daktari alimshtua:

"Mama mgonjwa wako yupo tayari unaweza kumchukua."

Alinyanyuka na kwenda wadini alipomkuta Cecy amekaa kitandani.

"Vipi mkwe?"

"Nashukuru sijambo."

"Tatizo nini?"

"Hata najua! Nimejikuta nikiona kiza ghafla," Cecy alipindisha ukweli.

"Imeisha wahi kukutokea?"

"Hata siku moja, hata mimi najishangaa, ila samahani mkwe kwa kuharibu sherehe ya mwanao."

"Hujaharibu kitu, sherehe inaendelea kama kawaida."

"Naomba uniende nyumbani."

"Hapana nitakupeleka."

Alimchukua na kumuwahisha kwao ili yeye ageuke awahi sherehe. Alipomfikisha alimpa elfu hamsini kwa ajili ya kujiangalizia hali yake.

"Mkwe ugua pole."

"Asante ma' mkwe."

Cecy aliagana na mama Colin na kwenda kugonga mlango, mama yake aliyekuwa hana amani na moyo wake toka aondoke mwanaye kwenda kwenye sherehe za usiku.
Muda wote alikuwa macho, mwanaye alipogonga aliwahi kufungua.

"Umerudi mwanangu?"

"Ndi..ndi..ndiyo mama."

Kauli ya Cecy iliyochanganyikana na kigugumizi, kilio ilimshtua.

"Cecy nini mama?"

"Ningejua nisingeenda," alisema sauti ya kilio.

"Kwa nini?"

"Yaani wameniita kuniumiza! Nimewakosea nini?"

"Kukuumiza! Kivipi?"

"Mama yaani sijawahi kuumizwa moyo wangu kama leo.


Itaendelea baadaye..........

======================================================================================================
bucho
culbby
tonyy

Jamani Naogopa Manundu!!!!!!
 
Last edited by a moderator:
Wakili wa Moyo - 15



Kwa kitendo walichonifanyia siendi tena kwao kuuza ndizi."

Kauli ya Cecy iliyochanganyika na kigugumizi na kilio ilimshtua.
"Cecy nini mama?"
"Ningejua nisingeenda," alisema kwa sauti ya kilio.
"Kwa nini?"
"Yaani wameniita kuniumiza! Nimewakosea nini?"
"Kukuumiza! Kivipi?"
"Mama yaani sijawahi kuumizwa moyo wangu kama leo.

SASA ENDELEA...



"Najua unaniona mtoto mdogo lakini nina hisia kama mtu mwingine, mama inaumaa," Cecy alisema kwa uchungu huku akishika mkono kifuani.

"Kuna nini mbona huniweki wazi?" mama yake alishtuka.

"Mama, Colin wa kuniita kunionesha mchumba wake?"

"Kukuonyesha kivipi?"

Cecy alimweleza kila kitu kilivyokuwa katika sherehe, mama yake alishtuka na kusema:
"Mwanangu unataka kujiua bure, nilikueleza na mapema tajiri na sisi kina pangu pakavu wapi na wapi?"

"Kwa nini mama yake ananiita mkwe wakati mwanaye ana mwanamke mwingine?" Cecy aliuliza macho yakijaa machozi.

"Kuna siku alikutamkia suala la uhusiano kati yake na wewe?"

"Hapana."

"Sasa kuumia huko kumetoka wapi?"

"Mama! Nampenda sana Colin."

"Ulimwambia unampenda?"

"Nilikuwa naona aibu."

"Siku zote moyo ni mfungwa wa mapenzi hasa kumpenda asiyejua anapendwa mdomo wako ndiyo wakili wa kuutetea moyo wako. Bila hivyo upendo wako utateketea kama mwanga wa mshumaa mchana wa jua kali, hakuna atakayeuona mwanga wake."

"Mama, Colin alionesha ananipenda."

"Nilikueleza toka zamani ule ni utani tu wala hakuna ukweli wowote."

"Kwa kitendo walichonifanyia siendi tena kwao kuuza ndizi."

"Mwanangu nikueleze mara ngapi kila kitu kinatokana na baraka za Mungu. Muombe yeye ndiye atakayekuchagulia mwanaume wa maisha yako."

"Asante mama kwa kunitia moyo."

"Basi badili nguo kisha uoge ule ulale."

"Mama hata hamu ya kula ninayo, wacha tu nikalale."

Cecy aliingia chumbani kwake kulala na kumuacha mama yake akiwa amesimama akiyafikiria aliyoambiwa na mwanaye. Alimuonea huruma kwa kujiingiza kwenye mapenzi ya kumpenda mtu mwenye mpenzi mwingine anayempenda.

Kingine kibaya ilikuwa hali yao duni ambayo ilikuwa tofauti na matajiri na wasomi. Alijiuliza kwa hali iliyomtokea mwanaye iliyopelekea kupatwa na presha kupelekea kukimbizwa hospitali itachukua muda gani kumtoka.

Aliamini ingemtesa mwanaye kwa kipindi kirefu na kumfanya akose amani ya moyo wake. Lakini aliamini atampatia ushauri nasaha utakaomrudisha katika hali ya kawaida. Aliachana na mawazo yale na kwenda chumbani kwake kulala.

Siku ile ilikuwa mbaya kuliko zote maishani mwake, aliyakumbuka maneno ya mama yake kuhusu Colin kumtamkia mpenzi wake zaidi ya utani wa uchumba.

Kwa vile kichwa kilikuwa kikimuuma, alimeza dawa za usingizi na kupanda kitandani kuitafuta siku ya pili.


***

Wakati hayo yakiendelea, Colin na Mage walikuwa kwenye furaha ya ajabu. Mage hakuamini tukio lililotokea usiku ule la kuvalishwa pete ya uchumba mbele ya watu.

Kilikuwa kitu kikubwa sana katika maisha yake, pamoja na kupendana sana na Hans kwa muda mrefu lakini hakikufanyika kitu kama kile. Aliamini Hans alikuwa mwamaume aliyeletwa kwake na Mungu kwa kuonesha ana mapenzi ya dhati na yeye.

"Colin asante sana mpenzi wangu," Mage alisema huku akiitazama pete yake ya kito cha Tanzanite.

"Kawaida tu, nina vitu vingi vya kukufanyia mpenzi wangu," Colin alijibu huku akichezea vidole vya mikono ya Mage.

"Colin nakuahidi kuwa mke mwema."

"Nashukuru, nataka harusi yetu isichukue muda mrefu."

"Hujui tu, ukitaka sasa hivi nipo tayari hata unioe bure kwa vile upendo wa kweli ni ghali kuliko kuitafuta fedha. Nakuhitaji kuliko kitu chochote chini ya jua."

Mage alisema huku machozi yakimtoka akikumbuka alichofanyiwa na mpenzi wake Hans, mwanaume aliyeamini ndiye wake wa kufa na kuzikana.

Lakini kilichotokea kilikuwa kinyume na matarajio yake, kiliufanya moyo wake kuingia wasiwasi wa kumkosa hata yule.

"Mage usilie nataka ulie kwa furaha ukiwa nami si kwa huzuni," Colin alimwambia Mage huku akichezea vidole vyake na macho yake kutazama usoni kwake.

"Nina wasiwasi naweza kutendwa tena, Colin ukinitenda nitakufa mwenzio nakuona wewe ndiye uliyeshika uhai wangu," Mage alisema kwa sauti iliyohitaji huruma.

"Nakuhakikishia furaha yako itapitia mikononi mwangu."

"Kweli Colin?" Mage aliuliza huku ametoa macho.

"Amini nakupenda sana Mage, wewe ni ua la moyo wangu sitachoka kulitunza na kulimwagilizia ili liendelee kustawi na kuchanua."

"Asante Colin, nami nitahakikisha chaguo la mama yako hutajutia maishani mwako. Hazina yote ya mapenzi nahamishia kwako."

"Asante mpenzi wan gu nami nitakuwa benki yenye usalama kwa ulichokiweka kila sekunde kinaongezeka faida ya upendo."

"Nimefurahi kusikia hivyo, nina imani kovu la kutendwa litaondoka."

"Niamini nikisemacho, kwa vile nami nahitaji furaha yangu itoke kwako."

"Asante mume wangu mtarajiwa," Mage alisema huku akimkumbatia Colin kwa mahaba mazito.
Baada ya sherehe, Mage alikataa kuondoka na mama yake na kulazimisha kubaki na Colin.

"Mage mwanangu muda wa kuwa karibu na Colin bado."

"Hapana mama, alichokifanya leo ni zaidi ya ndoa. Naomba uniache nina mengi ya kuzungumza naye usiku wa leo."

"Mama Mage mwache mtoto abakie na mwenziye, bado wana mengi ya kuongea wakiwa karibu," mama Colin aliingilia kati na kufanya mama Mage kukubaliana na mzazi mwenzie kumuacha Mage alale na Colin siku ile.


ITAENDELEA.................
 
Mkuu shukrani saana kwa kunitag. Ubarikiwe ila ukisahau kunitag lazma nikutoe nunduz za kutosha



Wakili wa Moyo- 14



Ilipoishia:
Baada ya zoezi la kulishana keki, Colin aliomba kipaza sauti na kuzungumza machache kuhusiana na sherehe yake kwa kuwashukuru wageni waalikwa.
“Kwanza nawashukuru wazazi wangu kwa kunizaa, mama yangu mzazi kwa kunilea na hata baba yangu ambaye ametangulia mbele za haki. Pia nawashukuru wageni waalikwa kwa kufika katika sherehe ya kuzaliwa kwangu.
JIACHIE NAYO...

“Leo ni siku muhimu na maalumu katika historia ya maisha yangu. Kitakachofuata ni hatua moja kuelekea katika maisha yangu ya kujitegemea. Wazazi wangu na wageni waalikwa, natumia siku ya kumtambulisha mchumba wangu kwa kumvisha pete.”

Kauli ile ilisababisha moyo wa Cecy ulipuke paa! Ulimfanya mapigo ya moyo yaende kwa kasi.
Alijiuliza kauli ile anayoisikia ni ya kweli au anaota ndotoni.

Akili yake ilipata jibu la kupewa nguo nzuri na kualikwa kwenye sherehe ile. Aliiona ndoto yake ya mchana kuwa mke wa Colin ilikuwa ikitimia muda si mrefu.

Alitulia akijipa ujasiri ili kunyanyuka kwenda kuvishwa pete mbele ya umati ule akiitwa. Colin aliendelea kuzungumza huku akiingiza mkono mfukoni na kutoa mkebe wenye pete ya uchumba.

“Jamani naomba mpenzi wangu wa moyo ambaye anatarajiwa kuwa mama wa watoto wangu asogee mbele.”

Kauli ilimfanya Cecy atake kunyanyuka akiamini kabisa yeye ndiye mchumba wa Colin. Kabla hajanyanyuka kwenda mbele alishangaa kumuona Mage msichana aliyetoka naye ndani akisogea mbele akiwa ameshika kifuani asiamini kilichosemwa.

Baada ya kufika hapo, MC alichukua kipaza sauti na kuongoza zoezi lile. Wakati huo Cecy alikuwa ameingiwa ganzi mwilini na kuona kama Colin kumuita kwenye sherehe ile ilikuwa amemtendea unyama.
Alijiuliza kitu gani alichomtendea Colin mpaka kumfanyia ukatili kama ule. Alijitahidi kuzuia hali ile kwa kushika mkono kifuani kuzuia mapigo yaliyokuwa yakienda kasi huku kijasho chembamba kikimtoka.
Wakati wa kuvishwa Mage pete, kilikuwa ni kipindi kigumu kwa Cecy. Ilikuwa sawa na kupasuliwa moyo wake kwa kisu butu bila ganzi.

Bila kujielewa presha ilimpanda, alishindwa kuizuia na kujikuta akianguka chini kama mzigo na kuwashtua waliokuwa wamekaa naye karibu.

Kitendo kile kilizua taharuki na kusababisha sherehe kusimama wakati huo zoezi la pete lilikuwa limeisha. Colin na mama yake walishtuka kusikia aliyeanguka ni Cecy.

Walikimbia eneo la tukio na kumkuta amezungukwa na watu.

“Vipi?” waliuliza kwa sauti ya mshtuko.

“Hata sijui, nilimuona akishika kifuani na kuhema kwa kasi kisha kufumba macho. Nilipotaka kumuuliza nilimsikia akisema Mungu wangu na kushangaa kumuona akianguka chini. Nilijitahidi kumuwahi, nilichelewa tayari alikuwa ameanguka chini,” alisema dada mmoja aliyekuwa amekaa meza moja na Cecy.

“Labda ana kifafa?” mmoja alichangia.

“Hapana kile si kifafa, kwa jinsi nilivyomuona si kifafa,” alijibu aliyekaa naye meza moja.

“Kifafa gani kisicho na povu,” mwingine aliongezea.

“Jamani tumuwahishe hospitali,” mama Colin alisema.

“Mama we’ baki na wageni acha mimi nimpeleke,” Colin alisema huku akipiga magoti na kushika kichwa cha Cecy aliyekuwa ametulia kama amelala.

“Hapana Colin wewe baki na wageni kumbuka sherehe ni ya kwako pia umemaliza kumvisha mchumba wako pete muda mfupi, hivyo unatakiwa kuwa naye karibu. Endeleeni na sherehe mimi ninatosha.”
Colin alikubaliana na mama yake, yeye alibaki na kuendelea na sherehe na mama yake alimchukua Cecy na kumuwahisha hospitali.

***

Cecy baada ya kufikishwa hospitali, alichukuliwa vipimo na kuoneka hana tatizo kubwa ila presha ilikuwa juu. Lilifanyika zoezi kuishusha mara moja na kurudi katika hali ya kawaida.

“Nafikiri tatizo siyo kubwa sana, baada ya kumaliza dripu nitamruhusu,” daktari alisema.

“Itachukua muda gani?”

“Si muda mrefu mtaondoka naye.”

Mama Colin alitoka na kukaa kwenye makochi huku amekasirika na kulaumu kitendo cha mwanaye kumualika msichana yule ambaye hakuwa na hadhi ya sherehe ile na kufikia hatua ya kuharibu starehe yake kwa kuacha shughuli ya mwanaye kwa ajili ya msichana kapuku kama yule.

Alipanga kupiga marufuku ukaribu wa Cecy na Colin kwa vile aliuona unataka kwenda ndivyo sivyo. Yeye alitengeneza utani ambao ulimtia wasiwasi kwa mwanaye kuamini ni kweli.

Akiwa katikati ya mawazo, daktari alimshtua:

“Mama mgonjwa wako yupo tayari unaweza kumchukua.”

Alinyanyuka na kwenda wadini alipomkuta Cecy amekaa kitandani.

“Vipi mkwe?”

“Nashukuru sijambo.”

“Tatizo nini?”

“Hata najua! Nimejikuta nikiona kiza ghafla,” Cecy alipindisha ukweli.

“Imeisha wahi kukutokea?”

“Hata siku moja, hata mimi najishangaa, ila samahani mkwe kwa kuharibu sherehe ya mwanao.”

“Hujaharibu kitu, sherehe inaendelea kama kawaida.”

“Naomba uniende nyumbani.”

“Hapana nitakupeleka.”

Alimchukua na kumuwahisha kwao ili yeye ageuke awahi sherehe. Alipomfikisha alimpa elfu hamsini kwa ajili ya kujiangalizia hali yake.

“Mkwe ugua pole.”

“Asante ma’ mkwe.”

Cecy aliagana na mama Colin na kwenda kugonga mlango, mama yake aliyekuwa hana amani na moyo wake toka aondoke mwanaye kwenda kwenye sherehe za usiku.
Muda wote alikuwa macho, mwanaye alipogonga aliwahi kufungua.

“Umerudi mwanangu?”

“Ndi..ndi..ndiyo mama.”

Kauli ya Cecy iliyochanganyikana na kigugumizi, kilio ilimshtua.

“Cecy nini mama?”

“Ningejua nisingeenda,” alisema sauti ya kilio.

“Kwa nini?”

“Yaani wameniita kuniumiza! Nimewakosea nini?”

“Kukuumiza! Kivipi?”

“Mama yaani sijawahi kuumizwa moyo wangu kama leo.


Itaendelea baadaye..........

======================================================================================================
bucho
culbby
tonyy

Jamani Naogopa Manundu!!!!!!
 
Last edited by a moderator:
Wakili wa Moyo - 16



ILIPOISHIA:
"Asante Colin, nami nitahakikisha chaguo la mama yako hutajutia maishani mwako. Hazina yote ya mapenzi nahamishia kwako."
"Asante mpenzi wangu nami nitakuwa benki yenye usalama kwa ulichokiweka kila sekunde kinaongezeka faida ya upendo."
"Nimefurahi kusikia hivyo, nina imani kovu la kutendwa litaondoka."

"Niamini nikisemacho, kwa vile nami nahitaji furaha yangu itoke kwako."
"Asante mume wangu mtarajiwa," Mage alisema huku akimkumbatia Colin kwa mahaba mazito.
Baada ya sherehe, Mage alikataa kuondoka na mama yake na kulazimisha kubaki na Colin.
"Mage mwanangu muda wa kuwa karibu na Colin bado."

"Hapana mama, alichokifanya leo ni zaidi ya ndoa. Naomba uniache nina mengi ya kuzungumza naye usiku wa leo."
"Mama Mage mwache mtoto abakie na mwenziye, bado wana mengi ya kuongea wakiwa karibu," mama Colin aliingilia kati na kufanya mama Mage kukubaliana na mzazi mwenzie kumuacha Mage alale na Colin siku ile.


SASA ENDELEA...


Cecy alishindwa kutoka kwao kwa siku mbili, muda mwingi aliitumia kuwaza na kujiona ni kiumbe kwenye mkosi ambaye hakufaa kuishi katika dunia ile. Alijiona hana thamani yoyote kutokana na kukosa kila kitu ambacho mwanadamu alitakiwa kuwa nacho.

Maisha yao yalitawaliwa na umaskini wa kutupa, elimu nayo ilikuwa duni ya shule za kata, kwake alichoambulia ni kujua kusoma na kuhesabu zaidi ya hapo hakuna alichokijua.

Kingine kibaya ambacho ndicho kilichomuuliza sana kukosa haki ya kupenda kwa vile tu hana elimu pia anatoka katika familia duni.

Japokuwa hakuwa msomaji wa vitabu lakini alikuwa akipenda kusikiliza vipindi vya usiku hasa vinavyohusu mapenzi na uhusiano. Alikuwa muumini mzuri wa vipindi hivyo kwa kujifunza vitu vingi. Aliweza kujua thamani ya kuwa mwanamke, pia mapenzi hayahitaji mtaji wa fedha wala elimu, bali hisia za mtu ambazo hupokelewa na mtu mwingine na kuwa kama ncha mbili zinasababisha umeme.

Siku zote mada zile zilimfanya ajiamini na kuamini anaweza kuwa na mpenzi wa aina yoyote mwenye hadhi yoyote kwa hali yake duni na elimu yake ileile. Alichojifunza kingine msichana kuwa msafi wakati wote hata kama anauza karanga hakutakiwa kijifuja na kutembea na nguo chafu au kutojijali.

Cecy aliamini kupendwa na watu wengi huku biashara yake ukiuzika sana ilikuwa ni kutokana na kujipenda kwa kununua nguo nzuri na muda wote kuwa msafi. Lakini kitendo alichofanyiwa na Colin kilimvunja nguvu na kuona hakuwa na sababu ya kupoteza fedha zake kununua nguo na vipodozi kwa vile hakuona umuhimu wake zaidi kurudia maisha ya zamani ya kuvaa nguo nzuri Jumapili atakapokwenda kanisani tu lakini siku nyingine atavaa hovyo.

Kitendo cha kutokwenda kwenye biashara kilimshtua sana mama yake na kutaka kujua kulikoni.

"Mwanangu kwa nini huendi kwenye biashara?"

"Mama yaani sijui nitatembeaje najisikia aibu naona kama kila mtu anajua kilichonitokea siku ile."

"Mwanangu, kilichotokea ni siri yako kwa vile hakuna aliyejua moyoni unawaza nini."

"Ni kweli, lakini moyo unaniuma sana mama."

"Kuumwa moyo ni kujitakia kwa vile Colin hakukutamkia wala wewe hukumtamkia kipi kikuumize."

"Kwa nini aliniita kwenye sherehe yake?"

"Kama walivyoitwa wengine."

"Mmh! Sawa, lakini nimeapa sitapeleka tena ndizi kwa mama Colin."

"Hiyo ni juu yako, lakini kumbuka katika sehemu uliyokuwa na uhakika wa fedha ni katika nyumba ile. Siku zote usiingize mapenzi kwenye biashara."

"Siwezi..siwezi mama watanionaje?"

"Wakuoneje, kwani wao wanajua nini juu ya kuanguka kwako?"

"Hata kama hawajui siendi," Cecy alishikilia msimamo wake.

"Siwezi kukulazimisha kwa vile wateja wale sikukutafutia uliwatafuta mwenyewe."

Cecy alipanga kuendelea na biashara yake mwisho wa wiki huku akisimamia msimamo wake wa kutopeleka ndizi kwa mama Colin.


***


Upande wa Colin alishtushwa na ukimya wa Cecy kutoonekana kwa siku tatu nyumbani kwao kupeleka ndizi. Akiwa chumbani kwake alichukua picha alizopigwa Cecy na kuzitazama.

Aliusifia uwezo wa mpiga picha kwa kumpiga picha nzuri za tofauti. Alituza macho na kuangalia uzuri wa asili wa Cecy.

"Hakika binti huyu ni mrembo," alisema kwa sauti ya chini na kurudia tena picha mojamoja.

Alitabasamu na kuamini wazo lake la kuanzisha kampuni ya mitindo litafanikiwa kwa kukusanya mabinti wenye uzuri wa asili wasiotumia madawa ya ngozi kama Cecy ambao angewatumia katika maonesho ya mitindo mbalimbali huku akiuza nguo.

Japokuwa elimu ya Cecy ilikuwa darasa la saba, kwa umri wake aliamini akisoma twisheni ya Kingereza kwa kipindi anajiandaa kufungua kampuni angekuwa amepiga hatua katika kuzungumza na kusoma Kingereza vizuri.

Alijikuta akitoka sebuleni na picha ya Cecy mkononi hadi alipokuwa amekaa mama yake.
"Mama mbona mchumba haonekani siku hizi?"

"Colin, wa nini kwani siku ambazo hakuja tumekosa ndizi?" mama yake alimuuliza huku akiondoa macho kwenye gazeti na kumtazama mwanaye.

"Hapana mama kumbuka alipata matatizo siku ya sherehe yangu huenda amezidiwa."

"Daktari alisema hakuwa na ugonjwa wowote alichopata ni mshtuko tu."

"Lakini kumbuka toka apate tatizo lile hatujamuona kuleta ndizi."

"Hata tukimuona atatusaidia nini?"

"Mamaaa! Mbona majibu yako kama yanaonesha chuki."

"Colin, mimi na wewe nani anamjua sana Cecy?"

"Wewe."

"Sasa kipi kinakufanya kutaka kuyajua mambo yake?"



Itaendelea.............
 
mizambwa usisahau kunitag pleeeeeaseeee


Sent from my iPhone using JamiiForums

Iendelee! Hadithi nzuri sanaa

Tuendelee mkubwa hadi imalizike...


Tatizo huyu Cecy analeta huzuni sana,

Anampenda Colin laini anashindwa kumueleza.

Amesahau kuwa siku hizi wanawake ndio wanatongoza mwanaume; yeye anasubiri kutongozwa. Mambo ya Utandawazi siku hizi hakuna kutafuna majani kama mbuzi au kula vidole na kuchezesha miguu
 
Last edited by a moderator:
Pamoja na yote lazma Cecy aolewa na mshkaji. Embu njoo endelea tuone inakuwaje




Tatizo huyu Cecy analeta huzuni sana,

Anampenda Colin laini anashindwa kumueleza.

Amesahau kuwa siku hizi wanawake ndio wanatongoza mwanaume; yeye anasubiri kutongozwa. Mambo ya Utandawazi siku hizi hakuna kutafuna majani kama mbuzi au kula vidole na kuchezesha miguu
 
Wakili wa Moyo-17




ILIPOISHIA:
"Wewe."
"Sasa kipi kinakufanya kutaka kuyajua mambo yake?"
SASA ENDELEA...


"Kwa kawaida mtu ambaye alikuwa akituletea biashara atoweke ghafla lazima nihoji."

"Hiyo picha ya nani?"

"Ya Cecy."

"Ya Cecy! Imefikaje kwako..hebu."

Mama Colin alisema huku akinyanyuka na kumfuata alipokuwa amesimama mwanaye na kuichukua picha ya Cecy aliyokuwa amekaa pozi tata.
Aliitazama kwa muda kisha alimuangalia mwanaye na kumuuliza.

"Hii picha umeitoa wapi?"

"Kwa nini unaniuliza hivyo?"

"Colin mwanangu sasa nimejua sababu ya Cecy kuja kwenye sherehe yako, yaani unajifanya unampenda Mage kumbe upo na Cecy."

"Mamaa!" Colin alimshangaa mama yake kusema kauli ile.

"Nasema hivi sitaki kukuona na uchafu huu na tena nitakwenda kumkomesha."

"Mama mbona unanihukumu bila kuniuliza?" Colin alizidi kumshangaa mama yake.

"Nikuulize nini, yaani uchafu huu sitaki kuuona," alisema huku akiichana picha ya Cecy na kuvitupa vipande chini na kumwita msichana wa kazi kuja kuvizoa.

"Mama unafanya nini, nilikueleza nini kuhusu production yangu?"

"Production na mapenzi yako na msichana mchafu maskini tena mbumbumbu hainiingii akilini," mama yake alisema huku akibinua midomo.

"Mama, Cecy si mpenzi wangu bali niliamini kwa muonekano wake pamoja na wasichana wengine wa muonekano kama wake angenisaidia katika kampuni yangu kufanya vizuri."

"Sitaki mazungumzo mengi nataka uvunje uhusiano wako na Cecy au nitamfanyia kitu kibaya ili nikanyogwe hawezi kuharibu mipango ya maisha yangu."

"Mama sina mpango wowote na Cecy, ulipoelekea sipo,"

"Naomba uondoke mbele yangu."

Colin hakusema kitu, aliondoka na kurudi chumbani kwake, alipofika alizichukua picha zote za Cecy na kuzificha kwa kuamini kwa jinsi alivyopendeza hata Mage angeziona angejua lazima ana uhusiano naye.
Itaendelea wiki ijayo.
Kitendo cha Colin kuwa na picha ya Cecy pia kumkaribisha kwenye sherehe ya kuzaliwa kwake, kiliamsha hasira za mama yake na kujikuta akimchukia Cecy ambaye aliamini kabisa mwanaye anampenda kuliko Mage.
Alinyanyuka na kutoka nje akiwa mwenye hasira hadi kwenye gari. Aliingia na kuondoka nalo kuelekea nyumbani kwao na Cecy ili kwenda kumkomesha aachane na mwanaye.
Aliendesha gari kwa kasi mpaka nyumbani kwao na Cecy. Alipofika aliteremka bila kufunga mlango na kwenye anapoishi Cecy na mama yake.
Alimkuta mama yake akitengeneza samaki wa biashara.

"Cecy yupo wapi?" aliuliza kwa hasira hata bila salamu.

"Dada yangu hata bila salamu?" mama Cecy alisema kwa sauti ya upole.

"Haitakusaidia, huyo kinyago wako yupo wapi?"

"Tatizo nini mzazi mwenzangu?"

"Sina shida ya maswali namtaka Cecy."

"Amekwenda kwenye biashara zake."

"Ooh! Kumbe ndiyo janja yake mwambie nimeisha mbaini. Akija mwambie sitaki kuvuruga maisha ya mwanangu nasema amkome."

"Kwani kafanya ni..." alikatwa kauli.

"Ee..ee, nimesema amkome kama ana tabia ya kenge basi damu itamtoka masikioni."

"Mbo..mbona ..si..si."

"Nimesema nikisikia tena usije kunilaumu, mwambie mwanao amkome mwanangu kama alivyokoma kwenye ziwa lako."

Baada ya kusema vile aligeuka na kuondoka na kumuacha mama Cecy ameganda kama sanamu asielewe chochote zaidi ya kashfa walizomiminiwa na mama Colin.
Alilitizama gari likiondoka kwa kutimua vumbi mpaka lilipopotea kwenye macho yake.

"Maama, " alishtuliwa na kauli ya Cecy aliyetokea nyuma ya nyumba akiwa na beseni tupu baada ya kumaliza ndizi.

Mama yake aligeuka na kumtazama mwanaye aliyegundua kulegwa kwa machozi kwa mama yake ambaye uso wake ulipoteza furaha.

"Mamaa! Kuna nini?" Cecy alishtuka.

"Mwanangu umaskini mbaya," mama yake alisema huku akielekea kukaa kwenye kizingiti cha nyumba.

"Kwa nini mama?"

"Umemfanya nini mama Colin?"

"Kivipi?"

Mama yake alimweleza yaliyotokea muda mfupi, Cecy alishtuka sana kusikia habari zile.

"Mama yaani ndiyo kasema hivyo! Hayo mapenzi na mwanaye yameanza lini?"

"Sijui."

"Mama namfuata sasa hivi anieleze kuja kututukana bila sababu, kama umaskini wetu tumeridhika nao."


Itaendelea baadaye............
 
Pamoja na yote lazma Cecy aolewa na mshkaji. Embu njoo endelea tuone inakuwaje




Waswahili wanasema "CHELEWA CHELEWA UTAMKUTA MWANA SI WAKO"


Cecy anashindwa kufunguka yaliyo moyoni mwake, bado yupo enzi za Ujima kuwa ni mwanaume ndiye anayeanza kwenye mapenzi,


KIGUGUMIZI KITAMPONZA............
 
Back
Top Bottom